WIFE MATERIAL 01
Naitwa Freddy ni mtoto wa Kwanza katika familia ya watoto wa tano,Leo hii moyo umenisukuma Sana kuleta kisa changu,naomba tufatane pamoja ili tuweze kupata kitu.
Nimelelewa katika maadili ya kidini sana,familia yetu ni ile familia yenye misingi ya dini sana.siku zote mama pamoja na baba walinisihi kuhusu kusoma kwa bidii na kuachana na Mambo ya kidunia…
Nilikua kwenye misingi hiyo Hadi pale nilipofika kidato Cha tano ndipo nilipoanza kujiona ni mwenye matamanio ya kimwili kutokana na barehe…ila kila nikikumbuka kauli za wazazi wangu niliachana na hisia zangu na kufanya kilichonipeleka shule,
Nilihitimu masomo yangu na kufanikiwa kumaliza chuo,nyumbani kwetu ni jijini mbeya,nilifanikiwa kupata kazi serikalini.
Nilifanya kazi vizuri,lakini siku zote hizo sikuwahi kuwa na mpenzi Wala kushiriki tendo la ndoa.siku moja tukiwa tupo mapumziko kazini Mimi na rafiki angu Abely tulienda kupata lunch.
Tulipofika hotel tuliagiza vyakula na katika mazungumzo yetu abely aliniuliza,hivi fredy kwako unaishi na mpenzi?nilicheka Kisha nikamjibu,hapana rafiki angu.akaniuliza Tena kwanini inamaana Kuna mpenzi kabisa?nikamwambia abely tuachane na hizo habari maana nilikua nikisikia mtu anazungumzia mwanamke Basi naona aibu Sana.
Kesho yake Tena kama kawaida,tukiwa tunapata kifungua kinywa abely alinifata na kuniuliza Tena like swali.nikamwambia jamaa mbona Kama umetilia mkazo Sana swala la mimi kuwa na mwanamke???
Abely alitabasam akashusha kikombe Cha chai chini Kisha akasema, Freddy jichanganye ,mh!!?kujichanganya kivipi?wewe ni kijana na kwa umri wako lazima upate Dem mkali Sana utulie nae,nilicheka Kisha nikamjibu Mimi kuoa kwa Sasa bado Sana kiufupi maisha yangu bado sijajipanga labda hadi nitakapojenga nyumba yangu.
Abely akasema sawa haina shida,Maisha yangu yaliendelea lakin hapo baadae niliona kweli nnahitaji kuwa na mtu,ila kila nilipowaza jinsi ya kumuingia mwanamke na kumwambia kuwa nampenda,nilijikuta nashindwa.
Ilibidi nitoke niende Tena kwa Abely kuomba ushauri,nikamwambia my friend kweli kabisa mie siwez ku aproch mwanamke na sijui maisha yangu yatakuaje,alitabasam Kisha akasema hizo ndo story nnazotaka kusikia kutoka kwako.
Nikamwambia nipange Sasa,akasema Kwan unampenda Nani???nikamwambia Kuna binti mmoja Anauza duka la vipodozi hapo mjini,anaitwa Natasha,akasema oooh wow Yan umelengesha mule mule ila hizi hisia jaman.hivi Freddy utaamini kuwa huyu Natasha ndo mtu nilitaka nikuunganishe nae???
Nikamwambia hapana sijui.akasema Basi ndo ivyo,siku zote huwa nakwambia uoe lkn Natasha ndo huwa ananituma kwako nimsaidie ila huwa naogopa kukuambia sababu haukua tayari.
Nikamwambia Basi sawa,tuweke mipango sawa ya kuweza kuwa nae karibu.kesho yake jioni tulimualika chakula cha usiku Natasha ili abely aweze kutuunganisha.
Tulienda hotel moja kubwa,Kisha nae Natasha akaja,kiukweli niliona aibu Sana nikawa nakosa hata Cha kusema,abely akasema naomba niwaache kidogo nitakuja baadae ili muongee,
Abely aiondoka akaniacha mim na Natasha,niliangalia chini kwa kuona aibu.sikuongea kitu chochote ndani ya dakika tano.natasha akaniambia Freddy usijali nmeshaambiwa Kila kitu na abely mie ni wako kwanzia Sasa mambo yasiwe mengi.
