TAMU YA MCHAWI
KIPENGELE CHA 09
ONYO: Watoto wasisome hii Hadithi
Kabla ya binti Changa kuanza safari yake ya kwenda moja kwa moja kwa Kapweto ili amuombe msamaha, aliona ni heri akajiandaa avae vizuri kisha aende ili aweze kuwa na mvuto wa aina yake.
Alikuwa mwenye umri wa miaka 19 tu lakini alijua kupangilia mavazi, mtu akimuangalia kwa jinsi alivyokuwa mzuri, kamwe asingeweza kuamini yule binti ni bonge la mchawi, mwenye nguvu nyingi za kuogopesha.
Changa alivaa nguo ndefu sana, kisha akachana nywele zake na kuzilaza nyuma, zilikuwa sio ndefu sana lakini zilikuwa laini maana alipenda kuzitunza, alijifunika na mtandio mweupe kichwani halafu akavaa viatu vya wazi na safari ilianza kuelekea mtaa wa Kagera
Alitembea taratiibu, lakini vile vile aliogopa maana tayari alikuwa ameshampenda mwanaume ambaye alienda kumuwangia usiku.
Alipofika karibu na pale alipokuwa akiishi Rasi Kapweto, binti alitazama kwa makini akagundua kuna wazee wengi sana wanapata vileo muda ule. Ikabidi asite na kuwaza namna ya kumuendea.
Akiwa anawaza ataendaje pale, ndipo alipopata wazo la kumuagiza mtu yeyote ambaye alikuwa anapita pale, hata hivyo haikuchukua muda mrefu sana, alipita mwanamke mmoja ambaye alikuwa akiitwa mama Asha.
Bila shaka mama Asha alikuwa ni mteja mzuri wa Hamis Kapweto na siku mbili kabla ya ile alikuwa amemuambia Hamis aachane na huyo mtoto maana ni mwanga na amevunja ndoa nyingi sana.
Binti bila kujua yule mama anamfahamu vizuri, alimuita “Samahani mama” alisema na mama yule aligeuka akakuta ni Changa, akashtuka na kusema
“Bila samahani” alisema mama Asha
“Shikamoo kwanza” alisema Changa
“Marahaba”
“Ah..mh unaelekea hapo kwa rasi??”
“Ndio”
“Basi naomba unisaidie kumuita mwambie niko hapa”
Mama Asha alimtazama juu mpaka chini, akakumbuka juzi tu alikuwa ameshampa onyo, ndipo akasema “Haya nitamuambia”
“Sawa asante”
Mama Asha aliendelea na safari yake mpaka akafika kwa rasi, ambapo alikuta watu wengi na aliwasalimia halafu akamfuata rasi na kumuambia
“Hamis, una mgeni wako kule”
Hamis Kapweto akashtuka na kuinuka akatazama, ni mbali kidogo na pale hivyo hakufanikiwa kujua ni nani, zaidi alijua ni mwanamke ambaye amevaa nguo nyeupe.
“Ni nani huyo??” aliuliza rasi
“Ni yule binti ambaye nilikupa onyo juzi, naona kaamua kukufuata mpaka huku”
Hamis alishtuka sana baada ya kusikia vile, akajiuliza kwanini yule binti alikuwa anajipendekeza kwa kiasi kile, ndipo akamuhudumia mama Asha halafu akamfuata Changa.
Alipofika kwa Changa alimkuta Changa akiwa anatabasamu tayari. Changa akamuamkia
“Shikamoo kaka rasi”
Hamis Kapweto hakujibu salamu, ila alimuuliza “wewe ndiye umeniita??”
“Ndio…nimeona watu wengi sana pale, nikaogopa kukufuata”
“Pole sana” alisema “Hivi nikuulize kwanza hivi jina lako halisi unaitwa nani??”
Changa akatabasamu na kujibu “Naitwa Changa”
“Nini? Shanga??”
Changa akacheka na kujibu “Sio shanga, ni Changa bhana” alisema
“Ahaaa…nina wateja niambie ulichoniitia”
“Ah nimekuja kukuomba msamaha kwa kile nilichokufanyia usiku” alisema
“Kwani ulifanyeje??”
