WIFE MATERIAL 11
Nilimuuliza seche baada ya kutoka kanisani huwa unaenda wapi?naomba useme ukweli maana laa sivyo nitawapigia simu wazazi wako pia nitakupekeka kanisani uende ukaongee mbele ya kanisa.
Basi akasema usifanye hivyo nipo chini ya miguu yako muda huo amepiga goti,Huku machozi yakivuja kifuanii kwake.Akasema Fred nisamehe mpenzi wangu,najua Itakua ngumu Sana kwako kuniamini Ila ukweli ni kwamba nikitoka kanisani huwa napita kwa rafiki yangu mwanakwaya mwenzangu tupo wanne,huko huwa tunaenda kuendeleza mazoezi ya kwaya.
Nikamwambia Sasa kulikua na umuhimu gani wa wewe kunificha???akasema nilijua usingeweza kukubali Mimi kufanya kazi za kanisa Hadi usiku.nikasema ok unaweza kunipeleka huko kwa uyo rafiki yako?akasema ndio nikamwambia nisubir naenda kuvaa nguo twende.
Niliingia chumbani nikabadilisha nguo wakati natoka nje sikumkuta seche ukumbini nilitoka moja kwa moja Hadi nje nikamkuta anaongea na simu ila baada ya kuniona alikata haraka Sana akawa Kama mtu mwenye wasi wasi Sana.
Nikamuuliza ulikua unaongea na Nani sechelela?akasema huyu rafiki yangu wa kwenye kwaya alikua ananiuliza Kama Leo nitaenda au sitaenda.
Niliichukua simu yake kuangalia nikakuta kweli ni jina la kike nikamwambia mpigie mwambie nakuja kwako saivi.
Alitii amri bila shuruti,alivopiga aikuchukua muda ikapokelewa sauti ilikua ni yajuu kabisa,akamuuliza uko wapi nataka kuja kwako.sauti upande wa pili ilijibu nipo nyumbani.nilikata simu nikamwambia twende.
Tuliianza safari ya kwenda kwa uyo rafiki yake,Wala sio mbali na nyumbani.tulipofika alibisha hodi yule binti akatoka ndani alitukaribisha ila nikamwambia Mimi siingii ndani Asante Ila nnashida na wewe.
Akasema ndio shemeji karibu nakusikiliza,nikamwambia baada ya kutoka mazoezini kanisani huwa seche anaenda wapi?akasema huwa nakuja nae kwangu na wenzetu baadhi kuendelea na mazoezi.
Kistaarabu kabisa nikamwambia ooo sawa nashukuru,ila kwanzia Leo siitaji tena mke wangu aje kwako Hadi usiku akasema sawa nimekuelewa.nilimtakia jioni njema tukaondoka na seche.
Tulipofika nyumbani nilipitiliza chumbani nikaenda kujitupa kitandani nilijilaza huku macho yanaangalia juu ya paa,nilijikuta tu moyo unajaa uoga na wasi wasi,nikasema hichi Nini kinataka kutokea Mambo ya Natasha yasije kujirudia hapa mbona najiona Kama Sina bahati??
Nilijiuliza maswali mengi kidogo akawa amekuja seche nikiwa nimelala chali alilala pia juu yangu akasema unawaza nini Fred??nikamwambia nakuwaza wew nna hofu kubwa Sana Kama ikitokea umebadilika.
Akasema Fred nimewaacha wazaz wangu nimekuja kwako ni sababu nakupenda.nikamwambia nakupenda pia,na Kama unanipenda naomba unisikilize nitachokuusia,akasema sawa nikamwambia Kwanza nipo na ombi moja kwako naomba uache kwaya Kama unanipenda kweli,iyo inamaanisha kwamba muda wowote nitaporudi nyumbani nitegemee kukukuta.akasema iyo Haina shida kwakua nakupenda.