WIFE MATERIAL 02
Abely alipoondoka niliona aibu Sana,kuongea na natasha,lakin cha kushukuru ni kwamba aliweza kuwa muwazi na kufunguka juu yangu,alisema mambo yasiwe mengi tuanzishe ukurasa wa mahusiano baina yangu Mimi na yeye.tulishikana mikono ikiwa ni ishara ya umoja wetu.
Na huo ndo ukawa mwanzo wa mahusiano yangu na yeye….alionesha kunijali na kunipenda Sana,ikumbukwe tuu sikuwai kuwa na mahusiano hapo nyuma…tuliendelea kuwasiliana kila mtu aliishi kwake,kazi kubwa iliyokuwepo kwangu ni ile nashindwa kumuita kwangu Yani naogopa Sana nitaongea vyote ila ikifika ilo swala domo linakua zito sana.
Nilimgharamia natasha kwa kila kitu nilisimama Kama mwanaume ndani ya miezi mitatu kwenye mahusiano,bila kufanya kitu chochote….nakumbuka ilikua siku ya jumapili sikuenda kazini Natasha alinipigia simu akaniuliza nnafanya nini?nikamwambia nimelala nataka kuamka ili nianze kazi ya kufua,akasema ok!naomba unielekeze kwako nakuja nitakusaidia,nikasema afadhari amesema mwenyewe,sikuchelewa nilimuelekeza Hadi mahali ninapoishi.
Alipanda usafiri akafika kwangu nilitoka barabarani nikampokea,tulifika kwangu akaniuliza fredy unaishi na Nani hapa??nikamwambia nipo mwenyewe vipi Kuna shida??akasema hapana akuna tatizo lolote,isipokua una matumizi mabaya ya pesa umepanga nyumba kubwa Sana alafu unaishi mwenyewe.
Nikamwambia nimefanya hivyo sababu ya ndugu zangu wakija siwez lala nao pamoja walau Kila mgeni alale kwa kujiachia.akasema ok wazo zuri,basi nilitoa nguo zangu nje akasema acha nitakua nafua wewe unaanika.alifua nguo zote mie nikawa naanika,tulipomaliza tukaamia ndani,mie nilifanya usafi wa nyumba nzima yeye nikamuelekeza vitu jikoni akaingia kuanza kupika.
Tulipomaliza tuliketi tukala,nilimshukuru kwa kuweza kunisaidia baadhi ya kazi,tulipomaliza hapo tukawa tumekaa tunaangalia tv.akaama kutoka Kochi moja hadi mahali nilipokaa Mimi alinisogelea akaniangalia usoni huku akitabasam namimi nikatabasamu pia.
Akasema Freddy ni miezi kadhaa Sasa kwenye mahusiano lakini hatujawahi shiriki kitu chochote Cha kutuunganisha sisi.nikamwambia ndio ni kweli.akasema sawa kwaio wewe unalichukuliaje hili swala?
Nikamwambia vyovyote utavyoamua wewe.yani muda huo namjibu lakini moyo wangu unakwenda Kasi Sana sababu ya uoga na aibu.akasema basi sawa,akaniuliza chumba unacholala wewe ni kipi?,nikamwambia Cha mwisho kabisa upande wako wa kulia.akasema sawa twende tukaongee huko.tuliinuka pale Hadi huko chumbani.
Nilimwambia karibu hapa ndo chumba nnachopumzika Mimi.akajilaza kitandani akasema njoo tupumzike,nilipanda kitandani huku naona aibu siamini kabisa kinachoendelea.akaniuliza hivi Freddy wewe una aibu Sana eeee!!!nikamwambia hapana,akasema Sasa mbona sikuelewi upo upo tuu…nilinyamaza kimya nikamsogelea karibu yake Kisha nikamkis ili aone tuu nnajiamini.
