Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

SITAMANI TENA KUOA

PART: 01

Ni siku ya jumatatu iliyokuwa imesubiriwa kwa hofu na matumaini makubwa na Ali Mapito aliyekuwa gerezani Segerea huku akisubira kupelekwa kisutu kwa ajili ya hukumu ya kesi yake ya ubakaji na mauaji ya mtoto wake Zuhura.

Akiwa amejilaza kwenye sakafu la Segerea huku machozi ya damu yakiwa yanamtoka, gafla askari Magereza alifungua mlango na kutoa amri.

“‘Ali Mapito!” Alimuita kwa mshutuko.

“Ndiyo afande..!”

“Toka nje haraka…”

Bila kuchelewa huku akiwa anachuruzikwa na Machozi, alitoka kwenye chumba hicho kisha akasogea na kupigwa pingu na kurushwa kwenye defenda iliyokuwa imelindwa na maafande sita wote wakiwa wameshikilia mitutu ya ukweli.

“‘Unalia nini mjinga wewe!, baba mzima unadiliki kumbaka mwanao na kumuua afu unamwaga machozi!, mpuuzi mkubwa wewe!, ebu toa upumbavu wako..!”

Ali Mapito alikanyagwa mgongoni na kuzama kwenye miguu ya buti za maafande.

Akiwa kwenye ulinzi mkali, safari ya kutoka Segerea kwenda Mahakama ya Rufani Kisutu jijini Daresalaam, ilianza.

Mnamo mida ya saa 2 na nusu za asubuhi, walifika kwenye viunga vya mahakama hiyo kisha wakamshusha na kumpandisha kizimbani.

Mapigo ya moyo yaliongezeka huku Machozi yakizidi kumchuruzika mpaka watu waliokuwa wamesubiria hukumu hiyo wakajikuta wanamshangaa.

Akiwa anasubiri dakika zake za mwisho kabla ya hukumu, Ali Mapito aliangaza macho yake na moja kwa moja yakagusana kwenye mboni za mke wake autwaye Sikudhani pamoja na mtoto wake Zuwena.

Baada ya kuangaliana, Sikudhani aliinamisha kichwa chake chini huku Zuwena naye akifanya hivyo kama mama yake.

Hayawi hayawi sasa yalikuwa mara baada ya mheshimiwa hakiwa kuingia ndani ya mahakama huku akiwa amevaa mavazi yake maalumu yaliyo na muundo kama mavazi wavaayo maaskofu au Mapadre.

Watu wote walisimama kama kutoa heshima kisha wakaketi.

Akiwa kizimbani, alitolewa na askari na kusimamishwa mbele ya mheshimiwa hakimu huku akiwa amefungwa pingu.

Alijikuta anatetemeka kama fundi cherehani huku Mheshimiwa hakimu akiwa anapokea faili la hukumu na kulipia.

“‘Eeh mwenyezi Mungu, muumba mbingu na dunia , baba mwenye kutenda haki, usiye na upendeleo, usiye chuki, usiye na hasira, nakuomba ..mimi mwanao unisaidie katika wakati huu mgumu kwangu kama ulivyowaokoa wanao kutoka utumwani Misri..” Ali Mapito aliomba kwa sauti ya chini.

Ndani ya mda mfupi, watu wote waliombwa kukaa kimya kwa ajili ya kusikiliza hukumu. Mheshimiwa hakimu alishika faili lake na kuanza kusoma hukumu..

“‘Ifuatayo ni hukumu ya kesi ya jinai ya ubakaji na mauaji namba 05 ya mwaka 2018 .

Mshitaki ni Sikudhani Kasimu ambaye ni mke wa Ali Mapito.

Mshitakiwa ni Ali Mapito ambaye ni mme wa Sikudhani Kasimu.

Mahakama imesikiliza kesi hii ambapo mtuhumiwa anatuhumiwa kufanya ubakaji na kisha kumfunga kwenye kiroba na kumtupa kusikojulikana binti yake mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Zuhura.

