WIFE MATERIAL 16
Basi nilimuacha pale seche huku moyo unaniuma Sana,kiukweli niliumia sana😔sikumtegemea Kama angeweza kunifanyia vile.kilichoniuma zaidi ni yule mtoto tuu,niliweka kichwani kuwa ni mtoto wangu na nilimpa upendo wa mwanangu niliumia Sana,nilimuonea huruma sababu maisha anayoenda kuishi ni maisha ya shida uyo mwanaume wake mwenyewe haeleweki,.
Niligeuka nikamwambia seche kwaheri,nilitoka pale Hadi kwangu.nilifika ndani nikajifungia nilishindwa kuzuia chozi langu la unyonge,nililia Sana.
Nikasema hivi Mimi nakwama wapi?mbona shida zote zinanizonga?hivi Mimi nnamapungufu gani?hawa wanawake mbona wanaishia kunitenda hivi?au siwalizishi?au siwapi Wanachotaka.ok basi sawa siwatimizii haha zao ndo waondoke kwenye maisha yangu na kuniachia maumivu kiasi hichi?
Kiufupi nilijiuliza maswali yasio na majibu.nilienda moja kwa moja kwenye kioo nikajiangalia na kusema mbona Mimi ni kama wanaume wengine tuu?sasa kwanini Mimi kila siku?hivi inabidi nitafute fundi wakuweza kunielekeza kuhusu mapenzi?
Kumbe hata ajali nilioipata ilitokea kwa sababu pale nilikua naepushwa kumuona huyu mwanamke.ningekua nimemuoa sijui ningekua nalia kilio gani sasahivi.kila kitu kinatokea kwa sababu nashukuru Sana kwa kuweza kuepuka hili swala.
Kwa siku hiyo sikuweza kufanya Jambo lolote,nililala asubuhi nilienda kazini kama kawaida,niliporudi jioni Jambo la Kwanza nilisema niwapigie ndugu zake ili niwape taarifa maana linaweza tokea Jambo baya alaf ikanicost Mimi.
Nilichukua simu yangu nikatafuta jina la mama seche nikapiga simu iliita……ikapokelewa,haloo baba b zauko?nzuri tu mama shikamoo.marhaba mnajisikiaje?…..aaah tunaendelea vizuri kwakweli,aaaa sawa mwanangu nafurahi kwa kuwa umenikumbuka asubuhi niliongea na sechelela akasema umeenda kazin,nikamwambia ndiyo mama.
Ila mama kuna shida hapa.mh!!!shida gani tena?seche nimempeleka kwa mzazi mwenzie….mzazi mwenzie ni Nani Kama sio wewe Fred mbona unanichanganya mwanangu?nikamwambia mama ni story ndefu ila ongea na mwanao atakuambia kila kitu,akasema sawa akakata simu.
Nilipotoka hapo nikampigia mama yangu nikamueleza kila kitu.kiukweli alishtuka sana akasema haiwezekani seche sio wa kukufanyia hivi.
Nikamwambia mama unatakiwa tu kuamini,akasema ngoja nitawasiliane nae kwanza.kweli nilipomaliza kuongea na mama nikampigia mama seche Tena nikamuuliza umeongea nae anasemaje???akasema nimeongea nae analia tuu haongei kitu,tusamehe Sana baba b seche ametutia aibu kubwa Sana sjui hata naweka wapi sura yangu.
Nikamwambia mama usijali huenda aikupangwa mim kuwa naye.akasema tutawasiliana zaidi,ila nimemwambia kesho namtumia nauli aje Kwanza huku nyumbani,nikasema sawa.
Kiukweli niliona aibu kuwaambia watu wanaonizunguka matatizo yangu,sababu nilijishusha thaman nikasema why me.
Siku zilienda ilipita wiki Sasa alinipigia simu mama seche akasema kuwa seche ametumiwa nauli na ajaenda nyumban na simu hapokei,nikamwambia subiri Kwanza aibu yake ipungue atakuja tuu.
Basi mie niliendelea na maisha yangu ya mawazo Sana sikutaka kujihusisha kwa chochote kwa kipindi hicho,niliwekeza akili yangu yote kwenye kazi yangu,nilikua bize Sana.