Alivoona hivyo akanipa kumbato,ilikua ilivokua tukawa tumeunganisha miili yetu.kwanzia hapo upendo ndani yangu ukawa umezid kufunguka,baada ya kumaliza aliniuliza hiv hii ndo mala yako ya Kwanza?nikamwambia yes!akasema ndo maana ila siku zinavoenda utazidi tu kuzoea.
Hakulala kwangu,aliondoka saa nne usiku,kwanzia iyo siku nilianza kuwa na wivu Sana juu yake,Yani ni mtu ambaye siwezi kukaa masaa sita bila kumuona nitampigia simu mala kwa mala asipopokea naumia sana.aliendelea kunipa huduma za penzi na zingine ambazo mke inabid amfanfanyie mume Kama kawaida.alikua ni mtu ambae akija kwangu anajituma Sana,anafanya kazi kwa bidii anahakikisha Mimi ni msafi muda wote.
Pendo liliponizidia nikasema hapana uyu naoa,anasifa zote za wife material ,lakin kabla sijamwambia chochote alisema mwenyewe,baby Mimi sitaki kuendelea kukaa mwenyewe nahitaji kuja kukaa na wewe huko nikamwambia sawa Haina shida.
Alikua amepanga chumba kimoja aliruhusu chumba na vitu vyake vyote alipeleka kwao.akaja tukawa tunaishi huku anaendelea na kazi ya kuuza vipodozi kwenye duka boss wake,ilienda hiyo Hadi pale aliponiambia babe najihis mchovu Sana siku hizi naumwa mala kwa mala kizunguzungu Cha hapa na pale.
Nikamwambia sawa pole mke wangu naomba asubuhi uwahi hospital ukapate matibabu.akasema sawa.asubuhi nilienda kazini niliporud jioni ananiambia Freddy nna ujauzito.
WIFE MATERIAL 03
NIliporudi kazini jioni Natasha alinipokea na kuniambia kuwa baby nna ujauzito.aisee hizo zilikua ni taarifa nzuri Sana kwa upande wangu.nilifurahi sana,ule upendo niliona sio kitu kwake nilitamani nimfanyie atakacho ilimradi afurahi.
Nilimuuliza unapika nini usiku huu?akasema anataka kupika ugali nilimwambia hapana,acha nakutoa nje ya nyumba uende ukale kitu utachokipenda.alijiandaa tukatoka.
Nilimpeleka sehem nzuri na tulivu.nilimuagizia chakula kizuri sana,nikaanza kimwambia mke wangu usitoe mimba yangu,nitafurahi Sana siku nitayoitwa baba,aliniangalia Kisha akasema,Freddy sijalazimishwa na mtu kuwa na wewe hata kuzaa pia sijalazimishwa ni upendo wangu tu kwako ndo umenisukuma.
Nilimshika mkono nikamkiss nikamwambia sawa nafurahi kuwa nawe.natasha your my life.nataka nikuoe,akasema nitafurahi Sana siku ukinivalisha Pete.
Nikamwambia sawa Sina muda wa kupoteza nataka nikutambulishe nyumbani wote wakujue wewe ni Nani alafu mipango mingine iendelee.
Vipi kuhusu dini?akasema dini sio shida kwake atanifata tuu mimi.nkamwambia sawa.tulifurahia muda wetu mahali pale Kisha tukarudi nyumbani.kesho yake sikutaka kusubiri nilianza kuwapigia ndugu wa karibu wote na kuwapa taarifa kuwa nimepata ubavu wangu nahitaji kuoa.kwa upande wa mama ni alifurahi Sana tuu.wakasema kuwa wanahitaji kumuona.
Niliwaambia likizo ikifika nitampeleka…nayeye alisema anaumwa mala kwa mala hivyo awezi kuendelea na kazi.nilimwambia pumzika tu mke wangu nitakuhudumia.basi nimlimuhudumia vizuri siku zote ndugu zake walinijua ikiwemo dada na mama yake.
Ilipita miezi mitatu ya ujauzito nilimwambia twende ukaanze clinic aliniambia kuwa ataanza tu muda ukifika hataki kuwai sana.
