NAOGOPA KUWA MWANAMKE 01
Ilikuwa ni asubuhi na mapema sana nikiwa ndani ya chumba changu kilicho rafu rafu nikisubiri jioni ifike niende kwenye mizunguko yangu..
Sikubahatika kuwa na wazazi kwani waliniacha tangu nikiwa mtoto yaani walifariki hiyo ilifanya nijilee mwenyewe kwani hata ndugu zangu sikuwa nikiwafahamu nilibaki kuwa mtoto wa mtaani.
Kulikuwa na Mama mmoja jirani yangu yeye alinisaidia kipindi chote ambacho wazazi wangu wamefariki lakini na yeye bahati mbaya aliachika na mumewe hiyo ilifanya aondoke na mimi kubaki bila msaada wowote..
Katika umri wangu mdogo nilishuhudia watoto wa kike wenzangu wakiwa wanabakwa mara kwa mara tena na wababa wakubwa wakubwa hiyo ilinifanya nichukie kuwa mwanamke sababu nilihofia sana uwenda na mimi ningeweza kufanyiwa ukatili wanaofanyiwa wenzangu..
Hii ilinianya nibadilishe muonekano wangu na hata jina pia tangu kuanzia hapo jina langu lilikuwa Mimuh na hakuna aliyeweza kunigundua kama ni mwanamke kwa kipindi chote hiko mpaka umri niliofikia japo sura yake iliwachanganya wengi sikuthubutu kuvua kofia pia nilikuwa na ndevu zangu za bandia sikuthubutu kuzitoa hata sekunde na kujiamini ndio ilikuwa siraha yangu..
Ilifika jioni nikiwa nipo pembeni ya barabara na kapu langu la karanga.. Hiyo ndio ilikuwa biashara yangu maarufu sikuhitaji kujichanganya na makundi ya watu hivyo huwa nakaaga pembeni kisubiri wateja..
Ghafla mbele yangu alipita mschana mrembo sana nilimtazama kisha nikanyanyua kapu langu na kumsogelea yule dada..
“Karibu sister karanga za moto..
“Wala sihitaj…. Kabla yule dada hajamalizia kauli yake alipita kibaka na kumpora mkoba alioubeba na kukimbia nao..
Yule Dada alianza kupiga kelele za wizi huku akinionyeshea kidole kwa kujua nimeshirikiana na yule kibaka..
Kama mjuavyo maeneo yaliyochangamka ukitaka kumuua mtu muitie wizi yaani ndani ya dakika kadhaa watu walishajaa na kuanza kunishambulia..
“Sema alipo mwenzako laa sivyo huchomoki hapa.. Alisema mbaba aliyeonekana kuwa na hasira kali huku akinitia mateke..
“Sihusiki na chochote mnaniua bure.. Simjui..
Nilisema kwa shida huku nikikohoa.
Watu bado walikuwa hawataki kuelewa ndio kwanza walizidi kunishindilia “Kijana mdogo unataka kupoteza uhai wako kwa tamaa za kijinga..
Alisema mbaba mwingine huku akinitazama nilikuwa nimechakaa kwa kichapo kapu langu la karanga likiwa halipo maeneo hayo..
“Kuna nini hapa.. Ilikuwa ni sauti ya mkaka ambaye ndio kwanza alikuwa anafika eneo hilo.
“Kuna mwizi hapo anapigwa si unajua vijana wetu wa siku hizi wameweka tamaa mbele..
Yule mkaka alipenya penya mpaka nilipo alinitazama na kuwageukia raia “Ameiba nini huyu!?..
Aliuliza na kufanya watu wote watazamane maana hawakuwa wanajua kimeibiwa nini..
“Ni mkoba wangu alikuwa yeye na mwenzake..
Alisema yule dada aliyeibiwa “Huo mkoba unaghalimu kiasi gani au ndani yake kuna kipi cha thamani..
Yule kaka aliwazuia watu kunipiga kisha akamsogeza pembeni yule dada waliongea mwisho alitoa pesa kumkabidhi alimpatia bussines card pia..
Alinifuata pale chini na kuninyanyua kisha aliniamuru nipande kwenye gari..
Tulifika kwake kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana alinipatia dawa za maumivu “Leo utalala ndani ya chumba hiki kikipungua chochote utawajibika..