Basi nilimshika kichwa nikamkiss niliona nimepata mtu muelewa na mwenye kupenda kujishusha Sana.usiku ulipofika Alinipa zawadi ya kitandani ikiwa ni sehemu ya yeye kukiri kile alichokifanya hadi kuniuzi,tulifurahia kuunganisha miili yetu,tulipomaliza tukapata usingizi mzito Sana.
Asubuhi na mapema aliamka Kama ilivyo kawaida yake,alinipikia chai alipasha maji Moto naa kuniandalia nguo zangu za kuvaa aliniandaa vizuri na kuhakikisha naenda kazini nikiwa nipo Safi kabisa.aliniaga kwa kiss zuri la mdomoni likisindikizwa na maneno matamu ya kufanya kazi kwa bidii.
Nilienda kazini nilipofika nilishika simu yangu na kukuta meseji ya seche ikisema nakupenda Sana honey nakutakia Kaz njema uwe na afya njema wa moyoni mwangu.
Basi nilifurahi Sana nikamjibu ubaki salama nakupenda pia babe.nilipata amani moyoni,nikiwaza na shoo nilizopewa usiku ndo nilizidi kuvulugwa.
Ikumbukwe siongei na Abel toka nilipogundua kuwa ni msaliti wangu,. Nikiwa darasani kweny kipindi alikuja madam mmoja anaitwa Anna akasema sir vipi nikamwambia poa!akasema kipindi bado Sana?nikamwambia Amna nawaandalia vitu kwaajili ya practical akasema sawa utapomaliza Nina mazungumzo nikamwambia sawa.
Nilimaliza kazi yangu nikamfata,nikamwambia enhe nambie madam anna.akasema hivi wewe na Abel amuongei kwanini?wakat ni watu mliopendana Sana stuff nzima? Nikamwambia kawaida tuu ni Mambo ya kawaida.
Akasema au mmegombana kisa mwanamke?nikamwambia ndio umejuaje??akasema mke wa Abel ni rafiki yangu na ameniambia kuwa Abel kwa Sasa anaishi na natasha,kwani Natasha mliachana?nikamwambia ndio imeshakua muda Sasa.
Akasema ndo ivo Basi Natasha ni nyumba ndogo ya Abel kwa sasa.aisee jaman😔
WIFE MATERIAL 12
Madam Anna aliniambia mengi Sana kuhusu Abel.niliishia tu kumsikitikia nikamwambia jamaa mie nashindwa kuelewa kwanini aliamua kufanya haya yote Hadi hivi Sasa.
Nikamwambia madam Anna kuwa kwanzia Sasa sihitaji Tena kusikia habari zake huyu Abel,maana Kila siku vihoja vyake vinazidi,na nikionana nae huwa ananikwepa sana.
Basi niliendelea na maisha yangu siku zilisonga seche aliacha kwenda kanisani mapenzi yalikua motomoto mke mtiifu ananipenda nakunijali nilijikuta najiachia Hadi ubonge ukaanza kunisogelea.
Mipango ya sherehe ilipangwa vyema,tulijuandaa na harusi,ndoa ilitangazw kanisani,mipango yetu ni kwamba tupate mtoto ndani ya ndoa,inamaana Hadi tutapofunga ndoa ndo tuanze zoezi la kutafuta mtoto.
Tulikubaliana hivyo na mzunguko wake aliushika yeye mwenyewe seche inamaana akiwa siku hatarishi kupata ujauzito huwa ananiambia kabla atujashiriki Mimi nnajua jinsi gani ya kuweza kuzuia Hilo swala.
Siku zilienda ilibaki Kama wiki tatu hivi tufunge ndoa,siku iyo nikiwa kazini seche alinitumia meseji.babe unarudi saa ngapi?nikamwambia muda sio mrefu Kwan Kuna shida?akasema hapana Ila ukija njoo na fenesi,mh!!!wewe na fenesi wapi na wapi seche?akasema niletee tuu babe nimeyamiss nikamwambia sawa nakuja nayo.