Katika kusikiliza kesi hii, shahidi namba moja ambaye ni mtoto wake aitwataye Zuwena, aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 05 mwezi wa 7 saa 12 za jioni, alimuona baba yake akifanya kitendo hicho cha kikatili na baada ya kuonwa, alimwambia atunze siri ili asimwambie mama yake.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa, baada ya tukio hilo, alimuona baba yake akiwa amebeba kitu kilichokuwa kimefungwa kwenye guni kubwa.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa, baada ya mama yake kurudi, alimnong’oneza kwa siri ndipo alipokwenda moja kwa moja mpaka kituo cha polisi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kwa upande wa mshitakiwa, alisomewa mashitaka na alikana katakata kuwa hakuhusika katika tukio hilo huku naye akidai anashangaa na hajui wapi mtoto wake alipo.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa, tarehe ya tukio kama ilivyotajwa, alikuwa kazini na rafiki yake lakini alipoombwa na mahakama kumleta rafiki huyu kama shahidi, alishindwa.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa, tukio hilo ni la mgogogoro wa kifamilia kati yake na mke wake ambao alidai walikuwa nao hasa baada ya kumtuhumu kutoka nje ya ndoa.

Mahakama pia ilipokea vielelezo vya kiushahidi kutoka kitengo cha polisi ambavyo vimeambatanishwa kama kielelezo namba 02.

Mwisho, mahakama tulifunga shauri na kuja na maswali makuu matatu yafuatayo..

1. Je tukio lilifanyika kweli?

2. Je kwanini atuhumiwe yeye?

3. Je sheria inasemaje kama amehusika au la?.

Mahakama imekuja na majibu haya mara baada ya kujiridhisha bila shaka lolote kutoka pande zote mbili…..”

( Mheshimiwa hakimu alifunua kitabu chake cha sheria huku watu wote wakiwa wametega masikio taharuki kubwa).

JE HUKUMU ILIKUWAJE?

PART: 02

ILIPOISHIA,

Mheshimiwa hakimu alianza kufunua kitabu cha sheria ili kutoa hukumu huku watu wote wakiwa wametega masikio kwa taharuki kubwa..

SONGA NAYO…

Mheshimiwa hakimu baada ya kumaliza kukagua kitabu chake, alikohoa kidogo kisha akainama na kutoa hukumu.

“‘Mahaka baada ya kuibua maswali haya ya msingi, imejiridhisha pasìpo na shaka lolote kuwa, Ali Mapito amehusika moja kwa moja katika makosa mawili ambayo ni ubakaji pamoja na mauaji huku akiwa anajua kuwa ni kinyume na sheria.

Hivyo basi, mahakama imemtia hatiani na atatumikia adhabu ya kifo. Mwisho, Rufaa iko wazi kuazia leo mpaka mpaka siku 30″

Alifunga kitabu chake kisha akanyanyuka na kurudi chumbani.

Ali Mapito, aliishia kumwaga machozi huku akiwa haamini kile alichokisikia.

Alimuangalia mke wake kisha akamwaga chozi .

Ndani ya dakika chache, askari walimvuta kwa nguvu na kumsukumizia kwenye defenda kuelekea Segerea.

Wakati anatolewa mahakamani hapo,

Zuwena alimuuliza mama yake,

“‘Mama..!mama!..ina maana baba hatutamuona tena?” Alitokwa na machozi.

“‘Aende zake . Utapata baba mwingine “

” Mhh.. baba mwingine!” Alishangaa

” Ndiyo…”

” Mhhh…” aliguna.

Taratibu walianza safari ya kurudi nyumbani huku Sikudhani akiwa mwenye furaha mara baada ya hukumu hiyo.

Huko upande wa Ali mapito, baada yakufikishwa Segerea, alivuliwa nguo zote kisha wakamuambia ainame na kumchunguza ili kuona kama kuna siraha yoyote.

” Inama mpuuzi wewe!” Askari alitamka.

” Kwanini mnanidharirisha hivi ili hali sina kosa lolote ?!” Alitamka kwa uchungu.

” Unataka kutuchokoza!, ” walimvuta kwa nguvu na kumtoa nguo huku akipokea buti zakutosha.

