NAOGOPA KUWA MWANAMKE 21
Ndio Broo Brayton Ila samahani sikukwambia mapem…..
Kabla sijamalizia kuongea alinyanyuka na kuondoka kwa hasira na kuniacha nikiongea mwenyewe..
“Ina maana ananiona mdogo!?.. Au sitakiwi kuwa na mahusiano.
Nilibaki niliwaza sikutaka kwenda kulala ndani nilijilaza sebren nikimsubiri basi alirudi mda wa usiku sana tena akiwa amekunywa yaani alilewa na hiyo haikuwa kawaida alipitiliza hadi chumbani kwake baada ya mda kidogo alikuja nilipokaa..
“Mimuh.. Aliita Brayton kwa utulivu nilikaa vizuri na kumtazama..
“Huyo mwanaume uliyemchagua umefuata vigezo vipi kwake.. Ni pesa!?.. Aliuliza Brayton akiwa amenikazia macho.
“Au muonekano wake wa nje umekuvutia zaidi.. Sema mbona upo kimya.. Alisema tena Brayton safari hii nilimjibu.
“Mimi nampenda tu.. Pesa sio kigezo kama umetaka niwe hivi basi acha nipate mtu wa kutengeneza nae Familia… Wala sikujua kauli ile kama ilikuwa mbaya kwa Brayton alinivuta mkono wangu kwa nguvu na kunyanyuka na mimi..
“Unataka kutengeneza familia eh!?.. mependa eeh.. Unajua kupenda wewe!?.. Alisema Brayton huku akinipeleka chumbani kwake alifunga mlango baada ya kuingia ndani..
“Mbona umenileta huku kaka Bra….. Kabla sijamalizia alinistopisha na kidole mdomo na kunikalisha Kitandani kisha nilimuona akivuta droo yake ndani kulikuwa kuna maburungutu ya pesa..
“Kama tatizo pesa chota humu.. Na kama hazitoshi nakuongeza.. Bado nilikuwa kimya hivi Brayton kapatwa na nini..
Mlango wa chumbani kwa Brayton ulikuea unagongwa aliusogelea na kufungua alikuwa ni Tina..
“Brayton ndio nini napiga simu hupokei!?.. Alisema huku akimsogelea Brayton alitupa jicho Kitandani na kuniona mimi..
“Unafanya nini humu!?.. Alisema Tina na kufanya ninyanyuke nilipiga hatua kuufata mlango Brayton alinizuia kwa kunishika mkono kisha alimgeukia Tina..
“Naomba uende Tina… Alisema Brayton lakini Tina hakutaka kutoka..
“Yaani siku zote unanizungusha kumbe unatoka na huyu mschana asiyejua hata kuoga..
Alisema Tina huku akininyooshea vidole………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 22
“Naomba uende Tina… Alisema Brayton lakini Tina hakutaka kutoka..
“Yaani siku zote unanizungusha kumbe unatoka na huyu mschana asiyejua hata kuoga… Alisema Tina huku akininyooshea vidole.
“Nimekwambia tokaaa… Alisema Brayton kwa sauti sana mpaka niliogopa basi Tina alitoka kwa hasira bila kusema chochote nilimuona Brayton akihema sana alinisogelea na kunivamia mdomoni na kunipa romance mikono yangu yote aliibana na kufanya nishindwe kufurukuta alivyoridhika aliniachia sijui nilipatwa na nini nilijikuta nimetulia mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio wala sikutamani aniachie..
Baada ya kuniachia aliondoka na kuniacha peke nilitoka nikikimbia na kwenda chumbani kwangu nililala kabisa..
Asubuhi niliamka nilikuwa nawaza kilichotokea jana nilinyanyuka na kuelekea nje hakukuwa na dalili ya mtu tena inaonekana jana hakurudi kabisa..
Sasa kaenda wapi huyu nilichukua simu yangu na kumpigia alikuwa hapatikani niliachana naye nilifanya usafi baada ya kumaliza kazi zangu nilijipumzisha ilifika hadi jioni bila uwepo wa Brayton nilikamata simu yangu na kumpigia Kelvin..
“Jana mbona hukunitafuta mpenzi!?..
Alisema Kelvin na kuendelea ” Na mbona ile pesa niliyokutumia umeirudisha!?..
Huyu anamasihara yaani mimi ninavyopenda pesa kabisa nimrudishie wakati nilishaitoa siku ile ile sitakagi masihara na ela kabla sijajibu chochote mlango ulifunguliwa alikuwa ni Brayton nilikata simu na kumsogelea “Vipi dogo!?…
Alinisalimia kwa uchangamfu na kunikabidhi bahasha pamoja na baadhi ya karatasi nilipokea..
“Hizo karatasi uzijaze leoleo kesho nazihitaji.
Alisema hivyo na kuingia ndani kwake cha kwanza nilichofanya ni kufungua ile bahasha nione kilichomo ndani yale makaratasi niliyaweka kando..
Nilishtuka baada ya kuona ni picha za Kelvin tena akiwa amepiga na waschana warembo tofauti tofauti yaani picha zilikuwa zaidi ya tano tena kila mmoja akiwa anamzidi mwenzake kwa uzuri nilizitupia chini sikutamani kuzitazama tena..