Kweli nilipotoka kazini niliingia mtaani nikamchukulia alichoagiza nikampelekea alikula sana,tukatenga chakula tukala.
Basi ilikua ndo tabia yake Kila siku anataka nimletee fenesi.siku nyingine nikiwa kazini tena,alinitumia mesej babe namm nimeshamjulia akiandika babe najua anataka fenesi,nikamwambia nakuletea mke wangu.akasema unaleta nn?nikamwambia fenesi,akasema Mie leo sitaki fenes ila uwai kurudi mie naumwa.
Nikamwambia meza Panadol upumzike nitarejea hivi punde.muda wa kazi ulipoisha nilienda kwangu ndipo nikamkuta toka alivolala asubuhi ajaamka nyumba yote chafu na sio kawaida yake.
Nikamwambia amka twende hospital,aliamka tukaenda hospital alichukua vipimo vyote maana alilegea akasema kichwa kinamsumbua sana.alipima vipimo vyote baada ya majibu kutoka,doctor alimuita ndani akamuuliza umekuja na Nani?akasema nimekuja na mme wangu akasema muite.
Seche alitoka nje akaja kuniita,babe doctor anakuhitaji nikamwambia sawa.niliingia ndani tuliketi doctor akasema mke wako nimempima hapa Hana tatizo lolote isipokua anaujauzito,
Mh!!!ilikua surprise Sana kwangu kwani sikutegemea kwa kipindi hicho,doctor akasema vipi nyie wote wawili mmekunja uso amjapenda kuitwa wazazi??nikamwambia hapana doctor ila haikua kwenye plan zetu ilo swala.Doctor akasema watoto ni baraka Kama mlipanga au kutokupanga inabidi tu mlipokee kwa mikono yote miwili,nikamwambia akuna namna.
Tuliondoka Hadi nyumbani,tulipofika nilimuita chumban seche nikamwambia Sasa ilikuaje adi tukateleza hivi??akasema hata yeye aelewi itakua alifanya hivyo akijua kamaliza hatari kumbe bado.nikamwambia sawa Cha muhimu kwa Sasa tujue tunafanyaje??
Akasema nakusikiliza wewe.nikamwambia ndoa inakaribia Cha muhimu ni kwamba ujitahidi Sana uepuke kuumwa umwa mala kwa mala ili Jambo letu lipite salama…akasema sawa.
Kwaio nilichokifanya nilimwambia awape taarifa kwao pia na kwetu na akafanya hivyo.mama alichokisema haitaathiri kitu kwakua ujauzito ni mchanga na siku za ndoa zimekaribia.
Basi nilimuandaa nikamwambia atangulie nyumbani Mimi nitakuja siku mbili kabla ya ndoa.basi akawa ameenda kuweka Mambo sawa,wakawa wamemuandalia na kitchenpart kwao walimfanyia.mchungaji wa kule nyumbani aliniambia niombe ruhusa niwai mafundisho kanisani ya ndoa walau siku tatu.kwaio nilijiandaa ilikua imebaki wiki moja ili niweze kuoa.
Mke wangu niliendelea kuwasiliana nae vizuri huku tukifurahia kuwa wazazi siku zijazo,nilijiandaa na safari…asubuhi na mapema nilikata ticket ya bus la saa 12:00 Nia yangu niwai kufika nyumbani,nilimuwaza Sana cha upole wangu seche kwani nilikua siwez kabisa kukaa nae mbali.
Njia nzima nilikua nikiongea nae kwenye simu huku tunachart,sikupata hata muda wa kuweza kuzoeana na abiria mwenzangu ambae alikua amekaa pembeni yangu.safari iliendelea Hadi tukamaliza nusu ya safari yetu.
