MWANAUME FANYA YAFUATAYO HAUTAKOSA MWANAMKE WA KUOA!
Ujumbe huu ni kwa mwanaume ambaye anataka kuoa lakini kila Mwanamke anayemhitaji hakubali kuolewa naye. Yafuatayo ni mambo ambayo mwanaume ukiyazingatia HAUTAKOSA MWANAMKE wa kuoa, inawezekana hautatafuta bali utatafutwa na kazi yako itakuwa kuchuja anayekufaa miongoni mwa kundi kubwa la wanawake wanaokuhitaji uwaoe. Yes, ndiyo hivyo.
Unafikiri kwanini zamani baadhi ya himaya za kifalme zilitangaza mabinti wa kike wanaotaka kuolewa na Mtoto wa kifalme wajitokeze katika siku fulani maalumu ili mtoto wa kifalme aweze kuchagua binti wa kuoa aliyemfaa? Unafikiri kwanini umati wa mabinti wengi sana walijitokeza ili waweze kuchaguliwa kuolewa na Mtoto wa kifalme?
Kijana wa kiume unayetafuta mchumba(binti) wa kuoa, hautatumia akili na nguvu nyingi sana kumpata mwanamke MAKINI wa kuoa iwapo utazingatia yafuatayo yaani utakimbiliwa kama mtoto wa kifalme uweze kuchagua umuoe nani!
1. Hakikisha Pesa inapita kwenye mikono yako. Tafuta pesa kwa nguvu zote uweze kuimiliki.
Mwanamke anamkimbilia mwanaume anayeweza kumtunza yeye,watoto ikiwezekana na kusaidia ndugu zake kama inawezekana. Pesa si kipaumbele namba moja kwenye mahusiano lakini ina nafasi yake katika familia. Hakikisha unaitafuta na kuipata,utajiongezea nafasi ya kupata mwanamke wa kuoa! Kama mwanaume pia, hakikisha unatoa mahari itakayokuheshimisha UKWENI na kukufungulia milango ya baraka katika ndoa yako. Hakuna mtoto wa kifalme masikini, kama unataka kukimbiliwa na kukubaliwa na mwanamke unayempenda awe mkeo basi kataa umasikini kwa nguvu zote.
2. Hakikisha ni mtu wa kujiamini,kujikubali na kujipenda.
Jipende kwa kuwa smart na kuvaa vizuri,jikubali jinsi ulivyo na jiamini. Kuwa mtu wa woga,hofu,wasiwasi na kutokujiamini kunaweza kukupotezea sifa ya kuwa baba mzuri na shupavu baadaye,hivyo basi mwanamke anaweza asivutiwe kuolewa na wewe. Watoto wa kifalme wengi wako vizuri kwenye eneo hili Kwasababu wanategemewa kuwa wafalme wa baadae, ndiyo maana hukimbiliwa na Wanawake wengi waweze kuwaoa.
3. Mwili wako uonyeshe ushupavu na uhodari.
Mwanamke akikutazama,amuone mwanaume kupitia sura na muonekano wako. Mwanamke akikuona(kukutazama) amuone mwanaume hodari ambaye anaweza kupambania familia yenu kutoka kwenye majanga au dhidi ya maadui kwasababu mwanamke anamchukulia mwanaume kama mlinzi na mtetezi wake. Mwanamke kamwe hawezi kukaa kwenye himaya ambayo anahisi hataweza kuwa salama. Watoto wa kifalme pia wa himaya za kale walikuwa vizuri kwenye eneo hili,wengi walikuwa shupavu na hodari katika Vita na mapambano.
Mwanaume, haupaswi kuwa legelege. Unafikiri kwanini wanaume wenye vifua na wafanya mazoezi wanawavutia wanawake wengi? Ni kwasababu wanaonekana hodari na shupavu. Hivyo ndivyo mwanaume anapaswa kuwa na muonekano wa KIUME. Hautakataliwa tena na mchumba unayetaka kumuoa.
4. Usimuache Mungu nyuma,bali awe kipaumbele chako namba moja!
Mwanamke anapenda ndoa yake iwe na furaha,upendo na amani. Iwapo mwanaume ukiwa mtu wa dini na kumuweka Mungu wako mbele, mwanamke atakukubali uwe mume wake kwasababu anaamini hautampiga wala kumnyanyasa,hautatelekeza familia yaani kiufupi familia yako itakuwa sehemu ya amani kwasababu unamuogopa Mungu wako!
Watoto wa kifalme pia,walikuwa karibu na imani zao.
5. Hakikisha unakuwa na sauti ya MAMLAKA.
Lakini, hii haiwezekani kama hauna pesa,haujiamini,haujipendi na haujikubali jinsi ulivyo. Sauti ya MAMLAKA ni sauti ambayo ukiongea unaweza kusikilizwa,hata watoto wa kifalme wa himaya za kale walikuwa vyema katika eneo hili. Kama unataka kuwa mwanaume wa kupendwa na mke wako, hakikisha unaonyesha sauti ya mamlaka mbele ya huyo unayemchumbia. Hapaswi kukuona kama mwanamke mwenzake!
Hakikisha una uwezo wa kusimama mbele za watu au kundi kubwa kujenga hoja na kuitetea. Kushindwa kuongea mbele yake na kuyasema ya moyoni mwako,hapo tayari umeshindwa hatua ya kwanza tu na kuonyesha udhaifu wako. ATAKUKIMBIA kwasababu utaonekana uko dhaifu! JIAMINI RAFIKI, UTAKUBALIWA TU NA HUYO MKE WAO MTARAJIWA!Nakutakia kila lenye kheri!