Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE

EPISODE 13

Prosper alianza kuishi na familia ya marehemu mzee Raymond kwa upendo wa hali ya juu, alihudumia familia hiyo kwa kila kitu, mavazi, chakula na mahitaji mengi tu ambayo mengine hata hayakuwa ya muhimu.

“Mama mimi nina nina jambo nataka kuzungumza nanyi” Alisema Prosper wakiwa wamekaa mezani wanakula. “Ongea tu baba ” Mama Belinda alijibu. “Ni muda mrefu sasa toka nimeanza kuishi nanyi, nimepita nanyi katika shida na raha na sasa tunaishi wote kwa amani na upendo. Ninachotaka kusema ni kwamba kwa sasa nataka kuoa, nataka nimuoe Belinda” Alisema Prosper.

“Ooooh thanks jesus”  Belinda Alishukuru kwa Mungu kwani walikuwa na kamda karefu mno hawajaongelea mapenzi yao kutokana na matatizo yaliyowakumba.

Basi Norah kusikia vile alitupa kijiko mezani kwa hasira akaamka na kwenda chumbani kwake akiwa amenuna sana. Hakupenda kabisa Belinda aolewe kabla yake ile hali yeye ndio mkubwa!

Mama yake alimfuata chumbani “Norah kulikoni umezira kula, au umechukia uliposikia mdogo wako anaolewa. Wewe huoni kuwa ni jambo la kheri hili tunaunganisha undugu na Prosper” aliongea mama Belinda kwa hisia kali sana.

“Hapana mama kwanza huyu kaka alianzaga kunitongoza mimi, leo iweje amuoe Belinda, hata kama niliwahi kumeharau lakini mambo hayo si tulishamaliza kwa msamaha, kwanini lakini”  Aliongea Norah huku akilia, make-up yote aliyojipaka usoni ikaharbika kwa machozi yaliyouloanisha uso wake chapachapa, hakika aliumia sana.

“Sasa unatakaje we sema tu mwanangu” Mama Norah alimuuliza bintiye, aliwadekeza sana mabinti zake hakutaka wakose raha maishani.

“Najua Prosper hawezi kunioa mimi tena, kama ni bahati nilishaichezea ila mama huyu kaka ana mali nyingi sana na cha ajabu hatukuwahi kuwaona ndugu zake na kila tukimuuliza anasema tusiongelee mambo hayo inamaana kuna madhila aliyowahi kupitia yakamfanya akose ndugu, hivyo sisi ni kama ndugu zake, unaonaje tumuue siku ya harusi kwa kumuwekea sumu kwenye chakula” Alisema Norah mama yake akashtuka sana huku macho yakimtoka mithili ya mtu aliyemeza tonge la moto likakwama koooni!

JE MAMA ATAFUATA USHAURI WA BINTIYE KIPENZI?

NA IPI HATIMA YA PENZI HILI LA PROSPER NA BELINDA AMBALO LIMEANZA KUPIGWA VITA KIMYA KIMYA!

HEBU TUONE MAMA ALIVYOSEMA ILI UJUE KUNA WATU NA VIATU

EPISODE 14

“Huyu kaka ametusaidia sana, alilipa madeni ya marehemu baba yako, na licha ya kwamba tulimkosea lakini baada ya mali za mume wangu kutaifishwa tukabaki hatuna mbele wala nyuma ametuchukua na sasa tunaishi naye bila tabu, huoni tukimuua tunakosea, wewe kama shida yako ni kuwa na Prosper usijali, nashauri tumuue Belinda, najua Belinda akifa Prosper   atahamia kwako kwani alianza kukutaka zamani kabla ya Belinda” Alisema mama Belinda.

“Heee mama tumuue Belinda, hivi upo serious kweli mama, yani hata uchungu hauna” Aliuliza Norah kwa mshangao. “Nasema hivyo kwasababu Belinda sio mwanangu wa kumzaa, Belinda tulimuokota akiwa mdogo ila yeye hajui anajua mimi ndio mama yake, hata wewe na watu wengine tuliwaficha! . Baba yako alikuwa anampenda sana Belinda na ni kwasababu tulimuokota!” alisema mama Belinda na kuzidi kumshangaza Norah.

