WIFE MATERIAL 26
Nikawaambia kosa langu ni lipi Hadi mnaniadhibu kiasi hichi?baba B aliweka panga mdomoni kwangu akiashiria ninyamaze.akasema yani seche amefariki na nilikua namtumia yeye kupata pesa kwaio wewe saivi ndo utakua kitega uchumi changu,sawa?alisema kwa ukali alichomoa kisu kidogo na kunionyeshea,nikamjibu sawa nipo tayari kwa lolote.
Walinipiga sana na kutaka niwaonyeshe ni wapi nimehifadhi pesa,nilisema Sina pesa kwa Sasa nikatoa noti ya elfu 10,iliyokuwa kwenye dresing table nikawapa,walikasilika Sana mmoja Kati yao alisikika akisema tumuue tuu anakaa anafaida gani na pesa hana.?
Huyo baba B akasema huyu anatufanyia makusudi ngoja nimuoneshe kuwa miemwenyew ni mafia,alichukua kisu akajikata sehem ndogo ya mkono wake,sijatahamaki akachukua kile kisu alichojikata yeye akanikata Mimi mkononi,alichana sehemu kubwa Sana.
Wenzake walimuuliza kwanin umejikata jamaa akasema sio lazima kila kitu mjue ila yeye mwenyewe anajua,hapo nimewekwa chini ya ulinzi.nilipigwa Sana nikawa nalia Kama mtoto mdogo Kisha wakaondoka wakasema wamevunja mlango mkubwa wa seblen kwaio kesho watarudi wakute pesa laa sivyo wataniua.
Jamani nimekaa nikaanza kutafakari ni kwanini amejichana Kwanza yeye na kile kisu ndipo akanichana Mimi,nikakumbula kuwa seche alikua muathirika hivyo hata yeye ni muathirika kwaio ameamua kufanya hivyo ili kunikomesha aniangamize ilihali Sina kosa lolote na yeye.
Nilivofikilia hivyo nilitoka upesi bila kujali ni usiku mkubwa mlango wa kuingilia sebelen umevunjwa,niliacha nyumba wazi nikawasha gari moja kwa moja hospital,mkono ulikuwa umekufa ganzi damu zinatoka Kama bomba.
Nilipokelewa haraka hospital kabla ya matibabu niliambiwa niende police kwanza,nilienda Kisha nikarudi kuendelea na matibabu nilieleza Hali harisi,Hadi matatizo aliyonayo alienichoma kisu.
Walichukua tahadhari nilishonwa na nikaanzishiwa dozi hapo hapo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.nilishonwa nyuzi sio chini ya 12,nikaruhusiwa kurudi nyumbani nikaambiwa ninywe dozi Hadi itakapoisha nije kupima.
Niliondoka Hadi kwa rafiki yangu mmoja ikiwa ni alfajiri maana hata kwangu niliogopa tena kurudi.alinipokea na kuniuliza Nini shida nikamueleza akasema umechukua hatua gani?nikamwambia Mimi nataka niwafunge maana kuendelea kwao kuishi watakuja kunifanyia kitu kibaya zaidi.
Akasema wazo zuri subiri Kwanza kupbazuke ili twende tukaombe ruhusa kazini ukaeleze kuwa ulivamiwa na majambazi ili utoke uweze kufatilia kesi yako.kweli kulipambazuka tukaenda shule ambapo nilieleza shida yangu Hadi wenzangu wakasema yan jamaa wewe kila siku ni majanga kwako tuu pole sana.
Nilitola pale Hadi police nilienda kuomba akamatwe kwanza muhusika mkuu yeye ndo atataja wenzake.
Tulitoka pale Hadi kwa baba b maana nnapafahamu vizuri kabisa.uzuri tulimkuta aamekaa nje ya nyumba na wenzake wawili wanavuta bangi walipigwa chini ya ulinzi.wakabebwa Hadi police wakatiwa ndani walipewa kipondo Hadi wakasema niwapi alipo mwenzao mmoja nae akakamatwa wakakamilika wanne.
Mie niliendelea kuuguza like donda Hadi likapona huku wasiwasi wangu mkubwa ukiwa kupata magonjwa,niliendelea kuomba kwa Imani yangu kuwa sitakufa Bali nitaishi tena nikiwa mwenye afya tele.
Alichukuliwa vipimo baba b kweli aligundulika no muathirika,roho iliniuma,niliona kabisa yeye ndo kaalibu future ya seche,.nikamuahidi tu kuwa ataozea jera.kesi ilienda walikosa mtu wa kuwatolea mdhamana,walifikishwa kizimbani na kusomewa kesi zao na kuhukumiwa miaka 30 jera.nilishukuru Sana ilikua no furaha kwangu isioelezeka.
Nilipomaliza dozi nilienda Tena hospital kupima nikaambiwa Sina maambukizi Mimi ni mzima,nilikaa baada ya miezi mitatu nikapima Tena nikaambiwa nipo mzima,niliandaa pesa kwaajili ya kupeleka kanisani ikiwa ni sehemu ya kushukuru kwa kuvushwa salama.