Siku zilienda nikiwa nasubiri likizo ya kazini ifike ili twende mbeya kwa wazazi,maana walikua wakimsubiri kwa hamu Sana.
Siku iyo ilikua ni alfajiri Sana mida ya saa 11.nilishtuka usingizini,nikachukua simu yake na kuangalia saa,nikagundua kuwa bado akujapambazuka vizuri.nilichukua simu yake na kuanza kuikagua bila sababu yoyote ya msingi.katika kukagua moyo ulishtuka Sana nilipoona Natasha anachart na rafiki yake,mazungumzo yao yalikua hivi:
Shoga ake:Natasha una hatari Sana wewe umemdanganya kaka wa watu akijua itakuaje??
Natasha:atajua Nani atamwambia??
Rafiki ake:siku zote uongo nikama mafuta na ukweli ni kama maji hivi vitu ukivichanganya kwa pamoja lazima vitajitenga hata hayo unayofanya Leo shoga ipo siku utajulikana tuu.
WIFE MATERIAL 04
Waliendelea kuchart Natasha na rafiki yake,rafiki yake akamwambia siku zote uongo hutengana na ukweli ipo siku utabainika.
Lakin Natasha alidai kuwa awez kugundulika.Rafiki yake akamwambia siku zitapoenda utamueleza nin akigundua kuwa Mimba huna???akasema kwamba awez kugundua nataka nijifanye imetoka bahati mbaya najua ataniamini.
Rafiki yake aliguna tu mhhhh!!!!sawa bwana unachokitafuta utakipata.huo ndo ukawa mwisho wao wa kuchart na walichat usiku wa kuamkia siku iyo,inamaana kabla atujalala ndo alikua akiwasiliana na rafiki yake.
Nilijawa na jazba.nikamuangalia usoni Natasha,nikasema hapana Natasha sio wa kunifanyia hivi.inamaana kumbe mimba Hana???hii aiwezekani.kwanini ameamua kunifanyia hivi?mbona ninachoamini ni kwamba ananipenda Sana sasa imekuaje??
Nilijiuliza maswali mengi ambapo nilikosa majibu kabisa kiukweli,niliamka nikaenda kuoga nilijiandaa nikasema nisimwambie kitu chochote ili nikamueleze rafiki yangu abely mambo ya Natasha alionifanyia.
Nilipomaliza kujiandaa nafsi ilisema hapana huyu lazima ajue hili swala kabla sijaondoka.ilinibidi nimuamshe alipoamka nikamuuliza Natasha nataka kujua asha ni Nani???Kwanza alishtuka Sana akasema amefanyaje?nikamwambia nimekuuliza naomba unijibu.akasema ni rafiki yangu nilisomaga nae primary ila kwa Sasa yupo dar.
Nikamwambia ok! ndo ukaamua kunidanganya kuwa una ujauzito kumbe huna?Natasha kwanin umeamua kunifanyia hivo?alipigwa na butwaa akaanza kutetemeka.nikamwambia naomba unijibu basi.akasema ni kweli baby mimba ninayo huoni inavonipelekesha?
Kinachonifanya nimuongopee asha ni mtu ambae anapenda Sana kunifatilia maisha yangu.ndio maana nmemwambia hivyo.nikasema ok jiandae naenda kazini kuomba ruhusa naenda kununua kipimo nakuja kukupima mwenyewe hiyo itakua aitoshi baada ya hapo nitakupeleka hospital kwenda kupima.akasema sawa siwezi kukupinga Freddy.
Niliondoka Hadi kazini nikiwa nimevulugwa nikasema kama kweli Hana kulikua na sababu gani ya kunidanganya?niliona navulugwa sana,nilimuita Abel nikamwambia my friend Natasha ameni disappoint pakubwa sana….akaniuliza imekuaje?nikamueleza kila kitu.akasema usifanye Mambo kwa haraka,tuliza moyo mfatilie vizuri hata mienendo yake.
Nikamwambia sawa best unaweza kunishikia vipindi vyangu vya mchana hapa kazini ili Mimi nimuwai nataka kwenda kumpima.akasema hapana mie sipo vizuri kiafya leo sitaweza kumudu.nikasema sawa.ilipofika mida ya kufundisha ilibidi niingie class nikafundisha wanafunzi wangu maana nafundisha form2 na form4 masomo ya sayansi.
