WIFE MATERIAL 06
Niliingia Hadi ndani ndipo nikamkuta yule binti yupo na mama bado wanapiga story,walingea pale walipomaiza Alisha akaondoka,iyo siku nikawa nimemkosa…ila nilishaweka mipango sawa ya kuweza kumnasa.
Siku zilikua zinaenda kila nikitaka kumuona private inashindikana nikasema likizo inakaribia kuisha na sijaweza kufanikiwa kuonana nae hata kufunguka hisia zangu kwake,ili ninapoenda kwangu niwe na jibu moja.
Ilikua siku ya ijumaa Kama kawaida yule binti alikuja pale nyumbani nilimpokea nikamkaribisha kwa ukarimu nilikua nje na mama alikua amepumzika ndani.alinisalimia akakunja na goti.upendo unazid ninaopoona zile heshima na upole wake.
Alianza kutaka kuingia ndani nikamwambia samahani kabla ujaingia ndani naomba tuongee akasema sawa nakusikiliza Fred!!! Fred???umelijuaje jina langu????nalijua tu sababu mama ako wanamuita mama Fred na watoto wake wote nawajaua isipokua wewe kwaio mawazo yangu wewe ndiye frenk.
Nikamwambia sawa tusipoteze muda sana,una simu?ndio nnayo.ok nipatie namba zako….mtoto hakusita wala kupinga alitoa namba za simu haraka Sana.
Nikamwambia usimwambie mtu yoyote Kama nnayo mawasiliano yako akasema sawa.aliingia ndani akampa mama maagizo ya kanisani akaondoka.
Sikumtafuta Hadi ilipofika usiku,niliingia chumbani kwangu nikachukua simu nikampigia…aikuchukua muda akawa amepokea ,tulisalimiana nikamuuliza samahani unaitwa Nani mpendwa,akasema Mimi naitwa sechelela,.
Nikamwambia seche jina zuri Sana Kama ww ulivyo.akasema Asante Fred,nikamwambia lini utakua na muda nataka tuonane tuongee,akasema muda wowote tuu mie nipo free kwanzia asubuhi Hadi jioni,ukipanga kuonana nitasitisha kwenda kwenye maombi na kwaya kanisani.
Nikamwambia vizuri naomba kesho tuweze kuonana,akaniuliza ni wapi?nikamwambia sio mbali unaweza tafuta sehemu rafiki kwaajili yetu kutulia.akasema sawa Haina shida tuonane JIRUSHE PUB.
Tulikubaliana pamoja na muda,ilipofika kesho yake moja kwa moja nilienda hapo jirushe pub sehemu ya ndani kabisa pamejificha,ndipo nilipomkuta tayari
ameshafika.
Nilimwambia agiza kinywaji aliagiza soda mirinda myeusi.namimi nikaagiza maji,sikutaka kuchelewa nilienda moja kwa moja kwenye point.nikamwambia seche kiukweli nimetokea kukupenda.nakupenda Sana Tabia zako zimenivuta zaidi kwako.
Alitabasamu na hakunipa jibu lolote.nkamwambia vipi mbona kimya au haujanipenda?akasema hapana Ila nakuonea aibu.nikamwambia hapana usione aibu funguka tu unajisikiaje kuwa na mm?hakujibu kitu.nikamwambia au una mpenzi?akasema hapana fredy Sina mpenzi,nikamwambia sawa Basi usipate shida utanijibu ukiwa kwenu,akasema sawa.tuliagana nikaenda nyumbani.
Nilipofika niliweka simu charge na baadae nakuta meseji ya seche iliosomeka ,Nakupenda pia Fred nitakuwa nawewe naomba usicheze na hisia zangu.
Nililuka kwa furaha nikajipiga kifua mala tatu Kisha nikasema Mimi ni mwanaumeđkashaingia huyu.basi nilimpigia simu alipokea tuliongea Mambo mengi Sana ikiwemo mipango ya baadae,
Kutokana na umri wake sikutaka kabisa kumchezea nilipanga niondoke kwenda kazini lakini nikifika niongee na mama kuhusu Natasha yote aliyonifanyia na nimtambulishe kwao seche,Imani yangu ni kwamba watampenda sababu Hadi hapo mama alionyesha kumpenda Sana.nilimuomba asibadilike heshima yake iendelee ivyo ivyo maana ni binti mdogo Sana kwa kipindi icho alikua na miaka 19 ametoka kumaliza 4m4 mwaka mmoja uliopita.
