MUME WANGU ALIVYOGEUKA SHOGA
EP 16
Mchungaji alifanya maombi kwa muda kidogo ili niweze kuongea lakini kila nilipojaribu kutoa sauti yangu, ajabu mtoto wangu wa miaka sita wa kiume alianza kuongea maneno ambayo yalikuwa kama muujiza wakati huo mchungaji akimrecord video mwanangu akiongea “Nitasema kila kitu, yule mzungu aliyetoka na baba Marekani ni mume wa baba, jamani baba ni shoga na yeye ndiye kampumbaza mama kwa kumuendea kwa mganga ili asiweze kusema lolote, kama sio Mungu huyu hata sisi tungelawitiwa” aliongea mtoto mchungaji akiwa anamrecord.
Hakika ulikuwa ni muujiza wa kuaminika kwasababu mtoto alikuwa hajui ushoga ni nini na wala ulawili ni nini, mchungaji alipomaliza kumrecord mtoto akasema atafunga siku tatu bila kunywa wala kula kwa ajili yangu nami nitaweza kuongea. Basi tulitoa Sadaka kidogo kisha tukaondoka kwenda nyumbani, rafiki yangu Vivian alinisaidia kazi mbali mbali kama kuwapikia chakula watoto, kunifulia na kazi ndogondogo za pale nyumbani,
Vivian hakutaka kutoa taarifa popote juu ya kile kinachoendelea bali tulisubiri polisi watuite kituoni. Kesho yake asubuhi nikiwa nyumbani kwangu pamoja na Vivian afande Boniface alifika pale nyumbani. Alianza kuongea na Vivian. “Dada tumefanya mazungumzo na watuhumiwa Brian na Nicolaus wamekataa katakata kwamba hawajachukua simu yako, sasa mkuu wa kituo amenituma nije nikague kama nitaiona maana kule tumewakagua kila sehemu lakini hatujaona nitajie nambari yako ya simu”
EP 17
Vivian alimtania afande Boni namba yake ya simu mara tu afande alipojaribu kupiga ile namba ikawa inaita, “Mbona inaita😳” alisema afande kwa mshangao. “Basi itakuwa humuhumu ndani endelea kupiga huku tukiendelea kuitafuta” Vivian alimwambia afande Boni tulizunguka nyumba nzima huku tukigawana maeneo ya kutafuta, mimi niliingia chumbani mara nikasikia simu ikiita uvunguni, haraka niliwaita Vivian na afande Boni Kibubu na kuwaonyesha kwa ishara kuwa simu ipo uvunguni, afande aliingia uvunguni na kuitoa.
“Hapa sasa ushahidi umekamilika ni dhahiri kwamba Brian na Nicolaus ni wahalifu dada simu yako tutakabidhiana kituoni mimi acha niende” alisema afande Boni. “Sawa afande lakini tumepata ushahidi mwingine” alisema Vivian kwa lengo la kutaka kumweleza afande Boni maneno ambayo mwanangu aliyaongea kwa mchungaji lakini kwakuwa afande alikuwa na haraka sana akasema ushahidi huo tutaenda nao kituoni kueleza hukohuko.
Basi bwana usiku majira ya saa mbili ajabu nilipojaribu kuongea mara sauti yangu ikaanza kutoka, hapo Vivian akamshukuru Mungu sana tena kwa maombi, nami nikamweleza Vivian kila kitu kuhusu Brian, kesho yake asubuhi sasa tukaongozana mimi na Vivian hadi kituoni kutoa ushahidi ili kama ni kufungwa Brian na Nicolaus wafungwe, ajabu sasa tulipofika kituoni😳..
EP 18
Tulipofika polisi tulisubirishwa nje kwanza kwa muda wa masaa mawili tukiwa tumekaa nje, mara nikashangaa kumuona Brian na Nicolaus wakitoka kwenye ofisi ya mkuu wa kituo huku nyuso zao zikiwa zimejaa tabasamu. “Mh😳 inamaana wameachiwa” Vivian aliniuliza. “Hata mimi nashangaa hebu tukamuone kwanza huyo mkuu wa kituo” Nilimwambia Vivian huku tukielekea kwenye ofisi ya mkuu wa kituo. “Haya na nyie mna shida gan?” mkuu wa kituo alihoji kwa kukomandi.
