SITAMANI TENA KUOA
PART: 11
ILIPOISHIA,
Mheshimiwa hakimu anaahirisha kesi huku akiwataka wote waje na barua ya uthibitisho kutoka Magereza yenye kuonesha kama Mapito yu hai au la!.
SONGA NAYO…
Baada ya tamko hilo, walitawanyika ndipo Sikudhani alipopokelewa na mme wake kwa nje.
“‘Enhee!, ebu niambie imekuwaje?” Salum aliuliza kwa hisia.
“‘Twende nyumbani mme wangu. Nitakwambia mwanzo mwisho…” alitamka
Wakati wanaendelea na mazungumzo, Mapunda akiwa na Rashid, walipita karibu yao huku wakiwa wanacheka kwa tabasamu.
“Hapa lazima waite maji mma. Yaani Hakimu kagusa penyewe” Rashid aliongea huku wakielekea kwenye gari.
Maneno hayo, aliyasikia Salum ndipo alipogeuka na kumuuliza Sikudhani,
“Kwani imekuwaje?, mbona wanacheka na kutasamu?
“‘Na wewe mme wangu mbona kama husikii?!, si nimekwambia nitakusimulia yote nyumbani?!, alitamka kwa hasira kidogo.
“Samahani …” Salum aliomba radhi.
Bila kuchelewa huku wakiwa na uso wa tabasamu, Rashid na Mapunda , waligeuza gari na kwenda moja kwa moja magereza ya segerea huku wakiwa na barua yakutaka uthibitisho kutoka mahakamani.
Baada yakufika, waliipeleka kwa askari kitengo cha mapokezi kisha akaiwasilisha moja kwa moja mpaka mkuu wa Magereza.
Aliisoma kisha akathibitisha kuwa Mapito yu hai na bado hajanyongwa.
“Nathibitisha kuwa mtajwa hapo juu, yu hai na salama na hajanyogwa mpaka hapo mda wake utakapofika kulingana na sheria inavyosema”
Baada ya uthibitisho huo, aligonga mhuri kisha akatia saini.
Walikabidhiwa uthibitisho huo kisha wakaanza kurejea nyumbani.
“Hapa ndo sheria huitwa msumeno. Yaani akishindwa kuthibitisha ina maana moja kwa moja kaidanganya mahakama na anatakiwa kuwekwa ndani..” Mapunda alimwabia Rashid.
“Hee! Kumbe na wenyewe wanaweza kuwekwa ndani!” Alitamka kwa mshangao.
“We endelea kufatilia maana jumatano sio mbali…” Mapunda alimjibu.
“Sawasawa naisubiri kwa hamu siku hiyo…”
( waliendelea na safari )
Huko nyumbani kwa Sikudhan, baada ya kupata chakula cha mchana , waliketi kwenye sofa kisha Sikudhan akaanza kusema,
“Mme wangu yaani hakimu sijamuelewa kabisa… “
“‘Kafanyaje?”
“Yaani eti twende Magereza wasaini kwenye kibarua alichotupatia ili wathibitishe kama yupo hai au la”
“Hahaha..yaani hata 40 yake imeisha. Waache wanajisumbua ila kwakuwa ni agizo la mahakama tutaenda tu japo ni kupotezeana mda”
“Yaani nilifoka mpaka akanitishia kuniweka ndani…”
“‘Hee! hajielewi huyo.”
“Sasa tunaenda lini?”
“‘Twende kesho asubuhi afu hizi gharama ziandike baada ya hukumu ya rufaa tutawadai fidia ya gharama zote…”
“Ni kweli mme wangu…”
Kesho yake asubuhi na Mapema, walielekea Segerea gerezani.
Baada ya kufika, waliwasilisha barua yao ili ikasainiwe.
Mkuu wa magereza alithibitisha kuwa Mapito bado yu hai na wala hajanyongwa.
Walipokabidhiwa barua hiyo, Walishagaa na kumuuliza askari wa mapokezi,
“‘Kwanini ameandika hivi?”
“‘We ulitaka aandikeje!, unamfundisha kazi eeh!” Askari aliwafokea
“‘Sio hivo afande yaani huenda amekosea maana huyo mtajwa ni mme wangu na siku yake ya kunyongwa nilikuwepo” Sikudhan aliongea
“Wewe ndo ulimnyonga au!?, ebu ondoka hapa!, badala ufurahi kuwa mme wako yu hai afu unang’ang’ania eti emenyongwa!, toweka hapa ..”
