JINSI YA KUEPUKA KUPIGANA NGUMI NA MKE AU MUME WAKO KWENYE NDOA YENU!
1. Sikiliza ili uelewe, sio ili ujibu.
Wakati mke au mume wako akiwa anazungumza msikilize kwa makini umuelewe na utafakari anachokimaanisha. Lakini, ukimsikiliza ili tu uweze kujibu basi utajikuta unaropoka au kuongea maneno ya kumkwaza kwasababu haujachuja faida na hasara ya kile unachotaka kuongea,mtagombana tu!
2. Ongea kwa upole na utaratibu,hata kama umekwazika.
Hata kama umekasirika, ongea kwa sauti ya chini na ya upole. Jikaze na zuia hasira zako, bila kufanya hivyo. Mtagombana tu!
3. Usibishane ili ushinde.
Kamwe usipende kubishana na mke au mume wako ili uibuke mshindi (Bingwa katika mabishano yenu). Mkiwa mnabishana na mke au mume wako basi kubali kushindwa, sio vibaya kumuacha mwenzako ashinde. Ukifanya hivyo, kamwe hamtagombana!
4.Omba msamaha kwa kumaanisha unapokosea.
Ukikosea, omba msamaha kwa kumaanisha kutoka moyoni. Usiombe msamaha ili uweze kupata nafasi ya kumkomoa mwenzako au kutenda kosa kubwa zaidi. Lakini pia, kamwe usirudie kosa ambalo umeshawahi kulifanya ukaomba msamaha na kusamehewa, ukifanya hivi, hamtagombana kamwe!
5. Toa nafasi(punguza ukaribu) kama kuna ulazima.
Wakati mwingine ukaribu kupitiliza na mke au mume wako unaweza kusababisha mgombane( Yaani kuwa pamoja kila wakati, kushinda naye asubuhi mpaka jioni, kwenda naye kila sehemu na kadhalika). Kuna wakati unapaswa kumpatia nafasi mke au mume wako ya kwenda kwenye shughuli zake au kutembea anakojua yeye. Hii ya kutokuwa naye kwa dakika, masaa au siku kadhaa itamfanya akumisi na kuona umuhimu wako kwenye maisha yake. Lakini, kuwa naye muda wote masaa 24, kuwa naye kila siku za wiki,mwezi, January mpaka December mko wote tu! LAZIMA MGOMBANE.
6. Unapozungumza zingatia neno “MIMI” na sio lawama kwa mwenzako.
Wakati wa kuzungumza tambua kuwa hata wewe sio mkamilifu unaweza kukosea. Kwahiyo, wakati unazungumza na mwenzako epuka kujitenga na makosa na kutupa lawama kwa mwenzako. Tumia neno MIMI badala ya WEWE katika mazungumzo yenu ukimaanisha kuwa sio makosa yote yanafanywa na mke au mume wako. Hamtagombana kamwe!
7. Heshimu kutofautiana katika maamuzi.
Tambua kuwa Kuna wakati mnaweza kutofautiana katika maamuzi , mawazo na misimamo yenu. Kwahiyo, epuka kumlazimisha mwenzako kufuata kile unachokiamini wewe wakati wote. Mtagombana tu!
8. Jikite katika “kusuluhisha matatizo” na sio kuyapa kipaumbele matatizo uliyonayo.
Mnappokosana na mwenzako au kutofautiana na mwenzi wako, jikite katika kusuluhisha tofauti zenu na sio kuyakatia tamaa mahusiano yenu. Utafiti unaonyesha kuwa wanandoa ambao wakigombana wako tayari kutengana au kuachana kwa uharaka pasipo kuwekeza jitihada za kusuluhisha tofauti zao,hawakupendana kwa dhati bali walioana kwa tamaa ya ngono,mali,vyeo au sababu nyingine yeyote na sio MAPENZI YA KWELI.
9. Mapenzi yako ya kweli yawe juu kuliko hisia zako.
Weka kipaumbele mapenzi yako ya kweli kwa huyo uliyenaye na sio hisia zako. Tambua kuwa hata mkiachana unaweza kupata mwenye kasoro kuliko huyo uliyenaye kwasababu hakuna binadamu mkamilifu. Ukifanya hivyo, kamwe hamtakwaruzana na kutupiana ngumi!