PENZI LA MZUNGU LILIVYONIHARIBIA MAISHA
SEHEMU YA 16
ONYO: Wakubwa tu ndio wasome hii hadithi 🔞
Sikuamini macho yangu nilipojua ukweli kuwa kila nilichokuwa nakifanya na mwanamama yule mzungu, Meranda kilikuwa kimepangwa yaani kilikuwa kwenye script, inamaanisha tulikuwa tunaigiza filamu (movie) ya ngono, vijana wakiita ‘XXX’ au kwa lugha ya mtaani ‘Pilau’ nilihisi kuishiwa nguvu nikabaki nimejishika kiuno nikiwaangalia watu hao wanne walioingia na vifaa vyao hivyo na huku wakizitoa kamera zote zilizokuwa zinajiendesha zenyewe ndani ambazo nilimuuliza mwanamama Meranda muda ule lakini akanipa majibu ambayo niliyakubali bila kujiongeza kwa akili yangu, sasa ndiyo nimeelewa kuwa kamera hizo zilitegeshwa kwa makusudi maalumu ili zirekodi kila kinachoendelea ndani hasa wakati tukifanya mapenzi, nilichoka zaidi baada ya kuliona lile gari dogo la kuchezea (toy) la kuendeshwa na remote likivutwa kwa remote na muongoza filamu (director) mmoja wapo mzungu, akaizima kamera kwenye gari hilo ambalo kumbe lilikuwa likituchukua uvunguni mwa miguu yetu tulipokuwa tunafanya mapenzi hasa sebuleni pale kwenye kochi (sofa) kubwa na hata yule paka mdogo mwenye manyoya mengi meupe mwilini kumbe nae alivalishwa kamera ndogo na alikuwa na kazi yake ya kuchukua matukio kupitia kamera aliyoivaa, nikabaki nimesimama huku nimeshikwa na bumbuwazi, na yule mwanamke mmarekani mweusi, Pamela akatoka bafuni akiwa amevaa chupi na sidiria, akionekana ametoka kujimwagia maji
“Do not forget that Camera in the bathroom (msiisahau na ile kamera ya bafuni)” aliwaambia
“Ina maana mpaka bafuni kumbe tulikuwa tunarekodiwa?” nilijiuliza mwenyewe huku nikijikuta nashikwa na hasira
“Danny?” niliitwa nikageuza shingo na kumwona mwanamama Meranda akinifuata taratibu
“What is this all about (nini hiki kinachoendelea)”
“It is a short reality sexy movie, pornographic movie, you gonna like it and am gonna pay you a lot of money coz you acted well, well, well Danny (ni filamu fupi ya kweli, ya mahaba, utaipenda na nitakulipa pesa nyingi Danny kwa sababu umeigiza vizuri, vizuri sana)”
“Sihitaji pesa na hiyo filamu niliyorekodiwa ifutwe kabisa” niliongea kwa hasira
“Oooh haiwezekani kufutwa Danny, coz it was watched live and many people around the world watched us when we were having a nice sexy (ilikuwa inaangaliwa mubashara na watu wengi ulimwenguni walikuwa wakitutazama wakati tukipeana mapenzi matamu)” aliniambia mwanamke huyo wa kizungu ambae nilimkata jicho
“Ningejua nisingethubutu kukufahamu, hayakuwa makubaliano yetu”
“Oky am sorry but I just wanted to make business with you, if you like there it is, your payment cheque, take it and that car is also yours as I told you once (samahani lakini mimi nilitaka kufanya tu biashara na wewe, kama ukipenda, hii hapa cheki yako ya malipo, ichukue, na lile gari ni la kwako pia kama nilivyokuambia muda ule)” alinipa cheki ya pesa ambayo niliitazama tu na kisha kumtazama yeye mwenyewe
“I don’t want either your money or your car, keep it with you, all of them (sihitaji pesa zako wala gari lako, baki navyo vyote)” nilimjibu kwa hasira na kutoka haraka haraka nikipiga mateke kamera nilizozikuta chini, wakinitazama tu na kuendelea kunizungumzia kwa Kiingereza kuhusu kukataa kwangu ofa yao ya pesa ambazo sikuzitazama ni shilingi ngapi, nikaubamiza mlango nilipotoka nikiwaacha ndani nikilifuata gari ili nitoke nje, nililipita lile gari dogo huku nikilitazama kwa uchungu, nikiwaza ni jinsi gani nitaonekana kwenye mitandao ya video za ngono nikifanya mapenzi na wanawake hao kwa nyakati tofauti na vipi siku ambayo watu wanaonifahamu wataziona video zangu hizo, simu ndiyo iliyonitoa kwenye dimbwi la mawazo ilipoita mfukoni nikiwa nimefika getini nataka kutoka nje, nikaitoa na kupokea akiwa ni rafiki yangu, Joel
“Oya Danny vipi mbona hurudi mwanangu nakutegemea ndinga hiyo nikampokee demu wangu anakuja usiku?” aliniuliza
“Sina gari ni…” nilitaka kumjibu lakini nikasita nikilitazama gari hilo ambalo nimepewa kama malipo ya kazi yangu
“Hauna gari, umelipeleka wapi, au umemaanisha?!”