“Mkuu ninashindwa kuwaelewa ina maana hawa wahalifu ndio mmewaachia” Vivian alimuuliza mkuu wa kituo. “Dada usifundishe jeshi la polisi kazi!, Sisi kama polisi tumefanya uchunguzi na kubaini kuwa wewe ndiye ulienda kumfanyia vurugu Brian nyumbani kwake na ndio maana akakunyang’anya simu” alisema mkuu wa kituo machozi yakaanza kunitoka😭 kesi ikageuzwa kinaga ubaga mwenye makosa akaonekana ni Vivian.
“Jamani afande mbona hivyo lakini au kwakuwa sisi ni wanawake ndio maana mnatukandamiza😭 huyu dada ni rafiki yangu na yaliyomkuta ni makubwa alifanywa bubu na mumewe kwa uchawi ili asitoe siri kwamba mumewe ni shoga na ushahidi huu hapa” Vivian akampatia mkuu wa kituo ile memory iliyorekodiwa mwanangu akiongea, polisi akaanza kusikiliza huku akicheka😁 akabofya bofya simu yenye ile memory kumbe alikuwa anazifuta zile record kupoteza ushahidi kwani Vivian aliporudishiwa memory akaweka kwenye simu yangu ndogo na kuzitafuta tena ajabu hazokuwemo.
EP 19
“Sasa mkuu mbona uzifuta baba yangu😭” Vivian aliuliza huku akilia baada ya kuona uonevu unatendeka waziwazi, “Dada kwanza serikali haiamini kuhusu uchawi upo, pili una kesi ya kwenda kufanya vurugu kwenye nyumba ya watu hiyo ni kesi lakini nikikuangalia wewe bado mdogo usipende mambo ya kesi au mambo ya kufuatilia maisha ya watu chukua simu yako ufanye yako laa sivyo yatakayokukuta tusije kulaumiana” Polisi alimwambia Vivian kwa vitisho vingi sana.
“Lakini mkuu huu ni uonevu wazi wazi ila Mungu ndiye anayejua” Nilimwambia mkuu wa kituo huku nikiwa nalia😭 hatukuwa na ushahidi mwingine au kidhibiti tena hapo tukawa wapole, mara Brian akarudi pale kituoni. “Afande huyu mwanamke simtaki tena na kama anataka kushtak akashtaki talaka yake nitampatia mbele ya mahakama mie acha niondoke na wanangu” Brian alisema kisha akawachukua watoto na kuondoka nao😭 nililia kwa nguvu sana pale kituoni mpaka majirani wa karibu na kile kituo wakasogea kuona kulikoni.😳
Je ikawaje sasa?
EP 20
Nililia kwa nguvu sana pale kituoni mpaka majirani wa karibu na kile kituo wakasogea kuona kulikoni😳 ajabu polisi waliwatawanyisha kwa kuwatishia na mtutu wa bunduki, “Ondokeni na mtuachie sisi polisi tufanye kazi yetu” alisema afande Jimmy baada ya hapo afande Emelda akapewa amri atusweke locap mimi na Vivian,, kweli tulichukuliwa na kutupiwa Locap😭 huku simu yangu pomoja na kila kitu changu nikimkabidhi afande Emelda kwa maandishi.
Kule locap sikuwa na wazo lingine zaidi ya kuwaza usalama wa wanangu, nililia😭 sana. Basi majira ya saa 11 jioni mumewe Vivian ambaye tulipenda kumuita baba kubwa kutokana na umbo lake kubwa na unene wake alifika pale kituoni akiwa na chakula, tulitolewa mule locap na kupelekwa kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kula. 😭 ndugu nyie acheni tu hata hiyo hamu ya kula nilikosa japo kililetwa chakula ninachokipienda sana.
“Haya na nyie kulikoni maana nimepigiwa simu kwamba mpo locap, nikaona niwaletee chakula pamoja na maji pia nijue chanzo” aliuliza Mumewe Vivian naye Vivian alimueleza kila kitu bila kificho. “Mh sasa mbona mimi polisi walovyonieleza ni tofauti.” Alisema mumewe Vivian. “Wamekuambiaje” Vivian aliuliza.
INAENDELEA