LILITH – MKE WA KWANZA WA ADAMU
Nakuletea Somo hili kwa Kutoa Ushahidi Wa kutosha Ndani Ya BIBLIA TAKATIFU, Maana Kuna Watu Wanapinga na watapinga Sana Elimu hii.
Sasa Nitakwenda Nao Sambamba Kwa Ushahidi Wa Ki-BIBLIA.
. LILITH NI NANI?
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.
Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.
Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?
Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono… Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.
Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.
Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.
Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwa wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.
Ibada za kutoa kafara katika satanism
Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.
Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.
Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.
Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.
Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.
Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?
Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!
Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.
Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.
Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.
Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.
Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!
MAMBO MAKUBWA AMBAYO YAMEFICHWA KWENYE VITABU VYA DINI
HAYA NI MAMBO AMBAYO HAYATAJWI WAZIWAZI WALA KUFUNDISHWA MAKANISANI HATA KWENYE MISAAFU (BIBLIA)HAYAJATAJWA.
Nakufungulia mambo usiyoyajua
Inawezekana zipo sababu za msingi za kuuficha ukweli huu na tunaweza kusema huu ndio ukweli pekee uliofichwa kwenye mafundisho yetu mbalimbali kuhusu mwanzo wa mwanadamu. Inawezekana wengi hatujui ukweli kuhusu mwanadamu wa kwanza au wanadamu wa kwanza kuumbwa. Na kwa sababu tu wengi wetu hatupendi kusoma ama kujisomea tumebaki kupokea kile tu tunachofundishwa na viongozi wetu huko makanisani na hatujipi muda wa kufanya utafiti kidogo kujua mambo makubwa yanayohusu uumbaji na binadamu wa kwanza kuumbwa. Siwezi kumlaumu mtu kwa kuwa hii ndio hulka yetu ya kutopenda kujifunza. Nipo kwa ajili ya kukufungulia mambo usiyoyajua.
Ni nani mwanadamu wa kwanza
Katika kujadili swali hii nitatumia zaidi kitabu cha Biblia kwa kuwa kinaeleza vyema kuhusu umbaji wa mwanzo kabisa, pamoja na vitabu vya kale vinavyoelezea masuala ya umbaji na binadamu wa kale (Old Testament of Medieval ages, The Atheist books, Tree of Souls, An Anthology of Midrashic and Oral Narratives)vitabu vyote hivi nimevitafsiri kwa kiswahili kwa ajili ya kuelimisha juu ya mambo haya ninayokwenda kueleza.
Kwa haraka haraka watu wengi wakiulizwa juu ya swali hili hutoa majibu ya haraka kuwa Mwanadamu wa kwanza ni Adam na mkewe Eva/Hawa walioumbwa na Mungu na kwamba Adam aliumbwa kutokana na mavumbi na Eva/aliumbwa kutokana na sehemu ya nyama ya ubavu wa kushoto wa mumewe Adamu. Haya majibu ndiyo yanayofundishwa huko kwenye masinagogi na kwenye mikusanyiko ya neno la Mungu au huko kunakohubiriwa neno la Mungu. Na sisi hapo ndipo tunapoishia na hatuendelei mbele kutaka kujua zaidi ama kujifunza.
Ngoja nikusogeze kwenye kitabu kitakatifu (Biblia). Ukweli uliofichwa ni kwamba BWANA Mungu aliumba wanadamu wa kwanza kwa siku moja na aliwaumba kwa jinsia mbili tofauti yaani mwanamume na mwanamke. Vitabu vya zamani vyote nilivyovitaja hapo juu vimeeleza ukweli huu.
Twende taratibu, twende na vifungu kwanza vya Biblia.
Mwanzo 1:26 *”Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki na baharini, na ndege wa angani, na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”* hapa BWANA Mungu alikuwa anaongea na malaika wake.
Mwanzo 1: 27 *”Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu aliwaumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba* hapa tunaona dhahiri kabisa Mungu akiwaumba Mwanamme na Mwanamke wote kwa pamoja kwa siku moja na umbaji huu ulifanyika siku ya sita soma Mwanzo 1:31
Tunaona baada ya umbaji huu BWANA Mungu anatoa maagizo kwa watu hawa wawili (maanake tayari wana akili na uhai ndio maana Mungu anatoa maagizo kwao)order of command ilianzia hapa. BWANA Mungu anasema zaeni, mkaongezeke, mkajaze nchi, na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,…Mwanzo 1:28.