Alisema yule kaka huku akitoka niliwaza sana sasa kanileta kwake kivipi ikiwa haniamini wala sikuwaza tena kuhusu maneno yake nilikuwa nikimshukuru mungu kwa kunipatia msaada maana isingekuwa yeye sidhani kama ningekuwa mzima..
****
Asubuhi na mapema nilikuwa nimeshaamka niliingia chooni kujimwagia kisha nilivaa nguo zangu niliyabana manyonyo yangu vyema ili yasionekane kama kawaida yangu nilihakikisha ndevu zangu zimekaa vyema na kutoka nje..
“Vipi dogo umeshaamka!?..
Ilikuwa ni sauti ya yule kaka alikuwa jikoni akikaangiza “Ndio nimeamka Broo.. Asante sana kwa msaada wako..
“Ni mjini hapa utakuja kufa kuwa makini.. Harafuu…..
Alisema hivyo huku akinitazama sana nilipatwa na hofu nilianza kuhema mfululizo nikihofia uwenda amegundua kitu kuhusu mimi.
“Jana sikukutazama vizuri mbon…
Kabla hajamalizia nilianza kukohoa mfululizo yote ilikuwa ni kumkatisha mazungumzo yake..
“Naitwa Mimuh.. Asante broo kwa msaada mimi naenda.
Nilisema hivyo na kupiga hatua kuondoka mwendo wangu sikuweza kuubadilisha nilikuwa natembea kibraza men………………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 02
Jana sikukutazama vizuri mbon…
Kabla hajamalizia nilianza kukohoa mfululizo yote ilikuwa ni kumkatisha mazungumzo yake..
“Naitwa Mimuh.. Asante broo kwa msaada mimi naenda.
Nilisema hivyo na kupiga hatua kuondoka mwendo wangu sikuweza kuubadilisha nilikuwa natembea kibraza men…….
“Subirii.. Alisema yule kaka na kunifuata.
“Brayton hapa.. Ukiwa na shida usisite kunijulisha wizi sio mzuri dogo.. Alisema hivyo huku akinipiga piga begani kisha alinikabidhi bussines card niliondoka hadi nyumbani nilifikia kulala tu huku nikiugulia vizuri maumivu yangu..
Ilifika jioni bado nilikuwa ndani sikuwa na hata mia ya kula niliamua kutoka nje nilienda hadi kwa mama G jirani yangu naweza kusema yeye ni kama mama angu mdogo amekuwa akinisaidia baadhi ya mambo madogo madogo na yeye pekee ndio anayejua jinsia yangu na mara zote nimekuwa nikimsisitiza abaki na hiyo siri..
“Jana sijakuona kabisa… Ilikuwa ni sauti ya mama G.
“Jana nimepata majanga nimesingiziwa soo yaani… Nilisema huku nikimuonyesha baadhi ya majeraha mwilini mwangu..
Alikaa kimya sekunde kadhaa huku akinitazama “Shamimu mimi nadhani huu ndio muda rasmi wa kubadilika utaishi hivyo hadi lini!?..
Katika majina siyapendi ilo ndio la kwanza yaani ananiita shamimu nilinyanyuka kwa hasira na kutaka kuondoka..
“Sisemi kwa ubaya.. Sasa umekua unahitaji kuwa na familia..
“Bhana mimi siwezi badilika.. Kama kuna chakula nipatie tu njaa inauma kinoma.. Nilisema huku nikirudi kukaa chini si unajua wanaume huwa hatuzili..
Nilipatiwa msosi na kula kisha niliaga sasa niliingia ndani kutafuta kiswaswadu changu nilikirekebisha chapu na kuchukua namba ya broo Brayton nikapiga..
“Oya Broo Mimuh hapa naongea..
“Aah Dogo vipi mbona hukunitafuta nilijua raia wameshakubandanisha.. Alisema Broo kwa utani.
“Amna nilikuwa naweka mazingira sawa.. Sema broo mimi nina shida.. Nilisema kwa sauti ya upole..
“Sawa subiri nipo kazini natoka mda si mrefu nitakupigia usiwaze..
****
Jioni Brayton alinipigia na kunambia niende kwake nilijiandaa chap nilipigilia jeans langu na T shirt kubwa bila kusahau mzura wangu ambao sikuthubu kuuacha hata sekunde..