Naingia kazini saa 12:30 asubuhi saa 8:40 mchana tunamaliza vipindi natumia dakika 20 kula napumzika kidogo saa tisa nnaanza kufundisha wanafunzi tution hadi saa moja usiku.wakitoka hao saa mbili usiku kuna wengine wanakuja wale wanaolisiti napiga nao kipindi Hadi saa nne au saa tano usiku…nikitoka hapo nakua nimechoka sana nafikia kulala tuu.
Iyo ilinosaodia Sana kupunguza mawazo na kutokuwaza mwanamke mwingine tena.yalikua ndo maisha yangu Hadi walimu wengine walikua wananishangaa na kunicheka kuwa sieleweki ila nilisema hii ni Siri yangu wacha waongee.
WIFE MATERIAL 17
Niliendelea na maisha yangu ubize na Mimi,sikuruhusu kupata muda wa kupumzika mapema maana iyo ingenijengea kuanza kuwaza Sana.
Siku zilienda baadhi ya walimu walinibeza sana ila sikujali Wala nini,nikapata wazo Sasa la kuanza kujenga nilinunua kiwanja nikafanya ujenzi nilikua nikijenga taratibu,nyumba ilikamilika baada ya mwaka kuisha.
Muda wote huo sina mahusiano naona wanawake wote ni walewale tuu.nyumba yangu ilipokamilika niliingia bank nikakopa pesa nikanunua gari yangu Kali sana.nafanya hayo yote ilimrad tu kuwa bize na Mambo yangu.
Niliamia kwangu,licha ya yote hayo sikuacha kufundisha tution,wengi waonilijitolea tu kuwafundisha bure.maana niliamini kujichanganya na marafiki kuna ponza,sababu nishapata usaliti wa rafiki.
Siku ziliendelea kwenda maisha yangu bila seche kwakweli yalikua magumu kila nitapokumbuka kuwa B hakuwa mwanangu.
Kuna mtu alinipa taarifa kuwa kuna mahali huwa anamuona seche sio salama.nikamuuliza ni wapi?akanielekeza akasema nenda mida ya usiku lazima utamkuta,.
Siku iyo usiku mida ya saa nne niliwasha gari Hadi eneo la tukio,nikabinya break nikapark gari pembeni walinifata wasichana kibao kila mtu anataka niondoke nae,nilipiga jicho simuoni seche nikasema au huyu jamaa kaniongopea??
Baada ya muda kidogo naona wameongezeka wanne tena na mmoja wapo alikua nissche,akauli,s wenzake akauliza vipi huyu anaela au kaaja kutuchola!?,,,,,,
Seche Alivaa nguo fupi sana mwili wote ulijichonga niliisi kutetemeka,muda huo yan seche ajajua Kama ni mimi nkamwambia nmekipenda sana we dada mwenye gauni nyekundu kujibu hivyo tu seche alitaka kufungua mlango aingie,nilimwambia kaa hapo nyuma.sikutaka anifahamu kuwa ni Mimi kwa kipindi kile.
Na sauti nilibadilisha,nilienda Moja kwa moja had kwake nilipompeleka siku ya kwanza kwa bwana wake,Kisha nikawasha taa ndan ya gari nikiwa nimempa mgongo nikamuuliza bei gan kwa siku?
Akasema bao moja ni 10,000 nikamwabia sawa,akasema twende basi hapa sio sehemu salama ni karibu na kwangu,.nilimgeukia na kumtazama🙄aliishiwa nguvu,alishtuka akasema ni wewe Fred nikamwambia yes ni Mimi.
Aliona aibu Sana,nikamwambia seche haya unayoyafanya hutakiw kufanya mbona umebadilika kiasi hicho?mtoto umemuacha na Nani ww unafanya ujinga huu,
Seche wew wa kuvaa nguo nusu utupu hapana.naomba ubadilike kwa faida yako na mwanao,inakuaje uyo mwanaume anakuruhusu kwenda kujiuza seche?wew wew bado mtoto mdogo Sana hayo unayofanya leo lazima utakuja kujuta baadae.