Sikudhan akiwa na Salum, waliondoka kinyonge sana kuelekea nyumbani.
“‘Hivi ni kweli alinyongwa au bado?” Salum alimuuliza Sikudhan
“Nina uhakika wa 100% kuwa alinyongwa tena kitambo sana” alimjibu.
“Mhh..hapa naanza kuona kama kuna mkono wa mtu. Hapa kuna Rushwa inatembea lakini uzuri kashanyongwa na hawezi rudi tena duniani” Salum alitamka.
“Wanajisumbua tu …..”
Kesho yake ile siku iliyokusudiwa iliwadia ndipo pande zote mbili walipojiandaa kuelekea Mahakamani.
Mnamo mida ya saa 2 na nusu, kesi yao ilitajwa ikiwa ya kwanza kisha wakaingia ndani.
“Niliwaagiza kila mtu aje na uthibitisho naamini mmefanya hivo” mheshimiwa hakimu aliongea.
“Ndiyo” Mapunda alijibu.
“‘Na wewe?” Alimuuliza Sikudhan.
“Nimeleta lakini sijaiafiki!”
“‘Ebu acha kutuchezea na kutupotezea mda. Umeenda mwenyewe na umethibitishiwa. Unakaa nini?, mahakama inatambua uthibitisho huu kuwa ndo halali. Ukweli umebainika na ni kweli kuwa Mapito yu hai na umeidanganya mahakama hivo kwa mamlaka niliyonayo, ninakuweka ndani kwa masaa 2”
Kabla hajajitetea, askari walimchukua Sikudhani na kumuweka Cello.
Alilia sana lakini kilio kisingepunguza hukumu yake.
Mle Cello kulikuwa na harufu nzito sana iliyomfanya ayaone masaa mawili kama miaka 100.
Baada ya masaa kutimia, walimfungulia kisha akarejeshwa chumba cha mheshimiwa hakimu.
“Nimepitia hoja za rufaa hii, sitaki nicheleweshe maamuzi kwa mara nyingine tena. Nimeagiza shahidi anaýeitwa Zuwena awepo mda huu ili athibitishe mbele yangu hivo tusubirie kwa mda mfupi maana ameshafuatwa”
Sikudhani kusikia hivo, alishutuka kisha akajikuta anatokwa na haja ndogo mbele ya Hakimu….
JE ZUWENA ATATHIBITISHA?
JE MAPITO ATAOKOKA AU NDO MWISHO WAKE?
PART: 12
ILIPOISHIA,
Zuwena anasubiriwa kuthibitisha ushahidi wake kwa mara nyingine mbele ya mheshimiwa hakimu..
SONGA NAYO…
Wakiwa wamekaa ndani ya mahama, walishangaa kumuona Zuwena akiwa anaingia ndani.
” Mheshimiwa huyu hapa shaidi namba 01″ askari alitamka.
Kwa utaratibu wa mahama, ushahidi ni siri hivo sikudhani pamoja na Mapunda, walitoka chumbani humo na kumuacha Zuwena.
Zuwena alikuwa anatetema sana huku akiwa hajui ameitiwa nini.
Alipewa kitabu kitakatifu na kisha akaapa ndipo mheshimiwa hakimu alipoanza kumhoji.
” Unaitwa nani?”
” Naitwa Zuwena Ali Mapito”
” Una miaka mingapi?
” 15″
” Dini yako?”
” Mwisilamu”
” Unamjua Mapito?”
” Ndiyo?
” Mna uhusiano gani?”
” Ni baba yangu”
” Zuhura je?”
” Ndiyo”
” Ni nani kwako?”
” Ni mdogo wangu”
” Yuko wapi?”
” Yupo nyumbani”
” Anafanya nini?”
Zuwena alikaaa kimya kwa mda kisha mheshimiwa hakimu akamuuliza tena,
“Anafanya nini?”
” Hapana nilikosea hayupo “
” Alienda wapi?”
” Aliuawa na baba”
” Wakati anauwawa ulikuwepo?”
” Hapana”
” Ulijuaje kama ni yeye?”
(Zuwena alikaa kimya)
” Jibu swali..”
” Nilisikia kama anamuua”
” Ulisikia wala hukuona si ndiyo”
” Ndiyo”
” Sawa alizikwa wapi?”
” Nyumbani”
” Kuna kaburi lake au hamna?”
” Kaburi lipo”
” Siku ya mazishi ulikuwepo na ulishiriki kumzika mdogo wako?”