Baada ya ukaguzi, walimpatia nguo maalumu za wafungwa zilizokuwa na rangi ya njano kisha wakamuweka kwenye chumba maalumu cha wafungwa waliokuwa wamesubiria kunyongwa.

Alisukumwa ndani na kuwakuta wenzake wakiwa wameshakata tamaa,

“‘Karibu muuaji mwenzetu..” wafungwa walimtamkia

Ali Mapito alishindwa kuitikia nakujikuta analia.

“Mwamba hata saa moja hujamaliza ushaanza kulia!, ebu tulia unatuaibisha” walimwabia

Baada ya mda wa lisaa limoja, mfungwa mmoja ambaye alikuwa amekondeana kweli, alimfuata Ali Mapito na kumuuliza,

” Ulifanya kosa gani ndugu?, mimi nilimuua mshua wangu ila mpaka sasa najuta kabisa.”

” Nimehukumiwa kifo kwa kosa ambalo sijlifanya. Kinachoniuma zaidi ni mwanangu aliyedaiwa kuuawa lakini pia mwanangu wa kwanza alienda mahakamani kutoa ushahidi kuwa aliniona nambaka na kumuua…” alimwambia.

” Hujahisika kweli!?”

” Sijahusika..” alitamka kisha akatokwa na machozi.

” Basi kwa kuwa njia yetu ni moja, utakutana nao tena mbinguni. Kikubwa tusali na kuomba sana “

Ali Mapito, alijikuta amekonda na kubakia kichwa tu kwa mawazo huku akiwaza siku ya kunyongwa itakuwaje.

Kila siku , walipokea chai ya bakora 10 kama sehemu ya adhabu huku usiku wakiachilia maji ya barafu.

Akiwa gerezani, waliokea taarifa kutoka kwa askari mmoja ambaye alionekana mwenye huruma,

“‘Hamjambo?” Aliwauliza.

“‘Ndiyo afande..” waliitikia.

“‘Sasa naomba mnisikilize kwa umakini sana na iwe siri yenu. Kwa taarifa ambazo zimetufikia kwenye chumba chetu cha habari,, mna siku 3 kabla ya kuuawa. Kama mna jambo la mwisho , basi huu ndo mda wenu wa mwisho. Taarifa hii ni siri na sitaki niisikie sehemu yoyote ile” aliwambia kwa sauti ya chini.

Baada ya kauli hiyo Ali Mapito aliishia kutokwa machozi kama mtoto mdogo huku akiwa ameshika tama.

Ndani ya dakika chache, askari huyo aliondoka kisha akafunga mlango wa chumba.

Wafungwa hao, walianza maombi kila mda kila saa huku wakijutia makosa yao waliyoyatenda.

Mnamo siku ya alihamisi mida ya saa tatu za asubuhi, askari waliokuwa wamevalia nguo nyeusi na miwani mieusi, waliingia chumbani walichokuwepo kina Ali Mapito kisha wakatoa amri,

” Nyoosha mikono na miguu!”

Walifanya hivo.

Baada ya hapo, walianza kuwafunga vitambaa vyeusi usoni kisha wakatia pingu mikononi.

Waliwainua na kutoka nao kuelekea chumb cha siri.

Walipofika chumbani humo, Ali Mapito alihisi kama kuna familia yake kwa nje ndipo alipowaomba,

” Samahani, najua mda wangu wakukaa duniani umeisha na sina dakika nyingi, nawaomba dakika hata 4 ili nikaagane na familia yangu kwa mara yangu ya mwisho.”

” Hee! unasema!” Askari alimfokea huku wakiwa wanaandaa vizuri mashine ya kunyongea…

JE NI KWELI FAMILIA YAKE IPO KWA NJE KUMUAGA?

JE ALIRUHUSIWA KUAGANA NAO?

JE ILIKUWAJE?