Brayton alitoka chumbani kwake na kuja nilipokaa..
“Mbona umezitupa chini!?.. Sikukupa ili kukurusha roho nimekuonyesha ili ujue aina ya mtu ambaye uko nae..
Alisema huku akizikusanya zile picha pale chini kisha sura yangu ilikuwa ndogo kama piriton nilikamata makaratasi na kusoma ilikuwa ni kuhusu shule..
“Shule!?……………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 23
Alisema huku akizikusanya zile picha pale chini kisha sura yangu ilikuwa ndogo kama piriton nilikamata makaratasi na kusoma ilikuwa ni kuhusu shule..
“Shule!?..
“Yeah.. Nataka ukasome uenda utakuwa ukiwa shule..
“Sasa nitaanzia dalasa la ngapi maana niliishiaga la tatu tu.. Nilisema kwa huruma mpaka Brayton aliangua kicheko sikujua kinachomchekesha..
“Kama una nia ya kusoma hata ukianza chekechea haina shida.. Nilibaki kushangaa yaani nianze vidudu aiiisei hapana nilirudisha makaratasi yake mezani..
“Bora hata niende ufundi kuliko kurudi dalasani tena nianzie mwanzo..
“Subiri nitafikiria.. Alinambia huku akielekea nje kupokea simu yake ambayo ilikuwa ikiita..
Nilienda chumbani nikiwa na mawazo sana ila mbona kama nilikurupuka kumkubalia Kelvin au ndio pesa zilinichanganya maana nilikuwa namfikiria Brayton akichanganya na zile romance alizonipa nilishaanza kudata nikiwa nawaza hayo yote Mlango wangu ulipigwa shuti moja tu na aliingia Tina..
“Wewe Malaya leo nitakuonyesha yaani Brayton ananikataa kwasababu yako..
“Mbona sina mahusiano na kaka Brayton.. Nilijitetea maana nilikuwa nikimuogopa Tina si mchezo amekuwa mkali kwangu mda wote pia hata kiumri sikuwa nampata.
“Etii.. Sina Mahusiano na kaka huna hata haya.. Sawa huna mahusiano nae pale Kitandani ulikuwa unafanya nini!?..
“Huna mdomo wewe?.. Sasa ngoja nikushikishe adabu kwanza..
Alisema Tina huku akinivaa kwa kuwa sikuwa na nguvu sikuweza kujitetea kwa lolote aliniangusha chini na kuanza kunisurubu sikujua David yuko wapi kwa mda huo maana kama bado angekuwa nje angemuona mda anaingia basi alinichakaza sana hata sikuelewa ilikuwaje ila nilipoteza fahamu…………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 24
Alisema Tina huku akinivaa kwa kuwa alinivamia sikuweza kujitetea kwa lolote aliniangusha chini na kuanza kunisurubu sikujua David yuko wapi kwa mda huo maana kama bado angekuwa nje angemuona mda anaingia basi alinichakaza sana hata sikuelewa ilikuwaje ila nilipoteza fahamu..
Niliamka nikiwa hospital mwili ulikuwa unauma hakuna mfano ndipo nilipokumbuka kipigo nilichochezeshewa jana nilifumba macho kwa hasira nikiwaza cha kumfanya Tina yaani ananipiga bila sababu mbona mimi sina mahusiano na Brayton..
Mlango wa wodi ulifunguliwa aliingia Brayton alinisogelea huku akihema sana alininyanyua pale na kunikunbatia niliangua kilio alikuwa ananibembeleza..
“Tina atalipa.. Tulia Mimuh.
Basi Brayton aliomba kuondoka na mimi japo niliruhusiwa lakini sikuwa sawa kabisa maana hata kutembea vizuri sikuweza aah mwanamke amekomaa yule utasema anaruka judoš¤£.
“Vua nguo ukaoge.. Jitahidi nimekuandalia supu ya kuku ukioga ntakuja kukufata. Alisema Brayton huku akitoka ndani.
Nilishindwa hata kunyanyuka maana mda wote nilikuwa natembea kwa msaada wa Brayton atakunyanyuka pia alikuwa akinishikilia.
Baada ya dakika kadhaa Brayton aliingia tena ndani na kunikuta nipo vilevile alivuta pumzi na kuninyanyua pale Kitandani na kunipeleka chooni taratibu..
“Jikaze kutembea utakuwa sawa sasa hivi..
Tulifika chooni akanikalisha pembeni ya kiti kilichopo chooni alinisogelea na kunivua Tshirt nilikataa kwa kugeukia pembeni kwani hata alinielewa alinikamata vizuri na kunivua nilibaki kifua wazi woga ulinivaa wala hakuwa na habari na mimi alivua na pens yangu nilibakiwa na chupi hiyo hakuangaika nayo nilikuwa mtu wa aibu wala sikumtazama usoni hata mara moja..
Alinisugua alivyomaliza alichomoa taulo juu ya msumali na kunirushia nilijifunga kisha akanirudisha chumbani..
