Mume Wa Mama
Sehemu ya 30
*Wakati anasoma nikamuona amekunja sura kana kwamba ulikuwa sio ujumbe mzuri, ŠØŇĞÃ MBĔĹĹÉ
“alipomaliza kusoma nikamuona akeirejesha mfukoni huku ananitazama usoni,
* Mme wangu nani kakutumia meseji.
nikakuuliza hivyo.
* Aah kuna mtu amekosea namba achana nae.
* Mh amekosea namba kivipi hebu nione alichokiandika.
* ungeniomba tangu mwanzo sasa nimesha ifuta achana nae
“Mme wangu akanijibu vile basi ikabidi nikaushe tu. maana nilikuwa sipendi kumuuzi naogopa asije akaniacha akarudi kwa Mama. Mda ulifika tukaingia kwenye ndege na ndege ikaanza safari.
“Huku nyuma sasa mambo yalikuwa kama hivi.
” Mama mkwe wa mama alifika nyumbani kwa Mama frenk. akamkuta mama frenk na Mama yangu mzazi niliye mpokonya mme wake hadi sasa nipo nae mimi.
* Mama mkwe kalibu sana.
* Asanteni mama Tina ila nimekuja na fundi kabisa wa vitasa nafikiri hatuna mda wa kupoteza Twendeni kwenye nyumba ya mme wako.
Mama aliambiwa vile na mama mkwe wake.
Basi wakaenda hadi nyumbani walipofika isaya akafungulia geti wakaingia Ndani. walipoigia wakashuka kwenye gari kisha wakaingia ndani ya nyumba sasa.
* fundi nataka mnifungulia vitasa vya milango hii mitatu. Mkwe wa mama akawaambia wale mafundi wa vitasa walikuwa wawili. kweli wakaanza kufanya kazi yao baada ya dakika 5 wakamaliza kuifungua milango yote mitatu tuliyokuwa tumeifunga mimi na mme wangu. baada ya kufungua wakalipwa ujira wao kisha Wakaondoka zao.
* mama tina hivi nafikiri unajua kilicho tuleta hapa ndenda ukachukue hadi miliki ya nyumba ili tukaibadili iwe ya kwako.
* Sawa mama mkwe.
“mama akajibu hile kisha akaingia chumbani maana alikuwa anajua hati ilipohifaziwa. Mama alipoingia chumbani akapekua kabati Lakini hakufanikiwa kuona akafungua madroo lakini pia hakufanikiwa kuona yani kwa ufupi Hati ilikuwa imehaamishwa.
baada ya kupekuwa bila ya mafanikio alitoka akamweleza. Mkwe wake pamoja na isaya.
* Mama Tina wiki na nusu ni nyingi mno wewe endelea kuitafuta taratibu utaiona tu.
Bandema hawezi kuondoka na hati miliki ya nyumba.
* Basi sama mama mkwe nitajitahidi kuzitafuta.
Mama akamjibu hivyo. Basi waliendelea na story zingine badae mkwe akaondoka pamoja na isaya.
nyumbani akabakia mama peke yake.
” ooh mungu nijalie niipate hati ya nyumba hii. najua mme wangu akikosa nyumba atarudi hapa kukaa na mimi ataachana na Tina.
Mama alijiombea hivyo.
maisha yakaendelea Mama akawa anaishi pale nyumbani huku akiendelea kuitafuta hati miliki.
Baada ya wiki moja.
* Huku india nilikuwa nimesha wekewa mguu wa bandia pamoja na mkono bandia Kusema kweli nilikuwa na furaha mno kwani nilikuwa naweza kutembea. kama vile ninamguu wa kweli.
“kweli niliamini Ukiweka pembeni Roho.
pesa inaweza kununua vyote vilivyo bakia.
* Mme wangu Sasa naweza kutembea kama mwanzo Lini tunarudi nyumbani
Nikamuuliza mme wangu mda huo tulikuwa tumepumzika kwenye hoteli tuliyofikia.
* Tina zimebakia siku mbili tu ilikodi yetu imalizike turudi Tanzania. Sasa Latiba iko hivi Leo tunapumzika kesho tunaenda madukani kununua vitu harafu kesho kutwa tunaondoka.
” Mme wangu akaniambia hivo nikamuelewa. basi tulikaendelea kufanya mahaba yetu.
hadi tukasinzia
Usiku wa manane wakati Tumelala Baba aliamka Taratibu akachukua kila kitu harafu akanitoroka ilipofika asubuhi wakati nimelala sijui chochote mara Ghafla mlango wa chumba ukagongwa. niliamka kiuchovu nikaenda kufungua.
* Dada fanya utoke mda wa kukaa chumba umesha malizika tunataka kupangisha wageni wengine.
* Mh mda umemalizika kivipi mbona sikuelewi. nikamuuliza yule muhudumu.