PART: 03

ILIPOISHIA,

Mapito alifungwa kitambaa cheusi usoni na kupelekwa kwenye chumba cha siri ili akanyongwe…

SONGA NAYO…

Kabla hajaingizwa kwenye mashine ya kunyongea, Mapito aliomba aonane na familia yake ambao alihisi ipo kwa nje.

Askari walimshangaa kwa hilo ‘

“‘Umewaona wapi ili hali upo chumba cha siri?” Walimuuliza huku wakizidi kumsukuma.

“‘Nawahakikishia wapo na nawaona…” Mapito alitamka.

Askari walicheka kwa tamko hilo kisha wakaendelea na kazi yao.

Akiwa amesimamishwa karibu na Mashine, alianza kusikia sauti ya vilio vya wafungwa wenzake ambao walikuwa wananyongwa mmoja baada ya mwingine.

Aliogopa sana na kujikuta anatokwa ns machozi yaliyoambatana na haja ndogo.

“‘Ee mwenyezi Mungu, muumba mbingu na nchi, zimebaki sekunde chache kabla ya kutoweka katika dunia hii iliyojaa uonevu, basi nakuomba utende miujiza yako  na uilinde familia yangu. Amina” Mapito alisali.

Kabla hajamalizia kusali, mlango wa chumba hicho ulifunguliwa kisha askari mmoja akatoa taarifa,

“‘Afande..!, Mapito anaombwa akaagane na familia yake ambayo ipo imemsubiria mara baada ya kuomba kibari na kukubaliwa”

“‘Hee! afu huyu mwamba mbona aliongea hili mapema?, au ana simu nini?” Walijiuliza kisha wakamkagua lakini hawakuona chochote.

Baada ya kusikia taarifa hiyo, Mapito alishusha pumzi yake huku akiwa na hamu ya kuagana na mtoto wake wa mwisho wa kiume aitwaye Mudy aliyekuwa na miaka 3.

Alitolewa kwenye chumba hicho mpaka uwanja uliokuwa umezungukwa na wavu huku akiwa chini ya ulinzi mkali sana.

Akiwa amebebwa na mama yake mara baada ya kukesha akilia akimuulizia baba yake, Mudi alimuona baba yake na kumkimbilia kisha akamkumbatia.

“Baba umevaa nini ” alimuuliza.

Mapito alishindwa kujibu chochote na badala yake alimwaga machozi tu.

“‘Baba!. Kwanini unalia?” Mudy alimuuliza tena baba yake.

Mapito aliishia kulia huku mtoto wake Zuwena akiwa amesimama na mama yake wakiwa nao na sura ya hofu na uchungu.

” Zimebaki dakika 2 tu, kama kuna jambo la mwisho mnataka kumwambia ongeeni. Baada ya hapa hamtamuona tena. Nami inaniuma sana lakini tupo kazini tunatekeleza na kutii maamuzi ya mahakama” askari alitamka.

Sikudhani pamoja na Zuwena, walisogea karibu kisha wakampungia mkono wa kwaheri japo hakuona.

“‘Mudy njoo tuondoke..” Sikudhani alimwambia.

“‘Mama nipo na baba …anaumwa..” Mudy alitamka huku akiwa amemkumbatia baba yake.

“Oyaa mda umeisha njoo mchukue mtoto” askari alitamka kisha akamnyanyua Mapito.

Mudy kuona hivo, alilia sana na kubaki amemshikilia baba yake huku akiwa hataki kumuachia

Askari alitumia nguvu kumtoa na kumrusha pembeni.

Mapito alirudishwa ndani.

Baada ya kuona baba yake kaondolewa, Mudy aliangua kilio kizito mpaka walinzi wakawafukuza ili kuondoa kelele.

Safari ya kurejea nyumbani mara baada ya kumuaga kwa mara ya mwisho lakini Mudy hakuacha kunyamaza kulia licha ya kupewa vitumbua na andazi.

Zuwena alimuangalia mdogo wake naye akahisi uchungu lakini hapakuwa na namna yoyote ile.

Walipofika nyumbani, waliwakuta watu wakiwa wamesimama kwa nje huku wakikumbuka maisha ya Mapito enzi za uhai wake hasa wema wake na upendo kwa watu.