Alinipatia nguo zangu alivyotoka nje tu nilijikaza na kuvaa nguo zangu kisha nilitoka huku nikiwa nimeshikiria ukuta..
Nilifika mezani na kukuta supu ya kuku iliyoandaliwa vyema nilikula kama sina akili nzuri nilivyoshiba nilijisogeza kwenye sofa iliyo sebren na kujilaza..
Sijui hata ilikuwaje nilimuona Tina akisukumiza lango na kuingia moja kwa moja aliniface mimi basi alikuwa akinisogelea kwa hofu niliyokuwa nayo kojo lilianza kunimwagika huku nikitetemeka “Aaah umeniweza Tina..
“Bado umeng’ang’ania tu kubaki humu ndani sasa subiri nikuonyeshe kwa mara nyingine..
Kavla hajanifanya chochote nilishangaa kabwagika chini kama mzigo Pwaah!..
Laahaula!. Alikuwa ni Brayton amemkata mtama..
“Imekuwa bahati umejileta mwenyewe ngoja nikufunze adabu.. Sijawahi kupiga mwanamke ila utanisamehe wewe si bondia aya nyanyuka tupigane.. Alisema Brayton huku akimnyanyua pale chini..
“you were just like a friend to me.. Yalikuwa nia maneno ya Brayton huku akimchezeshea makofi bidada Tina alivyoona amezidiwa alikimbia nje..
“Nataka kuondoka nyumbani… Nilisema huku nikilia Brayton alinisogelea na kunibeba kunipeleka nyumbani..
“Uendi kokote.. Hapa ndio kwenu……
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 25
Nataka kuondoka nyumbani… Nilisema huku nikilia Brayton alinisogelea na kunibeba kunipeleka nyumbani..
“Uendi kokote.. Hapa ndio kwenu..
****
Nililala chumbani kwa Brayton yeye alikuwa amelala sofani asubuhi yake niliamka nikiwa niko powa japo sio kivile nilinyanyuka na kusogea alipolala Brayton alionekana akiwa amechoka sana nilikaa pembeni yake nikimtazama nikakumbuka na ile romance aliyonipa siku ile nilijikuta natamani tu hata nimbusu mdomoni sijui ndio nilishaanza kupenda..
Basi nikiwa katika zoezi la kumbusu Brayton alifumbua macho nilirudisha nyuma uso wangu na kuongopa “Ni mdudu tu nilikuwa namtoa..
Brayton alitabasamu kisha akasogeza uso wangu kama ulivyokuwa mwanzo kisha akafumba macho kama alivyokuwa..
“Ok.. Acha niache umalizie kumtoa.
Ainu gani hii nimebambwa utamu wala sikutaka kubaki nilitoka nje safari hii niliweza kutembea mwenyewe..
“Ngoo! ngoo! ngo..
Yalikuwa ni makelele ya geti ishara mtu anagonga haraka haraka niliwaza atakuwa ni bondia Tina huyo nilitoa mbio hadi chumbani..
“Vipi!?. Aliuliza Brayton huku akinyanyuka.
“Tina anagonga geti leo mimi lazima niondoke.. Nilisema nikiwa mwilini mwa Brayton basi aliniacha ndani na kwenda kufungua geti baada ya mda nilisikia sauti ya vicheko na sauti za kiume nilitoka nje kuangalia walikuwa ni wanajeshi wenzake na Brayton..
Mmoja wao si ndio akakisogelea kile kiti nilichokojolea jana ili akae..
“Usikae.. Kuna mikojo.
Wa kwanza kushtuka alikuwa Brayton alinigeukia na yule alotaka kukaa alinyanyuka kama upepo..
“Aah mwanangu umevuta jiko kimya kimya.. Mnakojoleshana hadi kwenye viti..
Alisema yule kaka huku akicheka nilibaki nashangaa utani gani huu mbona kama unaendea kwenye ukweli sasa si watajua kama mimi ndio nimejikojolea nilivuta hatua kurudi ndani kinyonge kabisa..
Brayton aliniwahi kwa kunivuta mkono kisha akanisogeza karibu na wenzake “Amna bhana jana tulipata ugeni.. Si unajua watoto walivyo watundu choo kipo akakojoa hapo.. Ila aina mbaya kaa hapo.
Brayton alipoteza maboya huku akimuonyesha sehemu nyengine ya kukaa.
“Shem mambo.. Tuzoee tu sisi ndio wageni wako..
Alisema mwengine na kufanya nitabasamu yaani wameniita Shem niliitikia salamu na kuelekea jikoni kuandaa chai nilipika haraka haraka na kuwapelekea..
Walivyomaliza nilienda kutoa vyombo “Ahsante Shem chai tamu.. Brayton hii ndio chombo sio yule mwanajeshi wako sijui hata kama kupika anajua.
Nilitoa vyombo kinyonge sikujua ni kwanini ila ile kauli iliniuma kumbe Brayton anamwanajeshi wake basi nilikosa amani nilielekea chumbani kwangu mpaka mda wanaondoka niliagana nao juu kwa juu..
Brayton alirudi usiku nilikuwa nipo ndani alinigongea sana wala sikutaka kufungua…………..