“Naamini nilikuumiza nilipokukuta ukiwa na mwenzangu……”
“Ah usijali” alijibu rasi “Basi mi naondoka”
“Hapana usiondoke kwanz…..ninahitaji kitu kutoka kwako” alisema
“Kitu gani”
“Kaka Hamis naomba niwe mpenzi wako” alisema
“Khee tena?” aliuliza
“Ndio, mwenzako mi nimekupenda nimenogewa na penzi lako…..”
Hamis alimtazama Changa kuanzia juu mpaka chini kweli ni binti mzuri, halafu hata hatumii gharama, kila siku ni kupewa tu, binti akasema “Ila nataka niwe peke yangu usiwale wale wengine”
“Duuh….usiku unakuja?” aliuliza Kapweto
“Yes nitakuja”
“Okay tutaongea zaidi, ngoja niende kule wasije wakaniibia”
“Sawa ila”
“Ila nini??”
“Naomba namba yako” alisema Changa huku akiitoa lock simu yake
“Okay…..07……………….”
Changa aliiandika kisha akaondoka zake.
Binti aliondoka akarudi nyumbani akiwa na furaha tele, kiukweli hata Rasi mwenye alikuwa ameshamzimia mtoto Changa, alikuwa na penzi tamu, alikuwa fundi kushinda hata Vero, halafu ndo kabisa ni katoto, kuwa na katoto nako kuna raha yake.
Hamis aliendelea na majukumu yake ya kila siku
Sasa wakati Changa anarudi nyumbani, ndipo njiani akakutana na Vero, tena alikuwa amebeba kuku mweusi na anaelekea kule kule kagera kwa rasi.
Changa akashtuka na kumuuliza
“Unampeleka wapi kuku wako huyo?” aliuliza Changa huku akionyesha dhahiri kutokufurahishwa na kitendo hicho
“Embu pita zako, kwani yanakuhusu nini??” alisema Vero na kumpita akaendelea na safari
JE VERO ANAPELEKA WAPI KUKU MWEUSI?
KIPENGELE CHA 10
Changa alirudi nyuma na kumshika kwa nguvu “Unataka kwenda kumfanya zezeta kama ulivyoahidi si ndio?” aliuliza Changa kwa hasira
“Zezeta?? Embu niache bhana kila mtu apambane awezavyo mimi mwenyewe nimempenda” alisema yule binti Vero
Changa alimuachia Vero halafu akamtazama na kufikiria afanyaje akamtazama Vero huyo anaondoka anaelekea kwa rasi, ndipo binti akapata wazo achukue simu yake ampigie Kapweto lakini cha kushangaza simu yake kamwe haikupatikana.
Binti alipata wasiwasi mkubwa sana kwa sababu aliamini ameshaingia kwenye mashindano makali yeye na mchawi mwenzake kutaka mapenzi ya kweli.
Changa alikuwa sio mbaya lakini Vero alikuwa wa kawaida sana, hakuwa na urembo ule wa Changa, hata hivyo Vero alifanya hivi kwa sababu aliona kama vile wawili wale wameshaanza kupendana kiukweli, kwani hata usiku, Kapweto alipogundua kwamba yule ni Vero amelala naye na sio Changa, alishtuka na kuonekana kutokufurahia kile kitu.
Vero alitembea mpaka nyumbani kwa Kapweto, hakujali mtu yoyote pale, alimfuata moja kwa moja Kapweto, na Kapweto alikuwa kama kapumbazika wala hakusita kupokea ile zawadi ya kuku mweusi kutoka kwa Vero.
Alifurahi sana, ubaya mmoja ni kwamba Kapweto yeye alikuwa anajiona kama nyota imeng’aa kwa sababu mabinti wote walikuwa wameshampenda.
“umeniletea wa nini jamani?” aliuliza Kapweto huku akimpokea yule kuku
“Ni zawadi” aliongea kisha akamsogelea na kumnong’oneza “Natamani unywe supu ili uweze kunikuna vizuri nikija kwako”
“Mmmh sawa” alisema Kapweto
Vero akasisitiza “Hakikisha umemnywa supu Rasi”
“Usiwaze”
Baada ya kupewa yule kuku, alimtupia bandani kwake ambapo alichanganya na kuku wengine watatu aliokuwa akiwafuga pale nyumbani.
