NILIDHANI MGENI, KUMBE MKE MWENZA
(PIGO LA MKE MWENZA)
PART: 07
ILIPOISHIA
Ndani ya mda mfupi, walianza kunipapasa kila sehemuwa wakitafuta pesa mpaka wakanivua kaptula langu huku wakinong’onezana na kutabasamu.
SONGA NAYO….
Waliendelea kunisachi lakini wapi hawakuweza kuona chochote.
Kwa mbali nilipumua japo nilikuwa nimezibwa mdomo.
Baada ya kuzikosa, nilishutuka kumuna mmoja wao akianza kunivua blauzi yangu kisha nikabaki na blauzia tu.
Japo kulikuwa na kiza kinene lakini nilijiona kama nipo mtupu mbele ya umati wa watu.
Nilitupatupa miguu lakini haikuzaa matunda yoyote.
” Tumekwambia kuwa mpole laasivyo utaumia”
Nilianza kutetemeka kweli huku nikiww sijui kosa langu ni lipi.
Wakati sielewi hiki wala kile, nilijikuta maembe yangu yako nje huku brauzia ikiwa imetolewa.
Huko chini, nilibaki na nguo yagu yenye umbo la V huku ikiwa na zeep kwa juu na ndani kuna pesa.
Kijana mmoja alinikalia kifuani mwangu kisha bila aibu akaanza kutumia chakula cha mwanangu Furaha.
Wakati anakitumia, mmoja alinishika miguu na mwingine ameniziba mdomo.
” Fanya haraka bwana kila mtu anataka chakula..” walimwambia .
Moja kwa moja bila kupepesa macho, nilijua tayari nini kinachofuata ndipo nilipoomba miujiza itokee lakini wapi haikuweza kutokea.
Nguo pekee iliyokuwa imesalia mwilini mwangu, ilianza kutolewa ndipo niliporusharusha miguu mpaka akashindwa.
” Unanichezea eeh!” Aliongea kwa ukali kisha akachomoa kisu.
Kuona hivo, moyo wangu ulishutuka kweli mpaka nikawa mtulivu.
Bila huruma kabisa, aliivuta nguo hiyo kwa nguvu mpaka akachanika .
Sasa nilibaki mtupu kabisa kama nilivyoolewa.
Sura zao zilikuwa zinatisha kweli ndipo kwa aibu kali niliposhindwa kuwatizama.
Ama kweli macho hayana pazia, uvumilivu ulinishinda kisha nikachungulia nini kinafuata.
Nilichokiona, bora hata punda na sikuwahi kudhani kama mwanadamu anaweza kuwa hivyo
Kwa mara ya mwisho niliwahi kusimuliwa kuwa wamasai baadhi ndo wako hivyo.
Bila hata kuchomwa sindano, nilianza kuhisi maumivu yake.
Aliinama kisha akanisogelea huku akikaa mkao wa kula wa kukologa mboga kwa mwiko uliokuwa kama kipawa hivi.
Ni wakati mgumu sana ambao sikuwahi kuupitia huku nikiapa kujitoa uhai kabisa kwa fedheha na hatari ya kujikuta (positive).
Nikiwa nimeshikwa, gafla sauti za mikwaruzo na sauti za mbwa zilisikika kwa karibu sana huku wakiwa wanafukuzana.
Ndani ya sekunde kadhaa, kwa macho yangu niliwashuhudia mbwa wengi wakiume wakiwa wamemzunguka mmoja na wengine wakigombana.
( Bwei..bwei…guuh…!..buuu!..) milio ilitawala.
Asee walisogea mpaka tulipokuwa huku mmoja akionekana kuwa mkali sana.
Kama maajabu hivi, alikuja moja kwa moja mpaka akataka kutung’ata mara baada ya kutishiwa na watesi wangu.
Asee kumbe hata wao walikuwa waoga. Waliniacha chini kisha wakakimbia ndipo nilipojiona kung’atwa hadharani.
Wakati wanakimbia, mbwa walionekana kuwafuata hasa mmoja aliyekuwa na madoadoa meupe.
Katika vitu niliviogopa na nitaendelea kuviogopa ni mbwa.
Nikiwa sijielewi kabisa huku nikiwa mtupu, kumbe mbwa wengine walikuwa pembeni wakifukuzana.
“Mama…!.mama!..” nilipiga kelele huku nikitapatapa kukimbia.
Kama bahati hivi, mbwa waliendelea kugombana wenyewe ndipo nilipotembea kwa kunyata ili kujiokoa.
Nyumba za majirani zilikuwa mbali kidogo kutokana na miundombinu ya kijijini.
Nilipofika nyumbani kwa jirani yangu aitwaye kapipa kutokana na umbo lake la ufupi huku akiwa amenenepa mithili ya pipa, nilibisha hodi kuomba msada huku nikiwa nahema kama temba aliyefanikiwa kukimbia na kumuacha jogoo.
Ndani ya mda mfupi, mme wa kapipa alifungua mlango kisha akatoa sauti ya mshangao.
“Eboo..!” Alishika kichwa.
Asee nilishangaa kujikuta mtupu bila nguo yoyote.
“Naomba msaada..!” Nilimwambia huku kiganja kimoja kikishikilia dhahabu na kingine almasi.
” Hee! Shoga nini kulikoni..” Kapipa akiwa amejifunga kanga, aliongea kwa mshangao kisha akamvuta mme wake.
Ndani ya dakika moja, alinipatia gauni pamoja na kanga ili nijistiri.