” Ndiyo”
” Mwili wake uliuaga kwa mara ya mwisho?”
” Ndiyo”
“Alipomuua mwili wake mliupata wapi?”
” Hapana hatukuupata yaani aliufunga kwanye kiroba na kwenda nao”
” Alivyokwenda nao ulimuona?”
” Ndiyo”
” Ulikuwa na nani?”
” Na mama”
” Baada ya kumuona ulipiga kelele?”
” Hapana”
” Na mama yako je?”
” Naye hakupiga kelele”
” una mapungufu yoyote ya kiakili?”
” Hapana..”
” Uliyoyaongea hapa ni sahihi?”
( Zuwena alikaa kimya)
” Ebu jibu”
” Ndiyo”
” Upo tayari kuwajibika kwa lolote lile?”
( Zuwena kimya)
” Nakuuliza”
” Nisamehe”
” Ebu mpumzishe kwanza lisaa limoja ndani afu mrudishe” alimwambia askari.
Zuwena alipelekwa Cello ya watoto ndipo alipoanza kulia kama ndama aliyefiwa na mama yake.
” Nisamehe acha niongee ukweli..nisamehe!, “
” Hapa hatuwezi kutengua uamuzi. Utakaa ndani kwa lisaa limoja na ukirudi uongee ukweli” Askari alimwambia.
Alimfungia na kumuacha ndani akiwa analia huku akitamani kulina hata jua.
Wakati Zuwena yupo ndani, Mheshimiwa hakimu alimuita Sikudhan kisha akamuapisha na kuanza kumuuliza maswali,
” Unamfahamu Zuhura?”
” Ndiyo”
” Ni nani kwako?”
” Mwanangu”
” Sasa hivi yuko wapi?”
” Ameshatangulia mbele ya haki “
” Ulishirikia mazishi yake?”
” Ndiyo”
” Mwili wake ulifanikiwa kuuaga”
” Ndiyo”
” Ulijuaje kama ameuawa na Mapito?”
” Niliambiwa na Mwanangu Zuwena”
” Kwahiyo uliambiwa wala hukuona?”
” Ni kama nimeona japo sikuona”
” Ebu nyoosha maelezo. Uliona au uliambiwa?”
” Niliambiwa”
” Baada ya kumuua Mapito alikimbia?”
” Hapana “
” Ashawahi kuwa na upungufu wa akili?”
” Hapana”
” Huo mwili wa marehemu wewe uliikuta wapi?”
” Yaani inasemekana alipamaliza kumuua alimfunga kwenye gunia na kumtupa kwenye bahari”
” Mwili mliokota baharini si ndiyo”
” Hapana hatukufanikiwa kuuona”
” Mlizika udongo”?
” Ndiyo”
” Sawa”
” Una mapungufu yoyote ya kiakili?”
” Hapana”
Wakiwa bado ndani, Karani aliingia ndani kisha akampatia mheshimiwa hakimu kibarua ambacho alikiandika Zuwena.
Alikisoma kisha akakibana kwenye faili.
Kisha akatoa amri ya kukamatwa kwa Salim.
Akiwa amekaa kwenye benchi huku akisubia nini kinaendelea, alishangaa kupigwa pingu na kupelekwa moja kwa moja Cello.
” Uko chini ya ulinzi mda huu” askari alitamka.
” Kosa langu ni lipi?” Alimuuliza
” Mda si mrefu utaletewa hati ya makosa yako”
Baada ya lisaa limoja kuisha, Zuwena alifunguliwa kisha akarudishwa mahakamani,
Alifuta machozi kisha akulizwa,
” Ieleze mahakama ukweli uweze kuachiwa huru” hakimu alimwambia.
” Nilichosema ni kweli” Zuwena alitamka.
” Sawa”
Hakimu alinyanyuka kwenye kiti kisha akasema,
” Kwa taarifa niliyoipokea, inatupasa kama mahakama kwenda mpaka nyumbani kujiridhisha na hukumu itatolewa hukohuko”
Askari alibeba mkoba wa hakimu kisha akaambatana na Sikudhan, Zuwena , Mapunda na Rashid .
Mnamo mida ya saa 8 za mchana, walifika nyumbani kwa Sikudhan kisha wakaanza upekuzi kuanzia nje mpaka ndani.
Kijasho chembamba kilianza kumtoka Sikudhan huku akiwa anatetemeka….
JE ILIKUWAJE?