Tulifika mahali tulishuka tukala tukapanda Tena bus,lakin safari ikiwa inaendelea dereva alizidisha mwendo Kasi Sana,yani alitupelekesha Kama vile hajabeba roho za watu.kitendo kilichopelekea abiria ndani ya Basi tukaanza kumsema kwa kumwambia apunguze mwendo.
abiria mmoja alimfata akamwambia punguza mwendo acha ku ovatek utatusababishia ajari.dereva alichomjibu ni kwamba nikiwasikiliza nyie abilia hatuwezi kufika kwa wakati Basi aliongeza speed,nilipata wazo ya kuangalia kwenye vioo vya Basi nikaona namba zile za usalama barabarani nilizichukua nikapiga na abiria wengine nao wakapiga baadhi.
Haikupita muda Basi lilikua liki ovatek roli la mafuta liliacha njia likaenda kuivaa Costa ilikua imebeba abilia baada ya hapo tulijikuta tayari tupo chini,kuangalia kushoto na kulia nilisikia sauti za watu wakilia huku wakisema huyu mzima,Ila Kila nilipotaka kuamka nilishindwa sikusikia maumivu yoyote ila mwili ulijaa ganzi,na damu zilivuja Sana niliona nimechanika Sana eneo la paja damu zinatoka nyingi eneo la kichwa,nguo nilizovaa zote zimechanika nilichanganyikiwa kwa kweli hata niliokua nayaongea hayakuelezeka.
Watu wengi walikufa na walifunikwa nguo ikiwemo konda wa Basi Hilo ambae alishadadia kuwa dereva ongeza mwendo tuwai kufika mapema usisikilize abiria,.
Yalikuja magari ya serikali pamoja na ambulance tulibebwa haraka na kupelekwa hospital.kwanzia hapo nilipoteza Tena fahamu na sikuweza kuamka kwa mwezi mzima.
WIFE MATERIAL 13
Baada ya kupata ile ajari mbaya sikuweza kuelewa tena ni kitu gani kiliendelea ila nnachokumbuka nilijihisi Kama nimelala ghafla nikasikia sauti ikisema katingisha vidole,
Nikiwa nimefumba macho kila nikijaribu kuhisi ile sauti ni ya Nani nilikosa jibu.nilijitahidi kufungua macho ila nilishindwa.basi nikasema acha nijitahidi kuongea niweze kuwasiliana nao lakini pia nilishindwa kufungua mdomo.
Basi nilinyamaza tu kimya nikiwa najiuliza kwani nipo wapi na imekuaje Hadi nimefika hapa sikupata jibu lolote.
Nililala tuu ila yote yaliyoendelea niliyasikia.nilisikia sauti ya mtu mmoja ikisema ndugu wawili ingieni mje mumgeuze fred.hisia kama nageuzwa nilizipata ila siwez fanya chochote.
Muda ulienda nilipata usingizi nalala naamka ila kufumbua macho ndo nashindwa.kuna muda nilisema hapana sitakiwi kuwa kwenye maswali yasio na majibu Imani yangu leo nijue kila kitu nilijitahidi kutingisha mikono nikafanikiwa kinyanyua mkono mmoja juu.
Niliupeleka mkono huo Hadi sehemu ya uso nilipojipapasa niliona puani had mdomoni nnakitu sio cha kawaida,nilikivuta kwa nguvu baada ya kufanikiwa kukitoa niliona pumzi inakata kama nataka kuzimia.
Niliangaika Sana baada ya muda nilisikia watu wakiongea huyu ametoa mashine na hali yake bado mbaya hawezi kupumua kwa kujitegemea mwenyewe.nilisikia tu jitihada zao na wakinishika sehem ya usoni baada ya muda nikaona nimeanza kupata Tena hewa vizuri.
Nilikaa kwa muda furani nikafanikiwa kufumbua macho,nilijikuta nipo kwenye chumba chenye vitanda vitatu,viwili vina watu ambavyo ni Mimi na mwenzangu mmoja icho kitanda kimoja hakikua na mtu yoyote.