Nikiwa navaa, nilianza kutokwa na machozi kwa hasira kali sana juu ya aibu na kile kilichotaka kunitokea.
“Shoga umekuwaje?!, maana sielewi ebu niambie” Kapipa aliniambia.
“Nashindwa nikwambieje lakini itoshe kusema dunia haina huruma..”
Niliongea huku nikiwa nalia.
” Ongea sasa tukusaidie. Kwanini uko hivo?” Aliniuliza kwa sauti ya ukali kidogo.
Baada ya mda kidogo, niliwasimulia kisa kizima mwanzo mpaka mwisho.
Mme wa kapipa alionekana kusikitika sana kisha akasema kuna kikundi cha vijana wanabaka na kuwanyang’anya hasa akina mama ambao wanaonekana hasa mida ya usiku wakiwa peke yao.
” Sasa hilo tuliache ila hili la mme wako kukufukuza nyumbani na kutaka kukua , lipo kwenye uwezo wetu. Mda huu tuongozane twende kwa mwenyekiti maana hatuwezi jua usalama wa mtoto huko ndani” Mme wa kapipa aliongea huku akiwa anamalizia kuvaa shati lake.
” Mhh..mme wangu lakini haya mambo yaache kama yalivyo maana niyawanandoa” Kapipa alimwambia mme wake.
” Unafurahia kitendo hiki!, jaribu kuvaa viatu vyake uone kama unaweza kutembea. Uhai wa mwanadamu ukishatolewa huwa haurudi hivo lazima tuoshe ubinadamu” mme wa Kapipa aliongea.
Baada ya kuongea hivo, alimwambia mke wake ampatie rungu lake kisha akamulekeza kubaki nyumbani na watoto maana walikuwemo wawili wenye umri mdogo.
” Mme wangu kwani shida iko wapi tukienda wote?”
” Hakuna shida lakini sio busara kuondoka wote na kuwaacha watoto peke yao. Nakuomba ubaki”
” Sawa ila mhh..”
Kapipa alikubali kishingo upande.
Baada ya mazungumzo hayo, tulianza safari ya mwendo kama wa kilomita moja na nusu hivi kuelekea kwa maenyekiti wa kijiji…
PART: 08
ILIPOISHIA,
Niliongozana na mme wa kapipa kuelekea kwa mwenyekiti wa kijiji huku kukiwa na kiza kinene..
SONGA NAYO..
Safari ilianza huku nikiwa na hasira kwelikweli lakini kwa upande mwingine nikawa namuonea wivu shoga angu Kapipa kuwa na mwanaume anayejiheshimu na kujali utu.
Nilitamani kumwambia kuwa ni mtu mwema lakini kabla sijamwambia, alinishika mkono wangu wa kushoto kisha akaniambia,
” Usiumie sana maana hizi ni changamoto tunazopitia wanandoa lakini naona mme wako ameanza kuzidi kipimo”
“Ni kweli lakini kinachoniumiza yaani nyumba nimejenga kwa nguvu zangu mwenyewe afu leo hii analeta malaya wake wanalala ndani nami nateseka hivi!, . Ningekuwa na uwezo…” nilishindwa kumalizia kile nilichotaka kusema mara baada ya kuhisi kitu kimenikaba kooni kwa sababu ya hasira.
“‘Tulia najua inakuuma sana lakini ninaweza kukupa faraja yako ambayo imepotea kwa mda ila unatakiwa kutunza siri “
Baada ya kusikia kauli hiyo, nilipunguza mwendo kisha nikamuuliza,
“‘Unamaanisha nini?”
“‘Kwani hujanisikia nirudie?”
“‘Kukusikia nimekusikia labda niseme sijaelewa”
” Ohh kumbe hujaelewa, kidogokidogo utanielewa”
“‘Hahaha una mambo wewe” kwa mara ya kwanza nilicheka.
“‘Umeona sass mpaka umefurahi..”
“‘Nimecheka lakini moyo wangu unamakovu makubwa sana ambayo hayawezi kuisha”
“‘Hicho tu!, mbona tunayamaliza hata kwa stealwaya! Hahaha”
“‘Aya bwana..”
“‘Vipi lakini” aliniambia huku tukiwa tunatembea kwa mwendo taratibu.
“Nipo kama unavyoniona sina hili wala lile” nilimwambia .
“Huna hili wala lile?, mbona naliona?”
“‘Unaona nini sasa..”
“Hilo hapo…”
“‘Acha utani bwana..”
“Sasa utani upi wakati umesema huna?”
“Ebu tuongee mambo ya msingi tuone unanisadiaje”
“Kwani mambo ya msingi ni yapi na yasiyo ya msingi ni yapi?”
“‘Bwanaaa!..unapenda kunitania wakati unajua..”
“‘Mi sijui ndo maana nataka uniambie “
“Haya bwana umeshinda”
“Nimeshinda nini sasa..”alisema kisha akanishika kwenye mbavu zangu.
Nilshutuka na kuhisi kama amenitekenya ndipo nilipomshika mkono wake huo.
“Acha kunitekenya bwana mwenzio siko vizuri”
Baada ya kumwambia hivo, alisimama huku akiwa amenishika mkono kisha akanisogelea karibu sana.
“Nataka nikwabie neno tamu sana zaidi ya keki . Upo tayari kulipokea?”
“Mhh neno gani hilo…, ongea bwana.”
“‘Upo tayari kuliokea?”
” Sasa si useme ili nijue kama nitalipokea au la!.”