Siku zilienda hatimae tulipangiwa kwenda kusimamia mitihani ya kidato Cha nne shule mbali mbali…nilipamgiwa shule moja huko kijijini ambapo wasimamizi wote tulifikia kwa mwalimu mkuu kwani Kijiji hicho hakikuwa na guest house.
Tulipofika pale tulikutanishwa walimu wote kutoka shule mbali mbali na kuomba tujuane,tulijitambulisha kila mtu na tukajikuta tumekua Kama ndugu ama marafiki wa muda mrefu kwani mkuu alitupa vyombo akasema tutakua tunajipikia wenyewe ilikua kama tupo kambi,wanawake wanafata maji mtoni,wanaume tunafata kuni porini tunakuja kupika pamoja tunakula.
Tulisimamia vizuri mitihani siku ya kwanza jioni tuliingia kujipikia kuna madam mmoja akanifata akaniambia samahani naomba unipige picha kwenye simu yako alafu utanitumia sikukataa.
Nilichukua simu na kuanza kumpiga picha alikuja kuzitazama na kusema jamani zimetoka vizuri sana.nikamwambia ni kweli nzuri,akasema andika namba yangu utanirushia kwa wasap nikamwambia sawa.
Alinipatia namba zake nikasev jina alinitajia anaitwa evo,nikamtumia muda huo huo.ilipofika usiku tulienda kulala wanaume kwenye vyumba vyetu na wanawake vyumba vyao.
Nikiwa bado nachezea simu yangu iliingia meseji wasap Helo hujalala niliingia kuifungua ni evo,nikasema hapana sijalala,akasema ooo sawa jaman nimependa uchangamfu wako wewe Kaka siku ukiondoka tutakumiss Sana maana madamu wote hapa geto wanasimulia ukarimu wako.
Niliweka emoj ya tabasam😊😊Kisha nikasema Asante nashukuru.nitawamiss pia usiku mwema kesho tuwahi kuamka akasema sawa na kwako pia akaweka na ka emoj chenye vikopa🥰🥰aaaa nikazima data sikumjibu tena.kwakua bado sijalala niliona ni Bora niende msalani kabisa nikajisaidie haha ndogo.
Nilitoka hadi nje,kwenye choo Cha miti Kama mjuavyo vijijini,choo hakina mlango ila wameweka nguo ni kama pazia ili kuzia kuonekana,nikiwa nimesimama namalizia haja yangu nilishtuka muona mtu amenishika kwenye mbavu yupo mgongoni kwangu,nilishtuka,kugeuka namkuta madam evo anatabasam.
WIFE MATERIAL 27
Niligeuka na kukuta madam Evo amenishika huku anatabasamu,niliona aibu licha ya kuwa ni giza niliingiza haraka hataka fimbo yangu kwenye suruali….alicheka Kisha akasema Fred bwana sa unajificha Nini wakati nimekuona?
Nilibadilisha uso nikawa mkali Sana,nikamwambia wewe mbona binti mrembo Sana na unayoyafanya huendani nayo kabisa?hivi kwa mfano huyu mkuu aliyetuhifadhi hapa akikuta tupo msalani wote atanionaje Mimi?ebu jieshimu,yani wanawake wengine Kama mashetani,nilimsukuma uko pembeni nikaondoka zangu.
Nikiwa ndani nimelala niliwaza Sana sikupata hata jibu.nikasema ni nini hichi?mbona wanawake wa siku hizi wanakua Kama wabakaji?alianza Eliza Sasa huyu madam aaaa,wananipa shetani alafu nikishawatumia wanaanza kuniumiza hizo habari sizitaki hata kuzisikia maana hata Eliza licha ya kumtoa usichana wake ila sijamuweka moyoni Wala sijawai kumuwazia Kama mpenzi wangu hata siku moja.
Nilivuta shuka nikalala asubuhi na mapema tuu nikaamka na wenzangu wote tulijiandaa tukaelekea shule Kama kawaida,Safari hii nilimsalimia evo ila alionekana kuukunja Sana uso wake,Wala hakuitika salamu yangu eti kaninunia…sikujali Wala nini.
Chakula Cha mchana tulipikiwa na wanafunzi,jioni Kama kawaida tulirudi na kuanza kujipikia wwnyewe tulifanya kazi kwa ushirikiano,wanaume tunapika ugali wanawake wanaunga mboga…ilipikwa mboga samaki aina ya kambale kwani hao samaki wanapatikana kwa wingi Sana katika Kijiji hicho kwenye mto wanaoutumia kwa shuhuli zao zote.
Tulikula,baada ya kumaliza kula tuliwasha Moto wa kuni tukakaa pembeni tukiwa tunaota Moto huo ili mwili kupata joto.tulifanya hivyo huku tukiendelea na mazungumzo,mie nilikua ni muongeaji Sana kiasi kwamba walimu wote walinipenda wakike kwa wakiume,Yani ilikua nikitoa neno langu lazima wote waangue kicheko,walikua wanataman mie niongee tu muda wote.ila kila nikipiga jicho kwa evo kakunja uso,akiongea mwingine anacheka ila nikiongea Mimi Wala hafungui mdomo wake.