“Ngoja kwanza Joel” nilimkatisha na kuzima simu kabisa, nikalitazama gari hilo kwa umakini ambalo nililiendesha na kuonja raha yake, nilijikuta nikiwaza mengi kichwani, niliwaza kama kurekodiwa nimesharekodiwa na nimesharushwa mitandaoni sina cha kufanya kubadilisha hilo, hata nikikataa pesa na gari nitakuwa nimekula hasara mara mbili, nikageuka haraka na kuanza kurudi kule kule ndani nilipowaacha nikafungua mlango na kuwakuta wazungu hao wakitazama video zangu kwenye televisheni kubwa ya ukutani ya mwanamama Meranda huku mmoja akifanya kazi ya kuziedit, wote wakanigeukia na mwanamama Meranda akainuka na kunifuata taratibu
“Danny”
“Give me the money (nipe pesa)”
“Waaoh am happy that you’ve changed your mind, here it is, ten thousands dollars, and if you’ll work again with me am gonna pay you more than this, and your life gonna be changed, are you ready? (waoooh nina furaha kuona umebadili maamuzi yako, hizi hapa dola elfu kumi, na kama utafanya kazi namimi tena basi nitakulipa zaidi ya hizi pesa na maisha yako yatabadilika, upo tayari)” aliniuliza kwa kuninong’oneza sikioni huku akiwa amenishikisha cheki hiyo ya dola elfu kumi ambayo ni zaidi ya milioni ishirini za kitanzania, akiniuliza swali zito ambalo nilishikwa na kigugumizi kulijibu…..
SEHEMU YA 17
Sekunde takribani thelathini zilikatika bila kumjibu kitu mama huyo wa kizungu akiwa ameshanishikisha cheki ya pesa dola za kimarekani ambazo kazi yangu ilikuwa kwenda benki tu kuzitoa na kuzitumia
“Danny?” aliniita kwa sauti ya chini aliponiona nipo kimya
“I will tell you, give me a time (nitakwambia, nipe muda tu)” nilimjibu
“Is up to you but before it is too late coz I will be back to Scottland at anytime from now” aliniambia na kunibusu midomoni akanishika begani na kuniacha nimesimama pale pale nashangaa tu sina cha kufanya, yule mwanadada Pamela mmarekani mweusi alinifuata huku akitabasamu
“Changamka kidyana, vipi sasa” aliniambia kwa Kiswahili cha kuchapia akimaanisha kijana’ huku akijishika shika matiti yake kifuani, akiwa amevaa chupi na sidiria tu
“No, not now” nilimjibu nikitabasamu nae akatabasamu, nikaifuata funguo ya gari haraka na kuanza kuondoka taratibu nikitoka nje ya nyumba hiyo nikalifuata gari hilo kwenye maegesho (parking) kisha nikaliwasha na kuliondoa kwa kasi kama siyo mimi, karatasi ya cheki ya pesa nikiwa nayo mkononi bado, moja kwa moja nikafika mpaka kwenye benki moja ya biashara ambayo nilifungua akaunti yangu binafsi ambayo haikuwa na pesa yoyote, nikachomoa kiasi hicho cha dola za kimarekani elfu kumi lakini kwa pesa za kitanzania nikipata milioni zaidi ya ishirini na kuzihamishia kwenye akaunti yangu ya benki mpaka karani wa benki aliyekuwa akinihudumia akanishangaa akitamani kuuliza nilipozitoa pesa zote hizo kwa pamoja, nilipomaliza mchakato huo nilitoa milioni moja kwenye ATM na kuingia kwenye gari ikanisaidie matumizi ya hapa na pale, nikafika nyumbani na kupaki gari hilo dogo ambalo sikuwa hata na kadi yake ya gari bado, taratibu nikaingia ndani mpaka sebuleni nilipowakuta baba na mama wamekaa kumaanisha kuna jambo walikuwa wanalizungumzia na waliponiona wakanigeukia kwa pamoja ikionekana walikuwa wananijadili giza likiwa limeshaingia, nikipishana na mdogo wangu wa kike aliyekuwa anaenda nje
“Kaka umerudi, hela uliyoniwekea kitandani ila mama amenipora ameichukua amenipora eti amesema nimeitoa wapi wakati ulinipa wewe” alinilalamikia
“Nitakupa nyingine, kashushe mizigo kwenye gari”
“Kwani kaka Danny lile gari la kwako au?”