Nilimwambia kisha akaanza kukuna kichwa chake kwa sekunde kadhaa lakini badaye akasema,
“Neno moja tu ninalotaka kukwambia ni kukusuuza makovu yako uliyonayo moyoni mwako lakini siri kubwa inatakiwa ” aliongea.
“‘Hayo makovu utayatoaje kwa mfano…”
“‘Nisikuzungushe sana, nimekupenda sana na mda sasa lakini nilimuheshimu mme wako ila kwa sababu ameanza kukufanyia hivi, naomba unikabidhi moyo wako ndani ya mwezi mmoja atakusahau kabisa”
“‘Hapana sipo tayari maana mie ni mke tayari hata kama mme wangu ndo hivyo haeleweki lakini hilo si tatizo sana, tatizo ni mke wako ambaye uko naye afu ni rafiki yangu. Je akijua itakuwaje?. Kwa hilo hapana'” nilimjibu.
“Hawezi kujua afu hanaga shida huwa ni muelewa sana”
“‘Hapana kwa hilo hakuna mtu muelewa”
“Nakuomba sana unipatie moyo wako maana nahisi hata mda huu..”
“‘Kwani si unamke jamani, jitahidi kujizuia .”
“Siku zote mwiko unaokoroga mboga ileile kila siku, ladha yake hupotea”
“Mhhh.., ebu tuwahi kwa mwenyekiti maana mimi mwenyewe sijielewi na sijui mwanangu yu hali gani”
“Mtoto atakuwa salama wala usihofu kwa hilo.
Kama itakupendeza hata dakika 5, maana …”
“Mhh..mheshimu sana mke wako maana anakuheshimu sana”
“‘Hilo sikatai lakini jiulize utaweza kukaa peke yako kwa mda mrefu, maana kama ameoa mke mwingine basi hatakuwa na wewe.”
“‘Wee! Huyo Malaya wake hawezi kukaa kwangu labda amjengee na sidhani kama ana hata elfu 10. Kingine hawana chakula “
“‘Ebu tuyaache hayo, vipi sasa umekubali?” aliniambia kwa sauti ya upole sana huku akiniwekea mkono wake kwenye kifua changu.
Asee nilibaki kimya kwani alionekana kama hanielewi vile. Kukaa kwangu kimya, kulimfanya azidi kunisogelea mpaka zero distance.
Baada ya kuona hivo, nilimsukuma kwa ustarabu kisha nikamwambia,
“Basi ngoja tumalize jambo moja kwanza kwani mimi si nipo siku zote jamani?”
“‘Sawa kwahiyo umekubali au?”
“‘Niache nijifikirie kwaza afu nitakupa jibu…..” nilimjibu huku mapigo ya moyo wangu yakienda kwa kasi sana .
PART: 09
ILIPOISHIA,
Tukiwa njiani huku nikiwa nimeshikaa mkono, mme wa shoga yangu kapipa, aliniambia nimpe jibu nami nikamjibu asubiri nijifikirie..
SONGA NAYO …
Ama kweli moyo wangu ulibaki njia panda huku nikishindwa nini nimjibu kwa wakati huo.
Niliinamisha kichwa changu chini huku mapigo ya moyo wangu yakienda kasi kisha nikataka kutamka neno fulani lakini nikahisi aibu kali sana.
“‘Vipi bado unajifikiria tu..!:’mme wa Kapipa alinimbia huku akinishika kifuani nami nikasogea nyuma kidogo huku nikiwa nimeinama.
“‘Kwa sasa siwezi kukupa jibu sahihi ila jubu litakuwa zuri” nilimjibu huku nikihisi aibu.
” Kwani unaogopa nini?” Aliniuliza huku akiwa ananivuta taratibu.
“Siogopi chochote. Kuwa free mambo mazuri hayahitaji haraka. Naomba usiewe na wasiwasi” nilimjibu kwa sauti ya chini sana.
“‘Waoohh..!, asante sana” alisogeza mdomo wake karibu na wangu lakini niligeuza shingo pembeni kwa aibu kwani sikutaka mboni za macho yangu zigusane na yake.
Baada ya kufanya hivo, nilimvuta taratibu huku akiwa ananishikashika mpaka tulipofika nyumbani kwa mwenyekiti wa kijiji.
” Hodii..hodiii..” Nilibisha hodi .
( Hakuna aliyetikia)
“Ita huku ukigonga mlango” mme wa Kapipa aliniambia
Nami nilifanya hivo na bahati nzuri mlango ulifunguliwa kisha mwenyekiti akiwa amejifunga kitenge kama mwana mama huku mkononi akishikilia mkuki akasema,
“Nyie wakina nani usiku huu” aliongea huku akiwa amenyanyua mkuki juu.
“‘Mwenyekiti ni mimi hapa. Nimemleta mhanga huyu nadhani nisimuongelee atakwambia mwenyewe” mme wa Kapipa alimwambia.
Baada ya kuambiwa hivo, mwenyekiti alisogea karibu ndipo alipoweza kututambua vizuri kwa sura.
“‘Ohh kumbe ni nyie, karibu ndani”
Tuliingia ndani kisha nikaanza kumuelezea mwenyekiti mwanzo mpaka mwisho.
Wakati namuelezea, alikuwa ameshika kalamu na karatasi huku akiachukua notes.
“Umemaliza? ” aliniuliza.
“‘Ndiyo yangu ndo hayo..” nilimjibu.