Tulienda kulala Kama ilivo kawaida kesho yake Tena hivo hivo,jioni tulipewa viazi vitamu na mkuu alitoa shambani kwake,tuliviosha tukachemsha na chai tukanywa.usiku huo Kama kawaida ni lazima tukae kuzungumza nje,mmoja Kati yetu akasema hivi kwanini hapa tulipo tusijuane kwa historia fupi ya maisha?mh!!!niliguna,nikaulizwa vipi mbona unaguna mwalim.nikasema hapana ila iyo tungefanya siku nyingine Leo nimechoka Nina usingizi Sana.
Mwalimu mwingine akasema tutafanya lini?wakati kesho tunasimia mitihani ya mwisho kila mtu anaenda kwake?sio Kama nna usingizi ila kiukweli sikutaka kuelezea history yangu yenye aibu na maumivu ndani yake.
Ilibidi ninyamaze tuu akaanza mwalimu mmoja wa kike kwa majina nimemsahau,alijitambulisha pale akaeleza kuwa Ana watoto wawili na ni mke wa ndoa,hapo mwanzo alibadili dini kutoka mkristo kwenda uislam kumfata mume,na vitu vingine vingi.
Akafata mwalimu mwingine wa kiume nae akajieleza,ikafika kwangu ilibidi nifupishe Tena kwa kudanganya…naitwa Fred nafanya kaz mkoa huu ila ni mjini nilikua nna mke ila amefariki mwaka huu kaniachia mtoto mdogo wa kiume.
Nikawa nimemaliza sikutaka maelezo mengi,wote walionekana kuwa na huzuni walinipa pole sana,nikawaambia msijali nishapoa mbona.
Ilizunguka ikafika zamu yake Evo,naitwa Evodia nmeajiriwa kazi mwaka Jana,Sina mtoto Wala sijaolewa nipo single,nimeshapitia mahusiano mamoja tu Hadi Sasa,asanteni tutaendelea kujuana zaidi.
Kimoyo moyo nikasema mbona Kama ananishawishi kutupa ndoano baada ya kusema kuwa yupo single!!!basi wote walitoa historia zao wengine walizielezea kwa kirefu toka wakiwa wadogo Hadi hapo walipofikia.
Tulimaliza zoezi Hilo na kwenda kulala kesho yake ilikua ni mtihani mmoja tu wamwisho hadi kufika saa tano asubuhi tulikua tumeshamaliza kila kitu tukaagana na wanafunzi tulipata nafasi ya kupiga picha wasimamizi wote.
Tulirudi kupanga vitu vyetu ikiwemo nguo,tuliuliza Kama tunaweza kupata gari ya kwenda mjini kwa siku hiyo ila mkuu akasema hapa gari ni moja tuu mkiikosa iyo ndo basi Tena huwa inaondoka kijijini saa 12:30 asubuhi.yani Hadi nilijuta kwanini sikwenda na gari langu.
Tukasema sawa Haina shida kwa leo acha tuweke vitu vyetu sawa ili kesho tuondoke vizuri,mmoja alisema mnaonaje twende mtoni kufua ngui zetu,Kisha tukimaliza tuoge kabisa?tutasema ni wazo zuri tulikubaliana wote isipokua mama mmoja ni mtu mzima Sana,akasema nyie vijana nendeni tu mie nabaki hapa.
Tuliondoka Hadi mtoni kila mtu alifua nguo zake tulipomaliza tukavaa pensi zetu tukaingia kuogelea.wanawake nao wakaingia kwenye maji ila tulipeana mipaka,wanaume tulioga upande wa kushoto wa mto,wanawake wakaoga upande wa kulia wa mto.
Tuliendelea kuoga huku tunapiga story,mala kidogo tulishangaa kujikuta wote tumechanganyikana na wanawake ilibidi tu tuanze kucheka,imekuaje tumekutana?
Ghafla alinifata Evo akaniambia Fred nitakuja mjini kukutembelea kwako nikamwambia we si ulininunia?akacheka Kisha akasema kwaio hutaki wageni?nikamwambia hapana karibu tuu akasema Asante uzuri wote typo mjini tutaonana tuu.
Kisha akatoka ndani ya maji nguo aliokua ameivaa yote tepetepe maji umbo lake limejichonga na kuonekana Hadi rangi ya nguo ya ndani,ukianzia kifuani Hadi miguuni mashaaallah!!!!
Jambo Hilo lilifanya watu wote kwenye maji wakike kwa wakiume kumpigia kelele aliona sofa na kuanza kujitingisha,aaaa mwalim mmoja akasema Evo utatuumiza we binti.
Wote tukatoka kwenye maji na kuvaa nguo kuanza Safari ya kwenda kambi.tulipofika tuliandaa vitu vyote na kuviweka sawa alfajiri tulijidamka na kumuaga mkuu tukaondoka hao Hadi mjini tulifika saa nne asubuhi.
Tulibadilishana namba na walimu wenzangu,nikaanza safari ya kwenda kwangu wengi sana,tulikua no walimu wa pale mjin sema shule tofauti ni wachache Sana walikua wa wilaya jirani.