“Shida yangu ilikuwa ni pesa ya msingi wangu wa karanga jana nilipoteza kila kitu.. Nilimwambia baada ya kufika kwake.
“Haina shida ila hii kazi sio salama kwako yaani bado unaitamani tu..
“Sasa nitafanya kazi gani ikiwa elimu sina..
Nilisema hivyo na kufanya Brayton aanze kuniuliza vingi kuhusu mimi nilimjibu vyote lakini sikuthubutu kumuelezea kuhusu jinsia yangu..
“Ok mimi nitakutafutia kazi ya kujishikiza naomba ukae hapa kwa siku hizi mpaka nitakapofanikisha suala la kazi…
Alisema Brayton wazo lake halikuwa baya na ilikuwa ni zaidi ya msaada kwangu kama ningefanikiwa kupata kazi ningefurahi sana maana ningeweza kujimudu kwa kila kitu..
Siku hiyo nilishinda nyumbani kwa Broo japo mara nyingi sikutaka kujiweka karibu naye hofu yangu angenitambua..
Nikiwa naandaa chakula alifika Brayton..
“Oya dogo yule manzi wa jana amenipigia…
Bado nilikuwa sijamuelewa niliacha kukaanga na kumuuliza “Manzi ipi hiyo..
“Ni yule ulomkwapua mkoba wake jana… Alisema Brayton wala sikuifurahia kauli yake nilibaki kimya maana niliona kabisa kuwa hana imani na mimi..
“Ni hivi analeta shobo.. Alisema Brayton huku akibonyeza bonyeza simu ishara anachati mda wote bado nilikuwa kimya.
“Mimi sitaki kumpitia nataka nikuunganishe nae umpige miti bila huruma maana jana ulipigika sana au hutaki kurudisha mashambulizi..
Alisema Brayton na kufanya niangushe upawa na kujibu kwa hofu”Hapana.. Sinaga roho ya kisasi.
“Acha woga uko na Broo wako hakuna kitakachohari……………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 03
Acha woga uko na Broo wako hakuna kitakachoharibika..
Nilibaki kimya wala sikutaka kusema chochote teyari nilishaona hii nyumba hainifai..
Tulipiga menu na kuelekea vyumbani kulala kwa kuwa nilichoka sana haukupita mda mrefu nilikuwa nishapitiwa na usingizi..
Nilikuja kushtuka asubuhi mda umeenda nilinyanyuka chap na kuelekea bafuni nilivaa huko huko nilibana maziwa yangu vyema nilivyohakikisha niko sawa nilitoka nje..
Nilipishana na Brayton akiwa amevalia unform za jeshi nilibaki nikimshangaa sikudhania kama angeweza kuwa mwanajeshi nilimchukulia kama muhuni fulani hivi..
“Vipi dogo ndio unaamka.. mimi nawahi kwenye majukumu yangu baadae basi.. Alisema huku akitaka kutoka.
“Broo Mimi natoka pia naenda kwenye mizunguko yangu.. Nilisema huku nikiwa natoka pia.
“Baki hapa mimi kuna jamaa nimeongea nae kuhusu wewe amenambia atanipatia jibu baadae jioni nitakwambia nini cha kufanya… Alisema Brayton huku akichomoa noti ya 10000 na kunipatia..
Sikuwa na shida nilibaki nikisubiri jioni ifike kwa kuwa nilikuwa peke yangu nilijiandalia msosi baada ya kushiba nilielekea sebren ilipo Tv..
Niliwasha kulikuwa na CD nyingi nilichukuwa moja na kuweka ilikuwa ni Love story mda wote watu wanakiss na Romance tu..
Nilihisi hali tofauti nilizima haraka na kutoka nje nilielekea sehemu ambayo Brayton huwa anafanya mazoezi..
Nilianza kunyanyua vyuma si kwamba nilikuwa nina nguvu wala yote ilikuwa ni kujiweka sawa…
Nikiwa najikakamua kunyanyua vyuma alifika Brayton “Inabidi ukaze dogo.. Chuma akishikwi hivyo..
Alisema huku akinisogelea tayari alishakuwa karibu yangu alikaa kwa nyuma na kunishikisha chuma vizuri nilikuwa nikihema mno nikitamani hatoke nyuma yangu..
alivyohakikisha nimekishika vyema alitoka kwani nilikuwa na nguvu asa chuma kilinidondoka na kunibonda mguuni.
