Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

MUME WANGU ALIVYONIACHA NA KUMUOA MDOGO WANGU

PART: 13

ILIPOISHIA

Roho yangu ilianza kuvuja damu kwa ndani huku nikitamani kupasuka mara baada ya kuona picha ya Delila akiwa amevaa nguo ya ndani tu huku maziwa yake yakiwa nje yote.

“Hivi kampa nini ambacho sina mpaka anakuwa kama kichaa?!, yaani kumbe kuomba kote msamaha ni uongo mtupu!, haya ila kitaeleweka..” nilitamka moyoni mwangu.

Niliendelea kujifanya nimesinzia bila kumwambia chochote mpaka asubuhi yake.

Tulifanya maandalizi ya mwisho kuelekea nyumbani huku nikiwa na hasira kali sana.

Kesho yake mnamo mida ya 12 asubuhi, tulianza safari ya kuelekea nyumbani Tanga huku baba mkwe akiwa ameshatangulia kimyakimya na wazee wenzake wawili…..

SONGA NAYO…

Tuliendelea na safari huku speed ya gari ikiwa kali sana kiasi cha kufanya baadhi ya abiria waliokuwa wameketi seat za nyuma, kuanza kupiga kelele wakidai dereva apunguze mwendo.

Kwa hasira niliyokuwa nayo juu ya mme wangu na Delila, nilitamani nipae angani kama ndege ili nifike mapema.

Mnamo mida ya saa 10 za jioni, tuliwasiri nyumbani na kukuta maandalizi yotr yako tayari.

Tuliingia ndani kisha mama akatuletea chakula lakini nilishindwa kula hata kidogo kwa hasira kali.

Nilitoka ndani na kuelekea jikoni huku nikiwa namsaka Delila ndipo nilipokutana na mama ambaye aliishia kunishangaa.

“Mbona hujala chekula!, unaumwa?” Aliniuliza kwa mshangao

“Hapana mama!, sina nguvu wala siwezi hata kula chakula…:

“Hee!  Shida nini?”

“Ngoja kwanza nitulie kwanza…” nilitamka

Baada ya mda mfupi, walisikika watu wakibisha hodi ndipo nilipochungulia na kukutana na sura ya baba mkwe akiwa na wazee wawaili aliokuwa ameambatana nao.

Nilibana ukutani kisha nikamuita mama ,

“Mama!, baba mkwe amekuja!” Nilimwambia huku nikiwa napangusa machozi.

Mama aliingia ndani wakasalimiana na baba mkwe pamoja na baba ambaye alikuwa sebule ya pili.

Walianza kucheka na kutaniana kisha wakatengewa chakula . Baba alijumuika nao huku wakipiga story za hapa na pale.

Nikiwa nimejibanza ukutani, mama alinifuata kwa mara nyingine kisha akaniuliza kwa sauti ya chini.

“Mwanangu!, kuna nini? Au umefukuzwa?, ebu niambie..”

“Hapana mama!, hivi Delila yuko wapi?” Niliuliza.

“Yupo chumbani mwake amelala… “

‘Alichonifanyia ndo kinanitoa machozi mpaka mda huu hivyo baba mkwe kaja kusuluhisha…”

“Hee!, kafanya nini tena!” Alitamka kwa mshangao

“Mama…mama…! Mama…” nilishindwa kuendelea kwa uchungu ndipo mama aliponishika mkono.

“Ebu niambie shida ni nini?, mimi ndo mama yako huna mama mwingine zaidi ya mimi!, ebu niambie ..”

“De…li…la.!, anampenda na kutembea na mme wangu” nilitamka huku nikilia kama mtoto mdogo.

Baada ya kauli hiyo!, mama alibaki ameganda mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme.

“Hee!…ame!….” aliongea kwa kukata maneno

“Anatembea na mme wangu na wanapendana sana…:

“Basi!, nasema basi labda sio mimi!, yaani Delila na Elimu yake yote anatudharirisha kiasi hiki!, ngoja nimwambie baba yako kama hatomkata shingo hilo” mama alitamka huku akiwa anajifunga kanga yake vizuri.

Mda si mrefu, alimkonyeza baba ambaye alikuwa sebule ya pili pamoja na baba mkwe. Baba alitoka ndani kisha wakaanza kunena jambo ndipo sura ya baba ilipobadilika gafla.

“Hee!, aibu gani hii!, heshima iko wapi?! Ndo alichokwenda kufundishwa chuo!, sasa namkata miguu hiyo kama wananifunga wakanifunge! Aibu gani hji” baba alitamka na kuingia ndani kwa nguvu lakini mama alimvuta.

Mda huohuo, baba mkwe pamoja na wazee, walimfata baba kisha wakaanza kuongea naye kwa dakika kama 5 hivi ndipo baba aliponekana kupunguza hasira.

Baada ya mazungumzo hayo, waliingia ndani moja kwa moja mpaka sebule ya mbele alipokuwa mme wangu.

Nami nilijumuika nao ambapo tulimkuta Delila akiwa ameketi karibu na mme wangu lakini alipotuona, alinyanyuka na kutaka kutoka nje.

Mama alimuita na kumwambia akae hapohapo kuna mazungumzo. Akiwa amekaa, baba alinyanyuka na kwenda kumzaba kofi lakini walimzuia.

“Wewe mtoto wewe!, hivi unanijua vizuri ..” baba alitamka.

“Jamani tumekuja hapa kwa matatizo ya watoto wetu hawa. Huyu ni kijana wangu ambaye anamuoa mwanenu. Nimepata malalamiko kutoka kwa mke wake ndipo tulipolazimika kuja mpaka huku ili tupate ukweli wake na tunafanyaje kama wazazi” baba mkwe alitamka.