“We katoe mizigo kwenye gari” nilimpa ufunguo ili akashushe matunda na mizigo mingine kama mafuta ya kula, kiroba cha mchele na cha unga na vitu vingine nilivyobeba kwa ajili ya nyumbani
“Shikamoo baba, shikamoo mama” niliwasalimia
“Marahaba” mama aliniitikia
“Danny sogea hapa” Baba hakuniitikia aliniita, nikawasogelea, mama akataka nikae kwenye kochi nikafanya hivyo
“Naam baba”
“Danny wapi umepata pesa ya kununua gari hebu tueleze, maana ni ghafla ghafla tu?” baba aliniuliza akikaa vizuri
“Eeh usije ukawa unauza madawa ya kulevya hapa ukatusababishia matatizo bure, hebu tuambie hicho kitu unachokifanya ambacho kimekufanya ununue gari au umemuibia mtu?” mama aliongezea
“Mama, baba nimechoka saa hizi naombeni ruhusa nikapumzike, kesho nitawaeleza kila kitu, mimi ni mtoto wenu siwezi kuwaficha kitu kabisa”
“Sawa basi haina shida kalale ila kesho nataka majibu, na usiku huu nataka unipeleke kule kwenye kahawa nikatambe tambe kidogo kwa wazee wenzangu maana kuna mzee mmoja kila siku yeye tu kuongelea habari za mtoto wake kuwa na gari kama sisi wengine hatuna watoto teh teh teh”
“Mh baba Danny na wewe kha?”
“Utaniamsha baba muda unaotaka kutoka” nilimwambia nikainuka kwenda chumbani kulala nikiwaacha sebuleni, sikurudi tena kule kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yangu Joel……
……
Kulikucha mapema asubuhi baada ya purukushani za mambo yote ya jana, niliamka na kutazama simu yangu nikakutana na meseji na simu nisizopokea (missed calls) nyingi kutoka kwa Glory, aliyekuwa mpenzi wangu akitaka tuonane, nilipotazama muda ilikuwa ni saa mbili asubuhi wala mama hakuja kuniamsha kama kawaida yake, mdogo wangu wa kike akanigongea mlango na kuingia chumbani kwangu
“Kaka Daniel mbona umelala mpaka saa hizi, si ulisema utanipeleka leo shuleni kwenye kikao cha wazazi?”
“Kwani saa ngapi?”
“Saa mbili nawewe hata hujaamka”
“Ooh sawa nakuja”
“Fanya haraka na nataka twende na gari” aliongea kwa kudeka nami nikajinyoosha na kuamka nikatoka na kumsalimia mama kisha nikachukua ndoo ya maji na kitambaa nikatoka kwenda kulifuta futa gari kwa sababu halikuwa chafu sana, wakati nilipokuwa nikilifuta
“Daniel” niliitwa nyuma nikageuka na kumuona Glory amesimama nyuma yangu
“Glory, karibu”
“Asante naweza kuzungumza na wewe kidogo kama hutojali?”
“Bila shaka” nilimjibu akanisogelea na kunishika mkono wangu wa kulia
“Tafadhali Daniel, nisamehe kwa niliyokufanyia, naomba turudiane, nipo chini ya miguu yako” aliniambia kwa unyenyekevu huku akipiga magoti mbele yangu
“Glory?!”……
SEHEMU YA 18
“Danny tafadhali naomba unisamehe, turudiane” Glory aliniambia akiwa amepiga magoti mbele yangu
“Glory ndo unafanya nini sasa, inuka”
“Nisamehe Danny, turudiane, mimi nakupenda wewe tu, yule Dominic alikuwa ni muongo ananilaghai tu na kunichuna pesa” aliniambia huku nikimwona akiwa amevimba jicho moja likiwa jekundu kumaanisha amepigwa
“Umejifanya nini jichoni mbona umevimba?”
“Nimejiumiza tu” alizuga akificha nisijue kama ametandikwa ngumi
“Ooh pole sana”
“Asante Danny”
“Basi inuka kwanza” nilimshika na kumnyanyua taratibu na mdogo wangu akaja muda huo huo akiwa ameshajiandaa
“Kaka nachelewa shule nipeleke basi aah” alilalamika
“Basi nisubiri hapo nijiandae dakika tano tu, Glory nisubiri” niliwaambia, Glory akatikisa kichwa kiunyonge nikamwacha na mdogo wangu ambae wanafahamiana nae, akiongea nae sikujua alichokuwa anamwambia, nikaoga haraka na kuvaa nilivyojua mimi kisha nikarejea na kumkuta mdogo wangu ameshaingia ndani ya gari huku Glory akiwa nje nikamfungulia mlango nae akaingia ndani ya gari na kutulia tuli kwenye kiti cha nyuma nikawasha gari na kuliondoa taratibu safari kumpeleka mdogo wangu shule akiwa ameagizwa aende na wazazi kwa ajili ya kikao, tukafika na Glory akiwa ndani ya gari nikaenda kusikiliza kikao hicho kwenye shule hiyo ya sekondari ambayo ndiyo niliyosoma mimi kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne, walimu wakinishangaa na kikao kilipoisha walimu wawili wa kike waliowahi kunifundisha niliwapa lifti kuwapitisha makwao nikiwa nimebaki na Glory huku mdogo wangu akiondoka na rafiki yake nyumbani kwao kumtembelea nami nilipowafikisha walimu hao ikabidi nimpeleke Glory mpaka chumbani kwake alipokuwa amepanga,
“Sasa G tumeshafika, mimi naelekea kwenye majukumu mengine”
“Karibu basi hata unywe chai nyumbani”
“Hapana usijali nipo vizuri”
“No hujanywa chai, nakujua wewe Danny bwana huondoki bila kuingia kwangu kidogo kunywa chai”
“Sawa nitakuwa nje hapa” nilimjibu huku nikishuka kwenye gari baada yeye kushuka, tukasogea mpaka kwenye mlango mkubwa wa nyumba hiyo niliyopanga nikiwasalimia majirani wapangaji wenzake wachache waliokuwa wananifahamu, yeye akaingia ndani
“..nakupa mama pesa yako bado siku mbili tu jamani?” nilisikia akijibu kiunyonge ikionekana anagombezwa na mama mwenye nyumba, ikabidi niingie ndani kusikiliza nijue kulikoni
“Wewe unafanya kazi ya kubadili wanaume tu humu, leo John, kesho Juma, keshokutwa Ramadhani, sasa mbona hawakusaidii kulipa kodi wanakuja kujaza choo changu tu?”