Nilipomaliza tu nikaondoka kabisa eneo la kazi nilipofika kwangu nimekuta geti lipo wazi lote,nikaingia nikafunga.naingia sebleni nakuta seble ipo tupu inaniangalia…nilishtuka kidogo,nikasema inamaana Natasha ameamua kuama bila kunishirikisha???
Naingia dining akuna kitu naenda jikoni akuna kitu niliisi kuchanganyikiwa.naenda chumbani kwangu hakuna kitu Hadi nguo zangu zimebebwa,miguu iliisha nguvu nikakaa chini nikampigia simu Natasha alipokea nikamuuliza uko wapi?akasema nipo nyumban baby nikamuuliza nyumban wapi?akasema kwako.nikamwambia mbona hapa haupo?akasema nimeshamaliza kilichokua kimenileta Kisha akakata simu.
Hivi inamaana kumbe uyu mwanamke kwangu alifata Mali?nilitoka pale nikaenda chumba kimoja cha wageni nilikuta begi ninaloifadhia vyeti vyangu vyote vya masomo lipo chini.maana Hilo ndo muhimu.nililikagua nikakuta vyeti vyangu vyote vipo salama.nikasema afadhari.napiga jicho pembeni nakutana na karatasi,nikaiokotana kuanza kupitia yale maandishi.
Wako Natasha,
Pole kwa kila kitu nilichokufanyia fred.kiukweli sikuwai kukupenda maishani mwangu,siku zote niliforce tu kuwa na wewe lakini nilijitahidi Sana usiweze kujua kuhusu ilo Jambo.
Sasa ni wakati sahihi wa Mimi kuondoka na kukuacha na maisha yako.kwakua ulinitumia kwa muda nisingeweza kuondoka hivi hivi,nimebeba vitu vyote viwe Kama fidia ya kunitumia siku zote.
Nilikudanganya kuwa ni mjamzito ilimradi niwe karibu na wewe unifanyie Mambo makubwa pia uniamini.kiasi nilichokipata katika kabati kinaweza kwenda kunifanya niishi vizuri na nimpendae huko mbele ya safari.nakutakia maisha mema stay blessed.
Hapo ndo ulikua mwisho wa barua ile lakini ndo nikakumbuka kuwa ndani nilikua nna akiba ya milion 1 na laki 5.kumbe alizibeba.nilitoka nje ya myumba,sikutamani Tena kuendelea kuishi pale,nilimpigia simu Abely nikamueleza mkasa wote kwa yalionikuta.alisema nimsubili anakuja.zilipita Kama dakika kadhaa nilimuona abely amefika akaniliza ticha vipi?nikamwambia ndo Kama nilivokueleza.akasema ebu ngoja nihakiki.aliingia ndani baadae akatoka
,akassma kumbe huyu mwanamke ndo mjinga kiasi hichi.kwa yote uliomfanyia upendo uliompa lakini haya ndo majibu yake.nikamwambia ndo ivo.akasema cha kufanya twende tukatoe taarifa police.nikasema yes wazo zuri.tulienda Hadi police ilimrad lolote litalomkuta huko Mimi wasinihusishe.
Tulienda police tukatoa riport wakat tunarudi njiani nikapata wazo la kwenda kwa wazazi wake pengine amekimbilia huko.nikamwambia abely ebu twende kwao kwanza.akasema hapana tusiende uyo atakua njama moja na wazazi wake unaweza kuitiwa hata mwizi.nikasema sawa tu liwalo na liwe.akanisihi Sana nisiende,nilirud kwangu nikachukua kibegi changu cha vyeti nikampigia mwenye nyumba kuwa nimeama akaangalie nyumba yake.
Nilienda kwa abely ambae yeye alikua ameshaoa na ana mtoto mmoja.abely alisema kaa hapa Hadi mshahara utapotoka ndo utafute nyumba ununue vitu ukapange.nikasema sawa.usiku huo sikulala kabisa niliwaza mengi mno.lakini nafsi bado ilinisukuma kwenda kwao.