Kauli hiyo ilimfanya mme wangu ainamishe kichwa chake chini huku akiwa anatetemeka kwa aibu.

“Delila…” mama alimuita.

“Una mahusiano gani na mme wa dada yako?”

“Sina mahusiano yoyote yale!,  tofauti na kumfahamu kama shemeji”

Alijibu

‘Mwanangu, sisi wazee na umri wetu, tumeacha kazi kuja kwa ajili yenu hivyo kuwa muwazi  tujue chanzo ni nini?” Baba mkwe alitamka.

“Siwezi kudanganya!, haki ya Mungu sina uhusiano wowote na shemeji”

“Dada yako ni kichaa?” Baba mkwe alimuuliza

“Sijajua maana kinaweza kumshika mda wowote..”

Alijibu

“Ulishawahi kupiga naye picha au kumtumia picha chafu za mwili wako?”

Delila alikaa kimya kisha akajibu,

“Hapana sijawahi na haitokuja kutokea…”

“Unachoongea una ukweli nacho?”

“Ndiyo…”

“Huyu shemeji yako unamfahamu?”

“Ndiyo…”

“Ulishawahi kusikia au kuona anamatatizo ya akili?”

“Shemeji namfahamu sijawahi sikia kama ana hilo tatizo…”

“Sawa utajisikiaje kuwadanganya wazee na wazazi wako mbele ya macho yako?”

“Hapana sijawadanganya nimeongea ukweli…:

“Sawa,  Daudi!, unamfahamu huyu binti..?”  Baba mkwe alimuuliza

” Ndiyo nishemeji yangu” alijibu

“Bila kupepesa macho mbele yetu kama wazazi wako, naomba utwambie hadharani uhusiano wako na huyu binti…mpaka tukaamua kufunga safari kuja huku!”  Baba mkwe alitamka.

Baada ya kauli hiyo, mme wangu alibaki kimya bila kutamka chochote huku akiwa ameinamisha kichwa chini….

PART: 14

ILIPOISHIA,

“Bila kupepesa macho mbele yetu kama wazazi wako, naomba utwambie hadharani uhusiano wako na huyu binti…mpaka tukaamua kufunga safari kuja huku!”  Baba mkwe alitamka.

Baada ya kauli hiyo, mme wangu alibaki kimya bila kutamka chochote huku akiwa ameinamisha kichwa chini….

SONGA NAYO…

“Samahani naomba msamaha nilipitiwa bahati mbaya…” mme wangu alitamka.

“Hapana!, anafanya makusudi!, jana usiku walikuwa wanatumiana picha ilihali mchana alikuwa tayari kashaomba msamaha!. Sasa nataka aongee kama amenichoka aseme!” Nilidakia kwa sauti ya hasira.

“Hee!, wewe mtoto!, unataka tukufanyeje?, jana tumekuonya siku nzima kumbe masikoni umeweka pamba!, sasa wazazi wenzangu, naomba tuliwekee mkazo suala hili kwani litaleta balaa” baba mkwe alitamka.

Wakati anatamka hivyo, Delila alianza kumwaga machozi huku tukiwa hatujui nini kinamliza.

Baba alitikisa kichwa chake kisha akamuuliza mme wangu,

“Unataka uoe ndugu?”

“Naomba msamaha!, ni shetani…”

“Nakuuliza unapenda kuoa ndugu?, nilikuwa nakuheshimu sana tena sana lakini kwa kitenfo hiki umenifadhaisha sana”

“Sitorudia tena baba mkwe..” mme wangu alimjibu baba.

“Ni kitu gani kilikufanya mpaka unafikia hatua hii!, huyu ni mdogo kwako kwanini usimshauri?” Aliulizwa lakini mme wangu hakujibu chochote.

Wakati anazungumza hivyo, baba mkwe alikuwa anateta jambo na mama na baada ya kumaliza wazee nao walioambatana na baba mkwe, walitoa neno,

“Kwa jinsi mambo yalivyo huyu binti na kijana huyu wanapendana hata kama binti anakataa. Tunachoweza kushauri hapa!, kwanza wanapaswa kukiri hadharani bila shuruti. Adhabu kali inatakiwa kutolewa na mwisho wataandikishwa barua na kusaini kama ukumbusho” wazee walitamka.

Baada ya mazungumzo hayo, baba alikwenda chumbani mwake kisha akatoka na kipande cha karatasi na kalamu kisha akaanza kuandika. Baada ya kumaliza, alimpatia mme wangu asaini pamoja na Delila aliyekuwa anamwaga machozi.

Wote walisaini ndipo baba alipotoa kauli,

“Sipendi mwanangu ateseke, sipendi mwanangu aishi maisha ya kutangatanga!, kama umeshindwa kukaa naye!, ongea mbele yetu tukae na mwanetu sio ujinga na upuuzi wako!” Baba alimfokea mme wangu.

“Samahani mzee, nahisi kama ni mwenye masikio atakuwa amesikia. Mimi sipendi mambo ya kulea tabia za hovyo hivyo nakuhakikishia mwanao yupo mikono salama” baba mkwe alitamka.

“Sasa kama anapata ujasiri wa kulala na shemeji yake nani atamtuma mwanaye wa kike aende kwake!, ni fedheha kubwa ambayo haivumiliki” baba alitamka kwa hasira.

“Usimtukane sana huenda mwanao ndo alimfuata ” mama alimjibu baba

“Hata kama kwani ni mtoto?”

“Mhh..sasa maliza basi tuone inakuaje…” mama alitamka.