PART: 13
ILIPOISHIA
Sikudhan kijasho chembamba kilianza kumtoka mara baada ya ukaguzu kuanza…
SONGA NAYO…
Wakati askari wengine wanaendelea na upekuzi kwa ndani, wengine walienda moja kwa moja mpaka kwenye kaburi la Zuhura kwani lilikuwa hatua chache kutoka nyumbani hapo.
Waliendelea na zoezi la kufukua kaburi kwa mda wa dakika kama 30 hivi ndipo walipofika sehemu iliyokuwepo Sanda nyeupe ambayo ilikuwa imeanza kupoteza uweupe wake.
Bila uoga wowote, askari wakiwa wamevalia, walinyanyua sanda hiyo ili kujiridhisha.
Baada ya kulifunua, hawakukuta mabaki yoyote yale ya mwili wa Zuhura na badala yake walikuta mfuko uliokuwa na udongo kwa ndani.
Walipiga picha na kisha wakaandika ripoti.
Huko kwa ndani, ukaguzi mkali uliendelea lakini hawakuona chochote kile ndipo walipotaka kuondoka.
Sikudhan alishusha pumzi chini lakini cha maajabu askari alifanikiwa kunasa pakiti nzima ya vidonge kutoka kwenye mfuko wa suruali ya Salum.
“‘Nini hii?” Walimuuliza Sikudhan
“Sijui” alijibu.
“‘Nyie ndo mnashoriki kwenye madawa ya kulevya…” alitamka kisha akawaonesha askari wenzake.
Baada ya kuzikagua askari mmoja alisema,
“‘Hizi ni dawa za ARV”
“Hee!”..Sikudhan alishutuka.
“Sasa unashutuka nini wakati zipo nyumbani kwako?” Walimjibu.
Sikudhan alidondoka chini kwa mshutuko huku akiwa haamini kama atakuwa salama au la.
Walimpepea na baada ya mda mfupi alizinduka kisha akaanza kumwaga machozi.
Wakati ukaguzi unaendelea, Salum alijikuta anajiuliza maswali ambayo hakuyapatia majibu yake .
Aliendelea kukaa Cello huku akiwa chini ya ulinzi mkali sana.
“‘Wanataka kunifanyaje?” Alijiuliza huku akiwa anatetemeka.
Baada ya mda mfupi, alipakiwa kwenye defenda kisha akaingizwa kwenye chumba cha siri.
“‘Vua nguo zote” walimuamrisha.
“‘Nivue nguo mnataka kunifanya nini ?” Aliwauliza.
“Unaleta kuburi eeh!” Walimshika kwa nguvu kisha wakampiga pingu na kuanza kupata kipigo kitakatifu.
“Msiniue acha nivue…msiniue..”
“‘Pumbavu weeewe!” Walimfungua pingu ndipo alipoanza kuvua nguo mwenyewe.
Alipomaliza kuvua, walimwambia,
“‘Lala chini na usigeuze kichwa chako!” Walimuamrisha.
Akiwa anahema, alifanya hivo.
“‘Unalijua kosa lako?” Walimuuliza
“‘Mi sina kosa lolote” alijibu.
” Kwa mara nyingine!, unalijua kosa lako?”
Salum alikaa kimya kidogo huku akitafakari ndipo walipounguza kipande cha plastic kisha wakamdondoshea kiunoni.
“‘Mama!..mama!..mnaniua” Salum alipiga kelele.
“‘Bado mpaka utaje mwenyewe laa sivyo utainguzwa kila sehemu”
“Subiri nikumbuke nawambia..yooo!..yoo!” Alipiga kelele.
Akiwa anajigalagaza, alimwagiwa maji ya barafu kwelikweli kisha wakaanza kumpa kichapo.
“‘Hutaki kusema!, jiandae kufa yaani hapa hutoki bila kutaja kosa lako.”
Salum akiwa anasuburias kutoa tamko, Sikudhan na Zuwena nao waliwekwa kikaangoni kila mtu sehemu yake.
Walianza na Sikudhan,
“Tuna taarifa zako mwanzo mwisho!, tunachokuomba ni kuwa mkweli na utasamehewa. Kama hutaki kuwa mkweli, hakikia utakuwa mwisho wako kuliona jua “
“Ukweli upi?, nimeshaongea kila kitu nanyi mmekagua nyumba nzima sasa mnataka nifanyeje”
“‘Sawa suburi tukuoneshe kazi..” walimshika kwa nguvu na kumtia pingu mikononi kisha wakamfunga miguu.