Alinijibu kuwa usiniletee maubili kwenye maisha yangu fanya yako tusipangiane,nilimuangalia sikummaliza nikamwambia haha kwaheri naomb ushuke uende ndani,na nitampigia simh mzaz wako ajue ujinga wako.
Akasema sawa Haina shida mwambie siwez kuogopa binadam chini ya jua alitoka ndani ya gari akabamiza mlango akaondoka.
Nilipata mawazo Sana nisijue namsaidiaje niliumia sana kiubinadamu,niliweka kando Mambo yote ambayo alinifanyia hapo nyuma,nilikaa kwa muda mrefu pale bila kuondoka nikiwa nawaza namsaidiaje,kuja kuangalia saa ni saa sita usiku.
Niliwasha gari nikaondoka pale nilifika kwangu lakin niliwaza wazazi wake wapate taarifa kwanza.nilichukia simu gangu nikampigia mama,alipokea lakin alishtuka Sana…vipi baba B mbona usiku hivi??kiukwelk walizoea sana kuniita baba b hata walivojua kuwa mtoto sio wangu.
Nikamwambia mama nisingeweza lala kweny hii hali akaniuliza shida nini?nikamwambia mama seche anajiuza,.mama alishtuka sana akasema nimejuaje?nikamueleza kila kitu ilivokua akasema sawa kesho nitaenda kwa mama yake kumpa taarifa nikamwambia sawa usiku mwema mm sijaweza kumpigia moja kwa moja sababu ni usiku Sana sasa.
Basi nililala asubuhi na mapema nikaenda kazini kwangu mida ya saa tatu asubuhi simu iliita nikapokea ni mama seche,tuliongea pale akaniuliza kila kitu nikamuelekeza,.
Akasema sawa nashukuru isipokua seche nimeshamtumia nauli kama mala nne aje nyumbani lakin anakula pesa na haji.nikamwambia mama wewe ni mzazi inabid umuokoe mwanao naomba ufunge Safari uje umchukue maama amefika stage mbaya.
Mama yake akasema mie siwez kuja huko sababu baba yake anaumwa sana amepalalaz hajiwezi Mimi ndio kila kitu namsaidia kwaio itakua ngumu hiyo ndio Mana huwa namtumia nauli mala kwa mala aje lakin hataki.
Nikamwambia mama sawa nipatie namba zake niongee nae,najua jinsi ya kuweza kumfanya arudi tu nyumbani.
Kweli mama yake alinitumia namba nikampigia tuliongea nikamdanganya kuwa nataka tuludiane nimuoe sitaki kumchezea,nilijuta niliishia kutukanwa matusi makubwa makubwa na akapewa simu uyo muhuni wake naye akanitukana.
Siku zilisonga nikawa nimempotezea,ilipita kama miez mitatu alinipigia simu huku analia Fred nisaidie nikamwambia kulikoni?akasema nimepigwa na huyu mwanaume ataniua,nikasema yes kimoyo moyo!huu ndo wakati mzuri wa kumsafirisha kwao.
Nikamwambia usiteseke naomba uje kwangu ili nijue jinsi ya kuweza kukusaidia,akasema awezi kutoka kafungiwa ndani ila nimtumie pesa ili aweze kumuagiza mtu dawa akipata nafuu atakuja.nikamtumia pesa ndogo tuu 10,000 baada ya kutuma tuu ilipigwa simu nkapokea ni mwanaume akasema unaongea na baba B hapa Asante kwa kututumia pesa ya kuvutia bangi.wakaanza kucheka wote mwanamke na mwanaume.
WIFE MATERIAL 18
Kumbe walikua wananichora na bwana ake lengo lao wapate pesa,nikasema acha tu nimpotezee atajua mwenyewe ndo maisha hayo aliyoyachagua.
Niliendelea na mambo yangu,sasa kuna wanafunzi wa kidato cha nne nilikua nawafundisha tuition,una uyo mwanafunzi mmoja wakuitwa Elizabeth,yule mtoto alikua anajilengesha sana kwenye mitego yangu.