Sasa nimefumbua macho kuongea siwezi mdomo mzito sana nikaona nesi mmoja yupo kwenye kiti hapo pembeni anaendelea na shuhuli zake anaandika andika.aliponyanyua uso wake akakutana na Mimi namuangalia,alishtuka ila akuniongelesha chochote alichukua simu ya mezani akapiga Kisha akasema mgonjwa ICU ameamka.
Baada ya muda mfupi aliingia doctor mmoja akaniuliza unaona vizuri?sikumjibu nilimuangalia tuu.baadae akasema uwezi kuongea?pia sikumjibu,akasema jaribu kutumia kichwa chako au mikono kunijibu kwa ishara.
Basi akaniuliza tena unaona?nikamtingishia kichwa kwa ishara kuwa naona vizuri.akasema sawa unaweza kuongea?nikatingisha kichwa kuwa siwezi kuongea.
Alitoka na baada ya muda mfupi nilisikia nesi akisema inabid mzazi wake aruhusiwe kuja kumuona mwanae,.mama alikuja nikamuangalia naona kabisa huyu ni mama lakini kuhusu kufikaje ndo bado sielewi.mama aliniangalia Kisha akaanza kulia.
Alitoka nje kwa uchungu Mimi sielewi kitu iyo siku iliisha kesho yake sasa nilihisi kiu Sana nikajikuta nasema tuu maji maji maji,kha nimeongea.
Alikuja nesi akasema nimeweza kuongea muda huo nimetolewa na mipira ya kupumua nikawa natumia pua zangu kupumua na nilifanikiwa.
Niliondolewa kile chumba nikapelekwa wodi nyingine,nikawa naongea japo kwa shida Jambo la Kwanza nilimuuliza mama seche yuko wapi?akasema tulia anakuja muda si mrefu.nikamuuliza mama nimefikaje hapa?akasema ulipata ajali ya basi ni mwezi na nusu Sasa umepoteza fahamu uelewi anaoingia Wala anaetoka siku mbili zilizopita ndo ulifumbua macho kwa mala ya Kwanza hapo ndipo nikavuta kumbukumbu na nikakumbuka kuwa nilipata ajari ya basi.
WIFE MATERIAL 14
Nilimuuliza mama kwani nimeumia Sana?akasema kwa Sasa pumzika Kwanza tusubiri tamko la Doctor,nikamwambia sawa.
Baadae doctor alikuja akaniangalia alinihoji baadhi ya maswali akasema tuangalie Kwanza Kama kutakua na uwezekano wa kuanza mazoezi ya viungo hivi karibuni.
Doctor akaondoka baada ya muda mfupi alikuja seche aliponiona tuu aliangua kilio😰nilimuangalia kwa huruma Kisha nikamuuliza vipi kuhusu mwanangu?akasema mwanao yupo na anaendelea vizuri tumboni.ninachoshukuru ni kwamba kumbukumbu ziliwai kurejea.
Nikamwambia usijali seche niombee uzima na nguvu tuu,niombee niweze kuinuka nisiwe kiwete,nakuahidi nakuoa.seche aliendelea tu kulia baadae alitoka nje maana alishindwa kujizuia.mama akasema hiyo ndiyo Hali ya seche kwa Sasa toka umepata matatizo amekua ni mtu wa kulia tu ovyo.
Basi ilipita miezi miwili tena sikuweza hata kujalibu kuinuka japo nilikua naweza kuongea nakula kwa kulishwa nilivalishwa pempas najisaidia apo apo.
Seche mimba ilishajitokeza sasa.ikiwa ni miezi mitatu toka nipate fahamu,niliweza kuinua miguu yangu hapo ndipo madaktari wakasema naweza kuanza mazoezi ya viungo.
Taratibu nilianza mazoezi,niliweza kuinuka kwa msaada,miguu ilikua Haina balance vizuri.niliendelea na matibabu Hadi nikakaa sawa siku zilikua zimeshaenda kwakweli,.
