NAOGOPA KUWA MWANAMKE 16
Wakiwa bado wanang’ang’ania kuondoka na mimi niliiona gari ya Brayton ikifunga break mbele yetu kisha alishuka na kusema huku akisogea nilipokaa..
“Muachieni huyo..
Walikuwa wabishi Brayton alichomo bastora na kuipiga juu mlio wa risasi uliwatawanya wote na kufanya wakimbie….
Brayton alinifuata pale nakunikaomata mkono kuninyanyua kisha alinikumbatia kwa nguvu huku akihema mno.
Sikuwa hata na nguvu ya kupinga nilikuwa nikitetemeka kwa Baridi machozi pia hayakukauka..
“Sikujua Kama ni mdhaifu kiasi hiki..
Alisema akiwa bado ameniweka kifuani mwake “Samahani ..
Ilo ndio neno la mwisho kulisikia kutoka kwake sababu nilikata moto mda uleule wala sikujua kimeendelea nini..
***
Nilishtuka kama mda wa asubuhi nikiwa na wenge kinoma cha kwanza kuangalia ilikuwa ni maziwa yangu ahahah inafurahisha eti nimeangalia maziwa sijui nilijua yamenyofolewa au laa.
Nilikuta yako salama hayaonekani nilivuta pumzi kidogo afadhari lakini T shirt ambayo niko nayo sio ile nilovaa jana..
Nilijifunua shuka kwa chini kuangalia kama nguo yangu bado ipo nilikuta nikiwa na boksa tu ambayo nilivaa jana lakini suluari haikuwepo..
“Unashangaa nini.. Kunywa supu upate nguvu.
Ilikuwa ni sauti ya bezy la Brayton nilivuta pumzi na kuisogelea Bakuli ya supu na vile nilikuwa na njaa niliipiga yote..
Brayton alikuwa pembeni akiniangalia nilivyomaliza kula niliitupia bakuli pembeni kwa hasira ilidondoka na kuvunjika..
“Umejua kuhusu mimi eh!?..
Niliuliza huku nikihema Brayton hakunijibu alinitazama jicho kali kisha akasema kwa ukali “Haijalishi okota hiyo bakuli kisibaki hata kigae kimoja la sivyo nitakuchakaza sasa hivi..
Si utani nilikuwa nikimuogopa Brayton nilijinyanyua huku nikiwa nimeshikilia shuka nilijifunga kiunoni nilichuchumaa pale chini na kuokota vile vigae vyote kisha nikaviweka pembeni na kumuuliza.
“Nguo zangu ziko wapi..
Alifungua kabati na kutoa nguo nilizitazama zilikuwa ni nguo za kike niliziweka pembeni bado Brayton alikuwa amesimama tu..
Simu yangu ilianza kuita mama G anapiga.
“Jana Nilikuwa na dharula ila sasa hivi nipo njiani nakuja..
Nilikata simu teyari nilikuwa nimeshanyanyuka teyari kwa kuondoka nilitazama pembeni kulikuwa na pens ya Brayton nilivuta na kuivaa chap ilikuwa kubwa kiunoni lakini ningefanyaje sasa nilianza kupiga hatua “Unaenda wapi ni Kelvin huyo!?..
Wala sikumjibu niliusogelea mlango nikitaka kutoka kwani hata nilipiga hatua nyingi tayari Brayton alishanivutia kwake.
“Unafanya nini.. Unataka unibaka!?..
Machozi yalishajaa usoni mwangu nilijitahidi kujinasua mikononi mwake lakini nilishindwa kwa kuwa alinikamata mikono niliamua kutumia miguu yangu kujiokoa nilimgonga na kifuti cha mguu kwenye mali yake..
Aliniachia mikono yangu na kushika chini huku akiugulia
“iiiish..
Nilifungua mlango wa chumbani na kutoka nje niliangaika kufungua mlango wa barazani lakini ulikuwa umelockiwa………………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 17
Machozi yalishajaa usoni mwangu nilijitahidi kujinasua mikononi mwake lakini nilishindwa kwa kuwa alinikamata mikono niliamua kutumia miguu yangu kujiokoa nilimgonga na kifuti cha mguu kwenye mali yake..
Aliniachia mikono yangu na kushika chini huku akiugulia “iiiish..
Nilifungua mlango wa chumbani na kutoka nje niliangaika kufungua mlango wa barazani lakini ulikuwa umelockiwa..
Sikuwa na ujanja tena Nilikuwa mnyoge nikijua leo ndio mwisho wangu nikujaribu na kujaribu nilishindwa..