Yani akija tution mala kavaa shati vifungo wazi basi kifua chote nje,najitahid kujizuia muda mwingine akikaa kapandisha nguo juu mapaja yote nje basi ni taflani.
Nilijizuia namm nilishakaa muda mwingi bila mwanamke nikasema hapa uyu ibilisi ananinyemelea nikafikilia Kwanza mtoto mwenyew mwanafunzi atanipa kesi.
Ilibidi sikuiyo nimkatae mbele ya wenzake katikati ya kipindi ili ajieshimu.nilimwambia wewe Eliza naomba ujiheshimu kaa vizuri sitaki masihala kweny kipindi changu.alinywea gafla akakosa amani.
Ilikua ni njia nzuri kwangu siku ziliendelea kwenda yapata miezi mitatu siku iyo simu yangu iliita namba ni ngeni kupokea nilisikia sauti ikitoka kwa tabu sana,nikamuuliza wewe Nani?akasema Mimi ni seche nisaidie,moyo uliluka paaaah,,,,nikamuuliza seche shida nini.??
Akasema naumwa sana,nikamuuliza uko wapi?akasema nipo uliponipelekaga siku ya Kwanza,nikamwambia ok nakuja saivi,niliwasha gari moja kwa moja hadi kwake niliuliza hapo nje nikaambiwa niingie uko ndani,nilimkuta seche kalala hapo hajiwezi,.
Mtoto yupo pembeni nae kalala tuu,nilimbeba juu juu Hadi kwenye gari nilimpandisha nikamrudia na mtoto moja kwa moja Hadi hospital.
Alichukuliwa vipimo vyote baadae doctor anakuja kuniambia mbona mmemuacha muda mrefu bila dawa huyu?nikamuuliza dawa gani?akasema ameathirika!!!!
Nilishtuka sana nilikaa chini nguvu ziliisha ilibidi nimuombe ampime na mtoto,
WIFE MATERIAL 19
Basi,doctor alisema kuwa ameathirika,moyo uliniuma Sana,maana nikajihisi hata Mimi naweza kuwa nimeathirika.
Nikamwambia doctor naomba mpime na huyu mtoto,kwa kipindi hicho alikua amekua kua mtoto anatembea mwenyew ni Kama anamwaka na nusu au zaidi.
Doctor aliniuliza ni Nani yako huyu?nikamwambia ni mke wangu.akasema pole sana,sasa siku zote hamjui Kama mnaishi na maambukizi?nikamwambia doctor we acha tu ni story ndefu Sana.
Ikabidi nimchukue mtoto na Mimi wote nikamwambia atupime,niliwaza labda wakati anaondoka kwangu aliondoka nao.
Tulipimwa,tukatoka nje tukiwa tunasubiri majibu,nikampigia simu mama yake seche,hapo mwili wote unanitetemeka,meno yanagongana.nilimsalimia nikamwambia mama seche anaumwa sana.
Mama yake akasema shida nini?nikamficha Kwanza,nikamwambia ndo nimemleta hospital saivi anachukuliwa vipimo pia kapewa kitanda.akasema sawa basi utanipa taarifa ya maendeleo yake.
Nikakata simu nikaenda tena chumba cha daktari kuchungulia,akasema bwana Fred ingia tuu,nikaenda Hadi ndani nikaketi,akaniambia majibu yametoka ila upo tayar kuyapokea?nikamwambia doctor nipo tayari ila sitaki uongee Mambo mengi sana nataka kujua tu ninao au sina?
Doctor akasema hongera upo salama na mtoto yupo salama ila ujitahidi baada ya miezi mitatu upime tena.nikamwambia hapana siwez kupima tena sababu huyu mwanamke Mimi sijakutana nae muda ni mrefu Sana umepita,akasema sawa je mtoto ananyonya?nikamwambia Wala sijui.akasema kama ananyonya basi kwanzia leo asinyonye tena.
Nilimuaga doctor nikarudi nyumbani pamoja na mtoto nilimpatia chakula akalala,ilipofika asubuhi niliamka mapema nikaandaa uji nikampa mtoto akanywa mwingine nikaweka kwenye chupa kwaajili ya mama yake hospital.