Alikuna kichwa kwa dakika 1 kisha akaniuliza tena,
“Unaweza kulala hapa ili tulishughulikie kesho asubuhi au unaonaje?”
“‘Naomba kama inawezekana unisaidie kwa leo nilala kwangu maana nahofia sana mtoto wangu..”
“‘Sawa ngoja twende. Una elfu 6 hapo ya ofisi?”
Niliguna kimoyomoyo kisha nikataka kuhoji lakini niliamua kukaa kimya.
“Kwa sasa sina labda kesho maana hela zangu wamezichukua vijana waliodai ni sungusungu”
“‘Sasa itakuwaje!..hela ya ofisi ni muhimu”
“‘Ngoja nilipe ” mme wa Kapipa alinilipia.
Kitendo hicho kilinifurahisha sana mpaka nikajikuta natabasamu kwa kunijari huko.
Baada ya kupewa kiasi hicho, tuliongozana taratibu mpaka hapo tulipofika viunga vya nyumbani.
Tulinyamaza kisha tukaanza kusogea taratibu mpaka mlangoni ndipo sauti za kilio kutoka kwa mwanangu Furaha ziliposikika.
“Mama…oooo….uuuuu!…mamaaaaa!…mamaaa..”
Sauti hizo zilinitoa machozi hapohapo kwani sikujua yupo katika hali ipi.
“Tulia kwanza” mwenyekiti aliniambia .
Nilijifuta machozi kisha nikawaonesha ukuta aliobomoa na kuingia ndani.
Walishutuka sana kisha mwenyekiti akasema,
” Hii ni hatari sana!, kama amefanya hivi, basi angeweza kukuua.Sasa mda huu nataka tugonge mlango kisha tuone kama atafungua”
Mwenyekiti aligonga mlango kama mara 5 hivi ndipo mlango ulipofunguliwa,
Baada ya kutoa kichwa chake, alishangaa kumuona mwenyekiti ndipo alipokuwa mdogo kama piliton.
“‘Boss nina shida na wewe humo ndani sijui kama kuna usalama” mwenyekiti alimwambia baba Furaha huku nikiwa nimenyamaza kwa hasira.
“‘Haina shida mwenyekiti karibu..”
( Tuliingia ndani)
“Sasa nisipoteze mda twende moja kwa moja kwa kilichonileta hapa. Nadhani huyu ni mke wako wa ndoa na mnaishi wote siku zote. Kwa maelezo aliyonipa, umemtisha kumuua kiasi cha kufikia kutoboa ukuta kama kibaka. Mimi siyo hakimu lakini nataka nikwambie kuwa, kesi hii itakukamata na utazeekea jela. Sijui unasemaje..”
“Mwenyekiti aliyokwambia siyo kweli. Ni mke wangu na tunapendana sema nilipitisha pombe kidogo nikawa nimepoteza fahamu lakini sijamfukuza” alimjibu huku akiwa anatetemeka.
“‘Anadanganya!, si ulitaka kuniua wewe!” Nilidakia kwa hasira.
“Ebu twende taratibu, hivi ushawahi kufungwa au ulishasimuliwa kilichopo kule?” Alimuuliza.
“‘Mwenyekiti naomba samahani tuyamalize hapahapa maana …” akiwa anatetemeka alijibu.
“Hatuwezi kuyamaliza kama hauko tayari kuwa mkweli na kusema nini chanzo”
“‘Ngoja niseme ukweli, ni kwamba nimeoa mke wa pili hivo huyu anaonekana kumuonea wivu ndo chazo hicho”
” Wakati unamuoa ulimjulisha?”
“‘Hapana kwani ilitokea gafla”
“Sasa kabla ya mambo mengine kufuata, nataka usaini hapa kama ushahidi kuwa hutomfanyia kitu chochote cha kuhatarisha maisha yake. Na ikitokea, moja kwa moja sheria itafuata mkondo wake”
Kwa unyonge, baba Furaha alisaini kisha nami nikasaini pamoja na mme wa Kapipa ambaye alikuwa kama shahidi.
“Nakala hizi naenda kuzitunza. Kitu kingine, hakikisha usalama ndani ya nyumba niwakutosha na ikiwezekana mjengee nyumba yake huyo mke wako mdogo..Naondoka kuwa makini sana”
Mwenyekiti aliongea kisha akatoka nje huku akiambatana na mme wa shoga angu Kapipa.
Alinikonyeza kisha nikatabasamu huku nikiwapungia mkono wa kwaheri.
Nilifunga mlango kisha nikaenda moja kwa moja mpaka chumbani mara baada ya kilio cha Mtoto wangu Furaha kuongezeka.
Ile naongia chumbani, nilishangaa kuona mtu yu kitandani huku akiwa anakoroma.
“Hee!…” nilibaki nimeduwaa kwa mshangao na hasira kali sana huku nikiona kama gereza linanisubiria…
PART: 10
ILIPOISHIA
Niliingia chumbani ndipo niliposhutushwa na sauti za mtu aliyekuwa amelala pembeni mwa mtoto wangu Furaha…
SONGA NAYO..
Nilimsogelea karibu mtu huyo huku nikiwa nanyata kama panya anayetaka kuiba karanga wakati wenye nyumba wakiwa wameketi sebuleni.
Baada ya kumsogelea, nilimuangalia usoni kwa makini kabisa kabla sijafanya maamuzi magumu ndipo niliposhutushwa kuona sura kama ya Joy.