Baada ya kumfanya hivo, walichukua rungu na kumgonga kwenye kucha yake ya mguu wa kulia ndipo alipohisi kama anakata roho kwa maumivu hayo.
” Mnaniua!..mnaniua..!” Alipiga kelele.
Akiwa anaendelea kutoa kilio, walimponda rungu jingine kwenye jeraha lilelile ndipo aliposema ,
” Niache nasema, nasema..msiniue acha niwambie…”
” Tunakupa dakika 3 za kuandaa majibu ngoja tunshugulikie na mtoto wako”
Walimfuata Zuwena kisha wakambananisha lakini hakuongea chochote..
” Tubaomba utwambie ukweli wa hili swala” walimwambia.
” Mi sijui…”
” Sawa haina jibu utaongea tu..”
Bila huruma, walimshika na kuanza kumcharaza fimbo kama mtoto mdogo ndipo aliposema,
” Msiniue..msiniue…, mama ndo anajua kila kitu mimi sijui vizuri ..”
” Mama anajua nini!, hee! Ebu ongea…”
” Naogopa ndo maana niliandika barua na sitaki mama ajue…”
” Unauhakika unachokisema…”
” Ndiyo msiniue…”
” Tunakuua” walikoki bunduki kisha wakarusha risasi baridi ndipo Zuwena alipotaka kuchanganyikiwa
” Hawa mbona leo watataja kila kitu?, yaani ni suala la mda tu” askari mmoja alitamka huku akiwa anatabasamu.
Walimuacha ndani kisha wakamfuata mama yake yaani Sikudhan.
Sikudhan baada ya kuwaona, alitetemeka huku akiwa anaugulia maumivu makali ya kucha.
” Haya tumerudi!, dakika 1 umepewa ongea…”
” Nataka kuongea lakini naogopa…”
” Ongea hatutokufanya chochote. Ukiwa mkweli utasamehewa ila ukiendelea kudanganya utakuwa kwenye wakati mgumu”
” Ni kwamba ..yaani mimi sikuhusika moja kwa moja ..ila ..ila ..ni Mme wangu Salum”
” Kuhusika kufanya nini!, ebu ongea” walimlamba makofi.
” Samahani naomba abaki mmoja ili nimwambie maana naogopa..” alitamka.
” Acha kutupotezea mda, nje yupo mheshimiwa hakimu amefunga ofisi kwa ajili yako..”
” Nimeomba , “
” Sawa ebu ongea…”
Askari wengine waliondoka chumbani humo na kumuacha askari mmoja mzee wa kazi jicho nyanya ambaye hajui kutabasamu na wala hajawahi kutabasamu.
” Ebu ongea …” Askari alitamka huku akiwa ameteka kamera ya simu yake anamrekodi.
” Afande nipo tayari kukupa chochote lakini unisaidie niokoke kwa hili maana naweza kuishia pabaya..”
” Unataka kunipa nini cha kukuacha! Hee! ” alitamka kwa hasira.
” Sogea nikunong’oneze “
” Hivi unanionaje?. Ebu acha utani, nitakuvuruga dakika 1″
Baada ya kujibiwa hivo, Sikudhani alivuta kigauni chake kwa juu kidogo na kuyaacha maumbile yake ( mapaja) nje kabisa kisha akamsogelea Askari huyo ambaye alitia jicho moja …
JE ILIKUWAJE ?
JE SALUM ANATAGUNDUA KOSA LAKE?
NA JE KUNA SIRI GANI MPAKA WANAOGOPA KUSEMA?
PART: 14
ILIPOISHIA,
Sikudhan yupo na askari mmoja chumbani ….
SONGA NAYO….
Askari huyo alimuangalia Sikudhani jicho kali sana kisha akamtamkia,
“Sina shida na uchafu wako. Nipo kikazi! Jiheshimu”
Sikudhan kwa aibu kali aliinamisha kichwa chini mithili ya aibu aipatayo kunguni mara baada ya kumulikwa na mwanga.
Askari alizidi kusubiria majibu kutoka kwa Sikudhan lakini hakupata chochote kile.
Kwa hasira kali, askari alitoka chumbani humo kisha akawafata wenzake.
“‘Huyu anatuchezea akili zetu lakini ukweli tunamchekea.” aliongea askari mmoja.
Wote walikaa kimya na kuwaza ndipo walipomfuata Zuwena huko chumbani.