“iiii.. shiiii.. Nililalamika huku nikikaa chini..
“Acha kuwa mzembe mzembe nyanyuka uje uchukue spirit… Unadhani wanawake wanamaind wanaume wa dizain yako piga Tizi..
Alisema Brayton huku akiingia ndani nilimfuata huku nikichechemea alinipatia spirit..
“Niliwasiliana na yule jamaa wa kazi mipango imefeli.. Nimekutafutia nafasi jeshini..
Alisema hivyo na kufanya nidondoshe kichupa cha spirit yaani mimi nijiunge jeshi hapana kwa kweli..
Aliniona nilivyoshtuka ila hakusema chochote aliokota spirit na kunambia nikae chini nilikaa aliukamata mguu wangu apake dawa lakini alibaki ananitazama miguuni niliutoa mguu wangu na kunyanyuka..
” Oya Broo Nipe nitaenda kupaka mwenyewe..
Nilisema nikiwa nishampokonya teyari niliondoka chumbani nilianza kuwaza hapa ni kuondoka tu jeshi halinifahi hata..
Nilimaliza kujipaka na kumrudishia dawa yake..
“Leo tunatoka dogo…
“Amna.. Mimi leo naelekea nyumbani..
“Kufanya nini.. Wewe usiwaze leo tunaenda kununua viwalo vikali sana weekend hii kuna part ya mwanangu au unataka kwenda mtaani wakakubandanishe wakuue.. Harafu huo mzura wako uwe unabadilisha au mara moja moja uwe unavua mtu anashindwa kukuzoea..
Alisema kiutani na kufanya nicheke kupoteza maboya maana kauli yake haikuniingia akilini yaani nivue hii kofia “Unajua nini dogo.. Yule demu wako kaingia line ila sio type yang..
Mda anaendelea kuongea simu yake iliita alitabasamu na kunikabidhi simu nipokee niliichukua bila shida “Oy nambie..
Niliongea huku nikimtaza Brayton ambaye alikuwa akinikonyeza akitaka nipige sound nilioa liwalo na liwe kuliko nikatae aanze kunishuku maana kikawaida wanaume huwa hawarembi..
“Broo ametoka.. Ila nimejikuta nimevutiwa na sauti yako unaitwa nani mrembo..
Mda wote Brayton alikuwa akicheka hana mbavu “Naitwa Queen kwahiyo anarudi saa ngapi!?..
“Achana na habari za broo yupo na mkewe mimi nimetokea kukuelewa ila sema nitakutafuta…
Nilisema hivyo huku nikikata simu na kumtazama Brayton aliyekuwa amekolea kwa kicheko wala sikufurahia nilimuuliza huku nikikaza sura “Nini sasa!?……………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 04
“Achana na habari za broo yupo na mkewe mimi nimetokea kukuelewa ila sema nitakutafuta…
Nilisema hivyo huku nikikata simu na kumtazama Brayton aliyekuwa amekolea kwa kicheko wala sikufurahia nilimuuliza huku nikikaza sura “Nini sasa!?…………….
“Unakuwa kama bikra wa kiume bhana sasa kwanini umekata simu ilitakiwa uanze kumpamba kwanza na maneno matamu..
Wala sikumjibu jioni tulijiandaa na kutoka moja kwa moja tulielekea kwenye maduka ya nguo tulichagua nguo kali gharama zote zilikuwa juu ya Brayton.
Nilinunua kofia pia bila kusahau raba baada ya yote tulielekea sehemu kupata msosi Brayton alianza kunywa pombe taratibu..
Mwishoni alianza kulewa nilimzuia kunywa tulianza kurudi nyumbani kwakuwa sikuwa najua kuendesha gari dereva alikuwa yeye aliendesha gari umbali mrefu kisha alisimamisha gari..
“Kwa hali hii siwezi kwenda nyumbani acha nichague kipozeo..
Alisema huku akinionyesha pembeni ya barabara kulikuwa na wanawake wengi waliovaa nguo za kuacha miili yao wazi moja kwa moja nilijua wanajiuza nilibaki nikimshangaa..
“Kwanini umekunywa pombe ikiwa unajijua huna uvumilivu..