Kilichowauma zaidi ni mtoto Zuhura aliyedaiwa daiwa kuuawa na baba yake bila hata kupata mabaki ya mwili wake.

Waliungana kwa pamoja kisha wakatangaza msiba wa baba na mwana kwa pamoja.

Baada ya wiki moja, waliangua matanga lakini bado mtoto Mudy alikuwa akiendelea kulia na kumuulizia baba yake.

Waliendelea kumbembeleza na kwa mbali akaanza kunyamaza japo afya yake ilianza kuwa dhoofu mara baada ya kulia kila siku.

Afya yake ilizidi kudidimia sana na alipopolekwa hospitali, waliambiwa mtoto ana msongo mkubwa wa mawazo hivo wanatakiwa kumuweka kwenye hali tulivu.

Mnamo mida ya saa 12 za jioni jua likiwa limeanza kuzama, Zuwena alisikia mlango wa geti unagongwa ndipo alipohisi ni mama yake kisha akaenda kuufungua.

Ile anafungua alikutana na sura ya kijana aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 hivi akiwa amejaza kifua kama tembo huku akinukua marashi yakizanzibar

“Karibu…” Zuwena alitamka huku akiwa hajui ni nani

“‘Asante…, mama yako yupo?” Alimuuliza.

“‘Hapana ametoka kidogo ila mda si mrefu anakuja…”

Alimjibu.

“‘Ok haina shida .Mi naitwa Salum…, we unaitwa nani?

“‘Naitwa Zuwena…”

“‘Ohh Zuwena, jina zuri..una miaka mingapi?

“‘Nina miaka 15..”

“‘Kweli!, mbona unaonekana kama una miaka 19 hivi…”

“Hahaha..hapana ni mwili tu” Zuwena alicheka.

Wakiwa wanaendelea na mazungumzo sebuleni, gafla mlango ulifunguliwa na mama Zuwena akaingia ndani.

Bila kupepesa macho, alijikuta anapatwa na mshangao mara baada ya kumuona Salum…

“Hee!”..alishangaa….

JE SALUM NI NANI?

JE MUDY ATAPONA?

JE MAPITO ALINYONGWA AU LA?..

PART: 04

ILIPOISHIA.

Sikudhani anashikwa na mshangao mara baada ya kumuona Salum akiwa ameketi na Zuwena sebuleni…

SONGA NAYO…

Sikudhani alibaki ameganda huku akiyageuza macho yake kama groli kisha akamwambia,

“Ni wewe!”

” Ndiyo ni mie au umenisahau…” Salum alijibu.

Taratibu, Salum alinyanyuka na kumkumbatia Sikudhani mpaka Zuwena akajihisi aibu.

Baada ya kukumbatiana, Sikudhani alimkaribisha Salum chumbani,

“Karibu chumbani” alitamka.

Bila kuchelewa, Salum alizama chumbani kisha mlango ukafungwa.

“‘Huyu ni nani?” Zuwena alijiuliza maswali lakini hakupata jibu.

Baada ya mda wa lisaa limoja hivi, Salum alitoka chumbani akiwa amejunga kanga ya Sikudhani kisha akaelekea bafuni.

“Mhh…”‘Zuwena aliguna huku akiinamisha kichwa chini.

Akiwa yupo bafuni, alimuona mama yake naye akiwa amejifunga kanga akiingia bafuni.

Zuwena alijibanza ili asionekane kwani alihisi aibu kweli.

Alitoka sehemu hiyo nakuelekea jikoni.

Baada ya mda, Salum alikuja kuketi sebuleni kisha mama Zuwena naye akaketi pembeni yake.

“Zuwema..” alitamka.

“Abee mama” aliitika.

“‘Huyu umemfahamu?” Alimuuliza huku akionesha sura ya tabasamu.

“‘Hapana mama…” alijibu.

“Huyu ni baba yako tangu leo. Mnapaswa kumuheshimu ..”

Baada yakuambiwa hivo, Zuwena alitabasamu kisha akamuangalia baba yake mpya.