Kapweto aliendelea na kazi zake lakini Vero aliondoka pia. Ilikuwa ni hatari kwa afya ya Kapweto.
Bila kufahamu kinachoendelea Kapweto ilipofika usiku wateja wote wameshaondoka, yeye akamkamata yule kuku mweusi na kumchinja halafu akajichemshia supu nzito kabisa na kuanza kuinywa.
Kutokana na utamu wa ile supu Kapweto alipata usingizi mzito mapema tu saa tatu alilala sana, wala alikuwa halali kiasi kile.
Hata hivyo ilipofika usiku wa saa sita, wachawi waliungana kwenye mkutano wao, siku hiyo jahazi lilikuwa linaongozwa na Bi Sophia ambaye alikuwa amesimama kwa niaba ya bi Mpwele.
Kwa kuwa mchana Changa alishamuambia bi Sophia ampange kwenda mtaa wa Kagera basi alimpanga bila hiyana, lakini kiukweli Vero hakuwa hata na wasiwasi, kwa sababu alijua kitu alichokifanya
Changa aliinua ungo akapepea mpaka katika mitaa aliyokuwa akiishi rasi, kiukweli alikuwa ameshasahau jukumu lake la kuloga yaani kila muda alichotaka yeye ni dudu tu ya mtaalam.
Changa akazama ndani ya chumba cha Kapweto akamkuta Kapweto anakoroma, jasho jingi linamtoka, taa ameacha ikiwa inawaka, binti akapatwa na wasiwasi kwani alikuwa anajua rasi alikuwa halali mapema sana kutokana na uvutaji wa bangi na mihadarati mingine.
Changa aliketi kando yake, akaanza kumfuta futa jasho lakini bado mwamba alikuwa anakoroma sana, hata hivyo baada ya muda binti alimpanda kifuani akaanza kumchezea, ndipo Kapweto akagutuka usingizini na kushangaaa.
“Wewe” alisema kwa mshangao huku akimuangalia machoni Changa
Changa akatabamu na kusema “Nini jamani”
“Unafanya nini hapa??” Kapweto aliuliza huku akimsukuma kwa nguvu binti akashuka kitandani na kusimama
“Nimekuja kukuona mpenzi wangu,….”
Kapweto aliketi kitandani kisha akashika kichwa na kuuliza kwa mshangao “Mpenzi???????”
“Ndio….hujanijua??” aliuliza
“Wewe si Changa?? “
“Ndio”
“Sasa mimi mpenzi wangu ni mmoja tu…..Veronica” alisema mtaalam
“Tena?? Mbona umebadilika hivi?? Mchana si uliniambia uko tayari tuwe wapenzi?”
“Mimi??” Kapweto aliuliza kwa mshangao kisha akashika tama na kusema “Embu ondoka we unaota”
“Jamani rasi, mimi Changa, hujanikumbuka jana tu tuliongea ukasema unanipenda jamani wewe”
“Ondoka Changa, mpenzi wangu anakuja sasa hivi”
Changa alipomuangalia Kapweto aligundua kwamba mtaalam yuko serious sana, anaongea kutoka moyoni, yaani hamkumbuki kabisa, ndipo akaelewa kwamba tayari kuna kitu amefanyiwa.
Yaani kumbe muda wote mambo hayo yakifanyika ndani, Vero naye alikuwa amejibanza ukutani nyumaa ya nyumba anasikilizia, halafu akafurahi kwa ushindi wa kuuteka moyo licha ya kutumia nguvu za giza
“Ondoka””” Kapweto alisema kwa hasira halafu ghafla mlango ukagongwa kuna mtu alikuwa anahitaji bhangi usiku ule
“Oii rasi nipate msuba kaka” alisema mtu huyo
Binti Kapweto akagundua ni mwanaye mmoja anaitwa Esau, ikabidi atoke akampatie
Sasa wakati anatoka binti akatazama kulikuwa na sahani pale chini iliyokuwa na nyama za kuku ndipo akagungua tayari ashapigwa na kitu kizito ameshamchanganya Vero kwa uchawi hivyo ni ngumu sana kwa mtaalam kumpata tena.