Nilifika kwangu nikapumzika kidogo nikaamka mchana nikaanza kuandaa vitu ili nipike,nimesimama jikoni namenya nyanya huku najiimbia wimbo wa kizamani sana,WANAUME TUMEUMBWA,MATEESO MATESO KUANGAIKA,
niliendelea kuimba huku naandaa vitu,nikasikia sauti kwa mbali ikipiga hodi uko nje,nkasema ingia,wala sikujua ni Nani,alieingia ndani ni Eliza,alifurahi kuniona alinifata na kunikumbatia,nikamuuliza we vipi?akasema poa tu nnafuraha nimemaliza mitihani licha tu ya kimaliza nnaona kabisa ntafanya vizuri siku ya matokeo nimesoma kwa bidii Sana kwaajili yako Fred ili tu nifauru unioe.
Nilimuonea huruma jmn yule binti ni Kama niliathirika kisaikolojia sikuwa na upendo na mwanamke nikasema moyoni,wote walikuja Kama Eliza ila mwisho wa siku walichonifanyia Wala sikuamini.
Nikamwambia sawa nasubiri majibu wewe saivi bado mwanafunzi Hadi matokeo yatapo toka,akasema sawa,akaniambia acha nikusaidie kupika, navile nimechoka nilimuachia jiko nikawa nimekaa pemben namuangalia anavoandaa vitu ghafla simu iliita uko seblen ikabidi niifate.
Ooo ni Evo anapiga,nikapokea haloo yes!Mr Fred umefika salama?nikamwambia yah sijui wew akasema hata Mimi nimefika salama weekend hii ntakuja kukutembelea,nikamwambia sawa karibu.tuliongea mengi sana ya kawaida tuu Hadi chakula kikaletwa pale nilipo na Eliza,nikamwambia Basi baadae acha nipige msosi.
Nikaanza kula huku Eliza amekaa pemben nikamwambia njoo ule akasema ameshiba,nilipomaliza alitoa vyombo akaenda kuosha.
Alipomaliza alirudi na kukaa pembeni yangu huku amechukua kifaa cha kukatia kucha akawa ananikata kucha za mguuni,nikamuuliza vipi Eliza mbona unajari Sana?akasema ni sababu nakupenda na Leo ntalala hapa ma wewe.
WIFE MATERIAL 28
Niliguna mh!!Kisha nikarudisha mguu nyuma ule aliokua akiukata kucha,nikamwambia we binti usinitanie,,,alitingisha kichwa Kisha akasema,tatizo lako Fred no moja tu wewe ukali wako wa should huwa unauleta Hadi nyumbani,Yani unataka kuniendesha Kama unavoniendesha darasani.
Nilikunja uso Kisha nikamwambia,wewe bado ni mwanafunzi tuu,kwaio naomba uwe na heshima,aliepo mbele yako ni mwalimu wako,alafu nafasi yako kwangu ni mwanafunzi tuu,zaidi ni Kama mdogo angu Sina hisia zozote za kimapenzi na wewe sijawahi kukupenda Eliza.
Kwaio naomba ujiheshimu nakukwepa ni kwasababu kichwa changu kimevurugika,nyie wanawake mnafanana nimeshapita mahusiano kadhaa na wenzako walikuja kwenye maisha yangu Kama malaika lakin mwisho waligeuka mashetani na kuishia kucheza na hisia zangu.
Alichonijibu yule binti ni kwamba,naitaji mtu was saikolojia ili anisaidie maana kwa maelezo yangu naonekana nimealibika kisaikolojia.
Nilicheka kwa kejeri Kisha nikamwambia Eliza hayo ni matusi Sasa unanipa,akaniambia Basi sikuacho na Leo siondoki hapa kwako,nikamwambia nilishakwambia Hadi siku ukiona umefaulu ndo uje hapa kwangu ila kwa Sasa naomba Leo iwe mwisho,na Kama unanipenda kweli utanisikiliza.
Alipata hasira akainuka na kuongoza nje moja kwa moja,huku nyuma niliumia Sana nilijiona Kama nimekua na roho ya kishetani mno,ila nikasema siwez kuwa na Eliza nitamchezea mimi,saivi upendo wa dhati Sina nitamuumiza mtoto wa watu namuonea huruma kwani ni binti mdogo Sana.
Nikasema ni heri niwe na Hawa magume gume lika langu au niwe nimewazidi kidogo mtu unajua unapiga shoo unapita hivi.niliwaza hivyo.nikatoka na kuelekea nie kwenye bustani yangu ya maua,mala simu ikaita.ni madam evodia.
Haloo Evo vipi?
Nzuri tu za muda fredy!
Niko poa wangu.
Unafanyaje?
Nipo nimetulia.
AAA ok nataman kampani yako,uwezi Amin nimekumiss Sana.
Weee evo acha masihara umenimis kivip?
Aaa fredy nimemis tu ule uchangamfu wako ukiongea lazima mtu afurahi na vile nna mawazo Sana nataman sana ukaribu wako.
Nikamwambia sawa unakaribishwa,akasema Asante,nilimuaga akakata simu.
Usiku nikiwa nimepumzika mesej iliingia namba ngeni,nakupenda fredy from me eliza.usijibu ujumbe huu simu ni ya mama.