” Hee! Ina maana amefikia dharau za kulala mpaka chumbani mwangu!, hakika kama nikufungwa nifungwe ila simuachi” nikiwa nahema, nilijisemea moyoni kimyakimya kisha nikasogea kinyumenyume mpaka mlango wa chumba.
Niliangaza kila kona walau nipate hata kipande cha jiwe au tofali lakini sikuweza kufanikiwa ndipo nilipoamua kufungua mlango ili nifuate kisu kilichokuwa sebuleni.
Wakati natia mguu mmoja, nilikutana na baba Furaha akiwa amesimama karibu na mlango .
Nilishutuka lakini niliamua kuendelea na mambo yangu.
Bahati nzuri nilifanikiwa kupata kisu ndipo nilipokuja kwa hasira kali sana.
Ile nazama chumbani, nilimkuta Furaha tu huku sehemu alipokuwa ikiwa tupu kabisa.
Kwa hasira nilichomeka kisu moja kwa moja kwenye godoro huku chozi linikinitoka.
“Huyu alokuwemo ni jini au ?!, ngoja niliangalie vizuri” nilijisemea kisha nikaanza kuchungulia uvunguni lakini sikuweza kumuona mtu yeyote.
Nilichomoa kisu ili kisije mchoma mwanangu ambaye alikuwa amesinzia.
Nilijilaza lakini moyo wangu ulikataa katakata ndipo nilipotoka chumbani taratibu na kwenda kusikilizia chumba walichokuwemo mwanzo.
Nilibana karibu na mlango kisha nikanyanyua masikio yangu mithiri ya Sungura aliyehisi harufu ya mbwa.
Nikiwa nimetega masikio, niliwasikia wakiwa wanaongea kwa sauti ya chinichini ndipo nilipoishiwa nguvu kabisa.
“Niache nilala nimechoka mme wangu itakuwa hapo asubuhi” Joy alisikika akilalama.
“Dakika 4 tu zinatosha afu tulale” Baba Furaha alimjibu.
“Mhh hapana kwani haraka ya nini?, kuku ni wako na umemfuga mwenyewe sasa kwanini uteseke kumfukuza wakati usiku ataingia mwenyewe ndani?” Joy aliongea.
“Nakupenda sana na siwezi kulala bila ….”
“Mhh..baby, nielewe basi maana sasa hivi sijisikii. Mbona utanichoka tu..”
“Siwezi kukuchoka maana huyo ndo nimeachana naye tayari”
“Yaukweli hayo unayoongea mme wangu?”
“Hilo halina pingamizi..”
Baada ya mazungumzo hayo, ukimya ulitawala kidogo lakini baada ya mda kama dakika 5 hivi, sauti za kinanda zilianza kusikika huku zikiwa zinapanda na kushuka.
Kusema kweli nilijisikia vibaya sana mara baada ya mwili wangu kujikuta unapata kiu ya haraka sana isiyoweza kumalizika kwa maji ya mvua wala mtoni.
Kwa unyonge huku mapigo ya moyo wangu yakiende kwa kasi sana, nilirudi chumbani ili kujipumzisha.
Asee mwili ulijawa na upele wa gafla ambao haukuonekana kwa macho ya kawaida.
Nilianza kujikuna taratibu ili walau nipunguze makali lakini wapi.
Taratibu hali ile ilianza kupungua ndipo nilipoanza kuwaza hatima yangu ya ndoa.
Nilimuwaza sana mme wa Kapipa usiku ule kama kumkomoa baba Furaha lakini ukosefu wa simu ulikwamisha kila kitu.
********
Kesho yake asubuhi na mapema, niliamka kisha nikahamisha mazao yangu yote kwenye chumba changu ili nione nini watakula.
Niliandaa uji wa mtoto wangu na baada ya kumaliza, nilimtengea. Wakati namtengea, baba Furaha alitoka chumbani akiwa amejifunga kanga ya Malaya wake ndipo nilipotema mate chini kwa kuhisi kichefuchefu .
Sikumuongelesha wala hakuniongelesha. Tukiwa tunapata uji, nilimuona kama anashangaa kuona hakuna hata punje ya chakula sebuleni hapo.
“‘Mtakufa na njaa zenu. Si mmejifanya wajanja” nilijisemea moyoni mwangu huku nikiwa natabasamu.
Baada ya kuona hivo aliamua kuongea,
“‘Wewe ndo umehamisha chakula hapa sebuleni!” Alilngea kwa sauti.
“‘Chakula kipi!, kuna nguvu yako umrweka hapa!, “
“‘Unasema?!”
“‘Nasema nini hunielewi au?. Naomba umwambie mbwa wako huyo aishi atakavyo ila asiguse vyombo vyangu nilivyonunua mimi au chakula changu”
“Wivu tu unakusumbua” alinijibu huku akitoa cheko la kejeli.
“Wivu gani lione, kwanza niwe na wivu na wewe! Una nini labda umaskini tu” nilimjibu
“Sasa naomba tuelewane, ulikuja hapa mikono mitupu , vitu vyote umevipata kupitia ardhi yangu hivyo basi huna chako hapa.”
Alitamka kwa sauti.
“Thubutu!, kama ni vyako thubutu uone kama hutoishia gerezani”
“Unajisumbua ila utarudi nyumbani kwenu”
“‘Siendi , nasema siendi hapa ni kwangu na mali ninazotumia ikiwemo ardhi nisimkute ameweka miguu yake”
“Tutaona kama ulitoka nyumbani na mali au mikono mitupu” alinijibu huku akichekacheka.