Hasira zilimjaa sana binti Changa, aliamua kuondoka akasepa na kumuacha Kapweto. Alipofika angani tu, na Vero aliingia ndani kumsubiria mpenzi wake.
Yaani Kapweto alipomuona tu, alifunga mlango na kumkumbatia kwa nguvu kwani alikuwa ameshapagawa kutokana na uchawi aliokuwa amefanyiwa.
Walianza kufanya yao kwa muda mrefu, lakini ilikuwa imeshatangazwa vita ya mapenzi kati ya wachawi hao wawili.
Walipofika baadaye katika kikao cha kurudi nyumbani, Changa akasema “Vero amenikosea, amenichukulia mpenzi wangu kule kagera, nataka aachane naye mapema kabla sijaanza naye vita ya kichawi”
“Siachani naye na haunifanyi chochote” aliongea kwa jeuri, kwani siku hiyo walikuwa na uhuru kutokana na kutokuwepo kwa kiongozi wao mkuu bi Mpwele
“Mpenzi gani huyo??” aliuliza Mashaa
“Huoni kila siku anang’ang’ana kwenda huko, hafanyi kazi, siku zote ni kufanya ngono tu”
“Anhaa…kumbe mnapong’ang’ania kwenda kagera mnafuata mambo mengine sio” aliuliza bi Sophia
“Mwambie aachane na mpenzi wangu” alisema Changa
“Siachani naye mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumpenda” alisema Vero na kupaa kwa kutumia ungo wake, akaelekea nyumbani
Wanga walishindwa kuelewa wafanye nini…….
JE ITAKUWAJE??
KIPENGELE CHA 11
Tulipoishia
“Anhaa…kumbe mnapong’ang’ania kwenda kagera mnafuata mambo mengine sio” aliuliza bi Sophia
“Mwambie aachane na mpenzi wangu” alisema Changa
“Siachani naye mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumpenda” alisema Vero na kupaa kwa kutumia ungo wake, akaelekea nyumbani
Wanga walishindwa kuelewa wafanye nini
ENDELEA
Hata hivyo liliishia pale, kwani hilo lilikuwa suala lililokuwa nje na kazi yao waliokuwa wakiifanya kila siku.
Kila mmoja aliondoka kurudi nyumbani kwake lakini kichwani Changa na Vero walikuwa tayari wameshaingia kwenye ugomvi mzito sana.
Asubuhi na mapema, bi Sophia aliamua kumtembelea bibi Mpwele kwa ajili ya kumueleza yaliyojiri mida ya usiku, alipofika kwa Mpwele, alimkuta amelala wajukuu wanacheza cheza pale ndani, akakaa kwenye kiti na kumuuliza
“Waendeleaje na hali??”
Bi Mpwele akajibu
“Niko salama vipi wewe?”
“Salama pia….leo utaweza kuja?” alisema bibi huyo, lakini hata hivyo bibi Mpwele alimtazama kwa jicho ambalo lilimshtua Sophie hii ni kwa sababu pale kulikuwa na wajukuu, alitakiwa asiropoke ropoke maana uchawi ni kitu ambacho kinafanyika kwa siri sana.
“We Rabia,” bi Sophie aliita mjukuu mmoja wa bi Mpwele ambaye alikuwa amekaa pale nyumbani
“Abee” alisema Rabia
“Haya kachezeni nje” alisema bi Sophie
“Sawa”
Wale watoto walitoka na kuwaacha ajuza hao wakiwa wanaongea mambo ya kichawi kabisa
“Ulikuwa unaniuliza nini?” aliuliza Bi Mpwele
“Nilitaka kujua, leo unakuja?”
“Leo sidhani bibie, lakini vipi mlifanikiwa?”
“Kidogo sana, ulitokea ugomvi mkubwa baina ya Changa na Vero” alisema Sophie
“Ugomvi wao ni juu ya mapenzi?” aliuliza
“Ndio kumbe unalijua hili?” aliuliza bi Sophie
“Nilikuwa ninasikia kila kilichokuwa kikiendelea, ndio maana mwanzo sikutaka watoto kwenye utawala wangu, ninahisi hawa ndio wanachelewesha mipango yangu” alisema kwa hasira bi Mpwele
“Ni kweli, hasa huyu Changa, bado utoto unamsumbua bi Mpwele”
“Nitawapa adhabu, watafungwa kuzimu miezi minane”
Upande wa Hamisi Kapweto, alikuwa ameketi nyuma ya kibanda chake cha kuuzia bangi, alikuwa anajisikia rah asana akivuta msuba taratiibu.