Nilimwambia Broo Brayton “Nina miezi kadhaa sasa hii savana imeharibu kila kitu…
Alisema huku akielekea walipo wale wadada nilibaki nimesimama nikiwaza sana nitafanya hivi hadi lini si bora nirudi kuishi maisha niliyoyazoea..
“Oya dogo njoo..
Aliniita Brayton nilikimbilia eneo lile nikijua ananiitia kitu cha maana “Vipi broo?..
“Chagua hapa mimi ndio naondoka na huyu.. Alisema Brayton akiwa amemkamata mdada mmoja aliyejaaliwa mshangazi.
“Hapana kaendelee tu utanikuta kwenye gari.. Nilisema huku nivuta hatua kuondoka.
Lakini nilivutwa nyuma na mmama mmoja kisha akanikumbatia “Jamani wala usiogope mimi nitakupa vitu hadimu.
Nilimtoa kwa kumsukumizia pembeni na kufanya anguuke chini kama mzigo Puuh!
Sikuongea chochote niliondoka kwa hasira nilifika kwenye gari nilijikuta nikianza kulia hivi nitaishi hivi hadi lini na siwezi kuongea chochote kwa Brayton kuhusu maumbile yangu kivyovyote..
Nilikaa kwenye gari mpaka nikapitiwa na usingizi nilikuja kushtuka baada ya Broo kunishtua..
“Sorry dogo nimechelewa sana.. Alisema Brayton huku akiwasha gari lakini wala sikuwa nimemjibu alielewa kuwa nimekasirika.
Tulifika home aliingiza gari ndani moja kwa moja nilielekea kwenye chumba changu nilisanya baadhi ya nguo zangu na kumgongea Brayton aliniruhusu nipite chumbani kwake..
Nilisukumiza mlango na kuingia ndani hamadii nilimkuta Brayton akiwa anajifuta maji tena alikuwa amevaa boksa tu.
(Mwanamke ni mwanamke tu yaani nilijikuta nimepata mshangao wa ghafla niliona aibu na kutazama chini..
Brayton alinisogelea nilijikaza kiume na kunyanyua sura yangu lakini sikuwa na ujasiri ambao niko nao siku zote..
“Naenda nyumbani..
“Kufanya nini? kesho nakupeleka mazoezini unatakiwa ukaze.. Maana mwezi ujao unaenda jeshini nishaandikisha kila kitu..
Alisema hivyo huku akivaa bukta yake na kumalizia na pensi..
Ooh jeshini tena nilijikuta nimeishiwa nguvu licha ya kujifanya mwanaume kiukweli sikuwa na nguvu kabisa.
Asubuhi ilifika kweli nilipeleka kwenye sehemu ya mazoezi na yeye alielekea kazini kwake.
Mazoezi yalikuwa magumu kiasi kwamba nilishindwa yaani kati ya wanaume wote peke yangu ndio nilikuwa lege lege.
Kulikuwa kuna wanawake kama wawili hivi ndio nilikuwa nao sawa maana hata push Up sikuwa naweza.
Ilifika mda wa kuondoka tulienda kuoga then nilikaa nikimsubiri Brayton aje..
“Mambo.. Ilikuwa ni sauti ya mdada ambaye tulikuwa tukifanya nae mazoezi.
“Poa.. Nilijibu kwa sauti ya bezi huku nikiishusha vizuri kofia yangu..
“Mimi nimependa tuwe marafiki nimevutiwa jinsi ulivyo pia hupendi kuchanganyika na watu.
Alisema huku akiitoa simu yake ambayo ilikuwa kubwa nilifikiria mara mbili mbili niliona bora nimpe namba ya Brayton..
Tukiwa tunapiga piga story alifika Brayton nilimuaga na kuondoka mda wote alikuwa akinitolea tabasamu..
“Kumbe videmu kama hivi ndio unavielewa yaani jana umeliangushia chini limama la watu.. Sema unatakiwa ukaze upiganie future yako………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 05
Kumbe videmu kama hivi ndio unavielewa yaani jana umeliangushia chini limama la watu.. Sema unatakiwa ukaze upiganie future yako………..
Alisema Brayton nilikubaliana nae zilipita siku kadhaa nikiwa bado naendelea na mazoezi kwa mbinde..
Siku hiyo nilishindwa kwenda kwenye mazoezi mwili wangu ulikuwa ukiuma sana nilipanga kurudi nyumbani kwanza..