Chumbani kwa Brayton kulikuwa kimya sana mpaka nilianza kuogopa nilisogelea mlango wa chumba chake huku nikinyata nilisimama sana mlangoni lakini hakukuwa na natumaini yoyote..
Nilisukumiza mlango na kuingia ndani Brayton akuwepo kitandani amelala chali huku mkono mmoja ukiwa upo ikulu alikuwa akiugulia sana kwa kubimbilika machozi yalianza kunitiririka mashavuni nilichuchumaa alipo..
“Samahani kaka Brayton sikukusudia kukuumiza..
Nilisema huku nikimtazama usoni “Kaniletee maji ya moto..
Alisema kwa sauti huku akinitazama jicho kwa jicho kali akipona huyu mbona ninalo..
Nilikimbilia jikoni na kuchemsha maji ndani ya sekunde kadhaa nilishamletea maji..
“Weka hapo kachukue kitambaa kabatini..
Nilifanya hivyo na kumkabidhi kitambaa alichonituma.. “Unanipa ili iweje umeniumiza makusudi nani wa kunikanda sasa..
Alisema Brayton huku akishusha suluari yake chini nilibaki nimeduwaa yaani mimi wa kumkanda kidume mwenzangu muhogo wake..
“Ilikuwa ni bahati mbaya unadhani ningefanya nini kama mwanamke..
“Kumbe wewe ni mwanamke eh.. Alinisanifu Brayton kwa kuniuliza hivyo nilibaki kimya..
“OK.. chukua iko kitambaa uje unikande ni vile najikaza tu.. Umeniumiza sana. Alikazia Brayton huku alinirushia kitambaa teyari alibakiwa na boksa nilikafumba macho na kukaza roho nilimsogelea huku nikiwa natetemeka..
Nilichovya kitambaa na kuanza kumkanda nilifanya haraka haraka na wala sikuwa namtazama usoni kwanza macho nilifumba nilisikia Brayton akitoa miguno tu sasa kwa wakati huo ata sikuelewa kama ya maumivu au utamu nilivyoona inatosha nilifumbua macho.
Nilikuta Brayton akinitazama sana sikujali nilimuangalia nilipokuwa namkanda palianza kutuna niliogopa nisije nikafanywa kitu mbaya nilichukuwa kitambaa changu na kupiga hatua kumbe chini kulikuwa na maji saa ngapi nisiteleze kwenye tailizi..
Nilipiga mweleka mmoja matata sana kabla sijafika chini Brayton aliniwahi kwa kunikamata mkono na kunivutia alipo.. Nilishangaa maana alikuwa faster lakini hiyo ndio ilikuwa pona pona yangu la sivyo ningebamiza kichwa badamu bangemwagika.
“Kuwa muangalifu umemwaga maji harafu unakanyaga..
Alisema huku akiniachia mkono na kujilaza tena nilitoa vyombo nilirudi kufuta maji kisha nilisimama pembeni..
“Mbona unanisimamia.. Potea hapo.
Alisema Brayton huku jicho lake kali likinitazama.. “Funguo hakuna Broo nimetafuta sana.
“Wewe ongea sauti yako usijifanye unakoloma harafu kama unataka kuendelea kubaki kaa.. Ila nitakufanya mboga sasa hivi.. Alisema kwa kuuma meno sasa nitaondokaje bila funguo jamani niliona ushakuwa msara nilifungua mlango na kutoka chumbani humo…………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 18
Alisema Brayton huku jicho lake kali likinitazama.. “Funguo hakuna Broo nimetafuta sana.
“Wewe ongea sauti yako usijifanye unakoloma harafu kama unataka kuendelea kubaki kaa.. Ila nitakufanya mboga sasa hivi.. Alisema kwa kuuma meno sasa nitaondokaje bila funguo jamani niliona ushakuwa msara nilifungua mlango na kutoka chumbani..
Nilikaa sana mama G alikuwa anapiga sana simu sikutaka kupokea maana hata ningepokea ningesema nini safari hii simu ilita tena alikuwa ni Kelvin boss..
“Habari yako Miss Angel!?.
Aliuliza Kelvin nilitabasamu na kujibu “nzuri Broo Kelvin nambie.
“Upo wapi nije kukufata nahitaji tuongee biashara.. Kuna sherehe kubwa sana wiki ijayo nahitaji uwe dance kuna 1M..
Ninavyopenda pesa yaani sikuuliza kingine chochote nilikubali..
Niliahidi kwenda kesho ili tuongee vizuri yaani milion moja kuikamata kwa siku moja lazima niende.