“‘Sasa unajichekesha nini, sitoki hapa !, nitaishi hapa na nitazikwa hapa labda uhame wewe na utahama mda si mrefu”
Baada ya kumwambia hivo, alielekea chumbani kisha wakaanza kuongea.
Kwa hasira kali nilizokuwa nazo, niliamua kutangaza vita vikali sana juu yake ambayo itamuumiza sana.
Mda huohuo, nilimkabidhi mme wa Kapipa moyo wangu wote bila kubakiza hata chembe.
Nilichoogopa ni juu ya Shoga wangu Kapipa kujua uhusiano wetu na mme wake lakini siyo baba Furaha.
Mnamo mida ya saa nne hivi za asubuhi, nilitamani kumuona mme wa Kapipa ambaye kwa jina lake anajulikana kama Majura.
Kwa kuwa sikuwa na simu, nilimbemba mtoto wangu mgongoni kisha nikaelekea kwa shoga yangu ili nimuone Majura.
Bahati nzuri nilifanikiwa kuwakuta wote wakiwa sebuleni huku wakipekechua karanga ambazo hazikuwa nyingi kivile.
Nilikaribishwa kwa furaha zote nami nikatoa tofauti shukrani zangu kwa msaada walionipatia.
Tulipiga story mpaka chakula cha mchana nilikipata hapohapo.
Wakati Kapipa anaanda chakula nilipata wasaa mdogo wakuongea na Majura ( mme wa Kapipa) japo kwa tahadhari kubwa sana.
Ili kumkomesha baba Furaha, nilimwambia Majura aje nyumbani mida ya jioni ili nimwambie kitu.
Mwanzoni alionekana kusita na kukataa lakini nilimuangalia kwa jicho la mwisho wa mwezi mpaka akakubali.
Moyo wangu ulisuuzika kabisa kwa kujaa furaha isiyo na kifani.
Mnamo mida ya saa 12 jioni, Kapipa alinisindikiza kuelekea nyumbani huku tukiwa tunaronga mawili matatu.
Baada ya hatua chache, aliniaga nami nikamuaga.
Nilifika nyumbani bahati nzuri nyumba ilikuwa imefungwa kuashiria hamna mtu.
Nilichukua funguo kisha nikafungua. Harakaharaka, nilijimwagia maji kisha nikavaa nguo laini sana huku nikimsubiria Majura .
Nikiwa nimeegeshea mlango huku kwa mbali kiza kikiwa kinaanza kutanda, mlango ulisikika ukigongwa .
” Ng’ong’oo…”
” Karibu..” niliitikia.
” Njoo kwa nje…” bila kupepesa macho nilijua ni sauti ya Majura moja kwa moja.
“Ingia ndani nipo peke yangu” nilimjibu huku nikimalizia kujipakaa mafuta.
PART: 11
ILIPOISHIA..
Nikiwa namalizia kujipakaa mafuta, gafla nilisikia mlango ukigongwa na huku sauti kama ya Majura ikisikika ndipo nilipomwambia aingie ndani..
SONGA NAYO…
Baada ya kumwabia aingie kwa ndani, alionesha kutaa kabisa ndipo nilipomfuata kwa nje kisha nikamwambia,
“Karibu ndani” kwa sauti laini huku nikitabasamu, nilimwambia.
“‘Asante lakini nakuomba tusogee kwa mbele nikwambie jambo fulani” Majura alinijibu huku akikwaruza miguu yake chini.
“Mhh..tuingie ndani maana giza limeanza kuingia afu mbu ni wengi kweli.” Nilimjibu.
“‘Hapana. Ni hatari sana kuingia ndani” kwa sauti ya chini aliniambia.
“Kwani unaogopa nini?” Nilimuuliza
“Mme wako .” Alinijibu kwa sauti ya chini.
“Makubwa!, mme yupi sasa. Amenishanikataa hivo kuwa huru hii ni nyumba yangu afu kitu kingine, hayupo..” nilimjibu.
“Mhh..najua hata kama mmegomba lakini atakuwa na wivu kwako..”
“‘Hee! Sasa wivu unanihusu nini!, we usiogope chochote kwanza hatakuona”
“Sawa ila…” alinijibu kisha tukaingia ndani.
Siku hiyo jua halikuwaka vizuri kiasi cha kuzifanya taa kuwaka mwanga hafifu .
Bila kuchelewa, niliingia moja kwa moja mpaka chumbani kisha nikatandika mashuka mazuri.
Nilipomaliza, nilitoka chumbani kisha nikamfata Majura sebuleni .
“‘Njoo chumbani nikwambie ” nilimwambia.
“‘Hapana ebu niambie hapa ” Majura alikataa.
“‘Kwanini unakataa?, siwezi kukwambia ukiwa sebuleni hapa” nilimjibu.
“‘Hapana ..”
Baada ya kunijibu hivo, moyo wangu ulisikitika sana ndipo nilipomsogelea kisha nikashika mkono na kumnyanyua.
Licha ya kuonekana mwenye nguvu na mwili wa miraba 7, nilimvuta naye akavutika mithili ya boya kwenye bahari.
Baada ya kuingia chumbani, nilifunga mlango vizuri kisha nikamlaza Furaha kwa pembeni.
“Niambie” nilimwambia Majura ambaye alionekana kutetemeka.
“Safii , nakusikiliza wewe” alinijibu huku akiambatanisha kicheko.
“‘Mhh..hivi nikuulize kitu?” Nilimwambia
“Ndiyo uliza..”
“‘Hivi unanipenda kweli au unataka kunichezea?” Nilimuuliza.
