𝗛𝗨𝗬𝗨 𝗠𝗪𝗔𝗡𝗔𝗨𝗠𝗘 𝗞𝗔𝗟𝗢𝗚𝗪𝗔
Mimi ni mama wa watoto wawili, mwanangu wa kwanza nilizaa huko nyuma huyu mwingine ndo nimezaa na huyu mkaka niliyekuwa nimepanga sehemu nakaa peke yangu naendesha maisha yangu nikakutana na huyo kijana yeye alikuwa anakaa na wazazi wake basi tukawa marafiki mwisho tukawa na mahusiano wakati huo yeye anaishi kwao na mma yake wa kufikia alikuwa anasema anamtesa tesa nikamwambia atufute chumba apange akasema hawezi kupanga kwa sababu hana kazi nikamwambia wewe ni mtoto wa kiume pambana tu utapata kazi.
Basi kuna ishu alienda kufanya akapata pesa akapanga akaniambia rudisha vitu kwenu tuishi wote, sawa nikakubali tukawa tunaishi wote lakini wakati hana kazi maalumu Mishen Town tukawa tunavumiliana hivyo hivyo maisha yakaenda alikuwa hana kazi lakini alikuwa ananipenda mpaka najisikia raha ananijali mpaka najiuliza nilichelewa wapi mimi?
Basi maisha yakaendelea akapata kazi akaniambia; “Naomba unizalie maana mimi sina mtoto wenzangu wote niliocheza nao wana watoto” Sikusita ila nilimwambia kama unataka mtoto naomba akili yako itulie kuzaa so kazi, kazi ni kulea mtoto, basi akanitambulisha kwao familia nzima wakawa wananijua vizuri akaenda. Ukweli nilikaa wiki wiki mbili nikarudi maisha yakaenda nikapata mimba nilivyopata mimba alifurahi sana na akasema natamani mwanangu wa kwanza awe wa kike na kweli mungu akaitika dua yake nikazaa mtoto wa kike alifurah sana.
Maisha yakasonga, mimi nikamwambia tufunge ndoa yeye akawa ananijibu tutaoana subiri kwanza nataka siku ya harusi yangu mtaa mzima wajue na waishangae harusi hiyo.
Maisha yakasonga ila baadaye akafukuzwa kazi tukawa na maisha magumu bala mimi nikamwambia twende nikupeleke kwa mjomba wangu ukipata dawa mjomba ni mganga wa kienyeji kweli tukaenda kwa mjomba akamuangalia akampatia tiba akafanyiwa madawa pale nyingine akaambiwa akatumie nyumbani basi tukarudi akatumia madawa kuna siku akapiga simu kwamba kuna kazi huku ya mshahara mwinzo wa mwezi basi akaenda kufanya kazi, mwanzoni akipata mshahara tulikuwa tunanunua vitu vya ndani kwa sababu tulikuwa na kitanda tu bila godoro ila baadaye tukanunua vitu muhimu baadaye tukanunua hadi kiwanja.
Sasa nikawa namwambia tujenge maana hiyo kazi ya msimu, siku ukifukuzwa je? aaaaahh akaanza kubadilika akipokea mshahara nikimuuliza ananijibu hela naweka benki mara ooh usiniulize matumizi ya pesa, mmmhh akanza kubadilika mimi nikienda nyumbani kwetu au kwao yeye halali ndani anaendaga kulala kwa mwanamke wake huko, ukipiga simum usiku anapokea mwanamke, tena anamwambia huyo mwanamke wake eti mwanamke tu nimezaa naye natoa tu huduma kwa mtoto dah roho yangu iliniuma sana nikarudi nyumbani nikamuuliza kumbe nikiondoka unalala nje kumbe una mwanamke mwingine? anajibu ooh naendaga kujipoza tu..! yule mwanamke akawa anapig simu usiku na akipiga simu hapokei mimi napokea ile simu nasikia “niambie mume wangu” ukimuuliza anajibu simjui wakati huyo anamtaja mpaka jina mimi ikabidi niite familia tuongee, tuliongea kifamilia akakili kosa na akasema atajilekebisha.