“Mh kumbe Linda sio mdogo wangu, yani vile alivyokuwa akimdekea baba na baba anamtetea sometymes kumbe aliokotwa” Norah aliongea huku akizidi kushangaa. “Ndio hivyo ila usimwambie mtu maana hata yeye mwenyewe hajui” Alisema Mama Belinda.

“Mh bora life pengine ningezaliwa mwenyewe baba angekuwa anampenda  sana kama alivyokuwa akimpenda Linda, alimpenda sana Linda kumbe sio mwanae life tu” Norah alikubaliana na ushauri wa mama yake kuwa badala ya kumuua Prosper, mtu mwenye moyo wa dhahabu ni bora siku hiyo ya  wamuue Linda!

Basi kidogo moyo wa Norah ulifarijika, maisha yaliendelea huku mipango ya harusi ya Linda na Prosper ikifanyika kwa kasi sana. Prosper aligawa kadi kwa watu mbalimbali. Hatimaye siku ya harusi iliwadia, ilikuwa ni harusi kubwa ya kukata na shoka, yani haikuwahi kutokea kwani ilifanyika  bichi yani ufukweni mwa bahari, hakika ilikuwa ni harusi ya kipekee na ya aina yake.

Norah alisimamia kitengo cha mapishi, huku mama yake akikaa meza moja na maharusi. Ndoa ilifungwa bila pingamizi, na baada ya Prosper na Linda kuvalishana pete kwa furaha hatimaye muda muafaka wa chakula ukawadia. Kwa kweli Linda alikuwa na furaha kubwa sana ilikuwa ni siku ya kipekee kwake aliyokuwa akiiota miaka na miaka.

Basi Norah alipakua sahani tatu za maharusi. Akampa maelekezo binti ambaye ni msaidizi wake kuwa katika sahani tatu alizopakuwa, yani ya Linda, Prosper na mama yake, ahakikishe akifika mezani anampa Linda ile sahani nyeupe” Norah alimsisitiza sana Doris msaidizi bila kumwambia kwanini ile sahani asimpe mtu mwingine, lakini ukweli ni kwamba chakula cha sahani hiyo kiliwekwa sumu. Basi Doris akachukua Trei la chakula na kupeleka chakula kwenye meza ya maharusi. Lakini alipoweka tu chakula mezani, mara akashangaa…..

JE NINI KILITOKEA CHA KUSHANGAZA?

MPANGO WA NORAH UTAFANIKIWA AU LITAIBUKA LIPI????

EPISODE 15

Doris alipoikaribia meza ya maharusi alipatwa na kitu kama kiini macho, akashangaa pale alipokuwa amekaa Belinda anaona mama Belinda ndio amekaa na  pale alipokuwa amekaa mama Linda anaona Linda ndio amekaa.

Ilibidi asimame kidogo na kuanza kujiuliza, “Hee inamaana hawa watu wamebadilisha viti au ni mimi naona vibaya” Alijiuliza Doris lakini ukweli ni kwamba watu walikuwa wamekaa vilevile kama walivyokuwa wamekaa awali. Akajikuta akienda kumpa mama Linda ile sahani nyeupe yenye sumu akijua anampa Linda, na nyingine mbili zilizobakia akimpatia Prosper na Linda. Akarudi jikoni.

“Umempa ile sahani nyeupe Belinda” Norah alimuuliza Doris. “Ndio na tayari wameshaanza kula. Doris Alijibu kwa ujasiri bila kujua tayari alishayakoroga mambo kiajabu ajabu bila kujua nini kilitokea mpaka akaona mawenye kama sio mazingaombwe. “Ok na nyie pakueni muendee kula” Norah aliwaambia wapishi huku akitoka nje na kwenda kuangalia kwenye jukwaa la maharusi nini kinachoendea.

Ile anatoka nje na kuangalia pale jukwaani, mara alishtuka “Oooh my goodness!” Alisema Norah kwa mshangao huku akirudi ndani alipo Doris baada ya kuona Doris amempa mama Belinda ile sahani nyeupe yenye yenye sumu. Alipofika ndani alimuuita Doris pembeni kusudi wapishi wengine wasisikie “We Doris nini umefanya lakini, nani kakuambia ile sahani nyeupe umpe mama kwanini hufuati maelekezo lakini!” Norah alimgombeza Doris.

