NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE
EPISODE 07
Usiku baba Belinda akiwa nyumbani amepumzika na familia yake akiwemo Norah bintiye mara akapigiwa simu na msimamizi wa kampuni yake kubwa inayomuweka mjini. Akapokea akijua ni taarifa nzuri ya michongo ya pesa, mara akasikia.
“Hallo bosi kumetokea majanga huku kwenye kampuni jengo lote la kampuni limeungua moto” Sauti upande wa pili wa simu ilisikika ikimtaarifu Mr. Raymond baba yake Belinda. “Oooh shit! chanzo cha moto ni nini jamani ” Aliuliza Mr. Raymond huku akikuna kichwa chake kwa kuchanganyikiwa. “Ni shoti ya umeme bosi” Sauti upande wa pili wa simu ilisikika ikiongea, Mr. Raymond akakata simu yake. “Baba kwani nini kimetokea” Norah bintiye aliuliza baada ya kuona baba yake kama kavurugwa vile.
“Jengo la kampuni limeungua moto” alijibu Mr. Raymond huku machozi yakimtoka. “Uuuuu umasikini huo tayari umeshabisha hodi Mungu wangu yani sijui itakuwaje na vile kampuni ilikuwa inaendeshwa kwa mikopo sijui tutapata wapi pesa za kulipa mikopo” Alisema Norah wakati huo familia nzima walikuwa kama wamepagawa sio Mr. Raymond, mkewe wala watoto wake akiwemo Belinda wote walikuwa wamepagawa kwani kampuni hiyo ndiyo ilikuwa inawafanya waishi mjini.
Wakiwa wanalia kwa kuomboleza mara wakasikia “hodi” Mr. Raymond akashuka kidogo. “Jamani hiyo sio sauti ya Prosper kweli hebu kafungue mlango” Alisema Mr. Raymond huku akiwa amepigwa na butwaa, hakuamini kama Prosper anaweza kuwa hai mpaka muda ule kwani tayari alishamkabidhisha kwenye mikono ya wauwaji.
Mama Belinda alienda kufungua mlango na ndipo akakutana na Prosper, alimkaribisha ndani, Prosper aliingia. “Mzee shikamoo”Prosper alimsalimia baba Belinda. “Marahaba” alijibu Mr. Raymond huku akitizama pembeni kwa aibu kwani alitarajia kupewa taarifa na wale wauwaji kwamba Prosper amekufa.
“Mzee najua hauna furaha baada ya kuniona lakini nataka niwaambie kuwa pesa na magari ni vitu vya kupita, leo una pesa na unatumia pesa zako kuangamiza wanyonge, kuua lakini kumbuka kuna maisha mengine baada ya haya na pia kuna hukumu kuu siku ile ya kihama, pesa na magari utaziacha hapa duniani, ulitoa amri mimi nikauwawe lakini Mwenyezi Mungu kaniokoa” alisema Prosper huku akibubujikwa na machozi.
“Haaaa baba kumbe ulitoa amri Prosper auwawe, mbona nilipokuuliza kaenda wapi ulisema kaenda kwao, hayo ndio malipo yako sasa ona kampuni imeungua na unadaiwa mikopo kibao, heri tuonje umasikini ili tujifunze kuishi na watu” Belinda alimwambia baba yake lakini muda huo mzee Raymond alikuwa ni wa kulia tu.
“Oooh mzee pole kumbe mmepata majanga Dah pole sana mzee” Prosper aliongea huku akiwatia moyo mmoja baada ya mwingine akahamia kwa Norah. “Dada Norah poleni sana majanga kama haya yanatokea kwa mipango ya Mungu hatujui ni kitu gani Mungu kakipanga hivyo tunapaswa kushukuru kwa yote” Prosper alimwambia Norah. “Na wewe hebu nitokee hapa! Wewe jua kuhusu kazi yako ya ulinzi mambo ya familia yetu hayakuhusu na sasa sijui utapata wapi pa kula mbwa wewe nyumba hiii itapigwa mnada sijui utalinda wapi?” Alisema Norah kwa hasira. Prosper akakaa kimya.
“Heri yake yeye ana fani ya ulinzi wewe una fani gani? Yeye nyumba ikipigwa mnada anaenda kuomba kazi kwingine wewe utaenda wapi na kusoma hujasoma kwasababu tu una kiburi cha utajiri!” Belinda alimwambia Norah. Hakika usiku ule ulikuwa ni usiku wa majuto kwa familia ya mzee Raymond. Kesho yake asubuhi watu watu wanaodai pesa zao mbali na wale wa mikopo ya bank walikuja kudai baada ya kusikia kampuni ya Mr. Raymond imeungua. Mr. Raymond alikuwa ni wa kulia tu hajui awajibu nini watu wale kwani kila mmoja alikuwa amemchachamalia balaa.!
“Jamani wote jumla mnadai shilingi ngapi?” aliuliza Prosper. Kila mmoja alisema anachodai, Prosper akapiga mahesabu na kubaini kuwa mzee Raymond anadaiwa milioni mia na sana madeni tu ya kawaida.
“Basi acheni nampigia mtu alete hizo pesa” Alisema Prosper kwa ujasiri na kuwafanya watu wote waduwae kwani aliongea akiwa siriasi, Norah alicheka sana mara akashangaa Prosper aki……
JE NINI KILIENDELEA SASA?