“‘Sasa mheshimiwa hakimu ametutuma kwa mara ya mwisho, ebu uongee ukweli maana ukishindwa adhabu yake ni kifungo cha maisha”
“Ngoja niongee ila msimwambie mama”
“‘Ongea…”
“‘Ni kwamba, mama alimshika mdogo wangu aitwaye Zuhura kisha akamfunga kitambaa mdomoni mikono. Baada ya hapo, walimuweka kwenye stoo ya vyombo “
“Ina maana Yupo?”
” Ndiyo yupo lakini kwa sasa hivi nilizuiliwa kumuona”
“Halafu ilikuwaje kusema ameuwawa na mzee Mapito mahakamani?”
“‘Mama aliniambia niongee uongo mara baada ya kuniahidi kuninunulia gari na baba wa kambo ambaye ni tajiri”
“Sawa.., unaweza kutupeleka alipo huyo mdogo wako?”
“Ndiyo….”
Waliongozana huku wakiwa hawaamini mpaka kwenye stoo.
Walipofika sehemu hiyo, walishangaa na kuona kama anawadanganya kwani walikuwa wameshakagua.
“Ni hapahapa au sehemu nyingine?” Walimuuliza.
“‘Ni humu kwa ndani..”
“‘Mbona tumeingia hatujaona chochote?”
“Yupo njoo niwaoneshe..”
Walinyanyua vifaavifaa ndipo wote walipobaki na mshangao kwa kumuona Zuhura akiwa amefungwa kitambaa mdomoni pamoja na mikono.
Walistaajabu ndipo harakaharaka walipomvuta huku akiwa amekonda sana mpaka amebadilika sura.
Walimfungua na kumtoa mpaka sebuleni kisha wakamleta Sikudhan na kumuuliza,
“Mama..huyu unamfahamu?”
( Hakujibu chochote).
“‘Huna hata uchungu. Unafikia hatua ya kumtesa namna hii mwanao tena wakumzaa mpaka unamchimbia kaburi!. We ni muuaji.”
Ndani ya mda mfupi, walimbeba Zuhura kuelekea hospitali ya Muhimbili ili kupatiwa matibabu japo matumaini ya kupona yalikuwa hafifu sana.
Bila kuchelewa mheshimiwa hakimu alitoa hukumu palepale kama alivyokuwa amepanga.
“Kwa mamlaka niliyonayo, natengua hukumu ya mwanzo ambayo ilimtia hatiani Ali Mapito. Na kuanzia mda huu natangaza yupo huru na aachiwe bila vikwazo vyovyote. Pia mahakama imewatia hatiani Sikudhani pamoja na Said Salum kwa kutaka kutekeleza jaribio la mauaji kwa mtoto Zuhura Mapito. Hivo basi watatumikia adhabu ya miaka 30 jela. Pia mahakama imemfunga kifungo cha nje Zuwena Mapito kwa kipindi cha miaka 2”
Baada ya kutamka hivo, walimtia kwenye defenda Sikudhan kisha wakampeleka Gerezani Segerea.
Akiwa kwenye chumba maalum, Salum naye alisomewa hukumu kisha akapandishwa mpaka Segerea.
Mnamo mida ya saa 12 za jioni, shangwe vigelegele na nderemo vilitanda nyumbani kwa Mapito mara baada ya kutolewa jela na kukikwepa kifo.
Watu walikusanyika kwa wingi huku Mapito akiishia kulia tu hasa baada ya kuona kaburi lake.
“‘Mwanangu nyamaza. Uliambiwa uanaume ni kazi. Muachie Allah atatenda” mama Mapito aliongea.
Mapito alimtizama mwanaye Zuwena kisha akainamisha kichwa chake chini ndipo Zuwena alipomwambia baba yake kwa uchungu.
” Nisamehe baba!..nisamehe baba. Nilitenda kosa kubwa sana ambalo nilidanganywa na mama”alitamka huku akimwaga machozi.
Rashid pamoja na watu waliokuwepo, walitaka kumshambulia Zuwena lakini Mapito aliwambia,
” Muacheni alitenda kosa ambalo halikuwa kosa lake” Zuwena alisogea kisha akakaa pembeni mwa baba yake.
Baada ya wiki moja, Zuhura alirudishwa nyumbani akiwa amepona kabisa huku Mapito afya yake ikiwa imeimarika kwa kiasi chake.
Alipomuona baba yake, alimkumbatia , Nuru ilitanda furaha ikarejea amani ikatawala na giza likatoweka.
######NA HUU NDIO MWISHO WA SIMULIZI YETU#######