Rais Aliyemuoa Mwalimu Wake
Rais wa Ufaransa wa sasa, Emmanuel Macron na mkewe, Brigitte.
Hawa wawili wamepishana kwa miaka 25, yaani mwanamke ana miaka 72 na mwanaume ana miaka 47.
Umri ni namba tu, hawa watu wapo pamoja mpaka leo hii.
Emmanuel Macron alianza kumpenda mwalimu wake wa darasani aliyeitwa rigitte Trogneux, kipindi hicho Emanuel Macron akiwa na miaka 15 huku Mwalimu rigitte Trogneux akiwa na miaka 39
Macron akiwa katika huo umri mdogo, alikuwa mwanafunzi mwerevu sana.
Alikuwa mwanafunzi katika shule ya kibinafsi ya Wajesuiti, Amiens ambapo, Brigitte baadaye alisema “alikuwa na uhusiano wa ngazi sawa alipokuwa anahusiana na watu wazima” badala ya kujichukulia na kuzungumza kama kijana aliyekuwa ndio tu amebalehe.
Alieongeza: “Nilitekwa na werevu wa mvulana huyu.”
Jina lake la kuzaliwa ni Brigitte Trogneux, na alikuwa mrithi wa kampuni ya kutengeneza chokoleti ambayo ilikuwa maarufu sana kwa sababu ya macron.
Alisoma na kuwa mwalimu wa somo la kuigiza na kisha akaolewa na mfanyakazi wa benki André Auzière, walijaliwa watoto watatu.
Wazazi wa Emmanuel waligundua kwamba mtoto wao alikuwa ameingia kwenye mapenzi, lakini yamkini hawakufahamu nani alikuwa mpenzi wake.
Badala yake, mwandishi wa hadithi kuhusu maisha yake Anne Fulda ameandika, walidhani alikuwa amempenda Laurence Auzière, msichana waliyekuwa katika darasa moja. Lakini, kumbe alikuwa amempenda mamake msichana huyo.
Wazazi wa Macron walipogundua hilo, walimwamuru Brigitte kukaa mbali an mtoto wao hadi afikishe umri wa miaka 18.
“Siwezi kuwaahidi jambo lolote,” aliwajibu.
Alipotimiza miaka 17, Emmanuel alikuwa tayari amemwambia Brigitte kwamba angemuoa siku moja.
Ilikuwa ni mwongo mmoja baadaye, mwaka 200, alipotimiza ahadi hiyo.
Sasa, mamake Macron anasema huwa anamtazama Brigitte “zaidi kama rafiki” badala ya mkazamwana.
Brigitte ana watoto watatu kati ya hao wapo waliomzidi umri mumewe wakati Emanuel macron hana mtoto hata mmoja

Watoto wa Brigitte wamuunga mkono Macron
Laurence sasa ameibuka kuwa mmoja wa wanaomuunga mkono zaidi babake wa kambo na alikuwa kwenye mkutano wake wa hadhara Paris kwa mfano.
Mtoto mwingine wa kambo Tiphaine, 32, ni wakili ambaye alifanya kazi katika kundi lake la kampeni.
Wanafamilia wote walikuwa jukwaani Macron alipokuwa anasherehekea ushindi wa urais Jumapili katika eneo la Louvre, Paris.
Rais huyo mteule ana watoto watatu wa kambo na kupitia kwao, wajukuu saba.
Bi Macron alijiuzulu kazi yake ya ualimu baada ya mumewe kuteuliwa kuwa waziri wa uchumi, na akawa mmoja wa washauri wake wakuu.
Brigitte anasifiwa kwa kuathiri mtazamo wa Macron kuhusu wanawake katika siasa.
Ameahidi kwamba nusu ya watu wote watakaowania nyadhifa chini ya chama chake cha En Marche (Tunasonga) katika uchaguzi wa ubunge mwezi Juni watakuwa wanawake.
Na amesema anataka kufanya rasmi wadhifa na majukumu ya mke wa rais.
Katika mahojiano na Vanity Fair mwezi jana, alisema: “Nikichaguliwa – samahani, tukichaguliwa – atakuwa (Brigitte) hapo, atakuwa na majukumu na nafasi.”
Kama mwalimu wa zamani, huenda akaangazia zaidi kuwasaidia vijana akiwa mke wa rais.
Bw Macron amependekeza kwamba wadhifa wa mke wa rais hautakuwa na mshahara na kwamba sifa zake zitaongozwa na Brigitte.
“Atakuwepo, na atakuwa na usemi, na mtazamo kuhusu mambo. Atakuwa nami, kama alivyokuwa muda huu wote, atakuwa pia na majukumu mbele ya umma.”
Baadhi ya vibonzo Ufaransa vimekuwa vikimtania, na kumuonyesha Macron kama mwanafunzi anayepokea maagizo kutoka kwake.Na mpinzani wake Marine Le Pen wakati mmoja alimshambulia kuhusiana na asili ya uhusiano wao.
Alisema: “Bw Macron … naona unajaribu kuigiza kama mwalimu nami mwanafunzi. Lakini kwangu, siwezi kukubalia hilo.”
Bi Macron mwenyewe amedhihirisha kwamba anaweza kucheka suala la umri wao.
Amenukuliwa katika kitabu kimoja akisema: “Anahitaji kuwania urais mwaka 2017 kwa sababu 2022, tatizo lake kubwa litakuwa sura yangu.”
SEKESEKE – MACRON KUPIGWA KOFI
Mei 25 mwaka huu,
Mitandao ilifurika na maoni baada ya video kumwonyesha Mke wa Rais wa Ufaransa, Brigitte Macron, akionekana kumpiga kofi Rais Emmanuel Macron usoni Kwa muda mfupi, Macron alionekana kuchanganyikiwa alipokuwa akitembea kutoka upande mmoja wa ndege hadi mwingine kabla ya kurejea katika hali ya kawaida
Video hiyo ilinasa wakati ndege ya rais ilipogusa ardhi ya Hanoi, Huko Vietnam na Rais Emmanuel Macron akatokea mlangoni mwa ndege. Kilichofuata kilikuwa mshtuko wa ghafla alipopigwa usoni na mikono ya mkewe, jambo lililomshangaza kwa muda mfupi. Ingawa Mama wa Taifa hakuonekana wazi kwa sababu ya muundo wa ndege, mikono yake ilionekana bayana kwenye video. Rais alipata nafuu haraka, akageuka na kuwapungia mkono waliokuwa wakimsubiri, kisha akaanza kushuka ngazi za ndege — akiwa peke yake bila mkewe kukubali kushikwa mkono.
Awali, ofisi ya rais ilitilia shaka uhalisia wa video hiyo, lakini baadaye ilithibitisha kuwa tukio hilo lilikuwa la kweli.
Taarifa kutoka Ikulu
Uvumi huo ulilazimu taarifa rasmi kutoka Ikulu ya Elysée, ambayo ilipuuza tukio hilo na kulielezea kama “wakati wa ukaribu” na sehemu ya mchezo wa kawaida kati ya wanandoa hao.
Vyanzo vya Ikulu ya Ufaransa vilivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema kuwa tukio hilo lilinaswa ”wakati ambapo rais na mke wake walikuwa wakitaniana kabla ya kuanza kwa ziara yao”, huku Macron akisema “tulikuwa tunafanya utani kama kawaida”.
Hata hivyo, mitandaoni, wananchi wengi hawakuridhishwa na maelezo hayo rasmi, wengine wakitafsiri tukio hilo kama dalili ya msuguano mkubwa, au angalau hali ya kutodhibiti hisia kisiasa.