Siku zilienda akawa akija nyumbani moyo wangu unadunda nikiiona sura yake,na sauti yake,siku ya Mimi kuondoka ilifika na nilijiandaa na safari nilienda kumuaga tulikutana sehemu,nikamwambia sitaki kukuchezea seche mwezi ujao nakuja kukutolea mahali nikuoe,akasema sawa.nikamsisitiza kuhusu kujitunza,aliuzunika Sana alitoa machozi akasema nitakukumbuka Sana,tuliagana nikamwambia nitakuja mbeya kwaajili yako mpenzi.
Usiku kucha tuliongea alikua akilia tuu,sikuwai kumuomba sex hata siku moja,nilimuachia pocket money mie nikaondoka,mama na baba walinipa baraka zao.baada ya kufika niimwambia seche nimefika akasema sawa nafurahi kusikia umefika salama.
Kila siku alikua akisema kuwa nashindwa kuishi bila wewe fred nakupenda Sana,namimi namwambia kuwa mvumiivu my dear mwezi ujao nakuja anasema sawa.
Ilipita wiki nikiwa nimerudi kazini shule zimefunguliwa…nilitoka shule nikiwa nimechoka Sana,nikawa nachat na kipenzi changu,akaniuliza hiv ukianza kuja huko kwako ukitokea stand naulizia wapi??nikawa nimemuelekeza,akasema basi sawa.
Nikamuuliza kwann umeniuliza hivyo akasema nataka siku nikija nisipate shida,nikamwambia kuhusu kuja nakufata mwenyewe,Basi baada ya kupita nusu saa nashangaa anapiga simu Fred njoo unichukue barabarani.
Mh!!?Barbara gani?akasema hapa kwako,niliona Kama masihala,naenda nakuta seche ni yy kanifata,nikamwbia Kwan imekuaje umenisuprise Sana wazazi umewaagaje??akasema nimetoroka nyumbani kwaajili yako.
WIFE MATERIAL 07
Nilitoka kwangu Hadi barabarani huku nikiamini ni masihara ya seche kwani asingeweza kufika kwangu sio mipango yetu ile…kweli nilimkuta ni yeye nikamwambia wewe imekuaje?seche wazazi umewaaga vipi?akasema nimetoroka kwaajili yako.
Nikamwambia twende Kwanza nyumbani tukaongee vizuri…tulienda Hadi kwangu nikamkaribisha,nikwambia nenda kaoge alienda kuoga,nikampatia chakula akala,nikamwambia kwanini umeni surprise kiasi hichi?
Akasema ningekuambia kuwa nakuja najua usingenielewa ila kiukweli nimeshindwa kabisa kuishi mbali na wewe.nikamwambia seche nakupenda Sana ndio maana sikutaka kukuchezea ili kulinda heshima baina ya wazazi wangu na wazazi wako.leo hii wakijua mm ndo nimekutorosha unadhani itakuaje?
Akasema Kama hauniitaji kwako pia naweza kuondoka na kurudi nyumbani Fred sipendi kukuuzi nilifanya haya yote nikiamin nitakufurahisha.
Nikamuuliza nauli ulitoa wapi?akasema nauli ni ile pesa yamatumizi yangu uliyoniachia wakati unaondoka…kiukweli nilikua muoga Sana nikifikilia wazazi na uwezi ishi na mtoto wa watu hata wazazi wake wasijue yupo wapi ukozingatia umri wake ni mdogo miaka 19.
Nikamwambia ok karibu hapa ndo ninapoishi jisikie upo kwako.akasema Asante,nilimpokea kwa mikono yote miwili nilimuingiza chumban nikamwambia hapa ndo tutakapo lala siku zote,akasema sawa.tulipanda kitandani ila kabla ya chochote aliniomba tuimbe tenzi za rohoni na kusali.
Sikua na utaratibu huo,ila kwakua yeye alikua ni mtu wa maombi Sana ilikua kawaida kwake.tuliomba tulipomaliza,tukalala tukavunja moja Kati ya zile amri kumi.tuliungana kimwili mtoto mdogo ila kitandani si haba.
Tuliendelea kuishi pale huku line yake ya simu akiwa ameivunja amesajili mpya kuepuka usumbufu wa ndugu,alijichanganya pale mtaani nilipokua naishi kila mtu alimfahamu mke wa ticha fredy kutokana na uchangamfu wake,nidhamu aliokua nayo na kupenda dini,kanisani alijiunga kwaya,kweny jumuiya hakosi nguo zake ni zile za heshima kabisa awez vaa nguo fupi Wala ya kuonyesha maungo yake.