Nikasema katoto haka akakomi,nikaweka simu pembeni kikalala usingizi fofofo, alarm imeniamsha mda wa kwenda kazini nikajiandaa nikaenda kazin,siku zilienda hatimae iyo siku ilikua ni ijumaa,mishale ya saa 11 jioni,simu iliita no Evo,haloo Fred nielekeze hapo kwako nipo mtaa huu uliosema unaishi.
Nikamuelekeza nikatoka nje kwenda kumfata,natoka tu getini naiona sura na evo,kapiga kimini chake Cha kitambaa Kama muimba kwaya,nikamkaribisha ndani nikamwambia upo vzr unaelekezeka,umefika had mlangoni.
Akasema yeah!!!hiv Fred hapa ni kwako?nikamwambia ndio,akasema hongera umejitahidi sana,nilitaka kujenga ntakuj kuchukua hii ramani yako…tulikaa kwa muda mrefu baadae nikasema njaa inaniuma mgeni nnavokusindikiza unavoenda kwako tutapitia hapo bar tununue chakula.
Akasema no Fred mie ni mwanamke nimekuj kwako lazima nikupikie,sema tu unataka kula nini,nikamwambia pika ugali tu,saiv sikupanga kupika hata mboga Sina ila Kuna mayai utapik tule na ugali.
Alipika akatenga tukala muda unazidi tu kwenda,akasema nimechelewa ila najihisi joto Sana acha nioge niende kwangu nikasema sawa.sikumuingiza kwenye choo Cha chumbani kwangu,nilimpeleka public toilet nikamuonesha sehem ya kubadili nguo.
Alioga na alipomaliza alinifata sebleni,akaniomba mafuta,nikacheka kwa utani,nikamwambia mie napaka mafuta mazito,nyie watoto wakike hamtakagu kupaka mafuta mabaya.
Akasema hapana mie napaka tu we nipe nilitoka pale nikaenda ndani kumletea mafuta,alipaka lakin Cha kushangaza alianza kupaka sehem ya mapaja yake,huku anapandisha nguo aliyojifunga.
Macho hayana pazia kila nikikwepesha najikuta naangalia tuu,akainama Zaid Kama anachuma mboga akawa anapaka kwenye vidole vya mguu,huku nyuma nguo alioivaa ndani yote ilionekana,nikatingisha kichwa na kujisemea majaribu haya sasa.yani shetani anajileta mwenyewe kuzimu.
Nilimfata na kwenda kusimama nyuma yake,muda huo damu inanichemka,alipoinuka tuu akajigonga kiunoni kwangu aligeuka na kuniangalia huku anatabasam,tulipelekana Hadi kwenye sofa nikamtupa hapo,tukaunganisha midomo yetu muda huo akili imeama kabisa,nmesahau hata kuwa milango sijafunga.
Tukiwa tunaendelea hivyo ile kanga ilitoka akabaki alivyo na nguo ya ndani tuu.nilitupa vest yangu chini nikabaki na pensi tuu.ghafla niliona mlango wa seblen umefunguliwa nikakurupuka upesi,nakuja kuangalia ni Eliza kasimama analia.
Ticha ndo umeamua kunifanyia hivi haya asante nakushukuru sana.
WIFE MATERIAL 29
Eliza alipoingia na kukuta tupo kwenye kumbato la mapenzi,alitoa chozi na kusema ticha ndo umeamua kunifanyia hivi haya Asante nashukuru sana.hisia zote zilikata Kwan alinishtua mno,aligeuza akafungua mlango akaondoka.
Evo nae alikasirika,aliinuka akasema kumbe unamtu wako alafu unanidanganya kuwa mke wako amefariki nyie wanaume watu wabaya sana,kwaio hapa ulitaka Mimi nifumaniwe si ndio?nikamwambia itakua ngumu sana kuanza kujielezea ila unaweza kuamini unachokiamini.
Akasema usiniambie hivyo bwana Fred ninyooshee maelezo imekuaje?na huyu mwanamke ni Nani?nikamwambia huyu mwanamke ameanzisha mahusiano na Mimi ila Kama unavomuona ni mdogo na ni mwanafunzi,hivyo nafsi yangu imekataa kabisa kuwa nae namuonea huruma sana.sitaki kualibu malengo yake.
Akasema aaa sawa ila Fred mie napenda mwanaume mkweli sipendi kabisa hivi naanzisha mahusiano alafu baadae nakuja kuumia sipendi kabisa.
Nikamwambia sawa,ila kwa Sasa amka tu uende kwako,maana nmeshatoka kwenye mood kabisa,akasema sawa haina shida ila nakupa mda wa kujifikilia kuhusu mimi.nikamwambia sawa,nilitoka nje nikawasha gari nikamwambia panda nikupeleke,alipanda nikampeleka Hadi kwake,kumbe sio mbali kabisa na kwangu kwa gari ni mwendo usiozidi nusu saa kufika.
Nilimuacha hapo njiani sikutaka kufika kwake,akasema nitakuja kwako ijumaa nitakaa Hadi jumapili,nikamwambia sawa karibu. Njiani wakati narudi Sasa ndo nikaanza kuwaza,hivi huyu Eliza ni Nani alimwambia kuwa Mimi nipo na mwanamke ndani Hadi akaamua kuja ghafla.