“Jamani mama hayo yote yametokea wapi, si nimekwambia kodi yako nakupa jamani?”
“Unanipa lini sasa, leo siku ya ngapi, tarehe ngapi leo kwani?”
“Samahani mama ya miezi mingapi?” ilibidi niingilie kati mazungumzo yao hayo, mama huyo mwenye nyumba alinigeukia na kunitazama
“Nawewe Danny si unanilipaga wewe kodi halafu unajifanya hujui ya miezi mingapi, halafu mbona sikuhizi sielewi elewi nani mume humu ndani, ni wewe au ni wengine?”
“Jamani wewe mama vipi?” Glory alikasirishwa na swali hilo
“Ni elfu tisini miezi mitatu siyo?”
“Ndiyo, unayo mpaka unauliza?”
“Hii hapa” nilitoa elfu tisini kamili, kodi ya miezi mitatu na kumpa mama huyo mwenye nyumba ambae awali nilikuwa nikimpa kodi ya miezi miwili miwili
“Mambo si ndo hayo sasa jamani, mpaka tupigizane kelele kweli kha” aliongea akizihesabu pesa hizo kwa mate huku Glory akimtazama kwa macho makali
“Hujamzidishia kweli Danny?” Glory aliuliza
“Ushaanza, kwani nikizidishiwa au nikipunguziwa kuna nini, asante sana Danny jamani hapa ngoja nikachukue sare ya harusi mapema” mama huyo aliondoka akituacha mimi na Glory tumesimama tunamtazama na wapangaji wengine wakitutazama sisi
“Tuingie ndani Danny hapa watu wanatukodolea macho sijui kama kitu gani” alinishika mkono tukaingia chumbani kwake, kwenye chumba nilichompangia mimi mwenyewe, akaanza kuhangaika kuweka weka vitu vizuri
“Mimi nina haraka Glory, shika hii itakusaidia matumizi madogo madogo” nilitoa shilingi elfu thelathini
“Asante sana Danny yani hapa nadaiwa hela na fundi simu, mbovu kashaitengeneza yule Domi alinivunjia mshenzi yule, nikaigomboe simu yangu”
“Pole sana, ya simu hii hapa” nilimpa tena elfu ishirini, jumla elfu hamsini”
“Asante sana Danny, bado unanipenda eeh, niambie Danny unataka nini kwangu?” alinishika mikono akinitazams usoni
“Hakuna ninachotaka kutoka kwako, nimekusaidia tu kama rafiki ninayekufahamu, siyo vinginevyo Glory, samahani, nina haraka sana” nilimjibu na kufungua mlango
“Danny please turudiane Danny ni utoto tu ulikuwa unanisumbua mwenzio” alinishika mkono kunizuia nisitoke
“Glory utanikera, nielewe basi” nilimjibu nikimbadilikia uso na kuutupa mkono wake kisha nikatoka
“Danny, Danny pleaseee!” aliita akiwa mlangoni na kuanza kuangua kilio kama mtoto mpaka wapangaji wenzake wakaja mbio mbio kumbembeleza, nililengwa lengwa na machozi lakini nisingeweza kurudia matapishi tena nikaingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi, wapangaji wengine nikiwaacha wananishangaa huku wakinong’onezana, maana walinifahamu maisha yangu ya kuuza biashara ndogo ndogo walizonizoea nazo, nikiwa nimepanga kurudi nyumbani simu yangu iliita, namba ni ya mwanamama mzungu, Meranda
“Danny”
“Yes mamy”
“Kuna kazi, upo tayari?”
“Nipo tayari, mzigo upo wa kutosha?”