Wakiwa wameketi, Mudy mtoto wa miaka 3, alizidi kulia huku akimkataa Salum kuwa si baba yake..

“Baba! .. baba!! ..baba.”

“‘Nyamaza anakuja kaenda kukuletea pipi” alimbembeleza.

Kauli hiyo, haikufanya Mudy anyamaze ndipo Salum alipotaka kumshika lakini alikataa katakata.

Baada ya utambulisho huo, walielekea chumbani kulala huku Salum akilalia kwa mara ya kwanza kitanda kilichowahi laliwa na Mapito.

Ni usiku uliokuwa mrefu sana kwa wawili hao huku Sikudhani akitamani kurudisha umri nyuma ili aendee kufaidi mema ya dunia.

Baada ya safari ndefu yakupandishwa kilele cha mlima kilimanjaro kutimia, Sikudhani alishusha pumzi yake kisha akamwabia Sam’

“Baby…” alitamka.

“Naam ..mke wangu kipenzi…”

“‘Nikwambie kitu?”

“‘Niambie wala usijali …”

“Hivi unanipenda kweli..?”

“Nakupenda sana tena sana laiti ungekuwa na uwezo wakuona moyo wangu ulivyo….” alikatisha maneno.

Sikudhani aliangua kicheko cha tabasamu huku akimshika kwenye kifua chake.

Salum alilegeza mwili wake kisha Sikudhani akalaza kichwa chake mpaka hapo asubuhi.

Siku ya kwanza ilipita na hatimaye wiki sasa ndipo habari za chinichini zilipoanza kusambaa juu ya Sikudhani kuolewa na mme mwingine.

Miongoni mwa watu waliopata habari hizo ni Rashid ambaye ni kaka Mapito na shemeji wa Sikudhani.

Rashid alisikitika sana kwa taarifa hiyo ndipo alipoanza kushauriana na mama yake.

“‘Mama..” alimuita..

“‘Unasemaje?”

“‘Nasikia Sikudhani ameolewa na mme mwingine afu huyo mme anakaa kwenye nyumba alooacha kaka. Nimeumia sana . Kama anashida ya mme si aniambie niwe mme wake?, ..”

“‘Hee! Hizo taarifa ni kweli!, mwanangu hajamaliza hata 40 zake afu anafanya kitedo hicho!. Kwa raha zipi alizonazo mpaka anaamua kuolewa kwa kipindi hiki kigumu. …” Mama Mapito alishindwa kuendelea mara baada yakuanza kutokwa na machozi.

“Nyamaza mama, ila leo naenda na nikimkuta mwanaume huyo, ama nife ama afe au aondoke. ” Rashid alitamka kwa hasira.

“‘Mwanangu!, nakusihi utulie , wewe ndiye mlezi wangu ulobakia hivo sitaki nawe ulete kesi na uishie kunyongwa kama kaka yako..”

“Mama hii ni aibu lakini pia mali alizoacha kaka zitaisha bila kujua na watoto watakuja kuteseka. Niamini mama, naenda kumfukuza huyo mwanaume na kama anataka kuoa, basi ampeleke kwake. Ni aibu sana kwakweli..”

“‘Mwanangu nakusihi sana kwa mara nyingine, yaache kama yalivyo. Kama ni aibu kajiaibisha mwenyewe..”

Baada ya maneno hayo, Rashid alitikisa kichwa kama ishara yakukubali.

Alikaa kitako na kuanza kumuwaza kaka yake na kukumbuka enzi za uhai wake alivyokuwa mtu mwema na mkarimu mpaka akajikuta anatokwa na hasira.

“‘Kaka..pumzika kwa amani, ni ngumu kukusahau . Tukio ulilofanya nadhani ulirogwa maana mpaka sasa siamini kulingana na roho yako iliyotukuka..: Rashid aliongea peke yake .

Kwa uchungu mkubwa, alinyanyuka taratibu kwenye gogo la mti alokuwa amekalia bila kumuaga mama yake na kuanza safari kuelekea kwa Shemeji yake Sikudhani.