“Kwa maamuzi yangu ninayoyatoa kuanzia sasa!, Delila huruhusiwi kunyanyua mguu wako kwenda sehemu yoyote mbali na mazingira ya nyumbani, simu zako zote nitazipasua hapahapa hadharani na kuchoma moto mabaki yote.  Kwa upande wa mwanaume, nimekupiga faini la milioni 2, na kupewa onyo kali sana. Endapo nitasikia harufu yoyote ile, ..” baba alitamka.

Mme wangu alinyoosha mkono na kuongea,

“Naomba mnipunguzie adhabu kiasi hicho cha pesa sina…”

“Haipungui hata shilingi mia. Hakuna aliyekutuma kwa mambo ha hovyo kabisa. Badala mkae mjenge familia ya amani wewe hutaki…”

Mme wangu alibaki ameinamisha kichwa chini mithili ya kondoo huku akiwa anajipangusa kijasho chembamba.

“Leta simu hizo” baba alimwambia Delila.

Kwa unyonge, Delila alimkabidhi simu mbili ndipo bila huruma yoyote, baba alizipasua hadharani mbele yetu kisha akachoma moto mabaki ya simu hizo.

Delila alianza kupiga kelele kama mtu aliyechanganyikiwa huku nami nikiwa siamini kama baba huwa ana hasira kiasi hicho.

“Nasubiri ulipe faini kama hauna useme…” baba alimwambia mme wangu

“Kwa sasa sina nina laki 5 tu “

“Basi ondoka hapa!, siku ukipata utakuja…” baba alitamka.

“Samahani mzee mwenzangu!,  naomba mpe mda mimi namdhamini atalipa kiasi kilichobaki ili aende na mke wake waendelee kujenga familia” baba mkwe alitamka.

“Hapana, asipolipa dharau zitaendelea hivyo aondoke hivyohivyo…”

“Mme wangu, hela ni ngumu sana siku hizi, muache alipie kiasi hicho halafu atamalizia: mama aliingilia kati.

“Utamalizia baada ya mda gani?” Baba alimuuliza

“Baada ya mwezi mmoja..”

 “Njoo usaini hapa kama ushahidi…”  aliinuka kisha akasaini.

“Tunashukuru sana kwa kumaliza jambo hili salama bila ugomvi wowote. Hawa ni watoto wetu tunatakiwa kuwaonyq, kuwafunza na kuwaelimisha pale wanapokosea hasa katika masuala ya ndoa.

Jambo moja ambalo napenda kuwambia,  sitokuwa tayari kuvumilia wala kushilia aina yoyote ya unyanyasaji. Mwanenu akipatwa na shida yoyote, atamwambia mama mkwe wake naye ataniambia. Ikija ikajirudia tena!, narudia tena wasikie!, ikija ikajirudia tena! Maamuzi magumu yafuatwe kama ilivyoamuliwa nami nitakuwa mstari wa kwanza na adhebu kali itatolewa” baba mkwe alitamka

Wazee pamoja na  baba mkwe, walisimama na kuonesha ishara ya kuondoka ndipo baba alipowambia,

“Mnaenda wapi?”

“Tunarudi nyumbani mda huu tulipanda gari la private limetusubiria”walimjibu.

“Ohoo safari njema” walipeana mikono kisha akawasindikiza.

Mda huohuo, mme wangu aliniita kisha akaniambia,

“Tuondoke…:”

“Kwanini tusiondoke kesho?” nilimuuliza.

“Twende mda huu usafiri upo…”

Taratibu huku moyo wangu ukiwa umekunjuka kabisa,  na sura yenye furaha, nilimfuata mama kisha nikamuaga.

Mama aliingia ndani mara moja kisha akanipatia karanga kama kisado kimoja hivi pamoja na machungwa.

” Nenda salama mwanangu” aliniambia

” Asante mama..” nilimjibu kisha tukaanza kutembea kuelekea barabarani..

Tukiwa tumepiga hatua chache, gafla Delila alitokea kusikojulikana kisha akamwambia mme wangu,

“Shemu naomba namba ..ya..ko…” alitamka akiwa ameshika kipande cha karatasi na kalamu huku akiwa analia.

“Usimpe namba!…” nilimwambia kwa sauti ya ukali ndipo alipobaki ameduwaa huku akiwa hajui nini akifanye kwa mda huo…

PART: 15

ILIPOISHIA,

Tukiwa tumepiga hatua chache, gafla Delila alitokea kusikojulikana kisha akamwambia mme wangu,

“Shemu naomba namba ..ya..ko…” alitamka akiwa ameshika kipande cha karatasi na kalamu huku akiwa analia.

“Usimpe namba!…” nilimwambia kwa sauti ya ukali ndipo alipobaki ameduwaa huku akiwa hajui nini akifanye kwa mda huo…

SONGA NAYO…

Baada ya mme wangu kuombwa namba tena mbele yangu, alibaki ameduwaa huku nikisibiria ampatie tu.

Kama  bahati kwake, alikataa kumpatia namba huku akionesha sura ya ukali kwake.

“Unashida gani?, tumetoka kwenye matatizo unataka tena kuzua balaa jingine!?  Samahani sana” mme wangu alimjibu.

Baada ya kujibiwa hivyo, Delila alivunjika moyo na kubaki amesimama huku akimwaga machozi. Sikujua nini kinamliza na sikutaka hata kumuuliza.

Mda si mrefu, alirejea nyumbani nasi tukapanda Gari mida ya jioni kuelekea jijini Dar es Salaam Kigamboni.

Ilikuwa safari ndefu kiasi ya takribani masas 6 hivi kabla ya kufika nyumbani.