Mwanzo 2:2 *”Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya, akastarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya”* hapa ndipo tunapata ile sentensi ya kufanya kazi na kupumzika siku ya saba ilitokana na hili la BWANA Mungu kumaliza kazi yake yote ya umbaji na viumbe wa mwisho walikuwa wanadamu.
Mwanzo 2:4 *”Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa, siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi”* kwahiyo tunaona kazi ya umbaji iliishia hapa. Kwahiyo shughuli nzima ya umbaji iliishia hapa kwenye Mwanzo 2:4. Yaani naamanisha kuwa umbaji wa wanadamu wawili tayari ulikuwa umeshafanyika yaani mwanadamu Mwanamume na mwanadamu mwanamke.
Tuendelee kujifunza…
Mwanamume aliyeumbwa jina lake aliitwa Adamu na mwanamke aliyeumbwa jina lake aliitwa Lilith (hapa kuna utata wa jina la mwanamke wa kwanza. Wanathiolojia wa zamani wanataja jina la Lilith kuwa ndiye mwanamke aliyeumbwa na Adamu siku moja wote kutoka mavumbini lakini wapo ambao wanadai kuwa hawamtambui jina hivyo waliamua kumuita Eva/Hawa wa kwanza…the first Eve.
Naomba nikueleze kidogo kuhusu huyu Mwanamke wa Kwanza ama mke wa kwanza wa Adamu aliyeitwa Lilith.
Ni kweli kwamba mke wa kwanza wa Adamu aliitwa Lilith na ndiye aliyeumbwa pamoja na Adam toka kwenye mavumbi katika ile siku ya sita ya umbaji. Nimekuonesha Mwanzo 1:26-27 na mwisho wa umbaji Mwanzo 2:4. Mafundisho mengi hayasemi ukweli huu lakini mwishoni mwa makala hii nitakueleza ni kwanini ukweli huu hausemwi hadharani ama kwanini haufundishwi kwenye masinagogi.
Adam na Lilith waliumbwa siku moja na wote waliumbwa toka mavumbini. Vitabu vya zamani vinaeleza kuwa Lilith alikuwa mwenye akili nyingi, uwezo mkubwa na mwenye kiburi . Hakutaka kupelekeshwa na Mumewe Adamu. Lilith alitaka haki sawa na wala hakutaka kuonewa. Mambo mengi alitaka haki. Waandishi wanaeleza kuwa mwanamke huyu ni tunu na alama ya kudai haki za wanawake Duniani akiwa kama mwanamke wa kwanza . Unaambiwa Lilith alikuwa anataka kila kitu waende sawa na mume wake Adam. Tabia ya Lilith kudai dai haki haikumfurahisha mumewe Adamu na ndipo Adam alipoamua kumsema kwa BWANA Mungu kuwa mwanamke hamheshimu wala kumsikiliza. Utemi wa Adam ndio uliomfukuza Lilith kwenye Bustani ya Edeni na historia inaeleza kuwa baada ya Lilith kuondoka bustanini alienda kwenye miamba alikokuwa anakaa Shetani Mkuu (Lucifer kwa lugha ya kileo) watafiti wa mambo ya kale wanaeleza kuwa baadae Lilith aliolewa na Lucifer (Samael). Habari za usaliti wa mwanamke ulianzia hapa. Historia inaeleza kuwa mwanamke ndiye aliyekuwa mtu kwanza kumsaliti mwanaume.
Mungu aliwatuma malaika wake 3 kwenda kumfata Lilith na endapo atagoma kurudi kwa mume wake basi BWANA Mungu angempiga mapigo mazito yaani kuua watoto wake 100 kwa kila siku. Vitabu vya kale vinaeleza kuwa Lilith baada ya kuachana na Adam alikuwa na uwezo wa kuzaa watoto 100 kwa siku moja. Hapa kuna mambo ya demon (majini) baada ya kuachana na Adam.
Hivyo basi baada ya malaika wale kumfata Lilith kuwa arudi kwa mume wake, Lilith alikataa kabisa na kusema hawezi kurudi kwa Adam kwa kuwa Adam anao utemi ambao yeye hayuko tayari kuvumilia. Hii pia ndio sumu inayoendelea kuwatafuna wanawake ambao si wavumilivu kwenye ndoa zao .