Mnamo mida ya saa 11 za jioni, alikaribia maeneo hayo huku akiwa na hasira kwelikweli .

Alitoa kitambaa chake kilichokuwa na rangi ya blue na njano kisha akajipanguza machozi vizuri.

Wakiwa ndani wanacheza kadi, Sikudhani alisikia mlango wa geti unagongwa ndipo alipomuagiza Zuwena afungue..

” Zuwena..”

“‘Abee mama!..”

“Kaagalie ni nani anagonga afu mfunguli..” alimuagiza kisha wakaendelea na mchezo kati yake na mme wake ( Salum).

Zuwena alifungua mlango ndipo alipokutana na sura ya baba mdogo wake ( Rashid).

“‘Shikamoo baba mdogo…” alimsalimia huku akiwa na sura ya hofu..

“‘Marhaba.., mama yako yupo?”

“Ndiyo wapo wote na baba…” Zuwena alitamka .

Rashid alihisi kumwaga chozi lakini alijikaza ndipo alipoongozana na Zuwena kuelekea ndani ya nyumba….

JE NINI KILITOKEA?

JE RASHID ALIFANIKIWA ?

PART: 05

ILIPOISHIA,

Rashid aliongozana na Zuwena kuingia ndani…

SONGA NAYO…

Baada ya kupiga hatua mbili tatu, Rashid aliungia ndani huku akiongozana na Zuwena.

Alibaki ameshangaa mara baada yakumuona Sikudhani akiwa amekaa zero distance na Salum.

Sikudhan naye alishutuka huku Salum akibaki ametoa macho.

“Habari ya kwako shemu..” Sikudhan alitamka.

“‘Nzuri sijui za hapa..”

“Ni nzuri pia naona leo umetutembelea jioni…”

“Ni kweli japo kuna kitu kimoja kimenileta hapa na lazima nikikamilishe..” alitamka kwa sauti ya juu kidogo.

“Hee!..kitu gani hicho?”

Sikudhani alijawa na wasiwasi huku akiwa na shauku yakukijua.

“‘Hivi shemeji, unayofanya ni sawa?”Rashid alimuuliza.

“Unataka nini na wewe!? “

“‘Hivi hata arobaini za aliyekuwa mme wako bado pamoja na mtoto wetu Zuhura lakini unaanza kufanya mambo haya!, unatuongezea maswali mengi na uchungu ..” Alitamka.

“‘Maisha yangu yanakuhusu nin?, huyo katangulia lakini maisha yanaendelea. Siwezi kukaa peke yangu ili hali damu yangu bado inachemka . Kama unaona unateseka ni wewe na roho mbaya…”

“Ni wewe unayenijibu hivo!,hata kama katangulia mbele za haki kwa kukosea au kutokukosea maana mpaka sasa sijawahi amini lakini sio kwa kitendo hiki. Anakuona ..”

“Kwo siku hizi maiti anaona?, ebu nitokee zako na sikutaki nyumbani kwangu…”

“‘Unanifukuza kama nani, hii ni nyumba ya broo na huna nguvu yakunifukuza hapa. Uliikuta na utaicha!, naomba tuheshimiane..”

“‘Nenda kajenge yako ndo umuwekee mkeo masharti !..” Sikudhani alifoka.

Wakiwa wanaendelea na majibizano, Salum alinyanyuka na kumfuata Rashid kisha akamwambia,

“Broo!, nimekuheshimu sana!, unaongea na mke wangu unavyotaka tena mbele yangu!, sasa!..sasa!..nakuomba uondoe miguu yako kabla hayajatokea mengine…” alifoka huku akiwa amekunja sura.

“Hunitishi chochote!, nasema hunitishi chochote!, kama ni mkeo mpeleke kwako. Huna hata aibu unalala kwenye  kitanda alichonunua mme mwenzio!. Sasa leo nakwambia, nife mie au ufe wewe ila hubaki hapa..! Rashid alijibu Mapigo.

Bila kuchelewa, Salum alivua shati lake nakubaki na kaushi iliyokuwa na rangi nyeupe kisha akamrukia Rashid.