“Pesa ipo, njoo hapa nyumbani tuanze kazi mara moja” aliniambia nikakata simu na kuongeza mwendo wa gari mpaka kwenye nyumba (appartment) hiyo, geti lilifunguka nikaingia na gari na kushuka nikafungua mlango na kuingia ndani nikakutana na yule mwanamke Pamela na wengine wawili wenye miili kama yake wakiwa wamekaa pamoja nae pamoja na mwanamama Meranda, nikawapungia mkono na kukaa kwenye kochi (sofa) langu la watu wawili, mwanamama Meranda akainuka kwenye kochi (sofa) alilokaa akaja kwangu na kunikalia mapajani
“Are you oky? (Upo sawa)” aliniuliza
“Yeah nipo sawa”
“Did you eat (umekula)”
“Yeah, ready, am full (tayari, nimeshiba)”
“Kwa sababu leo una kazi nzito hapa na ukiifanikisha basi kama kawaida dau nono linakusubiri” aliniambia huku akinipitishia kidole kifuani kimahaba, akiwa amevaa taiti ya kuogelea iliyotengenezwa mithili ya chupi iliyounganishwa pamoja na sidiria yake huku ikiwa nyembamba imepita katikati ya matako yake, mapaja yote yakiwa wazi, na hata wale wanawake wengine nao walivaa hivyo hivyo, mmoja akiwa mnaijeria na mwingine mjamaika pamoja na Pamela ambae ni mmarekani, nikahisi leo natakiwa kufanya mapenzi na mmoja kati yao ili nirekodiwe na ni kweli sasa hakuna nilichokiwaza zaidi ya pesa tu maana raha ya kushika mamilioni nilishaionja
“Nipo tayari” nilitikisa kichwa kwa msisitizo
“Na hii kazi ukiifanya vizuri basi kuna dau nono, mara mbili ya lile la mwanzo”
“Nani kati ya hawa?”
“Subiri” alinijibu na kuinuka taratibu akielekea chumbani, nikabaki nawatazama wale wanawake waliobaki pale ambao walikuwa wakicheza karata huku wakinitazama, Pamela akanikonyeza nami nikatabasamu tu
“Hi!” nilisikia sauti ya kike ikinisalimia nikageuka na kutazama nyuma anayenisalimia nikamwona ni kijana mrefu ambae ni mwanaume lakini aliyevalia mavazi ya kike huku akiwa amejipamba akapambika
“Hi?” nilimsalimia kwa kusita sita
“Sasa Danny, kazi ndo hii, we wanna record the best film ever, as I told, you receive double payments (tunataka kurekodi filamu bomba sana kuwahi kutokea, kama nilivyokuambia, malipo yatakuwa ni maradufu)”
“Nini, huyu si mwanaume huyu ndo nirekodi nae nani mimi?” nilimshangaa mwanamama huyo mzungu, aliponiletea shoga….
SEHEMU YA 19
“What hard for you Danny, I will pay you double and after recording this video, we will go together to Scottland, me and you, spend time, enjoying and so and so, look at her, she is so baeautful (nini kigumu kwako Danny, baada ya kurekodi hii video nitakulipa maradufu, na tutaenda wote kwetu Scottland, mimi na wewe, tutainjoi na mambo mengine mengi sana, mwangalie, ni mrembo sana)” aliniambia huku akimgeuza mwanaume huyo si rizki ‘ shoga’ ambae aliniwekea mapozi kama ya kike, akiwa na wigi kichwani, nikamsogelea karibu mwanamama Meranda
“Nilikuwa na wewe kimapenzi na huenda ningezama zaidi, sikujua kama yatakuwa haya mengine, ya kwanza nimekubali lakini huku unakotaka twende sipawezi”
“Hutaki pesa Danny, umeridhika tayari mara hii?”
“Pesa nataka sana lakini siyo kwa staili hii mamy, am sorry”
“Unajua nini kitakachotokea utakapokataa kazi hii Danny, tutakuharibia tu kwa jamii yako inayokuzunguka, kumbuka zile video tulizokurekodi kwenye ile filamu ya mwanzo tunazo na hatujapanga kuzitoa hapa nchini kwenu kwa sababu ya sheria zilizopo zinazotubana, lakini ukikataa kumalizia scene hii basi itabidi tuitoe tu na jamii yako ya hapa ione kinachoendelea kwako, kwanza ukifanya hii kazi ya mwisho utapata pesa nyingi zaidi ya zile za mwanzo, mara dufu halafu pili wala wewe hufanywi ila wewe ndiye unafanya, sijui umenielewa?” aliongea (kwa Kiingereza) huku yule mzungu shoga akinyonya kidole akiniangalia huku akijipapasa papasa tumboni kimahaba, nywele zake kichwani akiwa amezipaka rangi za upinde wa mvua, akijaribu kunivutia kimapenzi ili nikubali ofa ya kuigiza nae tukavunje amri ya sita, lakini hakuweza kunishawishi hata kidogo kwa sababu mambo hayo siyatamani hata kidogo na hata sitawahi kuyatamani, mambo ya kutembea na mwanaume mwenye mkia’ wa mbele kama mimi
“Siwezi kufanya kitu kama hicho nimeshasema na narudia tena kusema kuwa siwezi kucheza hiyo party tafuteni mtu mwingine, mwisho!” niliongea (kwa Kiingereza) kwa msisitizo, na kugeuka kutaka kuondoka, mkono wangu ukakamatwa nikizuiwa nisiondoke nikageuka kumtazama aliyeukamata mkono wangu nikamuona yule mwanaume si rizki’ akiwa ananichekea chekea
“Am hot and sweet, just try me and you will never regret, I like you (mimi ni wa moto na mtamu nijaribu tu na hautojutia, nimekupenda) aliniambia huku akinilegezea macho, nikatabasamu tu
” am for women not for men coz am men, positive is for negative not for fellow positive (napendelea wanawake siyo wanaume kwa sababu mimi ni mwanaume, chanya ni kwa hasi na siyo chanya enzie samahani)” nilimjibu kwa msisitizo na kuutoa mkono wake kisha nikaondoka nikiwaacha wote wananitazama, safari hii nikiiona hasira ya wazi wazi ya mwanamama mzungu, Meranda
“Danny, you gonna regret your decision young boy, trust me (Danny utajutia uamuzi wako kijana, niamini)” aliniambia sikumjali nikatoka na kuingia kwenye gari hilo dogo, nikaliondoa kwa kasi na safari hii sikupanga kurudi tena kwenye hiyo nyumba ya mzungu huyo kwa ajili ya hayo mambo yao, niliendesha gari taratibu nikifungulia muziki kwa sauti ya juu sana huku nikitikisa kichwa safari mpaka kwenye mgahawa mmoja wa chakula nikasimamisha gari na kuingia kwa ajili ya kupata chakula, nilikaa kwenye meza moja na muhudumu wa kike akaja
“Nikusaidie nini kaka?”
