Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE

EPISODE 22

Prosper aliingia chumbani walipo Norah na mama yake huku akiwa ameishika simu ya Norah. “Kuna mtu ananipigia shemu?” Norah aliuliza. Prosper hakujibu kitu zaidi ya kulisafisha koo lake kwa kikohozi chepesi kisha akakaa kwenye kiti cha kifahari kilichokuwa mule chumbani.

“Siku zote kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho, ukianza kwa ubaya utamaliza vibaya, na ukianza kwa wema basi ni lazima umalize kwa wema. Leo mwisho wa ubaya wenu umefika?” Alisema Prosper akiwaambia wote kwa ujumla yani mama Belinda na Norah. Wakashtuka kidogo na kuanza kuweweseka kwa wasiwasi mwingi.

“Baba kuna nini tena jamani mh nyumba hii haiishi maneno” Alisema mama Belinda. “Norah cha kwanza kabisa useme ni wapi Belinda alipo maana nimegundua kila kitu?, Nimegundua kuwa wewe ulitaka kumuua Belinda kwa sumu siku ile ya harusi lakini kwa bahati mbaya chakula kile akala mama.  Achilia mbali hilo la sumu, nimegundua kuwa mlengwa uliyetaka afe siku ya harusi ni mimi lakini mama akakushauri mumuue Linda kwasababu ni mtoto wa kuokotwa ingawa Linda yeye hajui hilo. Nimegundua mengi kwa wewe ndiye uliyempiga Linda risasi siku ile ya kwanza kabisa Linda alivyonitoa out na kunipeleka utulivu Hotel, na kwa kufanya vile nawaza kama usingefanya vile hata baba yako mzee Raymond asingekutwa na maafa” Prosper aliongea wakati huo mama Linda na Norah wakiwa wameimamisha vichwa chini mithili ya watu wanaosikiliza hotuba ya majonzi msibani inayomuhusu marehemu.

“Yote tisa kumi nimegundua kuwa wewe ndio umefanya mchongo Belinda atekwe na majangili akauwawe, pia nimesoma Sms zako nikagundua kuwa mwanaume uliyekuwa unachati naye ni mtu wako wa karibu yani mpenzi wako na mpanga baada ya Belinda kuuwawa na mimi mje mniue mtawale mali! Hayo yote ya kweli au naongopa?” Aliuliza Prosper.

“Ni kweli Shemu naomba utusamehe mimi na mama, tulikuwa tunashauriana mabaya bila kujua mwisho wa ubaya ni aibu, fedheha au hata mauti, tusamehe Prosper” Alisema Norah huku akipiga magoti mbele ya Prosper. “Kabla ya kutoa maamuzi yangu juu yenu nataka haya yatekelezwe, piga simu hapa hapa waambie waomteka Linda na Doris wawarudishe mara moja,” Alisema Prosper akimpa Norah simu. Norah akafanya hivyo wale majangili wakasema ndani ya Lisaa limoja na watawaleta ila tu wakute pesa zao Norah alizowaahidi!. Sidhani kama Norah hizo pesa anazo maana alipanga Belinda akiuwawa, Prosper naye auwawe ili wauze mali za Prosper wawalipe wale magaidi..

UNAHISI ITAKUWAJE?

MAJANGILI WAKIKOSA PESA ZAO ITAKUWAJE?

UNAHISI PROSPER ATATOA MAAMUZI GANI?

MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU KWA NORAH NA MAMA YAKE?

EPISODE 23 & 24 & 25

Prosper, Norah na mama Belinda walitoka na kukaa sebuleni wakisubiri majangili walimteka Belinda na Doris wawarudishe. Walisubiri mpaka majira ya saa tatu usiku ndipo mlango ulipogongwa, Prosper alifungua na mara akashtukia kumuona Belinda akiingia pamoja na Doris huku wanaume watatu waliofunika nyuso zao kwa soksi maalumu wakiwa nyuma yao.

“Watu wenu hawa hapa sisi hatuna muda wa kupoteza tunataka tupotee eneo hili tupatieni chetu?” Alisema Jangili mmoja aliyeonekana kuwa ndio kiongozi wa wengine. “Haya Norah toa pesa ya watu, kama uliwaahidi kubwa utawapa pesa” Prosper alimwambia Norah.

Norah hakujibu kitu zaidi ya kutetemeka kwa woga. “Nyie naona kama mnatuzingua sisi tunaondoka na huyu tutakachomfanya hakika hamtaamini, yeye si anajidai kutoa kazi hana pesa. Broh tupe namba yako ya simu ya whatsapp tutakurushia picha za matukio yote tutakayomfanya ndugu yako laa sivyo msaidie kulipa” Alisema Jangili mmoja huku akiwa amemshika kwa nguvu Norah.

Prosper alimtizama kwa Doris na Belinda usoni jinsi walivyokuwa wamevimba na nyuso zao kuvia damu hakika alipata hasira na kusema “Nyie mchukueni tu mimi sina pesa”Alisema Prosper. “Jamani kaka Prosper nisaidieeee nisaidieeee  jamani nakufa.aa.”Norah alilia wakati huo majangili walimtoa nje na kumpakiza kwenye gari lao, punde waliwasha gari na kuondoka naye.