Mchana nilipigilia vizuri na kurudi nyumbani moja kwa moja nilifika kwenye kichumba changu kulala kwani usingizi ulikuja sasa nilianza kuumwa na tumbo yaani lilikuwa linauma mpaka linauma tena nilishindwa kuvumilia..
Nilivuta panadol zilizopembeni yangu na kumeza lakini haikufanya liache kuuma nilijikongoja hadi kwa mama G nilifikia kujilaza kwenye mkeka huku nikiugulia tumbo..
“Umekula nini leo!?…. Aliuliza mama G huku akinipatia dawa ambayo aliitengeneza kwa kutumia majani..
Nilikunywa na kujilaza nilikuja kushtuka tumbo likiwa limeshapoa nilinyanyuka na kutaka kuondoka…
“Wee.. Embu subiri hapo hapo.
Alisema mama G huku akinifuata “nimekaa mda wote hujasema chochote naondoka ndio unaniita.. Nilisema hivyo nikiwa nimesimama.
“Kumbe ulikuwa unableed kwanini hukuvaa ped!?. Alisema huku akinifunga khanga kiunoni niliganda dakika kadhaa na kujitazama nyuma nilikuta nimechafuka mno nilitoa macho niaje hii mbona miaka yote sikuwahi kutoa damu jamani matatizo gani haya..
Nilijikuta nimekaa chini tu sababu wala sikutegemea mama G alianza kupiga vigeregere “Sasa umeshakuwa acha utoto uliokuwa unafanya wewe ni wakike tu na hilo haliwezi kubadilika.
Alisema Mama G huku akinivutia ndani alinipatia maji nikaoge nilioga na kuangalia nguo zangu nivae zote zilikuwa zimelowekwa kwa maji alinipatia gauni..
“Unafanya nini.. Hapana siwezi kuvaa hivi.
Nilisema nikiwa bado nimesimama lakini mama G hata hakujali..
“Shika hizo ukajihifadhi na uvae hizo nguo..
Nilivaa ile gauni ambayo hata sikuielewa yaani mimi leo nimevaa gauni kwanza nilijiona kama kuna kitu kimepungua mwilini mwangu..
Basi nilienda sebren alipo mama G nilikaa pembeni yake nikiwa nimefura kweli kweli..
“Embu toa hizi.. Alisema huku akinivua ndevu zangu na kuzitupia chini niliziwahi na kuzishika mkononi..
“Yaani uzuri wako haufichiki.. Umependeza sana na imani hata wazazi wako huko walipo leo wamefurahi.. Alisema mama G kwa hisia na kufanya niangushe machozi niliwakumbuka sana wazazi wangu nililia sana laiti kama baba na mama wangekuwa hai nisingeteseka mpaka kuwa hivi..
“Bado hujachelewa badilika kuanzia sitakuacha kwa chochote.. Huna cha kuogopa tena wewe ni jasiri sana..
Alisema mama G nilinyanyuka na kuelekea mlangoni nilichungulia pande zote nilivyohakikisha hakuna watu nilitoka nduki hadi chumbani nilichukua kipande cha kioo na kuanza kujitazama nilichukua mustach wangu na kuubandika kidevuni..
****
Jioni Brayton alinipigia akinitaka nirudi yeye amesharudi lakini nilikataa tena wala sikuyahitaji tena maisha ya kule.
Zilipita siku kama tatu bila kwenda kokote nilikuwa nikishinda kwa mama G..
Alininunulia gauni zuri na kutaka nilivae nilikataa alinilazimisha sana mwishowe niliamua kulivaa alinisuka mnyoosho mustach wangu pia niliutoa hakika nilipendeza ila sasa sikuwa na swaga za kike kabisa..
Nilikuwa najitahidi kumsaidia mamaG baadhi ya kazi jioni moja nilikuwa naosha vyombo kwa nje nikiwa nimeinama nilisalimiwa.
“Habari yako dada!?..
Sauti niliitambua vyema alikuwa ni Brayton niliwaza mara mbili mbili huyu kapajuaje huku..
“Samahani Dada.. Umenionea Mimuh kwa siku ya leo… Alisema tena Brayton baada ya kuona niko kimya.
“Hapana sijamuona.. Nilisema bila kumtazama huku nikiingiza vyomb……..