EPISODE 08 & 09
Prosper alichukua simu ya Belinda kisha akaongiza namba ya Vicent, akampigia, Vicent alipopokea tu Prosper akaweka loudspicker🔊 ili kila mtu asikie. “Haloooo Vicent” alisema Prosper. “Naaam bosi” Vicenti akaitikia na kumfanya Norah aliyekuwa ametega sikio kusikiliza maongezi yale acheke kinafiki🤨🤣 “eti Bosi kwahiyo unatuletea maigizo hapa labda bosi wa utumbo 🤮🤮” Alisema Norah kwa kejeli , wala Prosper hakujali aliendelea kuongea. “Naomba uende hapo benki 🏦 unitolee tena milioni mia na sitini, kwenye ile nyumba niliyokuelekeza kuwa kuna mabinti wawili wazuri nataka nioe mmoja wao, fanya hivyo!” Prosper alitoa Amri. “Sawa bosi si pale kwa yule mzee tajiri sana, mzee Raymond?” Vicent aliuliza . “Yah!” Prosper alijibu na kukata simu.
“Hahahaha umaridadi bwana yani anaongea utadhani ni bosi, hapo pengine anaongea na mtu ambaye wanatanianaga, tena naomba usiwe unanisema kwa watu kuwa unanipenda mpende Belinda kishoia mwenzio” Alisema Norah akimwambia Prosper kisha akampandisha na kumshusha, akatema mate pembeni.
Prosper hakujali, alijiamini kwani alijua ule ndio muda muafaka wa kujidhihirisha kuwa yeye ni nani, walikaa kimya wakisubiri, huku mama Belinda pamoja na Norah wakikonyezana na kucheka sana. Nusu saa baadae mara wakasikia kengele ikilia kuashiria kuna mtu getini anabisha hodi. “Halafu Prosper unajitoa ufahamu eee umesahau kuwa wewe ni mlinzi wa getini hebu kamfungulie huyo anayebisha hodi huko usitutibue” Alisema Norah.
“Belinda kanisaidie kumkaribisha mgeni wangu eti mama” Prosper alimwambia Belinda kisha Belinda akatoka nje , punde alirudi na mgeni aliyevalia suti safi ya kikazi, mkononi alishika Brifcase kubwa, akimkabidhi Prosper huku watu wote wakiwa wametuwaa. Prosper akaiweka ile Brifcase mezani ile anaifungua tu baba Brenda alidondoka na kupoteza fahamu huku mama Belinda, Norah na watu wote waliokuwa mule ndani wakiwa wameduwaa tu.
Prosper aka…..
JE NINI KILIENDELEA?
EPISODE 10 & 11 & 12
Prosper akazitoa zile pesa kwenye Brifcase na kuzitandaza mezani wakati huo Norah na mama yake walikuwa bado tu wameduwaa, walikuwa hawaamini kabisa wanachokiona, kwao ilikuwa sawa na ndoto ya mchana.
“Jamani mimi nitawasaidia kulipia tu haya madeni madogo madogo ambayo ni milioni 160 hayo Mengine mtalipa wenyewe” Prosper alimwambia mama Belinda na Norah.
“Hata hivyo baba utakuwa umetusaidia sana japo kwa jinsi mzee anavyodaiwa hakika umasikini tayari ushabisha hodi, Dah ama kweli ndio maana waswahili wakasema binadamu wote ni sawa, kumbe pesa, mali na magari ni vitu vya kupita tu”Alisema mama Belinda huku machozi yakimbubujika, hakuwa yule mama Belinda aliyekuwa akitoa maneno ya kebehi sasa alikuwa mpole kama vile kamwagiwa maji ya baridi. Prosper alizigawanya zile milioni sitini kwa watu wote waliokuwa wanamdai Mr. Raymond baada ya pale wakampatia Mr. Raymond huduma ya kwanza kwani alikuwa amepoteza fahamu.
Mr Raymond alizinduka, alikuta madeni yake yote madogo madogo yamelipwa. Alishukuru sana na kusema. “Prosper Nisamehe sana kwani nilitoa maagizo uuwawe kisa wewe ni masikini unayetaka kumuoa mwanangu, sikujua maisha yanabadilika kama tarehe zinavyobadilika au misimu ya mwaka, ona leo hii licha ya kunisaidia kulipia hela zote hizo bado nadaiwa,. bado umasikini unaniita hakika nitauweka wapi uso wangu mimi, niacheni tu nife” alisema baba Belinda huku akihema sana, presha iliyosababishwa na madeni ilikuwa imepanda hakuchukua muda alifariki, vilio vilitanda, ndugu walikuwa mbali walipigiwa simu, mazishi yalifanyika lakini baada tu ya mazishi kufanyika hazikupita siku siku mbili, Bank zote zilizomkopesha mzee Raymondzilianza kudai, hatimaye vitu vyote vya mzee Raymond vilipigwa mnada,
Familia ya mzee Raymond haikuwa tena na hata sehemu ya kulala, Prosper aliwachukua na kuwapeleka kwake alipojenga, alimchukua Norah, mama yake, na Belinda. Walipofika hawakuweza kuamini kabisa walichokiona, Prosper aka…….
JE NINI KILIENDELEA HUKO NYUMBANI KWA PROSPER?
MAMBO NDIO KWANZA YANAANZA USICHEZE MBALI !
ITAKUWAJE SASA WAKATI PROSPER KAWACHUKUA MAADUI ZAKE NA KUISHI NAO PAMOJA?
JE NORAH NA MAMA YAKE WATAJIFUNZA AU NI KAMA VILE WASWAHILI WANASEMAVYO KUWA TABIA NI KAMA RANGI YA NGOZI YA MWILI KATU HAIWEZI KUBADILIKA??????!