Kwa kuwa nilichoka sana basi nilifunga mlango wa chumbani humo na kulala.
Niliamka mda wa usiku njaa ikiniuma mno nilielekea jikoni nilikuta chakula alikuwa amepika Brayton nilikula huko huko jikoni..
“Naomba pensi yangu.. Alisema Brayton baada ya kunifuata jikoni akitaka nivue pensi lake nililolivaa.
“Hivi unafikiria nini kujibadilisha jinsia.. Mungu amekosea kukuumba hivyo eh?.. Aliuliza Brayton baada ya mimi kuwa kimya lakini hata hivyo sikujibu pia.
“Ok.. Nahisi hujawahi kukutana na vidume vya mbegu ila mimi nitakuonyesha kama wewe ni mwanamke.. Andaa maji unikande uliponiumiza.
Niliacha kula na kumgeukia “Naomba uniruhusu nirudi nyumbani maisha tu yamenifanya niwe hivi lakini haimaanishi kama nilipenda kuwa hivi..
Nilisema nikiwa nimemuangukia chini Brayton
“Siku ya kwanza nilivyokuuliza kuhusu wewe mbona hukunambia.. Au umetumwa kunipeleleza..
Kibao kiliniangukia aliondoka na kuniacha pale chini nilibaki nikijuta kumfahamu Brayton sikujuwa kwanini nilimuamini kiasi hiki..
Mwili wangu ulinyongonyea sikutamani kuishi tena niliona bora hata niwafuate w
azazi wangu kama ni shida nimezipitia sana tangu nipo mdogo nimekuwa mtu wa kuangaika tu uwenda nikifa nitapumzika..
Kwenye droo za jikoni kulikuwa na sumu ya panya nilijivuta na kufungua ile droo nilivuta kikaratasi chenye sumu ndani yake nilikinga maji kwenye kikombe kisha nilimimina ile sumu na kukoroga haraka haraka na vidole nilivyoona inatosha niliinywa yote bila kubakisha shetani alinisimamia kwelikweli maana sikuwa nahofu ya kifo kabisa…………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 19
nilijivuta na kufungua ile droo nilivuta kikaratasi chenye sumu ndani yake nilikinga maji kwenye kikombe kisha nilimimina ile sumu na kukoroga haraka haraka na vidole nilivyoona inatosha niliinywa yote bila kubakisha shetani alinisimamia kwelikweli maana sikuwa nahofu ya kifo kabisa..
Nikiwa pale chini kama nilikuwa namuona mama yangu “Umefanya nini mwanangu?..
Alisema mama kwa sauti ya kunilaumu kwamba nilichofanya sio sawa nilitoa sauti kwa shida sana na kumjibu huku nikimnyooshea mkono wangu mama “Nakuja mama nipokee.. nimekukumbuka sana.
Lakini kumbe ilikuwa nafsi tu maana mama hakuwepo tumbo langu lilianza kuunguruma kabisa kama kulikuwa kuna kitu kinajisaga nilianza kuugulia sasa ndio niliuonja uchungu wa umauti macho yangu yalikakamaa nikiwa bado nakukuruka pale chini nilihisi mama yangu yupo pembeni yangu akiniangalia kwa huruma sana.
“Nakuja… Ma..ma nimechoka kupambana peke yangu hii vita siiwezi.
Ghafla aliingia Brayton alinikimbilia baada ya kunikuta vile lakini sikuwa naelewa chochote..
“Mimuh.. Dogo .. dogo…
Aliita Brayton nilisikia kwa mbali baada ya hapo sikuelewa chochote niliona kama vile ndio nimefika mbinguni baba na mama walinipokea kwa furaha sana…
“Kwanini.. Mliniacha kule nikiteseka baba!?…
“Nimekuja kuungana na nyinyi sitaki kurudi tena kule… Nilisema kwa uchungu huku nikiwasogelea kuwakumbatia kabla sikawAfikia kuna jitu liliwakamata wazazi wangu nakuondoka nao nilibaki nikilia lakini hakuwaachilia angalau wanikumbatie tu nilijikuta naita “Maa.ma.
Kumbe ilikuwa ni ndoto sijui vipi maana nilikuwa hospital tena nikiwa namashine ya kupumulia kelele zangu ziliwashtua baadhi ya watu wa kwanza kumuona alikuwa ni Brayton..
“Mimuh mama umeamka… Alisema Brayton huku akisogea nilipo sikuwa na nguvu ya kumjibu kabisa..