“Nakupeda sana . Penzi letu lidumu mpaka ziwa victoria litakapokauka”
“Hahaha..ayaa bwana. Sasa vipi kuhusu mke wako.Kapipa?”
“Wote nitakuwa nao maana nimetoka naye mbali sema inatakiwa siri kubwa ili asijue”
“‘Sawa. Upo tayari kulininda kwa lolote?” Nilimuuliza.
“Usijali nitakulinda na ikiwezekana nitakupangishia nyumba nyingine ili tuwe huru”
“Itakuwa vizuri lakini roho inaniuma kuacha nyumba yangu ambayo nimeijenga kwa jasho langu mwenyewe”
“Basi tutaona nini chakufanya. Kwa leo naomba uniache niondoke maana sijisikii amani kuwa chumbani humu”
“Jamani baby, unaondoka unaniacha na nani! , mi sitaki bwana…” nilimbembeleza huku nikimshika kifuani mwake.
Nikiwa nimenshika kifuani, alijikuta anakosa nguvu ndipo aliponisogelea kisha naye akaanza kupitisha mkono wake kwenye nyonga zangu.
Nilijihisi kucheka kwani alikuwa ananitekenya lakini nilijitahidi. Lengo langu kubwa lilikuwa kumkomoa baba Furaha ili asiendelee kunidharau.
Ndani ya dakika 5, kidari cha Majura ambacho kilikuwa kimezungukwa n love garden, nilikishuhudia kwa macho yangu .
Baada ya macho kuona, moyo ulianza kazi ya kusukuma damu kwenye mishipa yangu huku upele wa gafla ukianza kuniwasha.
“Mhh..baba..baby…, love you” nilimwambia huku mkono wangu ukizama kwenye love garden na kuanza kuitafuta sindano.
Majura ndani ya mda mfupi, alianza kuunguruma kama redio iliyoishiwa betri ndipo nilipobanwa na kicheko kilichoambatana na kikohozi.
“‘Khoo..koo..khoo..khooo…”
“Umekuwaje” aliniuliza
“‘Kikohozi tu ila sasa nipo sawa…”
“‘Ok …”
Baada ya mazungumzo mafupi, ukimya ulitawala huku mikono ikiwa anafanya kazi.
Tulijikuta kitandani huku tukiwa zero distance. Majura aliniangalia kwa jicho zimazima ndipo nilipogeuza mboni yangu kwa aibu.
“‘Baby naomba nizime taa” nilimwambia.
“Mhh..mbona mwanga ni hafifu?”
“‘Moto uliobaki ni mdogo sana utasababisha taa zizime usiku”
“‘Ohh basi fanya hivo”
Nilinyanyuka huku nikiwa nimejifunga kanga kisha nikazima taa.
Baada ya kuzima taa, aibu niliyokuwa nayo ilitoweka kwani nilikuwa nina siku kadhaa sijafyeka majani yaliyokuwa yamezunguka nyumba yangu.
Bila kuchelewa huku nikiwa natabasamu la moyo kama chura na maji, nilimsogelea kisha tukawa ndani ya shuka moja kwani kimvua kilikuwa kinanyesha taratibu huku kikiambatana na kijibaridi.
Kama naota hivi huku mwili wangu ukiwa ndo umeanza kulifukuza baridi, sauti ya baba Furaha ilisikika akisema,
“‘Hivi viatu ndani ni vyanani?”
“Mhh sasa unaniuliza situlikuwa wote jamani! Labda muulize mama Furaha” Joy alisikika akiongea.
” Afu vyakiume !!” Aliongea.
Kitendo cha kusikia hivo, nilishutuka kumuona Majura akiwa ameshajiingiza uvunguni huku akiwa anahema.
Sikutaka kumuongelesha ndipo nilipoamua kufungua mlango maana nilijua chumbani kwangu hawezi ingia ili nikapike chakula chausiku.
Ile natoa mguu mmoja nje, nilikutana na sura yake huku akiwa amebana kwenye ukuta…..
PART: 12
ILIPOISHIA,
Ile natoa mguu mmoja nje, nilikutana na sura yake huku akiwa amebana kwenye ukuta…
SONGA NAYO…
Baada ya kumuona, nilishutuka sana mpaka nikajikuta nataka kudondoka chini bila kusukumwa.
Nikiwa katika hali ya sintofahamu, nilifungua mlango wa chumba na kuwa wazi kabisa kiasi kwamba hata baadhi ya vitu vilikuwa vinaonekana.
Kufanya hivo ilikuwa kumuaminisha kuwa hali iko salama wala hakuna shida yoyote.
Sijui Majura alikuwa na hali gani lakini sikuwa na namna nyingine.
Niliacha mlango wazi kisha nikaanza kuwasha moto ili nipike chakula.
Ile namalizia kuwasha moto, moyo ulinidunda ” pwi..pwi..pwi” ndipo niliporejea chumbani kuona usalama wa Majura.
Ile naingia ndani, nilikuta baba Furaha akiwa na kibakuli pamoja na kimfuko akiwa anachota unga kwenye ndoo.
Aliponiona, alishutuka kisha akaweka mfuko wake kwa nyuma bila kujua kama nimeshamuona.
Kwakuwa chumbani humo alikuwemo Majura, sikutaka kumgombeza kwani huenda kikohozi kingeweza kumuumbua Majura aliyekuwa uvunguni.
Kwa aibu huku akiwa ameangalia pembeni, aliondoka chumbani humo huku tukiwa hatusemeshani.