* Dada hapa mmelipia siku 8 tu sasa zimeisha leo usiku fanya uondoke bahna unanichelewesha kufanya usafi.
* Mh aya harafu mbona mme wangu hayupo ameenda wapi.
* mme wako ameniachia maagizo nikwambie kwamba ukifanikiwa kufika utamkuta Tanzania.
“muhudumu aliponiju hivyo Nikahisi mpasuko wa moyo Na nywele sikasisimka yani hapo kisu kilichoma mfupa..
Sehemu ya 31
“Muhudumu aliponijibu hivyo nikahisi mpasuko wa moyo na nywele zikasisimka yani hapo kisu kilichoma mfupa.SONGA MBELEE….
” Dada nakupa dakika 10 nikirudi nikute umesha ondoka hapa. yule muhudumu akaniambia hivyo, kisha akaondoka zake kuendelea na kazi zingine.
” Nilifunga mrango nikarudi na kukaa kitandani nikaanza kujiuliza
“Nitarudije nyumbani mimi. nimemkosea nini mme wangu mpaka amenitelekeza huku india jamani’ eeeh mungu weeeh wanaume hawa nifanye nini sasa. nilijiuliza bila kupata majibu nikaongea mwenyewe kama chizi, kilio kikaniandama.
wakati nipo chumbani sijui nini cha kufanya.
” Mda huo Baba yeye alikuwa amesha fika eyaport alifika pakukatia Tiketi akapanga mstali.
“wakati yupo kwenye foleni ya watu wachache. *Ngoja nitoe paspoti yangu nikamate mkononi.
“Baba akajiambi hivyo, sasa alipojisachi mfukoni mara Ghafla akawahaeleweki kwa sababu alipojisachi paspoti yake pamoja na vitambulisho vyake havikuonekana.
“Baba alitoka kwenye foleni akaenda pembeni kisha akafungua begi lake dogo akatazama lakini hakuona paspoti wala vitambulisho.
kilicho mchanganya zaidi ni kadi ya bank,
nayo haikuonekana.
“Daah mkosi gani huu baba akajiuliza huku anakuna kichwa,
” Kwa upande wangu baada ya kulia kwa mda Nilichukua begi langu iliniondoke maana yule muhudumu alikuwa ananisumbua Sana.
Lakini wakati nataka kutoka nje mara Ghafla nikawa kama nimeambiwa na mtu kwamba angaria kwenye Droo.
kweli nikarudi nikafungua droo nikatazama ndipo nikakuta vitambulishi vyote vya baba,
“Heeeh hivi si vitambulisho vya mme wangu na paspoti.
inamaana kavisahau. nilijiuliza hivo kisha nikavichukua nikaondoka navyo
“dakika Tano tu tangu niondoke pale hotelini
“Baba alienda akaambiwa nimeondoka mda siyo mlefu. alielekezwa sehemu niliyo enda
“Baba hakutaka kupoteza mda akawasha simu yake maana alikuwa ameizima kwajiri yangu,
baada ya kuwasha akanipigia. japo nilikuwa na hasira lakini nilipokea simu akaniuliza sehemu nilipo nikamuelekeza akaja.
* kwahiyo ulikuwa unanitoloka.
* Nilikuwa nakupima imani tu ndio maana nikaacha vitambulisho vyangu vyote mle kwenye droo.
“baba akanijibu hivo.
* imani gani ambayo unanipima harafu kumbe unaishi na mimi bila imani.
* nilitaka kujua kama unanipenda zaidi maana mimi nakupenda hadi sijielewi. kama usinge pokea simu yangu ningejua hunipendi kama usinge chukua vitambulisho vyangu ningejua hunipendi,
lakini Mitego yangu yote umeinasua sasa ndio naamini kwamba unanipenda kwa dhati Tukifika nyumbani nakununulia Ghari mpya nzuri kama wewe,
“baba aliniambia hivyo hasira zote zikaisha. nikaanza kutabasamu.
mambo yalienda sawa
Siku hiyo hiyo tukaondoka india. upendo wangu kwa baba ulikuwa full, lakini yeye hakuwa ananipenda tena ila sikujua Baada ya safari ya mda mrefu Tukafika Tanzania.
* Tina hebu tangulia nyumbani nitakukuta,
* Jamani mme wangu nitangulie wewe unaenda wapi.
* Naenda hospitali kuonana na yule nesi kuna dawa aliniagiza india naenda kumpelekea tangulia nyumbani ukaniandalie juisi nzuri ili nije nywe mmeo,
* Aya mme wangu nenda Ukija nyumbani utakuta juisi ya matunda natumaini utaifurahia.
“nilimuluhusu akaondoka.
