Binti Yangu Wa Kambo Alichonifanyia
Nimekuwa nikimlea binti wa mke wangu (binti wa kambo) kwa miaka 15 sasa, nilimsaidia kwenye masomo yake mpaka akahitimu, na nilimnunulia gari alipohitimu, nimekuwa upande wake kila hatua ya maisha yake.
Jumamosi ijayo anafunga ndoa, ana miaka 27. Tumepanga harusi hii kwa muda mrefu, jamaa yake ana uwezo lakini bado nilitoa pesa kuhakikisha sherehe itakuwa ya heshima.
Alikuja nyumbani kumtambulisha huyo mwanaume, lakini mama yake akasema kwa kuwa mimi si baba wa kumzaa, mahari itachukuliwa na upande wa familia ya baba yake wa kumzaa, eti kwamba ndio mila zao zinataka, nikasema sawa.
Sasa nimegundua kuwa ni kweli walienda kutoa mahari kwa familia ya baba wa kumzaa huyu binti wa mke wangu, na kama hiyo haitoshi, binti yangu huyo alikuja kuniambia kuwa hataki mimi nisimame kumpeleka kwa mume wake siku ya harusi, kwamba mama yake amesema baba wa kumzaa ndiye anayefaa kufanya hivyo.
Akaongeza kuwa anadhani hiyo ndiyo njia sahihi, na kwamba itafanya familia ya mume wake waone tumewaheshimu.
Najua binti kila alichosema alifundishwa na mama yake, Binti niliyemlea ni mwerevu sana, hawezi kufikiria hivyo mwenyewe, mama yake ndiye aliyemchochea kuongea yote hayo.
Binti niliyemlea na kumlipia shule kwa sababu baba yake wa kumzaa hakuweza, kama baba yake alikuwa anampenda kwanini hakumuhudumia?Nilipokutana na mama yake hakuwa na kitu, alitelekezwa na huyo wanaetaka kumpa heshima eti kisa tu baba wa kumzaa, mimi nilimpenda na kuwakaribisha nyumbani kwangu na mwanae. Nikawapa maisha mazuri tena ya heshima na leo hii anaendesha gari la kifahari, binti yake anamiliki gari lake na anafanya kazi kwenye shirika kubwa kwa sababu nilimpambania apate kazi.
Nilifanya haya yote kwa upendo, nilimpenda huyu binti kama mtoto wangu wa kumzaa, sijawahi hata siku moja kumchukulia kama si wangu.
Sasa imefika wakati wa ndoa yake, na mama yake anasafiri hadi kumsaka baba wa kumzaa ili aje ampeleke binti yake kwa mume? Kwa nini? Ili aje kushuhudia mafanikio yao waliopata kwa pesa zangu? Hii imenishangaza sana na imeniumiza.
Unaweza kuamini kwamba nilimpigia simu binti yetu huyu leo asubuhi kuzungumza naye kuhusu hili, na akaniambia kuwa “Baba hiyo ndiyo njia sahihi, kila mtoto ana baba yake wa kumzaa, hivyo siwezi kumtenga, lakini haimaanishi kuwa sikupendi baba, mimi nakupenda wewe kuliko yeye na sina moyo wowote kwake, na hata mali zangu una asilimia kubwa ya kuzitumia wewe na si yeye, ila tu nielewe baba, sometimes ni mambo ya kimila”
Imagine binti niliyemlea mwenyewe tangu akiwa mdogo ananiambia hivyo! Hii ndiyo shukurani yao kwa yote niliyowafanyia kwa moyo wa upendo..? Nimewaambia kama ni hivyo sintahudhuria harusi, na baada ya ndoa, mama yake ataondoka nyumbani kwangu aende kwa baba mzazi wa mtoto wake,
Kama ni kuwapa nimewapa vya kutosha, kwanza hana hata mtoto wangu mmoja, inaonekana alikuja tu kupunguza shida zake sasa amekuwa vizuri ananidharau.
Pia nashukuru alinisaidia kulea watoto wangu wawili niliowapata na marehemu mke wangu.
Binti yangu wa kumzaa naye yuko karibu kufikia hatua hiyo, ana miaka 22 na anasoma nje ya nchi. Nitapata fursa ya kumsindikiza kwa mumewe akiolewa kwahiyo wala hawajanikomoa.
Kama kuna funzo nimejifunza nikiwa na miaka 51, ni hili, ‘kuwa makini sana na mwanamke ambaye tayari ana mtoto, inaonekana hawawezi kusahau wanaume waliowaacha.
Wanawake kama hawa asilimia kubwa ni matahira wajinga yasiyo jitambua hata kidogo, how come mwanaume anakuzalisha then anaku-dump hakuoi, hakupi heshima, hakutunzi hakuhudumii halafu eti unamkumbuka na kumrudia?! Mtapoteza wanaume wanaowapenda na kuwajali kwasababu ya utahira wenu huo.
Nilipokutana na huyu mwanamke hakuwa na chochote, mtoto wake alikuwa mkubwa kuliko wangu, lakini sikujali, nilimwona kuwa mtu ambaye angeweza kuwapenda watoto wangu kama wake.
Lakini hata hivyo, mara nyingi niliona hana upendo wa dhati kwa wanangu, yeye ndiye sababu iliyonifanya nisiruhusu watoto wangu wasome hapa nchini, nilitaka waende nje kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya mwanamke huyu .
Sasa amenithibitishia kwamba hakuwahi kunipenda kweli alikuwa anahitaji tu maisha mazuri.