Asubuhi ilifika ambapo ilikua jumamosi sio siku ya kwenda kazini.nilinawa tu uso hata chai sikunywa nikamwambia abely kuna mahali naenda sitachelewa Sana kurudi.
Nilitoka pale moja kwa moja Hadi kwao kwa kina Natasha nilikuta wadogo zake na mama yake.alinipokea vizuri sana.huku akiniuliza Kama Natasha ajambo.niliishia kutingisha tu kichwa.nilipoulizwa nikasema mama mwanao ametoroka na vitu vyote,akaniuliza shida nini au mligombama???nikamwambia hapana mm nimeishi na Natasha Kama malaika atukuwai kutofautiana hata siku moja.
Nikamueleza mkasa wote jinsi ilivokua.nikamwambia naweza kumpata wapi?yule mama aliinama chini Kisha akasema kijana mie Hadi nakuonea aibu.nikamwambia kwanini mama?akasema naomba nisamehe sana,Natasha sio mwanangu ni mtu ambae tumejuana ukubwani/kimjini mjini na aliniambia anakuja kukutambulisha kuwa Mimi ni mama yake lakini ukweli ni kwamba hata familia yake siijui kabisa….
WIFE MATERIAL 05
Yule mama fake wa Natasha aliponipa zile habari kiukweli ziliniumiza sana.niliwaza mambo mengi mno,moyo ulikata tamaa kiasi cha kuwa nilijiona Sina umihimu tena diniani.
Nikamuuliza yule mama,eti mama wewe unawatoto???akasema ndio ninao.nikamuuliza wangapi?akasema ninao wanne wakiume watatu na wakike mmoja.nikamwambia sawa,hivi utajisikiaje kama utaona mwanao amefanyiwa unyama Kama niliofanyiwa Mimi?
Yule mama alikaa kimya tuu hakujibu kitu chochote,nikasema sawa nashukuru kwa yote,kwani hata wewe ungeniambia kuwa sio mzazi wa Natasha toka mwanzo ungekua umeniokoa sana.akasema sikujua Kama atakuja kukufanyia hivo,niliinuka nikamwambia sawa kwaheri naenda.
Maisha yangu yakaenda kuanza upya nikawa nimeridhika na kila kilichotokea Natasha aliniblock nikipiga simpati.kiukweli nilikua naumizwa Sana kila nikimfikilia mpenzi wangu Natasha nilikua maona Kama ni ndoto ipo siku nitaamka.
Nilikaa pale kwa jamaa yangu alinikarimu siku zote hadi pale,nilipopokea mshahara,kwakua mshahara napokea mzuri wa degree,ulinitosha kabisa kwenda kuanza maisha yangu upya,pamoja na akiba nyingine niliokua nayo bank.
Nilitafuta nyumba nje kidogo ya eneo la kazi,nikanunua vitu muhimu kitanda godoro sofa set na vitu vingine vichache.nikasema vitu vingine nitaendelea kununua kidogo kidogo nikiwa kwangu.
Basi nikamuaga Abel pale nikaenda kuanza kujitegemea upya…mazoea mabaya Sana,nilishazoea kuishi na mwanamke nyumba moja Kama nimemuoa,matamanio ya kimwili yaliendelea kunisumbua moyo ulitaka kabisa kuanzisha maisha mapya ya mahusiano.
Kama kawaida nilimfata mshauri wangu wa mahusiano ili aweze kutia neno kuhusu ili swala.maana mambo yake yote huwa ananishirikisha hata ikitokea amepishana kauli na mke wake,hata mimi pia sikuona Kama kuna sababu ya kumficha Jambo.
Ilikua ni jioni tumetoka kuangalia mpira wa Simba na yanga.nikamwambia nataka tuongee akasema Haina shida.Tulienda sehemu nikawa napata chakula cha usiku,yeye akasema hawez kula hotel mke wake anapila nyumbani,kwaio akaagiza kinywaji tuu.
