MKE WA RAFIKI YANGU ANANITAKA ILI ALIPE KISASI KWA MUME WAKE
Ndugu zangu Moja Kwa Moja kwenye mada, nina mshikaji tumeshibana ki mtindo Japo mm nina mapungufu na yeye pia anayo ila tumechagua kusonga kama washikaji. Umri wetu ni 28+.
Mwamba alianza ku date na rafiki wamke wake ambaye ni jirani yake, kama mjuavyo mapenzi yalivo na nguvu ilikua ni ngumu kuyaficha, hatimaye yakafichuka mke (shemeji) akajua bahati mbaya mwamba kanogewa.
Harakati za mke wake kutaka kuwatenganisha zikagonga mwamba, jamma Kila nikimuasa aachane na bi mdogo abaki na mke jamaa anadai kumuacha mtu wake ni ngumu maana anapata mapenzi matamu zaidi ya Yale ya ndani, bi mdogo nae kiburi kimemjaa sometimes analeta dharau mpk kwa mke wa jamaa.
Kwakua mm na jamaa ni marafiki shemej akanichukia bila sababu akiamini kua mm nimechangua kumshauri mume wake amtongoze rafik ake kumbe sivyo.
Kuna siku walitibuana na mke wake mbele yangu shemej akanambia nawewe shemej nina kesi na wewe tena nina hasira na nyie wewe na rafiki yako , niliumia shemeji kunijumlisha kwa msela baadae shemej akanitafuta anataka kuujua ukweli nikamweleza kua mm sipo Wala sjamshauri mumeo, mala zote ushauri ninao mpa hua niwa kujenga familia yake sio kubomoa.
Nikamuahidi shemeji kua nitafanya mpango jamaa na Dem wake waachane Wala usijali shemejiii, kumbe mie nimemtania ili nitengenezee trust kwake, shemej kaiomba urafik fb nikakuta message zake za kutosha analalamika sana nikamtuliza wee tukichat sana.
Ajabu Kuna statement shemeji aliongea awali skuizingatia ila akairudia kama mala tatu, “natamani nitoke na rafiki WA karibu WA flani(mume wake) ili na yeye aone machungu ya kutoka na rafik angu.
Baada ya kuona shemeji anarudia statements hiyo Kwa sku karibu tatau nikabidi niingie kichwani Kwa shemeji nione mawazo yake yanacho kiwaza, nikamwambia basi shemeji nione Sasa mm kumbe nimechokonoa gogo lenye moto.
Kiufupi mpaka sasaiv shemej kabakiza siku ya kunipa mzigo nimle na mm ndo sipo serious mala niwe busy na hili mala na like nakuta sms za lawama tu kua nimemsusa.
Msimamo wangu ni kwamba hata iweje sitaruhusu kulala na shemej yangu Japo kua ikitokea shetani ndo wakulaumiwa.😂😂
Hili jambo limeniongezea uzoefu kuhusu wanawake ogopa sana mwanamke akiamia kulipiza kisasi