Inabidi nimpotezee moja kwa moja huyu mtoto maana ataniingiza majaribuni Tena hapana!moyo wangu umekua mzito Sana kwake sijui kwanini,Yani sielewi.labda naweza toka nae akawa sio mwanamke wa ndoto zangu akawa Kama wale.
Hapana acha niwe tu na huyu evodia yeye ni mkubwa na kashapitia mahusiano mengi hata ikitokea nimemuumiza Wala haotomuuma tofauti na uyu dogo.
Nilifika karibu na kwangu kuangalia mbele taa za gari zilipomulika pembezoni mwa Barbara upande wa fensi ya nyumba yangu niliona Kama Kuna mtu kachuchumaa alafu kajiinamia chini.
Nilibinya break na kumpigia honi,aliinua uso na kumuona no eliza,nilishuka kwenye gari na kumfata pale chini,nikamuuliza we Eliza unafanya Nini hapa?unajua saiv ni saa ngapi?saa tano kasoro hii ebu amka uko kwenu wanajua uko wapi?
Nilimuuliza maswali mengi ila aliishia tu kuniangalia huku machozi yanamtoka,roho ya huruma iliniingia,nilimsogeza kifuani kwangu,nikatoa kitambaa mfukoni na kuanza kumfuta machozi,alilia mfululizo Hadi kwikwi ilimpata.
Nilimshika mkono na kumuingiza kwenye gari,nilijiona mkosefu Sana,niliweka gari hapo pembeni nikampa kitambaa nikamwambia haya futa machozi Kwanza tuongee,alifuta machozi ila kwikwi ilipiga mfululizo,nikachukua chupa ya maji ambayo ilikuwa ipo tu kwenye gari nikafungua nikampa anywe ili atulize hasira.
Alikunywa alipomaliza,nikamwambia Sasa Eliza haya nipo tayari nakusikiliza naomba utoe yote yaliyopo moyoni mwako,sema yote usiache hata moja ili moyo wako uwe na amani.
Akasema sawa,yule uliekua ukifanya nae mapenz ndani ni Nani?nikamwambia acha wivu bwana sijafanya nae chochote,akasema Fred kweli Mimi ni mdogo ila sio wa kudanganywa kiivo yani sijui kusoma hata picha tu nisione? Sio kweli.
Nikamwambia naomba uniamini lizy Wala sipo hapa kwaajili ya kuchezs na hisia zako ndio maana nikakuambia soma Kwanza,sikutaka kukuchezea ndio maana mala ya mwisho nilikuambia tu sina hisia
nawewe.
Kwani ilikuaje ukaja kwangu usiku wote huu?na ukizingatia unakaa na wazazi,akasema kesho nasafiri naelekea kahama kwa shangazi,hivyo niliambiwa nilale guest karibu na stand ili niwai kuamka maana bus itaanza Safari saa kumi na moja alfajiri,nikaona nije nikuage ndo nakutana na Mambo Kama haya nimeumia Sana kiukweli.
Nikamwambia pole Eliza Sina nia ya kukuchezea ndo maana moyo wangu haunisukumi kuwa nawe naomba tu uende kahama,tutaendelea kuwasiliana namba zangu si unazo akasema nnazo.na sim ulipata?akasema mama ndo amenipa jioni ya Leo kwaajili ya safari,nnayo nikamwambia basi sawa tutaongea,acha nikupeleke guest uliofikia ukalale saa sita hii,.
Niliwasha gari Hadi guest husika,nikampa na pesa kidogo nikamuuliza itakutosha?akasema Asante itanitosha Sana,ilikua ni elf 80.nikamwambia nakutakia safari njema msalimie shangazi,akasema sawa alishuka kwenye gari kabla ajafunga mlango akaniambia nakupenda Fred Kisha akafunga mlango.
Niliondoka Hadi kwangu,niliingia ndani nikaenda moja kwa moja chumbani,nilijiegesha huku nawaza,lile tukio seblen,nilijikuta naona aibu,nikasema hivi Mimi Fred nmekuaje?ah nikapotezea,nikapanda kitandani,nikachukua simu nitegeshe alarm nikakuta mesej ya evo,aliniuliza Kama nimefika kabla sijajibu alinipigia moja kwa moja.
Tukaanza kuongea tulipiga Sana story usiku ule akasema Fred nataman kusikia siku unasema Evo nitakuoa.nikamwambia usiwe na haraka wakati ukifika nitakua wazi kwako kwa kila kitu ila kwa Sasa bado mapema Sana,akasema ni sawa tuu naheshimu maamuzo yako.
Nikamwambia sasahivi natafuta wife material,kwaio nnasheria zangu nazifata ili uwe wife material,akauliza ni zipi hizo?nikamwambia iyo Sasa ni Siri yangu.tuliagana pale,tukalala,ilipofika asubuhi niliamka nilikuta missed call na mesej namba ilikua ngeni nilipoingia sehem ya meseji nilikuta inasema Fred mie Eliza hiyo ndo namba yangu tumeshaianza Safari ubaki salama.
Nikamwambia nakutakia Safari njema dogo,nikasave namba yake nikaandika ‘Dogo’.