“Chizi na mishikaki na juisi ya matunda”
“Sawa jisikie upo nyumbani” alitabasamu na kugeuka kuondoka nikageuka kutazama tazama mazingira ya mgahawa huo nikaona jamaa wawili wakiwa wamekaa kwenye meza moja wakinitazama sana, sikujua kwanini walikuwa wananitazama namna hiyo na ikionekana wananizungumzia mimi, sikuendelea kuwafuatilia, chakula nilichoagizwa kikaletwa mezani kwangu na glasi ya juisi nikashukuru na kuanza kula na ndipo ghafla nikashangaa viti vingine kwenye meza yangu vilivyokuwa havina mtu vinavutwa na wanakaa wale jamaa wawili waliokuwa wananitazama sana na kunijadili
“Ndiye huyu si nimekwambia mimi?” mmoja alimwambia mwenzake, wakionekana wanabishana
“Siyo huyu bwana, wale wamarekani wale”
“Aaah wapi wakati code imeandikwa kabisa Tanzania pale, eti braza huyu anayecheza X si wewe huyu tazama mwenyewe” nilionyeshwa kwenye simu nikaanza kutazama na kweli nikaona video yangu na mwanamama mzungu Meranda nikimshughulikia sebuleni kwenye kochi (sofa) cha ajabu yeye alieditiwa kwa kuzibwa uso lakini mimi sikueditiwa chochote kile, naonekana kama nilivyo
“Siyo mimi” niliwajibu huku nikiendelea kula
“Ndiyo wewe bwana, si huyu unaonekana kabisa hebu mwangalie hapa anavyoonyeshwa kwa mbele akiwa amemkamatia hili jimama la kizungu cheki”
“Ndiyo kweli ndiye yeye nilikuwa nabisha vile vindevu vyake vya chini ya mdomo wa chini hivi hapa, halafu vimekaa vile vile mpaka vinaonekana kabisa” yule aliyekua anambishia mwenzake nae akakubaliana nae baada ya kunitazama kwa ukaribu
“Wazee kwani mmekuja kwa lengo gani sijawaelewa?” niliwauliza lakini hawakunisikia ndiyo kwanza walikuwa wanaikagua ile video ya X na muhudumu yule wa kike aliyenihudumia alikuwa ananiletea tishu kama nitahitaji nikimaliza kula nae aliposikia mabishano yao akasimama nyuma yao kutazama wanachokitazama
“Eti dada angalia vizuri huyu jamaa wa kwenye video si ndo huyu hapa tumekaa nae, au sisi tunaona vibaya?” walimwonyesha vizuri
“Aaah mnaangalia mambo gani mbona yanatisha hivyo, halafu huyo si ndo huyu kaka?” yule dada mhudumu nae alinishangaa, sikuweza kuendelea kukaa tena kula nikaiacha pesa mezani na kuinuka haraka haraka nikiwaacha bado wanaitazama video, muhudumu akaniona na kuanza kunikimbilia nao wakashtuka nimeshainuka wakaanza kunufuata, nikawahi na kuingia kwenye gari nikaondoka kwa kasi ya upepo wa kisulisuli, nilishusha pumzi ya wasiwasi nikikiona alichoniahidi yule mwanamama mzungu kuwa ataachia video hizo na jamii yangu itaziona, nikapiga konde kifua na kuongeza mwendo wa gari na ilikuwa lazima nipite njia ilipo nyumba anayoishi Glory mpenzi wangu wa zamani, nikakuta watu wamejaa wengi wengi nje kumaanisha kuna tukio, ikabidi nisimamishe gari na kumwita kijana mmojawapo wa watazamaji wa tukio hilo, kwenye hiyo hiyo nyumba anayoishi Glory
“Vipi mdogo wangu kuna nini?”
“Kuna mdada humu ndani alipanga amejiua kwa kunywa sumu leo”
“Anaitwa nani?”
“Glory, halafu ameacha ujumbe ‘MKITAKA KUJUA SABABU YA KIFO CHANGU MUULIZENI DANIEL”
“Tobaaa!!??” nilijikuta nashtuka kwa sauti baada ya kusikia tukio hilo la Glory kujiua na mbaya zaidi kuacha ujumbe wenye utata namna hiyo tena akilitaja jina langu…..