Mnamo mida ya saa 7 za usiku, tuliwasiri nyumbani kisha tukapumzika kutokana na uchovu wa safari.

Usiku huohuo nikiwa nimelala , mme wangu alinisogelea kisha akaniambia,

“Umefurahi kunidharirisha kiasi hicho?”

“Nimekudharirishaje, sikuwa najua chochote kama baba mkwe atakuja…:”

“Unafikiri mimi mjinga eeh!..”

“Jamani si yameisha?  Mbona unaendekeza maneno…?” Nilimuuliza

‘Yameishaje!, unajua nimetumia kiasi gani cha pesa?”

“Kwahiyo pesa ni muhimu kuliko utu wangu!, au kuna mtu alikutuma kufanya kile ulichokifanya?”

“Sawa ila sijapenda kabisa…”

“Hata mimi sijapenda kutembea na mdogo wangu..”

Baada ya kumjibu hivyo, alikaa kimya kisha nami nikamnyamazia ndipo nilipoanza kuwaza na kuwazua juu ya hatima ya maisha yangu.

Usiku mzima mpaka asubuhi, hakunisogelea wala kunishtua kama ilivyokuwa kawaida yake, nilimuita kwa sauti laini lakini hakuniitikia ndipo nilipolazimika kumsogelea mwenyewe kisha nikamwambia,

“Mme wangu!, nakuomba msamaha kama umechukia!. Nimefanya hivi kwa ajili ya upendo kwako. Ningekuwa sikupendi nisingefikia hatua hiyo.. ” nilimwambia

“Upendo gani?, sasa hivi sina amani kabisa mpaka najihisi kuwa mtupu mbele za watu..sababu yako.”

“Basi nisamehe yameisha tugange yajayo…”

Nilimwambia kisha ndipo alipokaa kimya huku akionekana mwenye hasira. Alivaa nguo zake na kuelekea kazini.

Jioni alirejea nyumbani kisha nikampokea lakini hakuonesha sura ya furaha.

“Mme wangu mbona uko hivi jamani?, unaniumiza moyo.wangu…” nilitamwambia

“Niko vizuri wala sina shida yoyote…”  alinijibu huku akionesha sura ya furaha.

Hakika nilijisikia vizuri kwani kiukweli sikutaka kumuona mme wangu akiwa hana furaha.

Nilimpikia chakula kitamu sana kisha nakamlisha kama mtoto usiku huo mpaka akaanza kutabasamu nami nikatabasamu.

Tulienda kulala na mambo yalikwenda vizuri sana kuliko siku za nyuma mpaka nikajikuta kileleni mwa mlima kilimanjaro.

Maisha yalibadilika na kuwa ya furaha kwelikweli. Baada ya miezi mitatu, nilianza kuhisi uchungu ndipo nilipomwambia mme wangu,

“Mme wangu, najisikia uchungu na clinic wameniambia mda wowote ndani ya mwezi huu nitajifungua “

“Ohoo!..ngoja tuwahi hospitali..”

Alitoka nyumbani kisha akakodi gari mpaka nyumbani.

Haisee!, uchungu wa kwanza ni mkali na wenye maumivu kwelikweli.

Niliingia kwenye gari na vifaa kama beseni na vingine kulingana na malezo niliyokuwa nayapata clinic.

Baada ya mwendo kama dakika 5 hivi, niliishiwa nguvu kabisa huku uchungu ukiwa mkali sana.

Nilipiga kelele ndani ya gari kwa sauti ya chini ndipo dereva aliposimamisha gari. Mda huohuo, nilijikuta najifungua ndani ya gari huku mwili mzima ukiwa umelegea.

Hakuna aliyekuwa na utaalamu wowote ule hivyo tulilazimika kwenda hospitali na kweli tulipokelewa vizuri na kupata huduma.

Baada ya masaa kama manne hivi, nilipata fahamu za kuuliza jinsia ya mwanangu ndipo nilipoambiwa ni mtoto wa kiume.

Nilijisikia furaha isiyo na kifani.

Mda si mrefu, mwili wangu ulianza kupata nguvu ndipo niliporuhusiwa kurudi nyumbani.

Nikiwa nyumbani, mme wangu aliniambia,

“Sasa ni vema ukaenda nyumbani kwenu ili upate msaada  mpaka hapo utakapokuwa sawa”

“Hee!  nyumbani tena!, labda ungeniambia niende ukweni ila siyo kwetu maana mtoto damu yenu”  nilimjibu.

“Vyovyote haina shida kikubwa upate msaada..”

“Lakini mme wangu kwakuwa tumebahatika kuwa na kijumba chetu, kwanini nisimuombe mama mkwe aje nyumbani?”

“Kwa umri wake ni kumtesa na joto hili hivyo unatakiwa uende mpaka utakapokuwa sawa…”

“Ngoja nimpigie nimuombe kama anaweza kuja…”

“Hata usipompigia kwani nimeshamwambia kuwa unakuja huko…”

“Sawa haina shida…” nilimjibu

Kesho yake mapema sana, nilipanda kwenye basi kisha nikaanza safari ya kuelekea ukwenj japo mwili wangu ulikuwa hujatengamaa.

Mnamo mida ya saa 10 za jioni, tuliwasiri na kupokelewa na mama mkwe kwa furaha.Nami nilijiona mwanamke mbele ya wanawake kwakuwa na mtoto.

Baada ya mwezi mmoja huku nikiwa napikiwa vyakula vya asili, mwili wangu ulianza kuwa na nguvu japo hospitali niliambiwa wiki 6.