Nilipo ingia kwenye Tax
Baba akazima simu yake kisha nae akaenda alipopajua yeye,
* Babu kwenye hile nyumba ndio nashuka mimi.
nikamwambia dereva wa tax tulipokalibia.
* ile nyumba nzuri
* ndio hapo hapo.
* Baba yako ananyumba nzuri.
* Nyumba ya mme wangu hiyo
*khaah wewe mtoto ulivyo na umli mdogo hivyo umeolewa.
* wewe babu usinichukulie powa mimi sio mtoto tukikutana ulingoni mimi na wewe unanikimbia utasahau hadi kuvaa boksa yako.
Nilimwambia vile yule derava tax akabaki kunishangaa tu maana. hatimae tukafika nyumbani kwangu dereva akanishusha harafu yeye akaondoka zake, sasa nikagonga Kengere Baada ya mda mrango mdogo ukafunguliwa
“Sikuamini macho yangu nilipo muona mtu aliye fungua mlango alikuwa ni mama yangu.
* Nikusaidie nini. mama akaniuliza hivo,,,,,
Sehemu ya 32
” Sikuamini macho yangu nilipomuona mtu aliyefungua mlango, alikuwa ni mama yangu,
* Nikusaidie nini, mama akaniuliza hivo.
“”SONGA MBELLE,
* Hahahah wewe kibibi unaniuliza mimi swali hilo kwanza nani kakuruhusu uingie kwenye nyumba yangu bila ruhusa yangu.
” Nikamuuliza vile mama huku nijitingisha tingisha kwa mapozi, nilikuwa tayari hata kupigana nae huku nimesahau kwamba nina mguu bandia na mkono bandia.
* Eti nyumba yako umeijenga wewe na nani au umepotea njia.
” Mama alikuwa anaongea kwa zarau mno tofauti kabisa na kipindi kile.
* Unajifanya jeuri ngoja nimpigie mme wangu aje.
” baada ya kusema hivo nikatoa simu kisha nikapiga namba ya Baba.
* Samahani mteja unaye mpigia hapatikani tafadhali jalibu tena badae,
Sauti ya mtandao ilisikiki kusema hivyo kila nilipo mpigia baba,
* vipi mme wako anasemaje.
mama akaniuliza,
* hebu nipishe niingie ndani mbwa wewe. nilimwambia mama huku nataka kuingia,
* Wewe weee Uingie wapi Tina usinichefue nakwambia hapa ni nyumbani kwangu hatimiliki za nyumba ninazo mimi naweza nikakufaya chochote kibaya tafadhali ondoka uniache kama nilivyo,
usichokonoe majeraha ya moyo wangu;
Mama alibadilika Ghafla akawa mkali kama mbogo.
na baada ya kuniambia vile akafunga mlango akaingia zake ndani.
” Mimi nilibakia getini kama mlinzi
“kila nilipopiga namba ya mme wangu ilikuwa haipatikani Hapo Sasa kichwa kikaanza kuchemka mdogo mdogo.
” Mh mama amesha pata hati ya nyumba.
mme wangu nae hapatikani, nilijiuliza hivyo.
huku nimesimama tu nje ya geti,
“wakati huo baba alikuwa kwa rafiki yake walikuwa wanaongea.
* Unajua Bandima wewe ulibadilika sana baada kuanzisha mahusiano na Tina. ulikuwa hushauliki
nashangaa leo unakuja kuniambia nikakuombee msamsha kwa mme wako.
* jamesi nakuomba unisaidie nimesha tambua kosa langu.
* mwana mke uliye mtelekeza akiwa katika hali ya upofu ukamfukuza nyumbani kwako,
kubwa zaidi ukachukua mtoto wake ukamuoa.
yani kiufupi mimi siwezi kwenda kukuombea msamaha maana utanisababisha niingie kwenye matatizo Bandima nenda mwenyewe.
* Niambie basi anaishi wapi niende nikaombe msahama.
* Yupo nyumbani kwako.
baba alipoambiwa vile alishituka.
* Nyumbani kwangu mimi.
* Ndio
baada ya kuambiwa hivyo baba aliondoka haraka kuelekea nyumbani wakati anavuka barabara mara Ghafla akagongwa na piki piki. watu wakamuwahisha hosipitali. baada ya kufanyiwa “vipimo ikaonekana kuwa amevunjika kiuno.
” wakati huo mimi nilikuwa nimeondoka nyumbani kwa mama nilikuwa naenda kwa rafiki yangu Zuu. Mara Ghafla simu yangu ikaita nilipokea haraka.
* Hellow Mme wako amepata ajari yupo hapa kwenye hosipitali ya mhimbili.
“baada ya kuongea vile yule mwanamke akakata simu.
Kama sio kuchanga nyikiwa basi nili changanyikana.