SEHEMU YA 20
Nilibaki nimetoa macho baada ya kusikia habari hizo kuhusu Glory na kuhusu mimi mwenyewe maana alinitaja kwenye ujumbe aliouacha kwa kuuandika kwenye karatasi kabla hajapoteza maisha msichana huyo mwenyeji wa mkoa mmoja (siutaji) ambao unasifika kwa matukio ya watu wake kujinyonga
“Glory kwanini umeamua kujikatisha uhai wako namna hii bila sababu ya msingi, kosa langu mimi ni nini, kukataa kurudiana nawewe au, mbona jambo liko wazi na ungeweza tu kuendelea na maisha yako mengine, ila sina hatia mimi nilishafanya sehemu yangu” niliongea mwenyewe huku nikijikuna kidevu nikiwa ndani ya gari nikatazama tena nje na kuona mwili wa Glory ukitolewa ndani ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe kitendo kilichonisikitisha zaidi, nikashindwa kuondoka nikabaki nimetulia tuli nikiangalia, askari watatu wakisimamia zoezi hilo, mmoja wa wapangaji ambae ananifahamu aliniona
“Afande, Danny mwenyewe yule pale” alininyooshea kidole watu wote wakanigeukia pamoja na askari
“Ooohoo huyu nae anaharibu sasa” niliwasha gari na kutaka kuliondoa lakini nikawasha vibaya na kujikuta nalizima kabisa
“Wewe simama” askari walianza kunikimbilia pamoja na watu wengine nikawasha tena kwa mara nyingine wakiwa wananikaribia walizingire gari nikafanikiwa kuliondoa kwa kasi wasije wakaniuzia kesi hiyo nzito ambayo wala hainihusu na sina kosa, niliendesha gari kama kichaa kwa kasi ambayo sijawahi kuendesha, almanusura nimgonge muendesha baiskeli nikamkwepa safari mpaka nyumbani nikasimamisha gari na kuingia ndani moja kwa moja nikifikia kujitupa chumbani kwangu chali, muda huo huo simu yangu iliita kutazama namba ni ya yule mwanamama mzungu, Meranda, sikupokea na namba yake nikaifunga (block) nikaitupa simu pembeni na kujinyoosha huku nikihema kana kwamba nilikuwa nimekimbia kwa miguu kumbe kwa gari, sikuwa na wasiwasi wa askari kunifuata nyumbani kwa sababu hakuna mpangaji anayepafahamu ninapoishi na ni mwendo wa dakika zaidi ya ishirini mpaka pale alipokuwa anaishi Glory, nilimkumbuka sana msichana huyo pamoja na mambo ya ajabu aliyonifanyia lakini pia alikuwa na mema yake, simu iliita tena nikapokea ilikuwa namba ya Joel rafiki yangu nika
“Joel?!”
“Duh mwana, niunganishe basi na hilo dili unalolifanya namimi nitoboe maana dah”
“Dili gani tena?”
“Si hilo mwanangu, ndo mambo yangu hayo, unaenda kimya kimya hata hunishirikishi mzee dah kweli nimeamini urafiki wa maneno upo”
“Unazungumzia kuhusu nini Joel?”
“Nimeona video yako mtandaoni, kuna mtu aliniambia nikambishia sasa ndo amenitumia, mwana yale mamama ya kizungu umeyapata wapi, ulienda nje au?”
“Joel imetosha, sitaki kuzisikia tena hizo habari yaani”
“Hamna kaka niunganishe namimi nitoboe dah maana siyo poa liwalo na liwe tu ilimradi namimi nipush ndinga na nipate mtonyo wa….” kabla hajamalizia sentensi yake nikamkatia simu na ndani ya sekunde hizo hizo simu ikaita tena ya namba tofauti tofauti za marafiki zangu wengine, hapo ndo nikagundua kuwa asilimia kubwa ya watu wanapita kutazama video za ngon** mtandaoni maana siyo marafiki zangu tu, wengine ni ndugu zangu na watu ninaowaheshimu ambao hawakuwahi hata kunipigia simu lakini leo niliona simu zao, nikalazimika kuzima kabisa simu, wasinitafute……
……….