Basi siku zilienda aliniheshimu Sana Mimi kama mme wake,ilifika wakati nikasema wewe ndo wife material kwangu.sina muda wa kupoteza naomba niongee na wazazi wako ili nikuoe.alikubali ila akasema watakua na hasira Sana nisiende kichwa kichwa,ila yy ndo ataanza kuwatafuta aongee nao Kisha awaelezee vizuri ikibidi mimi nitume posa na mahali.
Tulikubaliana hivyo,ilikua ni usiku.nikamuachia hiyo kazi nikasema naenda kazin asubuhi nikirudi jioni nikute jibu lako la kuongea nao,akasema sawa.
Jioni nilitoka kazini nikamuuliza enhe imekuaje?akasema nimeongea na mama kanielewa ila ameomba mtu mmoja aje aone ninapoishi kwanza.nikamwambia sawa Haina neno.tulituma nauli kwao akasema atakuja dada yake,siku ya safari ilipofika njia nzima alikua akiwasiliana nae tuliandaa chakula.alipofika stand nilimtuma Bajaj akamfate.
Ilibishwa hodi,seche akaenda kufungua mlango,lakin kabla ajaingia Tena ndani nilisikia seche akisema mamaaa????@!& Ikabidi nishangae mama kivipi Tena?mala kidogo watu waliingia ndani Kama Saba hivi wakiwo na mapolisi nikaambiwa nipo chini ya ulinzi kwa kosa la kumtorosha mtoto.
WIFE MATERIAL 08
Aliingia mama seche pamoja na polisi na baadhi ya ndugu zake,nikaambiwa nipo chini ya ulinzi.mama ake aliongea maneno mengi Sana ya laana juu yangu kwa kuonekana Mimi ndiye msababishi wa yote yaliyotokea.
Sikupinga kitu niliendelea kuomba msamaha ili yasifike mbali lakini aikuweza kusaidia nilichukuliwa Hadi kituo Cha polisi.nikawekwa ndani,lakini kabla ya yote niliwapigia simu wazazi wangu ili wajue tu kuwa nimewekwa ndani.mama alishangaa kwakua hakuna alilolijua.alitaka kuhoji Sana imekuwaje,nikamwambia mpigie simu mama seche atakueleza kila kitu…
Nilikaa hapo Hadi usiku ndipo nilipotoka kwa mdhamana nikasema hiv haya maisha Hadi lini?mapenzi siku zote lazima yaniletee matatizo,ila hapana nitapambania penzi langu seche ndio mwanamke ambae mwanaume yoyote anaweza kutamani kuwa nae sitaacha kumsifia siku zote za maisha yangu,upole,hofu ya Mungu,,nidhamu na heshima vyote ni sifa zake,mwanamke anaejua thamani ya mume katika maisha yake,upendo wake kwangu umepita viwango nitampenda daima.
Nilijiambia maneno hayo ya faraja nilipokua nimetoka polisi nipo ndani kwangu nimejilaza kitandani,mpendwa wangu seche hakuwepo kwa wakati huo niliisi atakua ameondoka na ndugu zake…niliwaza Sana kwan sikutaka kumpoteza kabisa.
Mawazo yalinichukua kwa muda mrefu Hadi kichwa kikaanza kuuma.nilishtushwa na simu yangu ndogo ilipoita nilichukua na kupokea bila kuangalia ni Nani amepiga,ilisikika sauti ya mama yangu mzazi ikiongea.
Siku zote mama angu ni mtu wa busara Sana naisi ulokole wake ndio sababu ya yeye kuwa hivyo haku panic isipokua aliniuliza kwa upole sababu alijua kabisa nitakua kwenye wakati gani kwa muda huo.
Alisema haloo fredy hujambo?nikamwambia. Sijambo mama shikamoo…akasema marhaba pole Sana kwa matatizo,nikamwambia asante mama.
Akasema imekuaje kwani Hadi mnafikishana polisi?kwani vipi kuhusu Natasha na ujauzito wake Hadi Leo hii nasikia Tena unaishi na sechelela.
Ilibidi niwe muwazi nilifunguka kwa mama angu kila kitu kuhusu natasha.mama alihuzunika Sana akasema tatizo langu Mimi ni msiri sana,kwani ningesema toka mwanzo kuhusu seche Basi zingefatwa taratibu za kuweza kumchukua kihalali lakin kwa nilichokifanya kitamzalilisha hata yeye Kama mzazi pale mtaani.