Mda huo nilijikuta nammis sana mme wangu kwani alikuwa anajisahau kunipigia hata simu mpaka nikawa nalalamika lakini aliishia kunijibi kuwa yupo busy na kazi.

Sikutaka kubishana naye wala kuonesha  sauti ya hasira.

Nilipotimiza miezi miwili, sasa nilikuwa fit kabisa ndipo nilipompigia mme wangu ili anipatie nauli ya kurejea kwangu.

“Baba Devi.., naomba nauli …”

“Nauli ya kwenda wapi?,

“Hee!,..maswali gani unaniuliza?, kwahiyo huku ni kwangu?”

“Nimekuuliza nauli ya kwenda wapi?, baki huko kwanza maana sina hela kwa sasa…”

“Yaani hela ya nauli ndo hauna!, basi ngoja nimuombe mama mkwe au baba mkwe”nilimjibu

“Ebu kata simu kwanza, kuna meseji nakutumia mda huu uisome…”

“Meseji gani?, si useme hapa ulichoandika?”

“Nimeamua nikutumie kwa meseji ….” alitamka kisha akakata simu ndipo nilipobaki na taharuki ya kujua nini katuma kwenye meseji ambacho hawezi kuniambia kwa mazungumzo?….

PART: 16

ILIPOISHIA,

“Baba Devi.., naomba nauli …”

“Nauli ya kwenda wapi?,

“Hee!,..maswali gani unaniuliza?, kwahiyo huku ni kwangu?”

“Nimekuuliza nauli ya kwenda wapi?, baki huko kwanza maana sina hela kwa sasa…”

“Yaani hela ya nauli ndo hauna!, basi ngoja nimuombe mama mkwe au baba mkwe”nilimjibu

“Ebu kata simu kwanza, kuna meseji nakutumia mda huu uisome…”

“Meseji gani?, si useme hapa ulichoandika?”

“Nimeamua nikutumie kwa meseji ….” alitamka kisha akakata simu ndipo nilipobaki na taharuki ya kujua nini katuma kwenye meseji ambacho hawezi kuniambia kwa mazungumzo?….

SONGA NAYO….

Niliweka kiganja cha mkono wangu kwenye kifua changu huku mapigo ya moyo yakinienda kwa kasi ya ajabu.

Nikiwa katike hali hiyo, gafla meseji iliingia kwenye simu yangu ndipo niliposhtuka na kuiangalia.

Nilianza kuifungua huku nikiwa  natetemeka ndipo niliposhikwa na bumbuwazi huku nikiwa siamini kama mme wangu kipenzi ndo kaandika mambo hayo.

Nilitupa simu chini kisha nikaangua kilio mpaka mama mkwe akanikimbilia kunipa msaada.

Hakika nilifadhaika sana mpaka nikaona dunuia chungu huku nikiwa nawaonea wivu wale waliokuwa na maisha ya furaha kwenye ndoa zao.

Meseji hiyo ilisomeka hivi

       “ASANTE KWA KUNIZALIA MTOTO, ASANTE KWA MDA AMBAO TUMEISHI WOTE,

 NIPENDE KUKWAMBIA KUWA SINA MPANGO TENA WA KUISHI NA WEWE KWANI SINA

 FURAHA KABISA NIKIWA NA WEWE. MTOTO WANGU MLEE VIZURI NA KAMA KUNA

 GHARAMA ZOZOTE ZA MATUNZO BASI NIAMBIE. NIKUTAKIE MAISHA MEMA KUANZIA

 SASA MIMI SIYO MME WAKO. ASANTE NA SAMAHANI KAMA NIKEKUKWAZA”

Ujumbe huo nilimsomea mama mkwe ambaye naye alibaki ameshika kichwa mitihili ya mtu aliyefiwa.

“Huyu mtoto karogwa siyo bure!, hee!, yaani badala ashukuru kwa kupata mtoto ila anafanya mambo ya ajabu!, mimi nimenyoosha mikono kwake” alitamka kisha tukaingia ndani.

Mda si mrefu, baba mkwe aliwasiri nyumbani hapo ndipo nilipomuonesha ujumbe huo aliokuwa ameuandika.

Alitikisa kichwa kisha akashika tama huku akiwa hana la kuongea.

“Mwanangu!, kilichopangwa na Mungu hakuna wa kupangua…hapa sina cha kuongea juu yake ila kuanzia sasa mimi na yeye basi. Kinachoniuma ni huyu mtoto ambaye hana makosa yoyote…” baba mkwe alitamka.

Maneno hayo yalizidi kunitia huzuni huku nikiwa sijui nini cha kufanya ,baada ya kutulia kidogo, walijaribu kumpigia simu lakini hakupokea ndipo mambo yalipozidi kuwa magumu.

“Sasa kama ameamua kuachana na mimi anipe talaka maana nimeweka jasho langu kwa mali ambazo zipo nyumbani. Siwezi kuondoka namna hii bila chochote..:

“Ni haki yako wala hilo halina kipingamizi chochote..” baba mkwe alitamka.

“Sasa kesho nasafiri kuelekea nyumbani ili nianze mchakato wa kudai talaka “

“Lakini kabla ya kufanya hivyo ni bora tungekaa kidogo kikao ili tuone tunafanyaje…”

“Kwakweli mimi nimechoka tena sana…kama tumefanya kikao juzi halafu leo hii ananiambia ameniacha!, basi tu siwezi kujipendekeza kwa mtu asiyenipenda”

“Sawa safari njema ila kitakachokuwa kinaendelea utanijuza ila msizue ugomvi…”

“Sina hata nguvu za kugombana naye…” nilimwambia baba mkwe.

