MUME WANGU ALIVYOGEUKA SHOGA
EP 21
“Mnatuhumiwa kuiba mtoto na huyo mtoto mpaka sasa hajapatikana na wanavyodai wewe Joan ndiye unajua alipo mtoto” alisema mumewe Vivian nikashangaa sana😳, jamani😭 sawa tu Mungu ndiye shahidi. Nilijibu huku nalia, “Ndio hivyo sasa na wanadai ushahidi wote upo kinachosubiriwa tu ni mfikishwe mahakamani” alisema mumewe Vivian na kumfanya hata Vivian ashindwe kuendelea kula. Akilini nikawaza jinsi binadamu wa kizazi hiki walivyokosa hofu ya Mungu hata ushahidi wa uongo unaweza kutengenezwa.
Basi baada kuonekana hatuendelei kula tulirudishwa locap ambapo huko Locap tulikuwa watatu tu mimi na Vivian na dada mmoja.Yule dada alijaribu kututia moyo kama ilivyo ada kwa watuhumiwa wanapokuwa Locap, basi bwana usiku ukaingia, tulilala kwa tabu huku mbu wakoniuma baalaa, asubuhi kukapambazuka. Majira ya Saa nne hivi tukatolewa locap na kupakizwa kwenye karandinga la polisi hao tukapelekwa kwenye mahakama ya wilaya tukiwa na pingu mkononi.
Tulipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka, pale mahakamani, ajabu alikuwepo mume wangu Brian tena alitajwa kuwa shahidi kwenye upande wa anayetushtaki, hapo nilikosa nguvu kabisa 😭 kwa kitendo cha kupewa kesi ya kuiba mtoto. ..
Kilichonisikitisha sasa baada ya Brian kupewa nafasi na muheshimiwa hakimu aongee anachokijua kuhusu mimi na Vivian ni hiki😳….
EP 22
Kilichonisikitisha sasa ni baada ya mume wangu Brian kupewa nafasi na muheshimiwa Hakimu aongee anachokijua kuhusu mimi na Vivian😭 “Muheshimiwa Hakimu nasimama mbele ya mahakama yako tukufu naye Mungu akiwa ni shahidi, huyu mke wangu siku moja alimleta mtoto na kumficha chumbani, nikamuuliza yule mtoto amemtoa wapi? akadai kuwa ni mtoto wa dada yake na Vivian, lakini ajabu ni kwamba kesho yake Vivian alikuja nyumbani kwangu akaondoka na mke wangu pamoja na yule mtoto, mke wangu akarudi usiku sana nilimgombeza lakini alijitetea kwa yule mtoto alikuwa anaumwa sana hivyo walimpeleka hospitali lakini kumbe yule mtoto walimuiba” Brian alitoa ushahidi huo wa uongo tena kwa kumtaja kabisa na Mungu😭 shahidi wa pili akaitwa naye akaongeza vile vile kama alivyongea Brian na kudai kuwa aliniona na mtoto😭
Upande wangu wa mashahidi walishindwa kunitetea kutokana na wao kuongea tofauti kila mmoja wao, hakimu alisoma kifungu cha sheria, mimi na Vivian tukahukumiwa kwenda jela miaka 30 endapo mtoto hatopatikana. Hivyo tulipelekwa kwanza mahabusu wakati uchunguzi dhidi ya mtoto ukiwa unaendelea,😭 ajabu ni kwamba tulipopelekwa mahabusu, tuliingizwa kwenye chumba kimoja ambacho mlangoni kiliandikwa Black room yani chumba cheusi,. Wakaingia maaskari jela wawili wa kike wenye sura za kigaidi , wakatuvia nguo zote. “Hapa ni black room ndani ya dakika mbili nataka mseme alipo mtoto hiyo ndio itakuwa pona pona yenu” alisema askari jela😭 hatukuwa na la kusema kwasababu tulikuwa hatujui chochote😭 tulipigwa sana ngumi za mbavu mpaka nikatapika damu,, baada ya hapo tukachapwa na mkia wa taa mpaka miili yetu ikavia damu lakini hatukuwa na la kusema😭
EP 23
“Nyie mnajifanya viburi eti? Sasa ngojeni” alisema Askari Jela kisha akachukua plaizi na kutubana vidole mpaka mkono wote ukafa ganzi, bado tulikuwa hatuna la kusema, basi tukarudishwa mahabusu baada ya kuonekana hatusemi lolote licha ya kupatiwa mateso makali. Tulikaa mahabusu siku 20, tukila ugali na maharage, siku ya 21 ndipo nikatembelewa na mama yangu mzazi, akaomba kuongea na mimi, nikatolewa kule mahabusu na kupelekwa kwenye chumba cha maongezi.
“Joan mwanangu pole sana kwa mateso uliyopitia, taarifa niliyoleta ni nzuri sana lakini pia inaweza kuwa mbaya sana kwako😭 ” alisema mama nikaogopa kidogo huku moyoni nikiwa na shauku ya kutaka kujua. “Mama ni taarifa gani hiyo?” Nilimuuliza.
