ISHARA SABA ZINAZOKUDHIBITISHIA MKE AU MUME WAKO ANAKUSALITI!
1. Akipigiwa simu mkiwa pamoja naye hapokei na akipokea anaenda kuongelea mbali na wewe inaweza kuwa bafuni,chooni au chumbani kwenu ilimradi tu usisikie mazungumzo yao!
2. Hapendi uguse simu yake au kupokea simu yake akiwa mbali na simu. Ukipokea simu yake bila ruhusa yake, anakuwa mkorofi mwenye hasira kama simba mwenye njaa kali!
3. Hajiamini na wakati mwingine ataanza kukukwepa ndani ya nyumba. Mnapotazamana uso kwa uso atakuonea aibu na pasipo shaka atatazama chini au kuangalia pembeni!
4. Ataanza kukudanganya kwa kutumia sababu zisizo na maana yeyote ili aweze kuruhusiwa kutoka nyumbani usiku na wakati mwingine anaweza kutoka bila taarifa, ataanza kuchelewa kurudi nyumbani bila taarifa au mchana anaweza kuondoka kusikojulikana bila taarifa. Unaweza fikiri yuko kazini kumbe hayupo! Unaweza fikiri umemuacha nyumbani kumbe hayupo! ATABADILIKA HARAKA TOFAUTI NA ULIVYOMZOEA.
5. Simu yake ina pasiwedi au nywila kila mahali!
6. Akirudi nyumbani anakimbilia bafuni kuoga pasipo kukuosogelea au kuruhusu mazungumzo yeyote na wewe ya ukaribu ili usihisi harufu yake mpya ambayo haujaizoea.
7. Ana tabia ya kuficha simu yake akiwa ameenda chooni au bafuni kuoga wakati mwingine anaenda nayo kabisa!
Rafiki, ukiona ishara hizi kama una roho ya paka fuatilia ujue ukweli kuhusu usalama wa NDOA yako. Kama hauna kifua na una roho nyepesi, kaa kimya na usimfuatilie milele.
Je, wewe una roho ya paka ya kufuatilia kujua ukweli ili umshuhudie mke au mume mwenzako au unakaa kimya milele watajijua wenyewe?