Wakati yote yanaendelea, nilikuwa sijawambia chochote kile upande wa nyumbani kwa hali niliyokuwa nayo.

Kesho yake asubuhi na mapema, nilianza safari ya kurudi Dar es Salaam Kigamboni huku nikiwa na hasira kali sana.

“Ole wake nimkute mtu ndani sijui malaya! Atanitambua…” nilijisemea mwenyewe.

Mnamo mida ya saa 11 za jioni, niliwasili viunga vya nyumbani kwangu ndipo nilipopigwa na butwa kwa kuona nguo za ndani za mwanamke zikiwa zimeanikwa kwenye kamba .

Machozi ya hasira yakinitoka huku roho ya kufanya jambo kali ikinijia kichwani mwangu.

Sikujua nani yumo ndani wala analinganaje hivyo ilinibidi nijipange kwanza. Taratibu nilifika mlangoni kisha nikagonga mlango kwani ulikuwa umefungwa kwa ndani.

Niligonga kwa mara ya pili ndipo ulipofunguliwa nami nikaishia kushangaa! Hee!  si mwingine bali alikuwa Delila ambaye alikuwa amejifunga kanga tu huku kichwani akiwa amevalia kofia ya kulalia.

Baada ya kukutana na sura yangu, alinifungia mlango ili nisiingie ndani ndipo nilipojaribu kupambana lakini nilishindwa.

Mda huhuo nilimpigia simu mama huku nikiwa na hasira kwanini Delila amekuja kwangu bila hata kutaarifiwa?,

“Shikamoo mama…” nilimsalimia

“Marhaba mnaendeleaje huko?”

“Mama sasa hivi niko kwangu kigamboni ila nilichokikuta mpaka sasa siamini!”

“Hee kitu gani tena mwanangu?”

“Mama kwanini mnapenda kunificha siri zenu?”

“Siri ipi tena?”

“Delila yuko wapi?””

“Ana kama mwezi tangu atoroke nyumbani hapa na hatujui yuko wapi?”

“Kwanini hamkuniambia kuwa ametoroka?, mda huu mme wangu kaniandikia meseji kuwa ameniacha na nimekuja kudai mali zangu ndipo nilipomkuta Delila akiishi kama kwake . Sasa mama bora nife mimi au afe yeye ila hawezi kukaa kwenye nyumba ambayo nimemwaga jasho langu halafu ananifungia mlango nisiingie ndani”

“Hee!! Jamani huyu mtoto!  Sasa njoo kwanza nyumbani maana mtauana bure hapo…”

“Mama!..yaani nimuache aishi nyumbani kwangu halafu mimi nihame!, nipo tayari kuishi peke yangu ila sitoki. Kitakachotokea basi…” niliongea kwa hasira kisha nikakata simu.

Nikiwa nimesimama kwa nje na mabegi yangu, niliamua kwenda kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa ii anipe usaidizi wa kuingia ndani.

Nilimueleza kisa changu chote ndipo alipoambatana na mimi mpaka nyumbani.

Aligonga mlango kwa nguvu lakini Delila hakufungua ndipo nilipompatia namba ya mme wangu kisha akampigia,

“Heloo, unaongea na mwenyekiti wa serikali za mtaa, nakuhitaji mara moja niko kwako”

“Kuna shida gani?”

“Hakuna shida bali  ni mazungumzo yakawaida tu…”

“Sawa nipo njiani kama dakika 5 ntakuwa nimefika…”.

Tuliendelea kumsubiria…..

PART: 17

ILIPOISHIA

Nilimueleza kisa changu chote ndipo alipoambatana na mimi mpaka nyumbani.

Aligonga mlango kwa nguvu lakini Delila hakufungua ndipo nilipompatia namba ya mme wangu kisha akampigia,

“Heloo, unaongea na mwenyekiti wa serikali za mtaa, nakuhitaji mara moja niko kwako”

“Kuna shida gani?”

“Hakuna shida bali  ni mazungumzo yakawaida tu…”

“Sawa nipo njiani kama dakika 5 ntakuwa nimefika…”.

Tuliendelea kumsubiria…..

SONGA NAYO…

Baada ya mda kama dakika 5 hivi, nilimuona mme wangu akiwa ameweka koti lake begaji ndipo nilipoketi chini kwa hasira kali ya kumuona.

Akiwa hajui kama nipo sehemu hiyo, alikuta uso kwa uso na mwenyekiti ndipo alipogeuza shingo na kukutana na sura yangu.

Alishtuka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme kisha akatamka,

“Hee!, umekuka kufanya nini?, au meseji yangu hukuiona!”

“Samahani, naomba tuingie ndani tuongee hiki ndo kimenileta hapa” Mwenyekiti alitamka.

“Sasa kama nishamkataa iweje mnilazimishe kuishi naye?, au una jambo lingine la ziada?” Aliuliza.

“Ebu fungua mlango kwanza..”

Baada ya kuambiwa hivyo, alimpigia simu Delila kisha akafungua huku akiwa amejifunga kanga tu iliyoishia kifuani, Moyo ulinidunda na kutamani kummeza mzimamzima lakini nilijikaza na kuomba Mungu anivushe katika jaribu hilo.

Tuliingia ndani ndipo Mwenyekiti bila kupoteza mda alipomwambia mme wangu,

“Huyu unamfahamu?”

“Ndiyo alikuwa ni mke wangu ila sasa nimechana naye”

“Mlifunga ndoa?”

“Ndiyo…”

“Umempa talaka”?

“Hapana kwanini tufike huko?, nimeshaachana naye ..”