Kunakucha mapema asubuhi siku nyingine, niliamka kitandani na kujinyoosha nyoosha kuondoa uchovu wa purukushani za siku ya jana, nilitoka mpaka sebuleni na kukuta televisheni inaongea peke yake na ikionekana ni taarifa ya habari, nilipita kwenda kutafuta maji ninawe uso wangu lakini nikasita baada ya kusikia habari ninayoifahamu nikageuka kuitazama…
“…habari zilizotufikia hivi punde ni kuhusu kukamatwa kwa mwanamke mmoja wa kizungu kwa jina anaitwa Meranda raia wa Scottland na wanawake wengine kadhaa wa kimarekani na wengine wa Jamaica na wanaume watatu wazungu kwa tuhuma za kujihusisha na kurekodi filamu za ngono kinyume cha sheria za nchi baada ya wasamaria wema kuripoti kutoelewa watu wanaoingia kwenye nyumba hiyo ya mzungu na zimekutwa video kadhaa zilizokwisha kurekodiwa na tayari wahusika wameshikwa na kutiwa mbaroni akiwemo kijana mmoja wa kitanzania aliyefahamika kwa jina moja la Danny ambae anatafutwa na jeshi la polisi ili aunganishwe kwenye kesi hiyo kutokana na kuhusika katika uigizaji wa…” nilizima televisheni haraka baada ya baba kutoka chumbani kwake
“Mbona unanizimia TV wakati nimeiwasha ili niangalie taarifa ya habari?” aliniuliza
“Oooh shikamoo baba, nilitaka kubadili chaneli ndo nikabonyeza vibaya, kuna chaneli nilitaka kutazama magazeti, ngoja nikuwashie” nilizuga na kuwasha tena televisheni hiyo na kwa bahati nzuri ile habari ilikuwa imeshapita, nikapumua na kupiga hatua kuondoka
“Danny?” aliniita
“Naam baba” nikasimama
“Hujaniambia ni kazi gani hiyo unayofanya iliyokupa pesa ya haraka haraka na mpaka gari, ni ya halali kweli?”
“Ndiyo baba ni ya halali na…”
“Hodi” kabla sijamaliza kumjibu baba nikasikia sauti ya mwanaume nje,
“Karibuni, Danny katazame wageni nje” mama aliitika na kunituma, nikaingiwa na mashaka baada ya kusikia sauti za vishindo vya miguu mlangoni kumaanisha kuwa ni wageni yaani zaidi ya mtu mmoja nikasogea na kuchungulia dirishani nikaona wanaume watatu waliovalia kiraia lakini kwa walivyojiweka weka nilijua tayari kuwa nia askari wakiwa wamekuja na gari dogo,
“Mh hili balaa sasa” niliguna na kugeuka haraka nikijifanya nimebanwa na mkojo nikikimbilia chooni nikapishana na mama njiani
“Wewe vipi mbona hufungulii wageni?”
“Mkojo mama” nilimpita yeye akaenda mlangoni kuwasikiliza nami sikwenda chooni kama nilivyodanganya, nikaingia chumbani kwangu na kuchukua simu yangu na kadi yangu ya benki pamoja na begi nililoweka nguo zangu chache, nikatega sikio kwenye dirisha langu lililokuwa upande wa kule kule mlangoni nikiwa ninajiandaa kuondoka muda
“Za muda huu, shikamoo”
“Marahaba karibuni sana” mama aliwakaribisha ila kwa wasiwasi
“Nadhani hapa ndipo anapoishi kijana mmoja anaitwa Danny”
“Ndiyo ninyi ni akina nani samahani?”
“Askari wa jeshi la polisi kutoka kituo kidogo”
“Askari, kuna nini, amefanya nini mwanangu?” mama aliingiwa na mashaka nikajua tayari nimeshafuatwa kwa suala lile lile la wale wazungu, sikutaka kusikiliza maongezi yao tena nikatoka chumbani haraka
“Wewe unakwenda wapi?” baba aliyekuwa hana habari ya kinachoendelea nje aliniuliza
“Tutaonana baba, nina safari ya dharura, nitawatumia pesa, tutawasiliana baada ya siku tatu” nilimjibu na kuondoka haraka haraka nikipitia mlango wa nyuma na kwa bahati nzuri ndipo ninapopaki gari nikimwacha baba anashangaa tu haelewi, nikawasha gari haraka na kuliondoa kwa kasi nikijikuta mzoefu ghafla wa kuendesha gari kwa sababu ya mikasa iliyonikuta, askari wawili walikuwa wameshaingia ndani na mama na mmoja alibaki nje akaniona wakati naondoka
“Mtuhumiwa wetu huyu huku anakimbia na gari, simama wewe kijana” aliwaita wenzake, nikampita bila kusimama na wenzake nao wakatoka ndani mbio mbio na mama na baba ambao waliniita wakinishangaa, askari hao watatu wakaingia ndani ya gari lao dogo walilokuja nalo nikiwa nimewaacha mbali wakaanza kunifukuzia nyuma lakini nilishaingia barabara kuu nikalipeleka gari kwenye maegesho moja na kulituliza wakapita kwa kasi nami nikalitoa gari hilo na kurudi upande waliotokea lakini sikurudi tena nyumbani, nikaenda nje ya mji kwenda kutafuta mahali pa kuishi kwa mwezi mzima mpaka mambo yatakapitengamaa, nilichofanya ni kuwatumia nyumbani pesa ya matumizi tu na ujumbe wa kuwaomba radhi kwa kitendo nilichokifanya na nikazima simu nisitafutwe, maisha yangu ya mwezi mzima yalikuwa ni ya kulala kwenye gari, sikutaka kuingia gharama ya kupanga chumba au nyumba, zile milioni kadhaa zilizobaki nilizipangia kazi nyingine, lakini cha moto nilikiona…..
Hakuna Baya au Jema lisilo na Malipo
MWISHOOOOOOOOOO!!!!