Wala sikutaka kusema kuwa seche ndio aliotoloka kwao Wala siku shiriki nae,lakin nilihofia kumualibia kwa wazazi wangu na wake,mama alisema pumzika Mimi kesho asubuhi nafunga safari had huko kwako tuje tuyamalize nikamwambia sawa.
Asubuhi na mapema niliamka nilishika simu yangu kubwa nilikuta missed call5 zikisindikizwa na meseji moja.simu ilikua silent,nilipoichukua niliangalia ndipo nikakuta aliepiga na kutuma meseji ni seche,moyo ulifanya paaah!!!!sababu nilitaman kumtafuta ila nilihofia Sana.
Meseji yakeilisomeka
Fredy mpenzi wangu nakupenda Sana siwezi ishi mbali na wewe nitafanya kila liwezekanalo niwe na wewe haijalishi ndugu watanichukulia vipi. Nakupenda Sana ur my life.
Nilishusha pumzi nikasema asante kwa kila kitu,nilimjibu nakupenda pia seche kwa Sasa uko wapi?akasema nipo huku huku bado atujaondoka tunamsubiri mama ako afike Kwanza tumepanga lodge nikamwambia sawa.
Nilienda kazini nikiwa mwenye mawazo Sana kama kawaida Abel ndio mtu wangu wa karibu Sana siku zote.alinifata tukawa tunaongea kuhusu Mambo ya kazi maana Mimi pia nilikua ni mwalimu wa michezo,Kuna mechi tuliipanga ya kirafiki na shule jirani ilikua ichezeke hiv karibuni nikamwambia naisi sijakaa sawa kiakili Abel utaenda kuniwakilisha.
Akasema kulikoni Tena Kuna tatizo?nikamwambia hapana ila Kuna mambo yametokea kweny familia ya seche Jana nilipelekwa polisi.mh aliguna akasema mbona ukunitafuta nije nikutoe?nikamwambia nilichanganyikiwa Sana,sikuweza kuwaza ilo ila nilipata tu mdhamana.
Akasema pole sana.nikamwambia sawa mwamba ila namsubili bi mkubwa aje yupo njiani tuweke Mambo sawa.akasema ni Jambo jema.basi niliingia darasani nikafundisha wanafunzi nilipomaliza kipindi nilienda ofisini ilikua ni mida ya mchana nilimpigia simu mama akasema amekalibia kufika niende stand kumpokea.
ilibidi nimtafute Abel ili nimuage,nilimuangalia katika madarasa yake ya kazi sikumuona ikabid nimpigie simu nikakuta anatumika.nilijaribu kuuliza mmoja kati ya wanafunzi mmoja akasema ticha nimemuona nyuma yamadarasa kwenye njia yakuendea kantin anaongea na simu.
Nilipiga hatua Hadi ilo eneo kweli nilimuona ni yeye ameweka simu sikioni,ameegamia mti anaendelea na kuongea na simu.nilimsogelea Hadi karibu yake,ila akuniona,kitu kilichonishtua nilisikia kweny mazungumzo yake akitaja jina langu.
ilibid nisikilize kwa umakini.ndipo nikagundua kuwa anaongea na Natasha anamueleza yaliyonikuta kuwa nilikua polisi,waliendelea kucheka huku abely akisema aisee yule jamaa ni mjinga Sana ulifanya la maana Sana kubeba vitu vyake vyote mbinu niliyokupa imekusaidia Sana.
Nilipigwa na butwaa nguvu ziliniisha nikasema kwa nguvu “Ama kweli kikulacho kinguoni mwako.”
WIFE MATERIAL 09
Nilipomsogelea abely niliweza kusikia maongezi yake yote baina yake yeye na Natasha nilihuzunika Sana kwani alikua mtu ambaye sikuweza kumdhania Wala kufikilia Kama angeweza kunifanyia hivyo.
Waliendelea kuongea huku wakicheka, Abel alijisemea kuwa yeye alifanya Jambo la maana kumpa mbinu Natasha ya kuweza kuniibia vitu.
Kumbe Mambo yote haya yanatokea abely ndo muhusika mkuu,inamaana kumbe hata Abel aliponiunganisha na Natasha toka siku ya kwanza lengo lao lilikua wanifilisi,
Uvumilivu ulinishinda nikamshika bega Abel aligeuka Kama mtu asie na Shaka lolote,lakin baada ya kukutanisha uso wake na wangu aliogopa Sana kiasi kwamba hata ile simu aliekua kaishika iliishia kuanguka chini.