Basi nikaanza nikamwambia Abel shida yangu mie sio kupoteza vitu vilivyochukuliwa na Natasha,kwani Hadi sasa hivi nimeshafanikiwa kununua nusu ya Mali zilizopotea…na kabla huu mwaka haujaisha naimani nitapata zaidi ya zilizopotea.
Abel akasema Sasa shida nini Fred???Nikamwambia sawa,shida ni kwamba natamani tena kuanzisha mahusiano mapya japo nashindwa kuwaamini tena wanawake.
Abel akasema sawa Fred nimekuelewa wazo lako ni zuri,isipokua usifanye Mambo kwa kukurupuka itakucost Sana hapo baadae.
Nikamwambia mbona kwa Natasha sikukurupuka na yametokea yaliyotokea?akasema ok uamuzi no wako,ila ingekua ni Mimi kwa ushauri wangu ningekushauri ukae walau mwaka mzima bila mahusiano.ili akili yako itulie Kwanza.
Nikamwambia sawa best nimekuelewa Sana,nashukuru kwa mawazo yako nitajitahidi kutulia kwanza,akasema sawa nafurahi kusikia unanielewa.
Tuliagana kila mtu akaenda kwake…siku zilienda nilipata likizo,nilienda nyumbani kusalimia,nilipofika mama aliniuliza kwanini nimekuja peke yangu??Wala sikuwahi kumwambia habari za Natasha niliona Kama aibu Sana.
Nilimwambia kua Natasha ametingwa Sana na kazi zake ila akiwa free basi atakuja kuwatembela yeye mwenyewe.mama alilizika nilikaa siku nilizokaa lakini kuna binti pale mtaani nilitokea kumuelewa.
Nikasema Sasa hapa nilisema niwe nae karibu hata wazazi watanichukuliaje?sababu wanajua kabisa Nina mwanamke naishi nae.
Nikasema hii acha iwe Siri ila kiukweli uyu binti lazima nipite nae.
Mtoto mzuri akija nyumbani alikua anamleteaga mama taarifa za kanisani,sikuwai kumuona amevaa nguo fupi Wala ya kumbana hata siku moja,sura yakeya upole rangi yake maji ya kunde.kiukweli alikua na sifa zote za kuwa mke…
Nilijaribu kumuuliza mdogo wangu wa mwisho kuwa huyu ni mtoto wa Nani mbona simjui???akasema wao wameamia tuu mbeya miaka miwili iliyopita baba yake yupo kikazi,
Nilitaka Sana kumtuma mdogo angu maana ndo rafiki yake mkubwa ili akachukue tu namba au kama anazo anipatie,lakin niliona ni ujinga kwanini nisimfate Mimi mwenyewe?nakumbuka nilimsubiri Kama siku tatu lakini sikuwai kumuona atokee pale nyumbani.
Siku iyo jioni nashangaa amekuja mama alimkaribisha,akamwambia enhe uko mmeimba kwaya leo?akasema ndio tumetoka mazoezi ya kwaya ila mchungaji kasema nikuletee hichi kitabu Cha tenzi,na jumamosi hii ni zamu yetu usafi kanisani.
Yani akiongea tu Mimi napagawa,ilikua ni mida ya saa 12 jioni,nilitoka pale ndani nikaenda nje nikajificha kweny uchochoro ambayo ndo njia lazima apite.baada ya muda kidogo nasikia Kama mtu anatembea anakuja nilipo Mimi kagiza kalikua kameshaanza kuingia,na iyo njia no wanaotoka na kuingia kwetu tu ndo wanapita kwenye uo uchochoro.
Aliposogea karibu na nilipo Mimi nikamvuta nikamwambia binti njoo hapa,nikamshika mkono.aligeuka na kuniangalia,hee kumbe mdogo wangu.wewe kaka muda huu unajificha hapa unanivuta unataka nin?nikamwambia unaenda wapi nilikua nakuzingua tuu nione Kama utashtuka.mh aibu imenipata naipotezea tuu.
Nilimuacha akaondoka nguvu ziliniisha nikagaili like zoezi kwenda ndani namkuta bado yupo na mama.
Inaendelea….