Niliendelea na harakati zangu siku zikaenda mwez wa 12 ulifika shule zikafungwa,hapo Kati sikuweza kuonana na Evo sababu alipata msiba alienda kuzika kwao njombe,.
Kwaio hado shule zinakaribia kufungwa ndo akawa amerudi.tulipofunga tu shule,Jambo la Kwanza niliwaza kwenda mbeya,Kwanza kabisa nilienda kwaajili ya kumuona B,maana shule zikifunguliwa tulipanga aanze kusoma,pili kwenda kuwaona wazazi wangu,na tatu kabisa kwenda kufanya ibada ya sechelela na mama yake,.
Niliipanga hiyo safari,na Evo alikua ndio mtu wangu wa karibu Sana kwa kipindi chote hicho,huku Eliza nikijitahid kumpotezea,yani ongea yangu na Evo ni tofauti na nnavoongea na Eliza Kwanza siwez kumtafuta Eliza had anitafute yeye,ila Evo mala kwa mala nilimpigia simu.
Nilipomuaga kuwa nasafiri,Evo akauzunika akasema jaman unaondoka lini?nikamwambia nafikilia kuondoka kesho kutwa,akasema hapana subiri wiki ijayo utaondoka,nikamuuliza kwanini wiki ijayo na siyo keshokutwa?akasema nahitaji kuwa nawewe ili nikuage tukiwa pamoja walau tuutumie usiku mmoja pamoja,nikamwambia unaweza kuja hata kesho sababu hakuna ratiba inayokubana Kama shule zimefungwa.
Akasema sipo vizuri kiafya ndio maana nilikuomba usubiri wanawake tuna mambo mengi nipo mwezini,nikamwambia sawa,haya Mambo mengine Wala sio kuforce,usijal naenda ntarudi kwaio tutaonana tu ni lazima niwai nikamtafutie shule mwanangu.na Kuna ibada kwaajili ya marehem mke wangu.
Sikuwahi kumwambia kuwa B sio mwanangu siku zake zote alijua kuwa b ni mwanangu wa kumzaa.kesho kutwa yake nilisafiri Hadi nyumbani nilipofika nililala asubuhi na mapema nikaenda nyumbani kwa Kaka ake seche ambae anamlea b nilimkuta b amelala ameongeza uchangamfu na mwenye afya nzuri,nilifurahi kumuona vile,mjomba wake akamwambia B umemuona baba?
Alinifata na kukaa miguuni kwangu,akasema baba aondoka wote?nikamwambia nitakuja kukichukua mwezi wa sita mwanangu kwasasa nenda shule kwanza.nikamuuliza nikununulie Nini?akasema gari.nilimchukua Hadi supermarket nikamtafutia vitoy kibao vya kuchezea watoto nikamrudisha nyumbani,
Tulilaa sasa na kuanza kuweka Mambo sawa,nilimuuliza anko ake anhe tunafanyaje kuhusu uyu mtoto maana naona ameshachangamka Sana anahitaji kuanza shule,
Akasema Sasa hapa tumtafutie shule,ila mzigo usiwe wako wote,tutagawana nusu ada,nikamwambia usijali bwana mie nitalipa kila kitu jukumu lako wewe kubwa ni kumlea tu b ayo mengine yote niachie Mimi.
Kaka ake alikataa akasema tunasaidiana na sio kukomeshana nikamwambia Basi sawa.iyo siku tulifanya kazi ya kutafuta shule Hadi tukapata shule nzuri na ada zake pia haziumizi kwani unalipa kwa awamu.
Tulifanikisha ilo zoezi tukaandaa ibada ya marehemu,tulienda makaburini tukalimia majani tukaita mchungaji tukafanya ibada.nilifurahi kumuona baba seche akiwa anaendelea vizuri japo yupo kwenye Hali ya kupooza mwili hawez kutembea ila alikua ni mwenye furaha.
Wazazi wangu waliniuliza ni lini naoa,niliwaambia waniache Kwanza nitapokuwa tayari nitawaambia,mama alisema anataman kuniona namimi Nina familia Kama ilivyo kwa vijana wengine,nikamuahid kuwa mwaka unaofata nitaoa,akasema kila raheli mwanangu.
Nilikaa siku kadhaa nyumbani Kisha nikaondoka kurudi kwangu,njia nzima ya Safari nilikuwa nikiongea na Evo huku nachart nae,nilijikuta naangukia mapenzini kwake,alikua anajali Sana kuhusu Mimi,mwepesi kuomba msamaha akihisi amenikwaza kidogo.
Nilijisemea moyoni akiendelea hivi basi mapema tu nitamuoa,maana na wazazi nao wanataka nioe,nilipofika kwangu nilimwambia kuwa nimefika ila nimechoma Sana,akasema sawa kesho nitakuja nenda kaoge namtuma boda akuletee chakula.
Haikupita muda chakula kikawa kimeletwa na boda nilikula nikampigia sim kumshukuru,nilimuomba kesho aje kwangu,akasema siwezi kukosa lazima nije baby nimekumiss Sana,mda sio mrefu tukiwa kwenye mazungumzo nilisikia sauti ya mwanaume ikisema unaongea na nani Saivi?.
