MAPITO YANGU
Mimi ni mama wa watoto wawili. Kabla sijampata mume wangu, nilikuwa nimeajiriwa kwenye kampuni moja hapa hapa Tanzania. Siku niliyopata kazi hiyo, wafanyakazi wengi walinishangaa sana walivyonitazama kana kwamba mimi ni kiumbe wa ajabu. Meneja akanita na kuniambia, โUnatakiwa ufanye kazi kwa bidii zote.โ Nikamjibu, โSawa kabisa.โ
Maisha yaliendeleaโฆ Baada ya wiki moja, nikiwa bize kazini, bosi akanita tena. Nilipoelekea ofisini kwake, nikaona wafanyakazi wananiangalia kwa jicho la ajabu. Kweli Mungu hakuninyima uzuri. Nina sura ya kupendeza, rangi yangu ni ya kati โ sio mweupe wala mweusi, na umbo langu limeumbika vyema. Kwa kifupi, nimejaaliwa.
Nilipofika kwa bosi, akanitisha namba ya simu akidai kuwa anahitaji namba za wafanyakazi wote. Bila kusita nikampa. Baada ya muda, nilianza kupokea meseji isiyo ya kawaida kutoka kwake. Iliandika:
โUsha kula mama watoto.โ
Nikaguna na kuuliza, โWewe ni nani?โ Akajibu:
โMimi ni boss wako. Kiukweli, nimekupenda sana. Nataka uwe mke wangu wa pili. Niko tayari kukupangishia chumba tuanze maisha.โ
Sikumjibu kabisa. Lakini kilichonishangaza ni jinsi alivyokuwa anatuma nauli kila siku kupitia kijana wake wa ofisini, wakati sijamuomba chochote.
Siku moja, nikiwa kantini nakula, mfanyakazi mwenzangu alinijia na kunicheka:
โHahaha, eti unataka kuolewa na boss! Tutaona kama utaolewa!โ
Baada ya miezi minne, hata kabla sijapangiwa hicho chumba alichosema, nilipatwa na homa kali. Ghafla, viungo vyangu vikaanza kupooza . Macho yakapoteza kuona, masikio yakashindwa kusikia, miguu na mikono vikawa havina nguvu. Niliumia mno.
Boss na wenzake walikaa kikao na kunishauri niache kazi kwanza ili nitafute tiba. Kwa uchungu mkubwa, nikarudi nyumbani.
Nikaanza matibabu huku nikizurura kwa waganga, mashehe, na wachungaji yote kwa kutafuta afya yangu.
Miaka ikaendelea bila mafanikio. Nilianza kukata tamaa . Siku moja, nikiwa kitandani, nikaona mama yangu akiingia na sauti ya huzuni. Alikuwa ameambatana na mtu mwingine. Nilimsikia akisema:
โKaribu sana mwanangu, mwenzio ndo huyu. Hata sijui niingie vipi ili apone.โ
Mgeni akasema:
โDada unaendeleaje?โ
Nikajibu:
โSijambo, ila wewe ni nani maana sikuoni?โ
Akaniambia:
โUsijali dada, mimi ni yule bodaboda aliyekupeleka hospitali jana.โ
Mazungumzo yakaanza, tukazoeana kwa sauti. Sikumwona kamwe, lakini alivyoendelea kunijali, moyo wangu ulianza kufarijika. Akawa kila siku anakuja kuniona, akinifanyia kila kitu kutoka kuniogesha hadi kunioshea vyombo. Alikuwa akinibeba hadi chooni na kuniosha kwa mikono yake mwenyewe . Hapo ndipo nilijua maana ya upendo wa kweli.
Tulizoeana, tukapendana. Alinichumbia rasmi na akanitambulisha kwao. Kwa mshangao wangu, wazazi wake walinipokea kwa mapenzi makubwa .
Baba yake alitafuta mtu aliyenisaidia kupata tiba ya macho yangu. Siku moja, nilianza kuona tena! Nilifurahi mno .
Baada ya miezi kadhaa, nikapata ujauzito. Licha ya hali yangu, mchumba wangu alinilea vizuri. Alikuwa akinipaka losheni na kuniweka marashi, nipendeze tu kama wengine .
Nilijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya kawaida. Furaha ilikuwa tele kwa kila mtu .
Mtoto alipofikisha miaka miwili, na mimi nikiwa natembea kwa magongo, mchumba wangu aliniacha . Bila ugomvi wala ishara, akaenda kuoa mwanamke mwingine. Niliumia sana
.
Nikabaki na sala. Kila siku nikiomba:
โMungu wangu, kama huyu alikuwa wa maisha yangu, nirudishie.โ
Na kweli, baada ya miezi kumi, ndoa yake ilivunjika na akarudi kwangu mwenyewe. Sikusita kumsamehe maana yeye ndio moyo wangu .
Baada ya miaka saba ya kupita na changamoto nyingi, tuliendelea kupendana. Mwaka jana tukafunga ndoa rasmi , na tukajaliwa kupata mtoto wetu wa pili.
Kwa sasa hali yangu si mbaya kama zamani. Naweza kufanya kazi za nyumbani, mume wangu ananisaidia sana. Mapenzi yetu yamedumu miaka 10 sasa, licha ya migogoro ya kawaida. Kiukweli, nampenda sana na yeye pia ananipenda. Hana tabia ya kuchepuka, na kama anazo basi sijawahi kugundua maana simu yake haina siri kwangu.
Ananiheshimu, ananitii, na ninajua:
MAPENZI YA KWELI YAPO.
USHAURI KWA WENZANGU
Ukiona mkeo au mumeo hamwelewani, msikimbilie talaka. Mwombe Mungu kwa dhati.
Mpende mumeo. Mjali. Mdekeze. Mheshimu. Naamini kwa kufanya hivyo, atabadilika kuwa bora zaidi .
Asanteni sana kwa kunisoma. Naomba ujumbe huu uwafikie wengi wapate somo.