Adam aliendelea kuishi maisha ya upweke bila mwanamke na alitoa ombi kwa BWANA Mungu kumuomba amtengeneze mtu wa kufanana naye kwa kuwa aliona dhahiri kabisa kuwa Lilith hakuwa mwanamke wa kufanana naye. Baada ya ombi hilo kuombwa kwa Mungu nini kilitokea?
Ngoja nikusogeze kwenye maandiko.
Mwanzo 2:21 *”BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pale,;*
Mwanzo 2:22 *”na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya, mwanamke, akamleta kwa Adamu”*
Mwanzo 2:23 *”Adamu akasema sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanaume”*
Twende wote kwa pamoja. Nataka nikupitishe taratibu kwenye mstari huo wa tatu Mwanzo 2:23. Hapa tunaona sasa Adamu anapata furaha na kukiri kuwa sasa huyu ni mfupa katika mifupa yake (hapa inamaanisha Adamu anamtaja mwanamke wa pili kwa maneno *sasa huyu* akimanisha alikuwepo mwingine kabla ya huyu. Na maneno ametwaliwa katika mifupa na nyama yake hapa anamanisha mwanamke huyu wa pili atamtii na kumheshimu zaidi kwa kuwa ametokana na yeye lakini yule wa kwanza hakutokana na yeye wala hakutoka kwenye mwili wake bali alitoka kwenye mavumbi hivyo ilikuwa ngumu sana kumheshimu.
Inasemekana kuwa baada ya umbaji huu wa pili (yaani mke wa pili wa Adam), maisha yalikuwa mazuri sana hapo kwenye Bustani ya Edeni kwa kuwa Adam aliishi kwa raha. Kumbe yule mwanamke wa kwanza Lilith alipata wivu (ile kauli ya wanawake hawapendani huu ndio msingi wake. Haya mambo hayakuanza leo)na kumbuka tayari alikuwa ameshafukuzwa Edeni na ameshakuwa Demon (Shetani/jini)alirudi kwa sura ya nyoka na kumdanganya Eva/Hawa kula matunda ya mti wa kati mti wa mema na mabaya (Mwanzo 3:1-19) ambayo Bwana Mungu aliwakataza kula. Baada ya kula kila mtu anajua kilichotokea. BWANA Mungu alitoa adhabu kwao.
Adam ndipo sasa alipomuita mkewe jina la Hawa/Eve kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai (Mwanzo 3:20)
Yapo mengi sana yaliyoandikwa juu ya mwanamke wa kwanza. Nafikiri kwa maelezo hayo kwa kifupi utagundua kuwa umbaji ulifanyika mara mbili kuna ule wa siku ya sita yaani Mwanzo 1:26-27 na huu baada ya Adam kuomba uliofanyika Mwanzo 2:21-23. Waandishi wa zamani wa mambo ya umbaji wa kale akina (John Mark, Atheist, H. Schwartz’s) wanaeleza kuwa ombi la Adamu lilijibiwa baada ya miaka 100 yaani Eva aliumbwa baada ya miaka 100 tangu Lilith kuondoka. (Mungu hujibu maombi hata kama ni kwa kuchelewa)
Let me put a little bit in English whoever who don’t understand swahili may catch a meaning in the following manuscript.
Kwanini ukweli huu ulifichwa?
Kwa kusoma kitabu cha Biblia unaweza usione jina la Lilith lakini watafiti wa maandiko matakatifu ya kale wameeleza kuwa jina hilo liliwahi kuandikwa kwenye kitabu cha Isaya 34:14 (Old Testament of Medieval ages) lakini kwa machapisho ya hivi karibuni kuanzia karne ya 15 jina hilo liliondolewa na kwa sasa huwezi kulipata.
Inawezekana stori hii haifundishwi kwa kuwa si nzuri kwa sababu ina usaliti ndani yake, kiburi na ujuaji wa Lilith na hatimaye mke wa pili ambapo inaaminika kuwa mke ni mmoja wa maisha yaani kufa na kupona. Lakini baadae kwenye Agano jipya tumejifunza Yesu aliruhusu talaka kwenye habari za uwasherati na ukahaba (Mathayo 5:29). Lakini hata kama ukweli huu umefichwa bado hatuzuiliwi kuutafuta .
AKHSANTENI.