Nilisikia sauti ya Evo ikijibu no rafiki angu mama recho,Kisha akakata simu,aisee Mimi nishakua mama recho Hawa wanawake hapana.aikupita muda simu yangu iliita Tena nikapokea Safari hii aliongea mwanaume,akasema ni Mimi mme wa evo ni wewe ndo unaempa kiburi mke wangu???
WIFE MATERIAL 30
Simu iliita Safari hii nilipopokea nilisikia sauti ya mwanaume,akasema Mimi ni mume wa Evo,ni weww ndo unaempa jeuri mke wangu???nikamwambia Kaka samahani,tuongee the kistaarabu kwani huyo mwanamke sio mtu mzuri hakuwahi kuniambia kuwa ameolewa siku zote.
*
Yule mwanaume akasema Kama hakukuambia mie ni mpenzi wake Tena ni baba wa mtoto nilijisikia vibaya niliona Kama nimekua mwizi bila kujua,ilibidi tu nimwambie,mwamba naomba umsamehe mke wako lakini pia naomba unisamehe Mimi haya maisha tu yanachangamoto zake,Ila kaa na mke wako mwambie mambo anayoyafanya leo,atakuja kuona madhara yake baadae.
*
Yule mtu akasema kuwa na amani mie nitajua jinsi ya kumalizana nae nilichokupenda no mstaarabu nikamwambia asante.nilikata simu nilijihisi kutetemeka sana nilijiona Kama hii dunia imenielemea nikasema kwanini Kila siku Mimi?
Nikasema kwani Mimi nakosea wapi Sana Sana mbona Mambo nnayokutana nayo sistahili?nashukuru tu sababu sikuwahi kutana nae kimwili.ila nnahitaji kwenda madhabahuni kuongea na muumba wangu ili nijue wapi nakosea,na nifanye nini ili niweze kuvuka mitihani ninayokutana nayo.
Niliwaza kwa mda mrefu baadae nilipigiwa simu na Eliza,alikua akinipigia simu ni kunipa Salam tu bas akuna Cha zaidi ya hapo sababu alishajua kuwa simuhitaji kwaio alilizika na ile Hali ukizingatia yupo mbali mkoa tofauti na nilipo.
Alivipiga nilikata,nikafonya Kisha nikasema pumbavu nyie wote ndo wale wale tuu,.nilipokata alipig Tena na tena nikasema ngoja nipokee,nilipopokea akasema shikamoo teacher,niliitika akaniuloza za huko nikamwambia nzuri tu..vipi B anaendeleaje? B hajambo niliongea nae Jana,haya ukiongea nae Tena msalimie,nikamwambia poa,akasema vipi mbona Kama haupo sawa nimekuudhi kukupigia simu,?nikamwambia hapana nna Mambo mengi tu kichwani usiku mwema Asante kwa kunitafuta.
Nilikata simu nikaendelea kuwaza zaidi Kila ya neno niliongea Hadi nikasema huyu binti,alikua Malaya tu toka mwanzo tulipoonana kule kusimamia mitihan sijui ni ibirisi gani aluyenivuta kwake.anyway Kila kitu kinachotokea kina sababu zake.
Siku zilienda nikiwa naendesha maisha yangu mwenyewe nikasema mie huyu saivi nitakua kivuluge,acha iwe ivyo huenda ikanisaidia kumpata mwanamke wa ndoto zangu.yani ataejipitisha mbele ya macho yangu nitapita nae bila kujali ni Nani,na Wala sitamubifadhi moyoni ni mwendo wa kupiga na kuacha.
Niliendelea na maisha yangu,hukunikiendelea kuwasiliana na Eliza Kama mdogo wangu,sikuwahi kumtafuta hata siku moja ni yeye ndo ananitafuta Mimi asiponitafuta Basi umetoka iyo.
Siku zilienda shule zilifunguliwa,nilijichanganya Sana nilikua Niko na furaha Sana ni Kama sijawahi pitia changamoto zote nilizokutana nazo.
Mala matokeo ya kidato cha nne yakawa yametoka,,,kwa mala ya Kwanza nilimpigia simu Eliza,maana hata yeye alishangaa imekuaje?alipokea haraka bila kuchelewa akaniuliza kwema?nikamwambia ndio kwema nataka kujua tu matokeo yako ndio maana nmekupigia sim akasema mbona mie sijui Kama matokeo yametoka?ebu naomba uniangalizie Basi maana nilipo ni kijijini hakuna intranet cafe.wala simu yangu Haina uwezo.
Nilicheka Kisha nikamwambia unajiamin Mimi kukuangalizia matokeo yako?akasema angalia tuu nilisoma kwa bidii kwaajili yako.nikamwambia acha maneno nitumie iyo namba yako ya mtihani kwenye meseji nikakata simu.
Muda huo hip meseji iliingia nikakuta namba ya mtihani,niliingia mtandaoni na kuangalia sikutegemea nilichokiona yule binti mawenge yote aliyokuwa nayo hata mitihani ya shule hakuwahi kufauru vizuri Ila alipata division two ya mwanzoni kabisa.
Nilijikuta nnafuraha Kama amefauru mdogo wangu au nmefaulu Mimi sikuamini kabisa ilibidi nimpigie Kwanza simu kumpongeza.
Inaendelea………