Nilipandwa na hasira aliinama akaokota simu yake haraka,akaniuliza vipi ndo unataka kuondoka saivi fredy?yan anafanya ivyo ili ajue Kama nimesikia maongezi yake au sijasikia.
Nilipandwa na hasira Sana nilitaka kupigana nae nilimpandishia sauti,nikamwambia wewe Abel wa kunifanyia hiv Mimi?
Lakini kabla sijafanya Jambo lolote nilikumbuka kuwa sitakiwi kuleta fujo eneo la kazi ama kupigana.nilihisi maumiv makali Sana yule niliemuamini amenitenda,
Nilitoka pale nikiwa nna mawazo mengi Sana,mawazo ya mwanamke wangu seche ambae sikujua ni Nini hatma yake,.pili Abel alinitonesha kidonda zaidi.
Nilifika nyumbani nikabadili nguo nikaelekea stand kumfata mama,kabla ya kufika nae kwangu tulipita mahali nikamuagizia chakula akawa anakula,
Aliniuliza fredy kulikoni Kuna shida yoyote?nikamwambia hapana mama,akasema nikiangalia uso wako naona kabisa unalazimisha kutabasam,nikamwambia ni kweli mama kuna mambo hayapo sawa.
Akaniuliza Tena ni yapi?au haya haya ya seche?nikamwambia ndio mama hata seche nae namuwazia Sana,ila kuna jambo lingine tena.
Ilibidi Sasa nianze kuelezea kuhusu Natasha Hadi Abel,mama alisikitika Kisha akasema pambana maisha ndivyo yalivyo.
Alinisihi Sana Kama nitafanikiwa kuishi na seche basi niishi nae vizuri kwan ni binti aliependwa na mtaa mzima,hata alipotoloka watu hawakuamin ni binti mweny heshima zake.
Nikamwambia sawa mama hata Mimi nimemuona toka nimeanza kuishi nae ni mpole na mcha Mungu.
Basi tuliweka mipango sawa tukaondoka Hadi kwangu ambapo tulipofika mama seche alimpigia mama akamwambia kuwa amefika wakasema wanakuja,baada ya nusu wakawa wamefika,awamu hii walikuja wakiwa wapole Sana.
Tuliongea mengi ilinibidi nipige goti kuomba msamaha.na seche pia aliomba msamaha,tuliambiwa tuishi tu kwa amani japo Jambo tulilofanya sioo zuri.
Tuliambiwa tufate taratibu za kuweza kumlipia seche,niliulizwa nia yangu nikasema nataka kumuoa,basi wakasema nifate taratibu zote wao wanaondoka,kesho yake wote waliondoka nilibakk na seche,
Walipofika nilitum posa nilapangiwa mahali pia nikatoa,baada ya hapo tulikaa kususbiri siku ya harusi ifike tulipang no miezi mitano mbele.
Yan tulikua tukiingoja kwa ham sana iyo siku tukikaa ndio story yetu kubwa kuhusi ndoa,seche alikua akiimba kwaya kanisani.
Siku moja,seche alienda kanisani na aliporud alikua kachelewa Sana.nilipomuuliza alisema kuwa anachelewa sababu wanaimba kwaya nyingi.
Nilimuitikia sababu sikupata waswasi nae wowote.siku zilipozidi kwenda ile tabia ilizid kukomaa,kurudi nyumbani ni saa mbili usiku anaondoka toka saa nane mchana,ikabidi nianze kuuliza viongozi kanisani wakaniambia kwaya huwa mwisho saa 11 jioni aisee nilivulugwa kiukweli.
WIFE MATERIAL 10
Nilipeleleza kwa marafiki wa karibu wa seche nikaambiwa kuwa kwaya huanza saa tisa saa kumi na moja inaisha,haikutosha ilibidi niulize wazee wa kanisa nao walinijibu hivyo,sikutaka waelewe chochote.
Mawazo yalinitawala kichwa changu,ila nikimuangalia seche na hayo Mambo nnayoyahis Wala siamini,hakuwai kunidharau ndio Kwanza heshima ilizidi ndani ya nyumba,siku moja jumapili tulienda kanisani na muda wa kucheza kwaya kweli alisimama na kucheza vizuri Tena ni hodari anacheza na kuimba vizuri.
Ibada ilipoisha tuliongozana Hadi nyumbani,tulipofika alipika tukala,tukiwa tumepumzika tuu nikasema lazima nimwambie hili swala ajue mapema.