“Lakini dada mbona nimempa  Belinda” Alijibu Doris huku akilia, moyoni alihisi kuonewa. “Kwahiyo mama ndio amegeuka kuwa Belinda?” Norah alizidi kugomba sana. “Lakini dada kwani kuna shida gani mama yako akila hicho chakula cha sahani nyeupe mbona chakula ni kile kile  tu” Doris alimuuliza Norah swali hilo lililoonekana kuwa gumu kama kumwambia mtoto wa chekechea atoe difiniton ya Low of achmedecy principle. Ilibidi tu amtulize Doris kwasababu alijua akiongea sana siri itabainika.

“Basi Doris usiwe shaka mdogo, mambo haya yaishie hapa hapa usimwambie mtu mwingine sawa!” Alisema  Norah. “Sawa dada” Doris aliitikia lakini alihisi kitu ila akaacha mambo yaende tu hivyohivyo.

Basi haraka Norah akaenda pale kwenye jukwaa la harusi na kumuita mama yake nyuma ya jukwaa ambapo hapakuwa na mtu, “Mama tumekoroga mambo chakula ulichokula wewe kina sumu ambayo inaua taratibu kwa kuozesha viungo vya ndani moyo utaanza kufeli hatimaye figo yani ndani ya masaa 24 unakufa. Nimempa maelekezo Doris kuwa sahani nyeupe ampe Linda nashangaa kakupa wewe” Alisema Norah huku akihema sana. Mama Belinda alitokwa na macho ya mshangao huku kijasho cha woga kikiacha kumchemka akajikuta akitetemeka mno kwa woga.

“Kwahiyo sasa?” Aliuliza mama Linda huku machozi yakimlengalenga.

JE NINI KILIENDELEA SASA?

IPI HATIMA YA MAMA LINDA? Y

AJAYO YANAFURAHISHA🤣🤣

EPISODE 16 & 17

“Kwahiyo sasa?” Mama Belinda aliuliza huku akiweweseka kwa wasiwasi sana. “Mama hapa hakuna cha Kwahiyo, twende hospitalini vinginevyo nitakupoteza mama yangu. Walianza kuondoka kuelekea hospitali bila mtu mwingine kujua walipoenda.

🍎🍎🍎

Bado Harusi ilikuwa inaendelea lakini mama wa bibi harusi na dada kipenzi wa bibi harusi walikuwa hawaonekani, walipoitwa madada wa bibi harusi watoe zawadi, Norah hakuonekana ile hali ndiye dada pekee wa Linda, hali hiyo ilimfanya bibi harusi atokwe na machozi na kuona kama dada yake amemsusia kwenye harusi yake. Hatimaye ikawa sasa ni zamu ya mama mzazi wa bibi harusi, ajabu naye hakuwepo hali hiyo ilimfanya Mc atoe tangazo kuwa kama kuna mtu mwenye namba zao awapigie simu.

😭😭😭

Haraka dada yake mama Belinda alizunguka nyuma ya jukwaa na kumpigia simu Norah, simu ya Norah iliita kisha ikapokelewa. “We Norah mpo wapi na mama yako yani mnahitajika harusini mtoe zawadi lakini hampo?” Aliuliza dada yake mama Linda. “Tupo hospitalini mama yupo hoi sana hajiwezi” Alisema Norah kwa sauti ya kilio na kukata simu yake. Dada yake mama Linda akabaki kinywa wazi bila kujua afanyeje, alienda moja kwa moja kwa Mc  na kumnongoneza taarifa hizo mbaya alizozipata.

😳😳😳

MC, akaona atumie busara kidogo ili asije akamvuruga bi, harusi. “Jamani mama wa bibi harusi pamoja na dada wa bibi harusi wameenda kuandaa ukumbi ambapo usiku maharusi na ndugu zao watafanya party 🎉 Kwahiyo hata huko wataweza kutoa zawadi.” Alisema Mc kidogo moyo wa Linda ukatulia lakini Prosper akawa anajiuliza tu mwenyewe Party gani tena hiyo ya usiku ile hali haikuwepo kwenye ratiba. Anyway au labda mama kaamua kutufanyia Suprise” alisema Prosper, wakati huo yeye waliitwa wazazi wake wakatoka watu aliowaweka kwani yeye hana wazazi.