Rashid alikwepa na kumfanya Salum ajigonge kwenye ukuta.

Akiwa bado anasikilizia maumivu, Rashid kumbe alikuwa amebeba kisu ndipo alipokichomoa mfukoni.

Aliruka mpaka alipokuwa Salum kisha akamuelekeza kwenye Moyo.

“Nichomee?..!,..nichomee?!”alitamka

“Usiniue!..usiniue..!” Salum aliongea huku akiwa anatetemeka

“Toweka ndani!, nakupa sekunde 1 tu..” Rashid alitoa tamko.

Alinyanyuka kinyumenyume na kutoka ndani kwa haraka kabisa ndipo Rashid alipofunga mlango.

Sasa ndani alibaki Rashid, Sikudhan na Zuwena.

Rashid aliketi kwenye Sofa kisha akashika tama kwa uchungu.

“‘Nina wasiwasi na wewe!, huna utu wowote na hufai kuwa mke.” Alimwambia.

Sikudhani hakumjibu chochote ndipo alipotoka nje kupitia mlango wa nyuma huku akiwa ameficha panga.

Wakati amelificha, Zuwena alifanikiwa kuliona ndipo alipoogopa.

Akiwa kwa nje, Sikudhani alimpatia Salum panga kisha akamwambia,

“Mme wangu, ametudharirisha sana kwa kitendo hicho!, sasa tunatakiwa tumtengeneze nyama afu tutajua pakumtupa maana bila hivo atatusumbua ..” alimwambia.

“Lakini tukimuua hawatajua?,maana kuna watoto wanaweza kufichua siri..”

Salum alihoji.

“‘Hapana!, Zuwena ni mtu muelewa na jasiri sana. Kama aliweza kutunza siri nzito, hawezi kushindwa kutunza hii..”

“‘Sawa vipi damu sizitamwagika ndani?”

“‘Hapana yaani utaingia na panga afu umtishie nami nitaleta kamba nimfunge. Kama atakaidi tutamkata hata shingo ila kwa hili inabidi tumtume kitu chochote Zuwena asiweze kushuhudia tukio…” Sikudhan alitamka

Baada ya kauli hiyo, Salum alitikisa kichwa chake juu kama ishara yakukubaliana.

Alishuka chini nakupiga pushapu kama 30 mfululizo .

Sikudhani alifarijika huku akiwa amejawa na hasira kali ya mauji.

Wakati yote yanatendeka, Rashid hakujua chochote na badala yake alibaki ameketi kwenye sofa akiwa amembeba Mudy huku mkono mmoja akiwa ameshika tama.

Baada ya kupanga mipango yote, Sikudhani alimuita Zuwena,

“‘Zuwena!..Zuwena..” alimuita.

“Abee mama””

Aliitika.

“Njoo nikutume…”

Alifika kisha akampatia kiasi  cha sh 3000 ili akanunue kilo ya sukari.

Zuwena alifanya hivo lakini baada yakupiga hatua chache, alikumbuka mipango waliyopanga ili kummaliza baba mdogo wake Rashid

“Mhh jamani kwanini wanataka kumuua,?” Zuwena alijiuliza huku akiwa analengwalengwa na machozi.

Dakika za Rashid kubaki duniani, zilianza kuhesabika mara baada ya Salum akiwa na mkewe Sikudhani kuanza kutembea kwa kunyata kuingia ndani.

Bahati mbaya sana, Rashid alianza kupitiwa na usingizi kwa mbali ndipo aliposhutushwa akiwa amewekewa panga likielekezwa kwenye paji la uso wake.

Alishutuka na kutoa macho huku akiwa haelewi ndipo alipopewa amri,

“‘Una sekunde 5 zakuomba kabla ya kuaga ulimwengu huu!” Salum alimwambia.

“Hee!, nimewakosea nini?, ” aliwauliza huku akiwa anatetemeka….

JE RASHID ALIPONA?

JE  NINI KILIFUATA?

NA JE SALUM ALIBAKI NYUMBANI HAPO?

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!