Maisha yakasonga, kuna siku akaniaga anaenda kwa mjomba nikamwambia poa akaondoka ilivyofika jioni mjomba yangu akanipigia akaniuliza unajua kama mwenzio alikuwa huku nikamwambia ndiyo nikamuuliza ana mapya gani akaniambia amekuja hapa anasema kuna mtu anamsumbua na huyo mtu ni mwanamke wake yaan mda mwingi anapiga simu anataka hela na asipompa anakuwa mkali akitaka penzi mpaka atoe hela kwa hiyo ujio wake nimfanyie dawa asiwe mkali na asiombe pesa nikamuuliza; “Je mwanangu anajua kama unamchepuka akajibu hajui na usimwambie yeyote!” Akaambiwa na mjomba lete pesa ndo nifanye hiyo kazi siwezi kukufanyia bure maana hiyo ni starehe yako, jamani yaani nilivyoambiwa vile na mjomba wangu nililia sana hiyo siku nilijiuliza maswali mengi mengi nikamsimulia mama yangu akasema hapo hamna tena maisha akili kichwani kwako alivyorudi usiku sikuumuuliza chochote nikamuangalia tu nikalala zangu. Ilifika hatua mimi na yeye tunalala hanigusi hanipapasi na mim nikawa roho yangu ishaingia kutu namuangalia tu.
Miezi miwili tunalala tu kama mtu na kaka yake kuna siku karudi usiku na nguo nikamuuliza; “Nguo hizo umenunua wapi usiku huu?” akanijibu kuna teja kapitisha ndo nimenunua.
Basi asubuhi kaniaga anaenda kwa mjomba akaondoka mimi sasa nikampigia mjomba wangu nikamwambia mme wangu kaja na mapya gani? mjomba akaniambia kwamba hana mapya kaja yale yale ya mwanamke wake bado anamcharukia na pia kamnunulia nguo lakini anaogopa kuzivaa.
– Je zina usalama lakini?
Mjomba akamwambia hazina usalama kuna sehemu kazipeleka kazifanyia madawa ukivaa tu mjomba atakuendesha hata familia yako utaisahau.
Basi akaondoka zile zilikaa kama siku tatu hajavaa huyu mwanamke akawa anampigia simu mme wangu, hizo nguo ushavaa au? tena anakua mkali hatari basi kweli zile nguo alizivaa hanaga tabia ya kurudia nguo lakini zile nguo alivaa siku tatu mimi nikawa namuaangalia tu wakati huo yeye anadhani mimi sijui kitu kumbe mimi najua kila kitu ile hali ya dharau nikachoka kuvumilia siku hiyo akaingia kazini usiku huku nyuma mimi nikaita gari nikabeba vitu vyote nikaondoka, vitu nikapeleka kwa mamkubwa.
Asubuhi yake nikaondoka kwa mama yangu nikamtumia message baki na maisha yako najua kila kitu kuhusu wewe na mwanamke wako mi nikaondoka.
Alivyorudi asubuhi nasikia kaingia ndani kakaa wewe akaenda kuoga akaondoka wapangaji wenzangu walinisimulia maana yeye tokea niondoke hajawahi kunipigia simu wala kutuma message mtoto tu yupo na bibi yake.
Bibi yake akampigia simu mwanao yupo hapa kumbuka kumhudumia alishangaa tu heey kumbe wapo huko?
Kinachoniuma maisha niliyomkuta nayo nikampambania mpaka anafanikiwa alafu Leo ananidharau kiasi hiki, kingine mwanangu alikuwa ananipenda sana, baba yake huko na Bibi yake akiamka anasema mpigie baba yake niongee naye lakini akipigiwa simu hapokei na huduma katuma mara moja tu na kaitwa kwao na wazazi wake hataki kwenda, mpaka leo hii mnanishauri nini wananchi wenzangu namuonea huruma mwanangu..!