Moshi aliuvuta ndani kisha akatabasamu na kusema, “Vero, hakika wewe ni malikia wa moyo wangu, hakuna awezae kunitenga mimi na wewe……niko tayari kuacha kila kitu ili niwe na wewe tu”
Alikuwa ameshachanganywa na kuku mweusi ambaye Vero alikuwa amemlisha siku moja tu kabla, alikuwa anajisikia kumpenda mpaka anataka kufa, alikuwa hataki kabisa mazoea na kale kabinti kadogo kaitwacho Changa japo mwanzoni alikuwa ameshaanza kumpenda penda ila kuku mweusi alikuja kuvuruga mambo
Wakati yeye anawaza hayo yote, kumbe masikini Changa kule alipokuwa, alikuwa analia sana sana sana. Kilichokuwa kikimuuma ni penzi lake, alikuwa amelitetea, muda mrefu hajapata mwanauem ambaye alikuwa anamtoa hamu zaidi ya hamis, halafu mwenzake aje achukue tu kirahisi rahisi
“Hapana sikubali…..Sikubali” alisema binti huyo huku akiwa anafuta machozi “Lazima nimkomeshe, hawezi nichukulia bwana angu”
Aliamini kuna namna atakavyofanya itasaidia yeye kuendelea kuwa na hamisi, binti aliamka, akaenda bafuni, akaoga vizuri, akavaa nguo safi akaweka nywele safi halafu akatoka huku akichezea simu yake.
Alitembea mpaka alipokuwa akiishi Kapweto, alipofika alikuta kapweto ameketi pale pale nyuma anakula msuba, huku mbele watu walikuwa wakinywa na kulewa, wengine walikuwa wanamuibia lakini yeye alikuwa anawaza tu kitumbua cha Vero.
Changa akazunguka nyuma ya kibanda kile kisha akaanza kuongea na Kapweto
“Rasi kipenzi” alisema Changa
“Nini???” aliuliza Kapweto kwa hasira
“Mbona umebadilika ghafla, message zangu hujibu mpenzi?”
“Message gani??? Za nini? Kwani wewe nani??” aliuliza Kapweto kwa dharau
“Jamaani” alisema Changa “Ina maana Vero ameshakuharibu na uchawi?” aliuliza
“Weee tena ishia hapo hapo…….usimuite mke wangu mchawi, ninawaza kumuoa” alisema
“hapana usifanye hivyo, yule hakupendi kakuloga haki ya Mungu”
Rasi aliinuka kwa hasira akamfokea “Malaya wewe…nimeshaambiwa tabia zako mbwa, toka kwangu”
Binti aliogopa, akarudi nyuma na kumtazama
Watu wote waliokuwa kule mbele wakipata vinywaji, waliamua kuinuka na kufuata baada ya kusikia kelele za kufokeana baina ya wawili hao……binti alipowaona, alijisikia aibu sana, akaondoka akiwa amenyong’onyea………..
JE ATAFANYA NINI??
KIPENGELE CHA 12
Tulipoishia
Rasi aliinuka kwa hasira akamfokea “Malaya wewe…nimeshaambiwa tabia zako mbwa, toka kwangu”
Binti aliogopa, akarudi nyumba na kumtazama
Watu wote waliokuwa kule mbele wakipata vinywaji, waliamua kuinuka na kufuata baada ya kusikia kelele za kufokeana baina ya wawili hao……binti alipowaona, alijisikia aibu sana, akaondoka akiwa amenyong’onyea
ENDELEA
Changa aliondoka akiwa anafuta machozi, hajui afanye nini, ameshazidiwa ujanja, akafika mahali akaketi chini ya mti, ndipo akaanza kuwaza achukue hatua gani zidi ya Vero, ili aweze kumuachia tamu yake, aligundua hakuna namna ya kufanya zaidi ya kupambana na Vero ili amuachie.