Japo sikua vizuri Sana lakin ilikua angalau.niliruhusiwa nyumban na niliandikiwa kufika hospital mala mbili kwa wiki ili kuchukua mazoezi…nilimuuliza mama nilipopatia ajali,mama alisema ni vijijini kabisa kabla ujafika mjini huko nyumbani.
Kwaio tulipelekwa hospital kubwa ambayo ndo ipo mjini.nilipofika nyumban ilikua ni mtu wa kula kulala nafanya zoezi kupitia magongo miguu haikujiweza Sana.siku zilienda ugonjwa ulichukua muda mrefu Sana Hadi seche akajifungua mtoto wa kiume mie bado sijatengemaa vizuri.
Mwanangu alifikisha miezi miwili toka amezaliwa namim nikawa nimepona walau naweza tembea bila msaada wa magongo,ikabidi nimchukue mke wangu nirudi kazini japo nikifikiria ajali sitamani kabisa kusafiri ila nilisema ajali ipo tu aikwepeki,na kifo kipo.
Tulisafiri na mke wangu niende Kwanza kazini huku tukiwa tumepanga tena miez mitatu ijayo ndo tufunge ndoa.
Nililipoti kazini nilipewa pole sana.nikaendelea na majukumu yangu,siku zilienda siku moja nimerudi kwangu sikumkuta mke wangu,nikamuuliza uko wapi?akasema nimemleta mtoto clinic nikamuuliza clinic gan saa kumi?akasema alichelewa kwenda.wala sikumfikilia vibaya.
Muda kidogo akawa amerudi.nikamwambia mlete mwanangu nenda ukapike njaa inauma.alinipa mtoto nikawa nacheza nae,simu yake pembeni yangu iliita,nikaangalia jina limeseviwa (roda kwaya) nikamwambia mama B roda ni Nani anakupigia?
Akasema mme wangu achana nae uyo rafiki angu nilikuaga naimba nae kwaya kabla sijaacha.wala sikufatilia nikaacha…aikupita dakika meseji ikaingia nikashika simu kufungua ile meseji…
RODA KWAYA seche nakupa siku tatu utachagua kusuka au kunyoa,naomba niletee mwanangu kabla sijaja kukualibia.mh!!!!miguu iliisha nguv nikamuweka mtoto pembeni nikachukua ile namba nikaangalia eatel money nikakuta jina la kiume.
Nilishtuka Sana muda kidogo simu ikaita tena nikampelekea nikapokea Nikamwambia naomba uongee,aliongea kwa wasiwasi,nikaweka loud yule mwanaume alipokea akasema umeiona meseji yangu?seche akasema hapana akasema iangalie alafu nijibu.nikakata simu nikaingia sehemu ya meseji nikamuonyesha nikamwambia umeona hii meseji naomba ubebe kilicho chako nikakukabidhishe kwa baba wa mtoto wako.
WIFE MATERIAL 15
Nilipoona zile meseji nilimuonyesha,kiukweli aliishiwa nguvu alibaki anatetemeka,nikamwambia beba kilicho chako unipeleke kwa uyo mwanaume.alikataa akasema huyu mtoto ni wako Fred lisitokee Jambo la kututenganisha kwani shetani yupo kazini.
Nikamwambia sawa nataka nikaonane na shetani live,nilimuangalia seche ila sikuamini kama ni yeye angeweza kunifanyia unyama kama ule,sikutaka kuamini kabisa.
Nilimuuliza uyo mwanaume anaishi wapi?akasema hayupo huu mkoa yupo huko nyumbani kwa wazazi…nikamwambia inamaana uliondoka na mimba?hapana sio kweli toka umekuja ulikaa muda mrefu Sana na nilishuhudia baadhi ya siku ulizoingia mwezini.
Naomba uniambie ukweli kwann umemsev jina la kike?akasema nimemsev sababu msumbufu niamini mme wangu sipo nae kweny mahusiano.