Nikamwambia seche Kama umemaliza kazi zako naomba ukae hapa tuongee,alinijibu sawa mme wangu nikupendae ila Kwanza acha nikaoge tuongee alafu niende kanisani kweny kwaya.
Mh!wewe seche kwaya gani hiyo Hadi jumapili??
Ndo ivo mme wangu tumeambiwa tusiwe tunapumzika kwa Hilo tu niruhusu…
Seche huendi kokote nenda kaoge uje tuongee,seche alibadilika akakunja uso Wala hakwenda kuoga,akaniambia haya ongea nakusikiliza.
Kwa mala ya Kwanza niliona sura ya seche ikiwa imejikunja ikiambatana na mdomo kuvimba.nikamuuliza Kwani kilichokununisha ni nini?
Akanijibu kwa sauti ya kawaida Wala sio ya jazba Wala ukali.fredy nakupenda Sana ila kwenye swala la kanisani tutachukiana tu kwakweli Kama unanikataza kwenda kanisani hatutoelewana kabisa.nimeanza kufanya kazi za kanisa toka mdogo toka nyumbani hata wewe umenikuta kwenye misingi ya Imani.
Nikamwambia seche kuwa kwenye Imani Wala sikatazi Ila inapofika mahali tunashindwa kusikilizana ama kuelewana aisee itakua ngumu kusonga mbele.
Akaniuliza kivipi?
Nikamwambia swali zuri sana.seche kumbuka nimekuchukua ukiwa mdogo ni miaka 19 tuu ndio nimeanza kuwa na wewe.japo sijakukuta bikra lakin ni msichana niliependezwa na mienendo yako toka siku ya kwanza.
Lakini kwa Sasa Kuna Mambo ambayo unayafanya yananifanya nakua Sina Imani na wewe kabisa,akaniuliza Tena kwa upole mambo gani fredy?nikamwambia Mambo yenyewe ni haya naomba unijibu maswali yangu kwa ufasaha bila kuacha hata swali moja,
Nikamwambia seche,kanisani huwa unaenda saa ngapi?akasema saa nane,nikamwambia mbona mazoez ya kwaya huwa yanaanza saa Tisa?akasema ni kweli fredy wangu lakini huwa naondoka hapa mapema sababu umbali wa kutoka hapa Hadi kabisani ni Kama nusu saa kwaio Hadi kufika inakua saa Tisa tayari.
Alijibu swali vizuri,nikamuuliza Tena enhee!!!kwaio kwaya mnacheza Hadi saa ngapi?akasema saa mbili usiku.nilicheka kwa hasira hahaha seche usinifanye Mimi mtoto mdogo,inamaana huko kanisani hawajui Kama unaishi na mwanaume?kwamba inabid uwai kurud kuhudumia familia yako?
Akasema wanajua ndio maana kabla sijaenda kanisani nahakikisha nyumba yote ipo vizuri kwanzia nje Hadi ndani naandaa mboga ya usiku na nikirudi nafikia kuandaa chakula tu na unakula kwa wakati.
Nikamwambia seche,ratiba za kanisani zote nazijua Hadi nimekuuliza Leo nimeshafatilia kwa kina Sana,seche kanisani mwisho saa kumi na moja,unaweza kuniambia huo muda mwingine huwa unaemda wapi?alibinua mdomo Kisha akasema aliekuambia kakuongopea kanisani mwisho saa mbili nikamwambia ok!naomba uinuke twende kanisani nikapate ukweli kuhusu ilo Jambo.
Alikataa akasema Kama simuamini Basi,nilipatwa na hasira niliinuka nusu nimpige lakin nilijizuia nikachukua simu nikasema Kama umekataa kwenda acha nimpigie Sim mchungaji Kwanza ili aweze kunielewesha mbele yako,simu ilianza kuita niliweka loudspeaker seche alipiga magoti na kusema fredy kata sim nitakuambia Kila kitu usimpigie mchungaji.
Nilimsikiliza nikakata sim,lakin baada ya kukata tu mchungaji alijua labda nimem bip akapiga nilipokea tukaongea mengi Huku seche kapiga goti ananisihi nisiseme kitu,nilimwambia mchungaji nilikua nakusalimia tuu,alifurahi akasema nibarikiwe.
Nilikata simu nikamuuliza unalia nn?
Kuna kitu unanificha?
akasema kweli kanisani huwa wanatoka saa kumi na moja enhee baada ya kutoka kanisani huwa unaenda wapi?