Nilitoka moja kwa moja Hadi kazin tukiwa njiani B akalala ilinibidi nimuache kweny gari nikafungua vioo ili hewa ipite ndani Kisha nikaenda ofisini,nikadanganya kuwa naumwa Sana hivyo nimekuja kuchukua ruhusa niende hospital.
Nilipopata ruhusa nikaondoka hadi hospital nilikuta hali yake bado ni mbaya zaidi tena alifunga na kauli.nilipiga simu kwa mama yake sasa ilibidi tu niwe muwazi nikamwambia kuwa mwanao ameathirika na hakuwa akitumia dozi ndio maana kazidiwa,yawezekana alikua hajui Kama ameathirika.basi mama ake akaanza kulia,nikamwambia kulia sio solution inabidi tufanye jitihada za kujua tunamsaidiaje.
Basi,mama ake akasema anampigia simu mwanae wa kiume pamoja na mke wake waje wakae na baba yake ili yeye aje.basi kesho yake mapema tu akawa amefika mama seche.
Akimuangalia seche kaisha hawezi hata kuongea basi mama yake analia tuu.ilipita wiki akapata nafuu,na aliweza kuruhusiwa sasa nyumbani.
Baada ya kuruhusiwa tuu nikamwambia mama yake waje tu kwangu alaf wajipange sasa waondoke kwenda huko nyumbani…ilibidi tu aelezwe hali harisi ya afya yake kuwa ameathirika,jambo la kwanza alitaka kujua kuhusu mwanae,,tukamwambia mtoto ni mzima kiukweli alisikitika na alinigeuzia lawama zote mimi.kwanini nimemwambia mama yake kua ameathirika?
Nikamwambia seche hukuwahi kunishukuru iwe kwa kidogo ama kikubwa.bila Mimi kuja kukuokoa ungekufa wewe.hakujali kabisa.
Mama yake akamwambia sawa basi jiandae kesho tuondoke uende nyumbani ukaugulie uko hadi afya yako itapokaa vizuri.seche alisema mama bora umekuja utaondoka na B mie siendi kokote siwez kaa mbali na baba B.
Hee seche unataka kufia mikononi mwa wahuni?kelele Fred usimuite mzazi mwenzangu muhuni.mie tena mdomo koma.nikamwambia sawa haina shida ila lolote litalokutokea kwanzia sasa sitahusika kwa chochote.
Akasema vyovyote utavyoamua nipo tayar usinitishe,mama yake akamwambia kama Mimi ni mama yako tutaondoka wote ila kama sio mama yako basi we baki tuu hapa hapa.
Unaacha kuishi na kijana mzuri mwenye akili na upendo unabaki kutapatapa kama mfamaji…basi mie sikutaka kuingilia tena majibishano yao niliingia ndani kwangu nikatoka na kiasi cha pesa nikamwambia mama hii 50,000 ya nauli wote wawili na hii 50,000 nyingine itatumika kula njiani na emergency yoyote itayojitokeza.
Kisha nikaingia tena ndani kwangu.asubuhi kabla sijaamka nilisikia hodi ikibishwa ndani kwangu nikajua ni mama tu anataka kuniaga,nilitoka nje nikamkuta ni yeye mama seche amembeba B mgongoni nikamwambia mama mpo tayar niwapeleke stand?akasema ndio nipeleke isipokua huyu seche ameshatoroka hayupo hapa atakua kaenda uko kwa mzazi mwenzie.
WIFE MATERIAL 20
Nilitikisa kichwa nikasema seche ni sikio la kufa,mama ake akadakia “halisikii dawa”
Nikamwambia mama kwaio tutafanyaje?akasema muache tu licha ya kujijua yupo na matatizo lakin bado anataka kuendelea kulanda landa,mie naondoka na mtoto kama ataona kuna umuhimu wa mtoto pale atapomkumbuka basi atakuja kumuona mwanae.