Kwakua simu yake ilikua mikononi mwangu ilibidi Sasa nichukue jukumu la kumpigia roda kwaya…simu iliita hatimaye ikapokelewa niliiweka sikioni Kisha nikasema haloo….sauti yake upande wa pili ilisika ikisema naam nakusikia,,,,nikamwambia naitwa Fred mwenzangu unaitwa Nani?Akasema haipaswi kujua jina langu wewe kama Nani Hadi unifahamu Mimi?alinifonya Kisha akakata simu.
Nilimwambia seche umeona ninavozalilika sababu yako?alijiinamia tu chini,sikuishia hapo niliamini kabisa yule mtoto ni wangu,nilimpenda Sana niliangaika kwa kila hali ili awe salama avae apendeze.
Nilimpigia simu yangu lakini hakupokea,baadae akapokea kwa ukali ni mtu aliepanic,unasemaje broo mbona umekua ni msumbufu Sana?nikamwambia Sina cha kusema zaidi ya kukuambia naomba uniachie familia yangu ukiachwa achika.
Alinicheka kwa sauti hahaha unachekesha Sana,mie ndo nikuachie familia yako au wew uniachie familia yangu?nikamwambia huyu mtoto ni wangu samahani Sana.
Akasema ndugu tusiandikie mate nangali wino upo.je unatumia wasap?nikamwambia ndio.akasema nitajie namba zako nikamtajia 0682………..24 akasema sawa washa data baada ya muda mfupi utapata majibu.
Nilikata simu nikaenda kukaa kwenye Kochi kusubiri nitumiwe.nilimuangali mtoto nilieamini ni wangu B nikamshika huku moyo unaniuma Sana nilimpakata nikamkumbatia kwa nguvu huku moyo umejaa uchungu wa hatari.
Muda mfupi iliingia namba bila jina wasap nilipofungua ilikua ni picha ya karatasi za DNA zilizoonyesha yule mtoto kafanana kwa asilimia zote na yule kijana.
Nilimuita seche nikamwambia hivi unajua kuhusu hili la DNA?akasema ndio najua nisamehe Sana mme wangu,nikwambia mlipima lini?akasema tulipima tulipotoka tu nyumbani tulipofika huku…..nikamwambia Kama unaitaji msamaha wangu naomba uwe muwazi na mkweli.
Nikamwambia majibu mmefata lini?akasema majibu tumefata leo,anhaa kumbe umenidanganya umeenda clinic kumbe mmefata majibu?Sasa mbona umenidanganya kuwa hakai mkoa huu???
Alikosa cha kuongea nikampigia yule kijana nikamwambia namruhusu huyu mwanamke aje kwako kiroho Safi kwanzia Leo mie sihusiki tena kila raheli.
Nilimuangalia seche nikasema kumbe ndio maana kipindi kile unadanganya unaemda kanisani kumbe unaenda kwa mwanaume?alikosa jibu.nikamwambia jiandae uende kwako.
Alilataa.nikamwambia basi acha niwapigie tu simu wazazi wako niwaambie,akasema usifanye hivyo basi naenda ila usiwaambie wazazi wangu.
Alikusanya nguo zote nikampeleka had kwa uyo mwanaume kanipeleka uswailini Sana tulipofika kwenye iyo nyumba nje tumekuta wahuni kibao,wanavuta bangi,walipomuona tu seche wakasema aaaa shemela tunaona umemleta ankoli wetu B mwanangu njoo jembe langu.
Muda kidogo nasikia mtu anasema woiii woiii woiii mama mtu eeee nilijua tu samaki atanasa kweny chambo,mala kidogo tukakutana uso kwa uso masikini ndo mme mwenzangu muhini,vibaya Sana.
Ila sura yake ilikua sio ngeni,ni Kama nilishawai kumuona mahali ila sikumbuki ni wapi.
Inaendelea….