“Poleni sana mke wangu pamoja na Doris” Alisema Prosper, Belinda na Doris walikuwa ni wakulia tu ikabidi usiku ule Prosper awapeleke hospitali kwa matibabu zaidi, hawakulazwa walirudi usiku huo huo na kumkuta mama yao amelala.

Kesho yake asubuhi Belinda alimuita mama yake sebuleni. Wakati huo Prosper pamoja na Doris wote walikuwepo. “Jamani siku zote huruma huzaa dhambi, huruma au upole ukizidi sana ni dhambi, mimi mama nimekusamehe lakini maamuzi yangu kwa sa…..” kabla Belinda hajamaliza kutoa maamuzi yake mara simu ya Prosper iliingiza meseji kwa mfululizo, zilikuwa ni meseji za whatsapp na kuna picha alitumiwa azifungue. Prosper alipofungua picha moja wapo ya zile picha alizotumiwa, alianza kutetemeka kwa woga na hakuchukua hata sekunde alipoteza fahamu!

JE HIZO PICHA ZILIKUWAJEEE TENAAA?

NI MAAMUZI GANI BELINDA NAYE ANATAKA KUTOA KWA MAMA YAKEE?.

EPISODE 26

Baada ya Prosper kuzimia ghafla, Belinda alichukua simu yake kusudi aone ni kitu gani kilichompa mshtuko Prosper kiasi cha kumfanya apoteze fahamu. Alipochukua simu ile na kutazama machozi yalimtiririka tu baada ya kuona picha iliyoonyesha Norah akiwa  kamezeshwa chupa ya mdomoni ikawa imetokeza kwa nje kidogo tu, jicho lilikuwa limemtoka Norah kuashiria kuwa hayupo hai tena, chini ya picha ile kuliandikwa maneno yaliyoandikwa maneno yaliyosomeka hivi “Hii ndio dawa ya maboss wanaotoa kazi wakati hawana pesa za kuwalipa wanaowafanyia kazi” Belinda aliendelea kutaza picha nyingine wakati huo Doris akiendelea kumpatia hewa prosper kwa kumuwekea feni karibu ili azinduke!

Hakika macho ya Belinda yalikosa ustahimilivu wa kuendelea kutizama picha zile ambazo Norah alifanyiwa unyama mkubwa. Belinda alilia sana hakutaka hayo yatokee kabisa, hakuwa na jinsi ya kuzuia mambo hayo kutotokea.

Punde Prosper alizinduka baada ya kupata hewa kwa dakika kadhaa, alikuwa amechoka sana. Machozi yalianza kumtoka hata mama Belinda naye alilia sana.

“Prosper na Belinda jamani mimi sistahili kabisa kuwa karibu yenu, niliwakosea sana naweza kusema mimi ndio kiini cha haya yote yaliyotokea!, Maana mimi kama mtu mzima au kichwa cha familia kwasababu mwenzangu Raymond tayari alishatangulia mbele za haki,nilipaswa kuwaongoza ninyi bila kuegemea popote. Lakini ajabu nikampa Norah kipajmbele kwenye kila jambo alilonishauri, Norah alishauri tukuue Prosper ili tuchukue mali lakini kidogo niliona aibu hata hivyo nilipaswa kumkemea na kumrudi badala yake ndio nikamshauri tumuue Belinda ili Norah aolewe na Prosper, hivi kweli kwa haya niliyotenda nitawezaje kuishi na nyie?. Hakika nilipanda mbegu ya chuki juu yenu na haya ndio mavuno yangu, haya ndio malipo ya ubaya, nasema sistahili tena kuwa nanyi” Alisema mama Linda kwa kilio, nyumba nzima ilikuwa ni kilio, sio Belinda sio Prosper sio Dora wote walikuwa na majonzi.

“Usijali mama siwezi kulipa baya kwa baya kwani sijui kesho yangu itakuwaje, mimi na mwenzangu Belinda tumekusamehe kwa moyo mmmoja, acha niwapigie hawa majangili simu tuone namna tutakavyoupata mwili wa Norah kusudi azikwe kwani naye ni binadamu anahitaji kusitiriwa” Alisema Prosper kwa sauti iliyojaa kilio cha kwikwi

Mara akashangaa simu yake inaingiza tena meseji, alipoangalia alikuwa ametumiwa tena picha akaifungua picha ile, hakika majonzi yalizidi kuongezeka baada ya kuona mwili wa Norah ukiliwa na mbwa wanaowafuga wale majangili kule msituni.

Hali hiyo ilimfanya mama Belinda kukimbilia chumbani na kujifungia huku akilia, Prosper na Belinda walimfuata kumbembeleza lakini mama Belinda hakufungua mlango alilia sana na baadae alinyamaza kwa muda sana mpaka ikampa hofu Prosper, akaamua kuvunja mlango na ndipo alipomkuta mama Belinda akiwa kajinyonga kwa khanga yake

R. I P mama Belinda😭,, 😭. R. I. P Norah. Duniani hakuna mkamilifu ila kupitia nyie tumejifunza kitu, tumejifunza pesa na mali ni vitu vya kupita hivyo tuishi kwa usawa kwani wote tuliumbwa kwa udogo.

*****MWISHOOOO******

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!