Kwa bahati mbaya, au nzuri kwa upande mwingine, wakati ana hasira za kumkosa mpenzi wake huyo, binti alipokea sms kwenye kiswaswadu chake akatazama ni Joel alikuwa anampigia, ni kijana mmoja machachari sana alikuwa anapiga bodaboda pale Ujiji, muda mrefu alikuwa akimtakaga Changa lakini Changa akawa hataki mazoea naye, hakumpenda tu
Ule ujumbe uliikuwa unasema hivi “Mambo Mrembo Changaaaa”
Binti akautazama halafu akasonya “mssssiiiiieeew” akaendelea kushika tama huku akikumbuka maumivu anayopitia licha ya kuwa mchawi sana.
Alipokaa akatafakari ana hasira, mtu anayempenda tayari amebebwa, basi Changa akaona ni heri akajibu ule ujumbe
“Safi mambo” alisema
“Safi, umeadimika sana mrembo”
“Nipo” alijibu Changa
“Upo wapi mbona hatuonani siku hizi?”
“Nipo hapahapa Ujiji”
“Mh mi nikajua labda umesafiri?”
“Nisafiri niende wapi? Kwetu ndio hapahapa”
“Tuonane basi” alisema Joel
“Tuonane wapi?”
“Hapa hapa bakwata” alisema
“Mh….ndo umehamia huko?”
“Ndio, niliona huko kwenu jau, halafu mtoto mwenyewe hata hunielewi sasa nabakije huko roho ingeniuma kila nikikuona”
“Hahahaa….makubwa hayo, mi sa hvi niko mtaa wa kagera….”
“Umehamia?”
“Hapana ninatembeatembea tu maana sikuwa na cha kufanya home”
“Sasa kama hauna cha kufanya si uje tu huku kwangu tupige story”
“mh mbalii” alisema Changa
“Nije nikuchukue na baiki?” aliuliza
“Njoo kama unaweza”
“Mtaa gani sasa?”
“Karibia na kwenye mwembe hapa kwa diwani” alisema
“Poa, dakika sifuri”
Joel alikuwa fasta katika suala zima la kufuata mademu, alikuwa kijiweni muda huo, lakini alichomoka kama hana akili nzuri, hakuogopa kuchoma mafuta ya pikipiki, lakini aliamini kama akienda kumchukua mtoto huyo wa kike basi atakuwa anaweza akapewa ile kitu tamu kuliko vyote duniani
Akafika mwembeni kweli akamkuta binti kavaa nguo yake ndefu kang’aa kweli kweli, alikuwa ametoka kwa bebi ila bebi mwenyewe kashamchinjia baharini.
Changa aliwea pikipikipiki, safari ikaanza kuelekea mtaa wa Bakwata, walipofika hivi, Joel alikuwa amepanga karibu kabisa na kwa bi Kamulenga lakini hakuwa anamjua bi Kamlenga kabla, hivyo aliingia tu ndani ya geto la Joel.
Alipofika ndani, alikuta Joel ana chumba chake cha kawaida tu, kuna kitanda na meza “Karibu” alisema Joel kwa mbwembwe, akipasha pasha viganja vya mikono yake
“Asante” alisema binti huku akikagua kagua chumba
“Karibu ukae” alisema Joel na kuketi kitandani
“Asante”
Changa aliketi kitandani halafu akatoa mtandio wake kichwani, joto lilikuwa kali
“Unahisi sana joto ee?”
“Ndio, yaani….acha”
“Nikakuletee soda gani?”
“Yoyote tu”
“Sawa”
Joel alitoka haraka na kwenda dukani, kulikuwa sio mbali sana lakini kulikuwa kidogo kuna foleni hivyo akasubiri kama dakika tano hivi ndio akapewa huduma
Joel alinunua mirinda nyeusi kisha akanunua mo xtra halafu akarudi navyo getoni, alipofika ndani alimkuta bado mtoto kakaa anawaza mambo yake kibao.
Akamfunulia soda na kumpatia, binti akanywa taratibu, sasa wakati anaendelea kunywa Joel akamuwekea mkono begani, Changa akashtuka
“Mh…” aliguna Changa…………
JE NINI KITAFUATA?