Brian na Nicolas yule mzungu wametiwa mbaroni kwa kosa la kumlawiti 😳mtoto wako mpaka kuf…… Kabla mama hajamalizia kuongea nilidondoka chini na kupoteza fahamu.
JE NINI KILIENDELEA?
EP 24
“Mama ni taarifa gani hiyo?” Nilimuuliza mama. “Brian na Nicolaus yule mzungu wametiwa mbaroni kwa kosa la kumlawiti😳 mtoto wako mpaka kuf….. Kabla mama hajamalizia kuongea nilidondoka chini na kupoteza fahamu.
Nilipozinduka nilikuwa nimelala juu ya kitanda cha chuma ambacho godoro lake lilitandikwa mashuka meupe, harufu ya madawa ndio iliyonifanya nipate utambuzi kwamba pale nilipo ni hospital, kumbukumbu zikaanza kunijia taratibu na kuanza kukumbuka maneno aliyoniambia mama, tumbo la uchungu 😭 lilinishika japo nilikuwa sina mimba na yote ni kwasababu ya ile taarifa aliyoniletea mama inayowahusu Brian na Nicolaus kumlawiti mwanangu wa kiume😭 hadi kufa. Nililia kwa nguvu sana hadi nesi na mama wakaingia kunibembeleza.
“Najua inauma sana Joan, lakini huna budi kuvumilia maana ndio imeshatokea😔 tusubiri tu sheria ifuate mkondo wake.” Alisema mama huku akinibembeleza sana. Basi nilipotolewa pale hospital nilirudishwa mahabusu kwasababu bado uchunguzi wa kesi yetu mimi na Vivian ulikuwa unaendelea, mama naye alirudi nyumbani kumsitiri 😭 mwanangu kaburini kwenye makazi yake ya kudumu.
Sikufanikiwa kuhudhuria mazishi ya mwanangu 😔 niliomboleza nikiwa bado nipo kizuizini. Hatimaye ilikuwa ni siku ya Jumatano,.nilitolewa gerezani na kupelekwa mahakamani kuna ushahidi nilitlhitajika nikautoe kuhusu Brian na Nicolaus. Nilipofika mahakamani Brian na nikocolus walikuwa kizimbani, Brian alinitazama kwa aibu sana pale hakimu aliponisimamisha mbele ya mahakama kunihoji.
Nakumbuka hakimu alikuwa ni mwanamama wa makadirio ya miaka 49 hivi, alianza kunihoji “Joan Valentino, tunataka udhibitishe mbele ya mahakama tukufu kwamba mumeo ni shoga tangu aliporudi nchini akitokea Marekani, pili utudhibitishie kwamba mzungu Nicolaus wameoana na mumeo kitu ambacho ni kinyume cha maadili yetu sisi waafrika, tudhibitishie hilo✋” alisema Muheshimiwa hakimu.
“Muheshimiwa hakimu nitasema ukweli mbele ya mahakama yako hii tukufu na Mungu akiwa ni shahidi wangu. Ni kweli mume wangu tangu atoke Marekani uume wake hausimami na wala hajawahi kunipa haki yangu ya ndoa, kuna wakati nilimfumania na mzungu wakiwa chumbani wanafanya mapenzi ya jinsia moja, niliwaeleza wazazi wake wakadai watalifanyia hilo kazi ajabu baadae wakaniweka kikao na kunieleza kwamba wamemuoza Brian kwa mzungu” Nilieleza kila kitu mpaka tulivyoenda polisi lakini polisi wakatuzunguka mimi na Vivian, wakawachia Brian na Nicolaus huru, mimi na Vivian wakatupatia kesi ya wizi wa mtoto.
EP 25
Niliongea huku mahakama nzima ikibubujikwa na machozi pamoja na vilio😭 vya uchungu hasa pale Muheshimiwa hakimu alipogusia suala la mwanangu kulawitiwa mpaka kufa, Mzungu Nicolaus alibanwa kwa maswali na kukiri kwamba aliwalawiti wanangu wote pamoja na yule wa kike lakini yule kiume ndio akafa, hata hivyo mzungu Nicolaus hakuishia hapo alikiri kuwa alimuoa Brian kwa mahari kubwa sana na chanzo cha kuwalawiti watoto ni baada ya Brian kuanza kumnyima haki yake ya ndoa” Nicolaus aliongea bila aibu huku mahakama ikimkazia sana macho.
“Inamaana hata kesi ya Joan na Vivian kuiba mtoto ni kesi ya uongo?” Muheshimiwa hakimu alimuuliza Brian. “Ndio muheshimiwa ni kesi ambayo tuliwahonga polisi wawape Joan na Vivian kesi hiyo ambayo niliamini watafungwa mimi kusudi siri yangu na Nicolaus isibainike” Brian naye alikiri hilo mbele ya mahakama baada ya kubanwa sana kwa maswali..
Hakimu 😭 alitokwa na machozi kisha akasema “Kwa Mujibu wa sheria zetu za nchi, nitaenda kutoa hukumu ya kesi hii kama ifuatavyo…….😳
Alisema hakimu huyu mahakama yote ikiwa kimya kabisa kumsikiliza.
JE NINI KITAENDELEA?