😋😋😋😋😋

Hatimaye harusi ilimalizika salama. “Jamani kinachofuata sasa ni nini tunaelekea kwenye hiyo party au maana usiku umeshaingia” Aliuliza Prosper. Ndipo Mc akaona atumie muda huo kueleza ukweli. “Jamani mimi nilidanganya tu kusudi nisilete mvurugiko kwenye harusi ila ukweli ni kwamba mama Belinda yupo hoi hospitalini hajiwezi” Mc alipotamka tu maneno hayo Belinda akaanguka chini na kupoteza fahamu. Alikuwa anampenda sana mama yake, laiti angejua sio mama yake, na angejua kinachoendelea kwa kweli asingemhurumia hata kidogo.

Basi watu walimchukua Linda na kumpakiza kwenye gari huku Prosper naye akipanda kwenye gari hiyo na watu wengine wakaelekea hospitalini, kabla hawajafika Linda akazinduka na kuanza kulia sana, mshenga wake alimtuliza mpaka wakafika hospitalini.

Walipofika hospitalini waliingia ofisini kwa doctor na kuulizia hali ya mama Linda. Doctor aliongea maneno ambayo yaliwafanya wote waliokuwepo pale waduwae, yalikuwa ni maneno ya husuni sana na kuhofisha nafsi ya Prosper na Linda.

JE DOCTOR ALISEMAJE?

IPI HATIMA YA MAMA LINDA?

EPISODE 18

“Doctor mama anaendelea na kipi kimemsibu?” Prosper aliuliza. “Mmmh vipimo vinaonyesha kwamba mama amepewa chakula chenye sumu” Alisema Doctor watu wote wakashtuka ila Doris akashtuka kwa sauti “Haaaaaa” Norah alimtizama na kumkonyeza. “Mh kumbe kile chakula nilichopewa nikampe Belinda kilikuwa na sumu, sasa mbona anataka kumuua mdogo wake, Dah kweli Mungu acheni aitwe Mungu yani hata sijui nilichanganyikiwaje nikajikuta nampa mama yake hiki kile chakula, Mungu hakupanga Linda afe kifo chake kilikuwa hakijafika” Alijisemea Dorah Mwenyewe kimoyomoyo wakati huo Doctor alikuwa anaendelea kuongea.

“Sumu aliyowekewa kwenye chakula inaua taratibu kwa kuozesha viungo vya ndani, kumtibu inawezekana lakini tayari sumu hiyo ishakimbilia kwenye figo na kuharibu figo zote jambo ambalo linaweza kusababisha kifo endapo mgonjwa hatapata figo nyingine aidha kutoka kwa mwanandugu.”Alisema Doctor Edward Wiliam na kuwafanya Prosper na Belinda washangae sana.

“Mh sasa itakuwaje? Kwani doctor kuna uwezekano wa mwanandugu kuchangia figo”aliuliza Prosper. “Ndio iwapo figo zako mbili zipo sawia basi utachangia kwasababu yeye zake zote zimefeli Kwahiyo utamchangia moja” Doctor Edward Wiliam alijibu.

“Basi Doctor mimi nipo tayari kumchangia mama  mkwe wangu figo hata ikibidi sasa hivi” Alijibu Prosper huku machozi yakimbubujika. Alifanya hivyo kusudi kipenzi chake asikose raha. Hakutaka Belinda akose raha.

“Jamani sasa nani mbaya huyo aliyeweka sumu kwenye chakula?” aliuliza Belinda. “Jamani hayo tutajadiliana badae tuokoeni kwanza maisha ya mama” Alisema Norah kisha wakatoka nje wakamuacha Doctor na Prosper. Ebwanaee kuchangia figo sio jambo la kitoto arifu, mtu akikuchangia figo mshukuru mpaka kifo chako.

Zoezi lilifanyika nchini kenya ambapo doctor alimwandikia Rufaa mama Belinda, wakaondoka na Prosper kuelekea Kenya kwa ndege ili wawahi.  Belinda Norah na watu wengine walirudi nyumbani.

Linda alikuwa na mawazo sana alikuwa akifikiria ni nani huyo aliyekosa aibu akampa sumu mama yake. “Dada Linda mbona una mawazo sana” Doris alimuuliza Linda. “Yani sijui ni jini gani huyo aliyetaka kumtanguliza mama yangu mbele za haki ila ningemjua walahi ni bora nisifike mbinguni” Alisema Linda huku akilia. “Dada mimi namjua” Doris alisema, Linda akashtuka. “Acha nikuambie” Kabla Doris hajaongea kitu Norah akatokea..