Kwa bahati mbaya au uoga wake, alishindwa kuuchukua unga huo hali iliyonifanya nicheke mwenyewe kimoyomoyo.
Baada ya kuvuka mtihani huo, niliendelea na mapishi huku Baba Furaha akiwa chumbani mwake pamoja na Joy.
Chakula kilikuwa tayari mnamo mida ya saa 2 na robo za usiku ndipo nilipokipakua ili nimpelekee kipenzi changu Majura.
Taratibu niliingia chumbani kisha nikachungulia uvunguni ndipo nilipomkuta Majura amejikuta kama kambale aliyebanikwa.
Nilikikuta naandamwa na cheko hafifu mara baada ya kumuona akiwa hivyo.
Kichwa chake alikuwa amekibamiza ukutanani huku miguu akiwa ameukunja utadhani kata.
Kwa sauti ya chini sana nilimuita ndipo alipozinduka .
Licha ya taa kuwa na mwanga hafifu, niliweza kumuona akiwa anatweta kwelikweli.
“Karibu chakula kipenzi changu” nilimwambia kwa sauti laini.
“Ebu niache niondoke..niache! Unataka nifie ndani humu” aliongea kwa sauti ya chini huku akiwa anatetemeka.
“Usiogope hakuna shida yoyote. Chakula hiki kitamu nimekiandaa kwa ajili yako” nilimwambia.
Majura hakutaka kunielewa kabisa ndipo alipokaa mlangoni huku akichungulia kama kuna upenyo.
Kwakuwa lengo langu lilikuwa bado halijatekelezwa, nilimng’ang’ania mgongoni mwake kama nyani na mtoto wake.
“Usiondoke tafadhari..” nilimwambia
“‘Hapana nina familia bado inanitegemea hivo itakuwa siku nyingine” alinijibu.
“‘Sasa utapita wapi?, subiri mida ya saa 7 usiku akiwa amelala ndipo nikufungulie uondoke” nilimshauri.
“‘Saa saba ni parefu sana. Mke wangu ataniuliza wapi nilipokuwa afu huyu mme wako ameniona vile maana kachungulia uvunguni hivyo huenda anajiandaa kutafuta silaha ili animalize. Ni bora nife nakimbia kuliko kufia ndani ” aliongea
“Kula kwanza basi…” nilimbembeleza.
‘Baada ya kumwambia hivo, alifinyanga tonge moja la ugali kisha akalimeza na kudai kuwa ameshiba.
Ama kweli nilifadhahika sana kuona mme niliyemtegemea kuwa mlinzi wangu anakuwa muoga kiasi hicho.
Kwa mbali moyo wangu ulianza kusinyaa juu ya penzi langu na Majura huku likiwa na mda mfupi sana.
Kwa uchungu mkubwa huku upele ukiniwasha mara baada ya kujua sina kucha, nilijilaza kitandani ” puuuh!” Kisha nikaaza kumuangalia Majura ambaye alikuwa na uoga wa aina yake.
Licha ya kujigalagaza kwangu, Majura alionekana kuwa na roho ya pakan ndipo nilipoamua kufungua mlango wa chumbani huku nikimwambia,
“‘Kaa hapa kwanza ngoja niangalie usalama au nakwambia” nilimwambia.
Majura aliniangalia kisha akainua kichwa chake juu kama ishara ya kukubali.
Taratibu nilifungua mlango na baada ya kufika sebuleni sikuweza kumuona mtu yeyote .
Nilisogea kwa karibu mpaka chumbani mwao ndipo nilipowasikia wakiwa wanaongea .
Kwakuwa sikutaka Majura ajue, nilimdanganya kuwa yupo sebuleni ili asiondoke .
“Baby…yupo sebuleni hivo usiondoke”
“Daah ! sasa itakuwaje?” Kwa sauti ya chini sana aliniuliza.
Sikumkumjibu chochote na badala yake nilimsogelea na kumkumbatia huku nikideka kifuani kwake.
Kwa mbali sana, alianza kunielewa kile nilichokitaka.
Nikiwa nimelaza kichwa changu kwenye kifua chake, alinishika kwenye shingo kisha akaanza kuushusha mkono wake taratibu mpaka kwenye uti wa mgongo wangu.
Hali hiyo ilinifanya nianze kumvuta taratibu mpaka kitandani ili asiondoke.
Ama kweli hakuna mkate mgumu mbele ya chai ndivo ilivyokuwa kwa Majura mara baada ya kushikwa kwenye sikio lake la kushoto.
Sasa hofu ilianza kumtoka japo alikuwa na uoga kwa mbali.
Tukiwa ndo tumejilaza, gafla mlango ulisikika ukifunguliwa.
Kufumba na kufumbua macho, Majura hakuwa alikuwa amechomoka chumbani humo huku akiwa amevaa bukta pamoja na kaushi yenye rangi ya pundamilia.
“Mwizi…mwizi…!.mwizi…” Sauti ya Baba Furaha ilisikita huku vishindo vikisikika
Asee niliogopa sana kumbe huenda baba Furaha alimuona kweli.
Kwakuwa alidai mi si mke wake, sikujali chochote na badala yake niliendelea kuomba wasimkamate wala kumuona sura ili kukwepa vita kati yangu na Kapipa.
Niliamka kisha nikaficha shati lake pamoja na suruali yake huku nikisubiria kama wamemkamata au kumuoana au la na nini atafanya baada ya kurudi nyumbani…
JE ILIKUWAJE?