Alikimbilia nje baada ya mda mfupi alirudi na dokta nilikuwa nikiwatazama Brayton macho yake yaliwiva sana kama mtu aliyekuwa akilia basi dokta alianza kupima mapigo yangu ya moyo na vinginevyo..
Aliingia Mama G baada ya kumuona machozi yalianza kunitoka..
“Si..ta..ki kuishi tena..
Nilisema kwa shida huku nikijitahidi kunyanyua mkono wangu na kuitoa ile mashine ambayo ilikuwa inanisaidia kupumua………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 20
Nilisema kwa shida huku nikijitahidi kunyanyua mkono wangu na kuitoa ile mashine ambayo ilikuwa inanisaidia kupumua..
Brayton aliniwahi kunikamata mikono yangu nilichomwa sindano ya usingizi na kulala fofofo usiku wake niliamka nilimuona Brayton akiwa amejilaza pembeni..
Niliachana nae m)wili wangu ulikuwa unaniuma mno hivyo nilijilaza kulikucha asubuhi nilikuwa niko kawaida kabisa mama G alikuwa pembeni yangu..
“Mimuh ebu mlaani shetani.. Usiruhusu akutawale kama kuna kosa tumefanya tueleze..
Nilikuwa kimya nikimtazama baada ya mda Brayton alikuja nilipelekwa kwa Daktari ili anipe ushauri nasaha alinieleza vitu vingi pia ilitakiwa nitafutiwe mwalimu wa saikoroj..
“Kukata Tamara ya maisha ni dhambi kubwa sana haijarishi unapitia mangapi usiwe mdhaifu.. Mungu anakupenda na amekuumba kwa makusudio yake aya unataka kujiua inamaana mungu amekosea kukuumba!?…
Yalikuwa ni maneno mazito ya dokta aliongea mengi sana nikishauliwa nisiache maombi maana shetani ananijaribu..
Baada ya yote tulirudi kwa Brayton mama G yeye alisharudi kwake..
“Ooh Brayton nimekusubiri sana… Alisema bint mmoja ambaye tulimkuta nje baada ya kumuona Brayton alimkumbatia..
“Aah Tina umerudi.. Karibu. Alimkaribisha huku tukiingia ndani.
Nilifikia kujilaza kwenye kochi licha ya kuwa niliruhusiwa lakini bado mwili wangu haukuwa vizuri.
“Huyu mschana ni nani!?.. Aliuliza Tina huku akinitazama sana..
Brayton hakumjibu alipitiliza chumbani kwake yule dada naye alimfuata mda nimejilaza simu yangu ilikuwa ikiita alikuwa ni Kelvin siku zote amekuwa ananitongoza sasa kwa vile nimeshakubaliana na jinsia yangu ngoja tu nimkubalie japo sikuwa na hisia kabisa kwake…
Mara nyingi nilikuwa naenda kuonana na dokta wa saikolojia ilinisaidia kukaa sawa wala sikuwa naichukia jinsia yangu japo nilikuwa napata wakati mgumu kutokana na mazingira niliyoyazoea..
Siku zilikuwa zinaenda kasi Tina mara nyingi huwa anakuja kuonana na Brayton lakini hakuna siku ambayo amekuja bila kunitupia maneno kiufupi hakuwa hajiamini akidhani labda natembea na Brayton..
Siku hiyo nilipanga kushtaki kwa Brayton “Kaka Brayton mueleweshe Tina mimi ni nani yako maana ananichukia sana..
“Bambie nimwambie wewe nani yangu!.. Alisema Brayton na kufanya nijiulize mara mbili mbili ila nilipotezea kabisa..
Siku hiyo tulipanga kutoka Weekend na Kelvin hivyo alinitumia pesa kwajiri ya maandalizi laki tano ili ninunue nguo pamoja na urembo mwengine maana nilikuwa nyuma sana kwenye kujiremba nilishanunua kila kitu nilikuwa nikisubiri siku ifike tu..
“Naomba hiyo simu yako.. Mmh tangu lini akaazima simu yangu huyu.
“Haina salio kabisa.. Nilisema huku nikitaka kuondoka maana simu yenyewe sifutagi chochote.
Brayton alinivuta mkono na kunipokonya simu na kuingia nayo ndani kwake.
Nilibaki niking’aa sharubu nisijue lengo la Brayton baada ya mda mfupi alirudi nilipo…
“Una mpenzi!?.. Aliniuliza akiwa amekunja sura huku akinipatia simu yangu.
“Ndio Broo Brayton Ila samahani sikukwambia mapem…..
Kabla sijamalizia kuongea alinyanyuka na kuniacha nikiongea mwenyewe…………..