JE NINI KILIENDELEA SIRI INAELEKEA KUBAINIKA JE ITABAINIKA?

Mambo ni 🔥🔥🔥 MoTo nichekishie mziki huo weweeee

EPISODE 19

“Dada mimi namjua aliyeweka sumu kwenye chakula cha mama!” Doris alimwambia Belinda. “Unamjua!?” Linda aliuliza kwa mshangao mkubwa. “Ndio namjua”Alijibu Doris “Ni nani huyo?!” Aliuliza Linda. ” Acha nikuambie….”Alisema Doris, mara ghafla Norah akatokea.

“Norah Doris anasema anamjua aliyemuwekea mama sumu kwenye chakula” Belinda alimwambia Norah. “Achana na huyu mtoto ni Muongo kama mama yake, yani karithi tabia za mama yake, Tabia za Kizaramo, yani hapa Baba mdogo ana hasara kwa kweli” Alisema Norah.

“Acha tu aongee unajua saa nyingine umbea nao dili huoni kina Soudy Brown wanavyotumbua maisha mjini na Ushilawadu wao, acha aseme” Belinda alimwambia Norah. Hapo Norah akamkazia Doris macho makali, lakini Doris akajikaza kwa ujasiri na kusema. “Dada Norah ndiye aliyenipa kile chakula nichompa mama akinielekeza kuwa nikupe wewe lakini sijui nikajihau vipi nikajikuta nampatia mama kile chakula nilichoambiwa nikupe wewe, dada Norah alinigombeza sana baada ya kugundua kile chakula nimempa mama na sio wewe!” Alisema Dorah wakati Norah alikuwa akimtizama tu kwa macho mabaya.

“Heee Norah ina maana ulitaka kuniua kwa sumu, kipi nimekukosea dada yangu?” Belinda aliuliza huku machozi yakimchuruzika. “Koma usiniite dada na nilitaka ufe baada ya kujua kuwa wewe sio ndugu yangu wa damu, kingine ulinipora mpenzi wangu Prosper na kama hujui sasa kwa taarifa yako mimi ndiye niliyekupiga risasi siku ile ukiwa na Prosper pale UTULIVU HOTEL VIEW PACK”Aliongea Norah kwa ujasiri sana huku Belinda akiwa ameduwaa tu.

“Eti mimi sio…sio…Ndugu yako wa damu” Belinda aliuliza kwa kigugumizi. “Ndio hivyo siri yote anayo mama na sasa subiri” Alisema Norah huku akichati na Simu bila Belinda kujua kuwa Norah anachati na majangili waje wamteke yeye na Dorah kusudi siri isisambae.

“Mimi hata siamini unayoongea nachojua wewe ni dada yangu tangu utotoni, pia kama ni Prosper wewe Mwenyewe ulimkataa kwa kusema huwezi kuwa na mwanaume ambaye hana pesa, huwezi kuwa na mlinzi, pesa zake mpaka ang’atwe na mbu mwezi mzima ukasahau kuwa maisha ni kama gwaride la jeshi nyuma geuka. Wa mwisho anakuwa wa kwanza na wakwanza anakuwa wa mwisho” Aliongea Belinda kwa uchungu huku Norah akisoma SMS zake na kucheka sana, mara Belinda akashangaa mlango umefunguliwa na watu waliofunika nyuso zao, wakamteka kisha wakamteka na Dorah. Watu hao wakaondoka na Belinda pamoja na Dorah.

Nchini Kenya matibabu ya Mama Linda yalienda Sawa bin sawia, Prosper alijitolea figo yake moja Kuokoa maisha ya mama  Linda hatimaye siku tatu baadaye waliruhusiwa kurudi nchini waendelee na matibabu wakiwa nyumbani.

JE ITAKUWAJE PROSPER NA MAMA LINDA WAKIRUDI NCHINI NA KUMKOSA BELINDA?

PROSPER ATAFANYAJE BAADA YA KUMKOSA KIPENZI CHAKE AMBAYE HATA HAWAKUSHEREKEA HONEYMOON YAO MATATIZO YAKATOKEA?

JE KIPI KILIENDELEA KWA BELINDA NA DORIS BAADA YA KUTEKWA MAANA SIKU TATU ZILIKUWA ZIMESHAPITA TATU WATEKWE?