“Sawa mimi kama mwenyekiti wa mtaa, nikiwa nawakilisha serikali naomba usimguse kwa njia yoyote ya kumdhuru wala kumfukuza katika nyumba hii mpaka hapo taratibu nyingine zitakapofikiwa.”

“Hee!, sitaki akae kwangj….”

“Najua hutaki lakini nimetoa amri ya kiserikali na ukikiuka, adhabu kali itachukua mkondo wake”

Baada ya kuambiwa hivyo, alikaa kimya kisha akaenda chumbani na kujifungia na Delila

Kwakuwa mwenyekit alikuwa amemaliza kazi yake, aliniaga na kurejea nyumbani kwake huku akinihakikishia kunisaidia

Kwa uchungu mkubwa, niliingia chumba cha kulala wageni kisha nikapumzike huku kichwa kikiwa kinaniuma kwa uchungu mkubwa.

Niliamka kwa tena na kurejea sebuleni ndipo nilipoanza kusikia sauti zao wakiwa wanacheka chumbani humo.

Hakika sikuwahi kupitia wakati mgumu sana kama siku ile. Nilipiga moyo konde huku nikiwaza nini nifanye lakini kwa wakati huo sikupata jibu.

Kwakuwa sikuwa na pesa kwa mda huo, niliwapigia mashemeji zangu wawili kisha nikawaeleza yote niliyofanyiwa na ndugu yao, ndipo waliponisaidia kiasi cha sh laki 5 kwa pamoja.

Nilishukuru sana na Moyo wangu ukapata japo furaha kwa mda.

Sikuhiyo nililalia mkate na juice tu kwani sikuwa na nguvu hata za kupika.

Kesho yake asubuhi na Mapema, niliamkia kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii kisha nikaeleza shida zangu ndipo walippnisikiliza na kunipatia barua ya kumuhitaji mme wangu.

Barua hiyo nilimpatia mwenyekiti ambaye alimpatia lakini alikaidi kwenda. Nilianza kufanyiwa vituko vya kila aina kama kunikomoa huku wakati mwingine wakikumbatiana na kupeana mabusu mbele yangu.

Uvumilivu ulinishinda mpaka nikawaza kuondoka na roho ya mmoja lakini nilikumbuka kuwa yote ni mapito tu na yana mwisho wake.

Baada ya kukataa wito wa kwenda kule,  nilirudi tena ndipo walipoanza kunisikiliza na wakaanza kuorodhesha mali zangu zote.

Nilitaja kilw kitu kwa kuanza na nyumba na mali zpte hata ambazo nilizikuta. Baada ya kuorodhesha, tuliambatana wote mpaka nyumbani na bahati nzuri walimkuta.

 Alishtuka sana kuwaona ndipo walipompatia nakala kisha wakampa maelekezo,

“‘Kwakuwa umeamua kuachana naye tena mke wako wa ndoa mwenye mtoto wako! , mtagawana mali zote kama inavyoonekana. Nyumba mnaweza kuamua kuuza au kugawana nusu . Kama unakubali utasaini hapo na kamw hubali utafunguliwa shauri la kuombwa talaka na kutelekeza mke mahakamani”

“Hee!, yaani nyumba na mali zote alizikuta hapa kama alichangia  ni kiasi kidogo tu hivyo hana chake hapa”

“Unazijua sheria za ndoa?”

“Hapana…”

“Basi kutokujua sheria hakukupi nafasi ya kuvunja sheria. Hata kama alikuwa anashinda nyumbani tu!, huo ni mchango kwani ulikuwa unamlipa kama mfanyakazi wako wa ndani?”

Maneno hayo yalimchanganya mpaka akaishia kushika kichwa huku akiwa hajui niniafanye.

“Mama unasemaje kwa kauli yako ya mwisho?:

“Anipe talaka na hela ya malezi kwa mtoto…”

“Ohoo!, tulisahau kuhusu gharama za malezi anatakiwa kulipia”

“Lakini kwanini tufike huko kote?, si arudi kwao?” Alitamka

“Hapa ni kwake labda wewe ukiamua kuonfdoka”

Alibaki kimya huku akiwa ameinamisha kichwa chake ndipo alipopewa karatasi asaini lakini alikataa

Baada ya kukataa, waliondoka huku wakimwambia mda wowote atahitajika mahakamani

 Usiku ule , Deilila alipita mbele yangu kisha akaninyooshea kidole na kunitukana ndipo nilipomrekodi kama kumbukumbu.

Sikutaka tena kupigana naye kwa hatua ambazo nilikua nimefikia. Nilimpigia simu mama na kumueleza jinsi hali ilivyo ndipo aliponiambia ,

“Mwanangu!  Achana na mambo ya makesi!, njoo nyumbani utulie kama wakati wa bwana ukifika utafurahi “

Kauli hiyo iliniacha njia panda ndipo nilipoamua ku….

PART: 18

ILIPOISHIA,

Baada ya kukataa, waliondoka huku wakimwambia mda wowote atahitajika mahakamani

 Usiku ule , Deilila alipita mbele yangu kisha akaninyooshea kidole na kunitukana ndipo nilipomrekodi kama kumbukumbu.

Sikutaka tena kupigana naye kwa hatua ambazo nilikua nimefikia. Nilimpigia simu mama na kumueleza jinsi hali ilivyo ndipo aliponiambia ,

“Mwanangu!  Achana na mambo ya makesi!, njoo nyumbani utulie kama wakati wa bwana ukifika utafurahi “

Kauli hiyo iliniacha njia panda ndipo nilipoamua ku..

SONGA NAYO…

Baada ya kutafakari maneno hayo, niliamua kufata haki yangu ili walau nipete sehemu ya kuishi na chochote cha kumtunza mwanangu.