Yani kiukweli niliumia namuonea huruma sana hali aliyonayo hakupaswa kanisa kuangaika hovyo,mama akaingia ndani kutoa vitu vyake namim nikajiandaa nikatoka tukaelekea stand nikamuaga nikamwambia mama kwa tatizo lolote utanitafuta kwenye simu kuhusu b kama baba yake hatoudumia basi hilo jukumu nitalichukua Mimi la kumlea.
Yule mama aliniaga lakin akiwa niweny huzuni sana.alipopanda tu bus,mie nikamuacha nikaondoka njiani nilisikia sauti ya meseji sikufungua,nilipofika shule nikafungua ile meseji kumbe n mama seche,ilisomeka hivi
“Asante kwa kila kitu Fred mwanangu kiukweli matendo ya binti yangu yananifanya Mimi naona aibu,nisamehe sana.”
Nilimwambia usijali mama haya yote ni sehemu ya maisha ya bunadamu,unapoenda nyumban kazana tu kumuombea mwanao atoke kwenye kifungo alichopo pia muombee aweze kuponywa ugonjwa alionao.
Nikiwa kazini mida ya mchana mama seche alipiga sim akasema kuwa ameshafika,isipokuwa tu mtoto ndo anasumbua anataka mama ake,nikamwambia huyo ni mtoto atazoea tu na atamsahau mama ake kabisa.
Siku zote za kumuuguza seche hata tution nilisitisha kwanza sababbu nilikua bize mno,ila iyo siku nilizunguka madarasa yote na kwenda kuwatangazia kuwa kwa sasa nipo free wananweza tu kuja tution.
Mchana nilirudi kwangu na wanafunzi wakaja tution kama kawaida.niliwafundisha lakin kwa uchovu sana nilikia nimechoka mno,nikawapa exercise nikawaambia naomba nikapumzike kidogo baada ya nusu saa nitarudi hapa,
Nilielekea chumbani kwangu nikiwa nimechoka mno,nilipofika tu nikasema ngoja niwashe radio ili inipigie kelele nitalala kidogo,ila nisipowasha kutakua na utulivu Saba nitalala mda mrefu.
Nikapanda kitandani haikupita hata dakika nikachukuliwa na usingizi mzito sana.nikiwa kama nipo ndotoni nilihisi kama kuna mtu ananishika na kunipapasa,niliposhtuka nilimuona yule mwanafunzi wangu anaitwa Eliza niliowahi kumkataza kujilengesha kwangu.
Nilikurupuka nikamwambia wew si nmekupa kazi huku umekuja kufanyaje,na umeingiaje ndani kwangu bila ruhusa yangu?akasema samahan sir,ila kiukweli nashindwa kujizuia kwako nakupenda sana,nikasema shit!!!usiniletee kesi we mtoto mwanafunzi.
Nikamsukuma huko nikaenda moja kwa moja mlangoni nia nifungue mlango nimtimue nje,lakin sikufanikiwa nimekuta mlango umefungwa kwa ndani.
Nikamwambia Eliza acga mchezo mchafu nitakuripot kwa uongoz wa shule sababu mwalimu mkuu amenipa kibari cha kuwafundisha na anajua mpo sehemu salama.
Nikamwambia umeweka wapi ufunguo?akaanza Julia ticha nipende nakupenda sana na usipokubali kulala na Mimi najiua🙄nikamwambia usinitishe jiue tu hiv wenzio wakijua upo humu ndani unazan utanijengea picha gani?
Akasema awawez kujua niliaga naondoka nimetoka had nje ya geti ila nikazunguka nyuma nimeruka ukuta hadi kuingia humu ndani.
Maana mie huwa nawafundishia nje kuna room nilijenga nikaiweka na ubao.kwaio kazunguka kafanikiwa kuingia ndani sijui hata chumba nnacholala mm kakijuaje uyu mtoto.
Nilichukua simu nikamtisha nataka kumpigia mkuu nimueleze,lakin alitoa pakti kwny sket yake Kisha akasema sir najiua,kuangalia hiv ni sumu ya panya,nikamwambia Eliza mbona unanipa majaribu sana?akasema naomba nitimizie,duh.
Inaendelea……