EPISODE 20 & 21

Majangili waliomteka Linda na Doris waliwapeleka mpaka msituni kwenye kambi yao. Linda na Doris waliogopa sana ndani ya msitu huo mnene na wa kutisha. “Yani nyie wala hatuwaui mlivyo warembo hivi nyie mtakuwa wake zetu wa kutupooza miili yetu tukiwa tumetoka kwenye kazi zetu na kuhusu kula msijali huku Mtakula kila mpendacho isipokuwa tu tutawawekea mlinzi wa kuwalinda msitoroke” Alisema jangili mmoja mwenye kovu kubwa usoni lililoshonwa na nyuzi zisizopungua tisini. Akatoa uume wake na kuwakojolea Belinda na Doris waliokuwa wameketishwa mbele Yake. Belinda na Doris walijifuta kwa kutumia khanga zao huku wakilia sana.

“Jamani mi naomba mniue, kwanini mnatufanyia hivi lakini. Kumbukeni sisi wote ni binadamu yani wewe kaka unamdhalilisha mwanamke kiasi hiki, hujui sisi wanawake ndio tumewabeba nyie kwenye matumbo yetu, mfano dada yako ndio anafanyiwa hivi utajisikiaje”Aliongea Belinda huku akibubujikwa na machozi, yule gaidi alimpiga ngumi nzito ya mdomo iliyopelekea lipsi laini za Belinda kupasuka, palepale alitema jino chini pamoja na damu nyingi huku akilia sana katikati ya msitu huo.

Ilikuwa yapata majira ya kumi na mbili jioni, Prosper na mama Linda tayari ndege iliyowabeba ikitokea Kenya ilishatua uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere. Prosper akakodi Taxi iliyowapeleka moja kwa moja mpaka nyumbani.

Alipofika tu mlangoni cha kwanza aliita “Lindaaaaa! Honeeeeeey” Lakini hakuitikwa na mtu, akafungua mlango wakaingia ndani, wakaketi Sebuleni ndipo Norah naye akatoka chumbani kwake.

“Where is my wife” Prosper alimuuliza Norah. “Mh Shem mbali na kufanya harusi kubwa iliyokugarimu pesa nyingi lakini ukweli ni kwamba Linda alikuwa anakusaliti, alikuwa na mtu wake ambaye wewe ukimpa Linda pesa, Linda anaenda kumpa huyo mtu wake, na Linda alipoona unaenda nchini Kenya kumchangia mama Figo akatumia njia hiyo kwenda kwa mpenzi wake, waliondoka toka Juzi ajabu Linda hapatikani hata kwenye simu, Doris naye alisindikizana nao lakini hawapatikani wote kwenye simu!” Alisema Norah.

“Ah hata siamini kama Linda anaweza kufanya hapana Linda wangu ninayemjua hawezi kufanya hiviiiiiii” Alisema Prosper na kutoa kilio kikali kama mtu aliyeng’atwa na ng’e.

“Mh jamani acheni mimi nikapumzike maana hali yangu bado haijatengama. Prosper baba we pumzika kwanza hayo mambo tutayaongea” Alisema mama Linda huku akielekea chumbani kwake. Norah naye alimfuata nyuma, aliona aibu kukaa na Prosper pale sebuleni kwani Prosper alikuwa analia tu kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.

Prosper akiwa peke yake pale sebuleni mara sumu ya Norah ikaingiza meseji nyingi kwa mfululizo. “Usikute mke wangu kasharejea hewani amenitafuta kanikosa maana simu imezima chaji kaamua kumtafuta dada yake hebu niangalie” Alijisemea kimoyomoyo Prosper huku akinyoosha mkono na kuitoa simu ya Norah kwenye chaji. Kwa bahati nzuri alizijua paswedi za Norah kuwa ukiandika tu jina lake simu inafunguka.

Akafanya hivyo na kwenda sehemu ya meseji, hapo akajikuta akifungua meseji moja ya namba ngeni. Akaanza kusoma meseji ile huku akizidi kukunja sura yake kwa mshangao, akabaki ameduwaa mithili ya mtu ambaye haamini anachokisoma. “Oky leo nimeamini dunia sio mbaya lakini binadamu ndio wabaya!” Alisema Prosper na kunyanyuka kwenye kochi akielekea chumbani walipo Norah na mama yake!

JE UNADHANI PROSPER ALIPATA JUMBE GANI?

OHOOOOO 🔥🔥🔥🔥 MOTO UMEWAKA SASA

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!