Kwa ukaribu na usaidizi mkubwa kutoka idara ya Ustawi wa jamii, nilifanikiwa kufungua shauri la kudai talaka ambalo lilisikilizaa mfululizo kwa takribani miezi mitatu ndipo nilipofanikiwa kupewa talaka kutoka kwa aliyekuwa mme wangu.

Habari njema kwangu, nilipata haki yangu kwa kugawana mali zote nusu kwa nusu. Kwakuwa nilikuwa nishapa haki yangu, nilifunga vyumba na sebuleni nilipokuwa naishi kisha nikapata wapangaji ambao walinipatia kiasi cha pesa nilizotumia kupanga sehemu nyingine.

Mali nyingine tulilazimika kuuza ili kila mtu apate chake. Nilitumia kiasi hicho kuanzisha biashara  ndogo ya genge la matunda na mbogamboga kwa takribani mwaka mmoja hivi.

Mtaji wangu ulianza kukua taratibu mpaks nikafungua saluni mbili za kike ambazo kwakeli zilinipatia kipato kikubwa sana mpaka nikajikuta nanua usafiri wangu.

Baada ya miaka 3, habari zilianza kusambaa kuwa kila mimba anayoibeba Delila, inatoks hali iliyopelekea kufukuzwa na Daudi aliyekuwa mme wangu.

Siku moja  nikiwa siamini, alinipigia simu kuwa turudiane ndipo nilipomjibu ” ukitapika huwezi kula matapishi yako”

Baada ya kumjibu hivyo, nilikata simu na kila alipokuwa akipiga sikupokea.

Maisha yangu yalianza kubadilika huku wanaume wakinifuata na kutaka kunioa lakini sikuwa tayari hasa nilipokumbuka maumivu makali niliyoyapata kwenye ndoa.

Hakika ni wakati niliomuombea aishi miaka mingi ili aone wema wa Mungu ulionizunguka ili awasimulie na wengine.

Baada ya mda ulivyokuwa unazidi kusonga, alianza kunitisha eti anataka mtoto wake lakini sikuwa tayari kwani hata kumuona alikuwa haji kumuona.

Nilimpeleka mwanangu shule kisha nikaendelea kupambana mpaka nikafanikiwa kununua kiwanja na kujenga ka nyumba kangu ka vyumba vitatu.

Delila alianza kunipigia simu huku akiniomba nimsaidie chochote mara baada ya maisha kumpiga lakini sikuwa tayari kufanya hivyo.

Sikuwahi kuamini kama mwanamke anaweza kumiliki kipato chake mwenyewe lakini kupitia matatizo yangu, nilisimama imara kwani sikuwa na sehemu tena ya kutegemea isipokuwa kwa bwana tu na mikono yake.

*******

Baada ya kuachana na Delila, alioa mwanamke mwingine ambaye naye aliondoka baada ya miezi kama 6 hivi kisha akaoa mwingine  ambaye alifariki baada ya miaka 2 .

Habari hizo zilinitisha sana japo tulikuwa tumeachana ili nilikwenda msibani na kumpa pole ndipo nilipomkuta amekonda huku mabega yakiwa yamechongoka.

Baada ya kuniona, alipiga magoti mbele yangu huku akilia kisha akaniambia,

” Sikujua kuwa ulikuwa ni mke mwema kiasi hiki!, alichonifanyia mdogo wako najuta mpaka mda huu, sina tena amani ya maisha, naomba unisamehe maana mda wangu wa kuishi ni mdogo sana hapa duniani ” alitamka.

Maneno hayo yalinitisha sana mpaka nikamuuliza,

” Kwanini unaongea maneno nakali kiasi hicho?”

” Nashindwa hata nikwambie kitu ila mdogo wako kaniua..”

” Amekuuaje…” nilimuuliza…

” Ameniambukiza virusi vya Ukimwi.Maskini mke wangu kafariki kwa tatizo hilo ambalo nilishindwa kumwambia mapema…”

Nilijikuta namwaga machozi huku nami mapigo ya moyo yakinienda kasi.

” Pole kumwa mwathirika siyo mwisho wa maisha yako . Mimi nilikuja kuwapa pole naondoka.”

Nilianza kurejea nyumbani huku nikiwa na wasiwasi mkubwa juu ya afya yangu  . Nilipita Dispensary kupima afya yangu na majibu yalionesha sina virusi vyoyote.

Nilishusha pumzi kisha nikaenda sehemu nyingine lakini majibu yalikuja yaleyale.

Baada ya miezi mitatu, nilienda kupima tena lakini majibu yalibali hivyohivyo ndipo nilipompigia mama na kumwambia habari nzima huku Delila ikisemekana anaugua magonjwa ya ajabu ajabu mpaka kashakonda na kubakia kichwa tu.

Mama aliishia kulia huku nikiwasihi wampeleke hospitali  na baada ya vipimo, alikutwa na Virusi vya Ukimwa ndipo alipoanzishiwa dozi ya ARV.

Mpaka mda huu yupo hai na amemuamu kuokoka na kumtegemea bwana nami nikaamua kumsamehe kama ndugu yangu ili kumpunguzia mawazo.

Kwa upenda wa Daudi mme aliyekuwa mme wangu  alikosa uvumilivu hali iliyopelekea kujinyonga nyumbani kwake siku chache baada ha kifo cha mke wake.

Apumzike kwa amani.

Kila lenye mwanzo lina mwisho wake, na huo ndo mwisho wa simulizi yetu. ASANTEE NA KARIBU TENA KWA SIMULIZI NYNGINE

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!