” mkosi gani huu jamani mimi nilijiuliza huku nasubiri barabara nipande iliniende huko mhimbili.
cha kushangaza kila daradara ikipita imejaza tu. ikabidi niite bodaboda nilipanda bodaboda baada ya mda tukafika mhimbili Lakini wakati nashuka kwenye bodaboda sijui ilikuwaje mara Ghafla muguu wangu wa bandia ukachomoka….
Sehemu ya 33
” Lakini wakati nashuka kwenye bodaboda Sijui ilikuwaje mara Ghafla mguu wangu ukachomoka….SONGA MBELLEE..
“Ooooh Mungu wangu mguu wa wangu umechomoka.
“nilisema hivyo huku nakaa chini maana nilikuwa siwezi kusimama bila huo mguu wa bandia.
* Pole dada kumbe unamguu bandia
“yule dereva wa bodaboda akaniambia hivo.
* Naomba unisaidie niingie ndani ya hosipitali nifungwe mguu wangu.
baada ya kumwambia vile yule mkaka akakubali aliniinua akanikokota hadi ndani ya hosipitali. Baada ya dakika 10 nilikuwa nimesha fungwa mguu ukawa powa.
* Kaka Tafadhali usimwambie mtu yoyote kama mimi nina mguu bandia iwe siri yako tu.
nikamwambia hivo dereva wa bodaboda mda
huo alikuwa anataka kuondoka,
* Usijari dada nitafanya siri Lakini nitakufata uniambie umepata wapi mguu maana kuna bodaboda mwenzangu alipatwa ajari akakatwa mguu.
* usijari kaka mimi nipo tu.
“baada ya kuongea kwa mda yule boda. akaondoka sasa nikachukua simu yangu nikapiga namba ya baba. punde akapokea mtu.
* Hellow mimi ni mke wa mtu mwenye simu hiyo aliyepata ajari naomba unielekeze yuko chumba gani.
nilijieleza hivyo.
” yule aliyepokea simu nae akanielekeza nilienda haraka nikaingia nikamkuta baba amelala kitandani.
* mh jamani mme wangu nini kimekupata
*Tina ni ajari tu Nakuomba umpigie simu mama yako aje anione.
“Baba aliponiambia hivo alinichefua.
mno.
* Mme wangu. unataka yule kinyonga aje kufanya nini hapa au unataka aje akukue kabisa,
hivi unajua kama amesha itapeli nyumba yetu
“hati za nyumba na magari zote anazo yeye. nimekwenda kule amenifukuza kama mbwa, “nilimwambia baba,
* Tina nakuomba mpigie aje hapa tuongee yaishe.
* Hapana mme wangu Sitaki simpigii na sitaki nimuone katika uso wa macho yangu”
* Tina usiseme hivyo unakosea mimi nataka anione tu.
* Mme wangu nimekwambia Mama hawezi kuja hapa nitakushughulikia mimi mpaka utapona.
* Samahani dada mda umeishi muache mgonjwa apumzike.
“Dokta alikuja akaniambia hivyo.
” Basi nilitoka Lakini nilitoka na simu zote yani simu yangu na simu ya baba,
nilifanya hivyo kusudi asije akampigia mama,
* unajua frenk dunia kuna mambo mengi yamejificha.
* kwanini unasema hivyo. Antonio.
* Leo wakati napita pita barabarani Si nikakutana na Tina. akaniita kisha akaniambia nimpeleke mhimbili. nikampakia tulipo fika,
” wakati anashuka mara ghafla akapiga kelele huku anasema mguu wangu umechomoka
Si kikaangalia sikuamini Tina anamguu wa bandia.
* Antonio achaongo bahna Toka lini Tina akawa na mguu wa bandia.
” frenk hakutaka kumwamini rafiki yake.
basi walibishana mwisho wa siku wakapotezea,
Lakini frenk aliliweka hakirini.
* Leo sijui nitalala wapi mh bora nikalale hotelini kesho nitatafuta nyumba ya kupanga,
Nilijiambia hivyo baada ya kutoka hospitali.
katika maisha niliyo kuwa naishi sikuwa na ndugu wa kalibu zaidi ya baba.
“ndugu na marafiki nilisha gombana nao
ila rafiki yangu Zuu. yeye aliniambia mpaka niachane na baba ndo urafiki wetu uendelee. Namimi siko tayari kwa hilo.
* ilikuwa ni majira ya saa tatu asubuhi nyumbani kwa mama maisha mazuri yalikuwa yanaendelea wakati ameketi mezani anakunywa chai na dada wa kazi. mara kengere ya getini ikalia.
* Amina hebu kafungue mlango.
mama akamwambia dada wa kazi.
kweli amina akainuka kisha akaenda kufungua mlango,
* dada hujambo.
* Sijambo shikamoo.
* Marahabaa vipi mama tina nimemkuta.
* Ndio yupo ndani.
* ok nenda ukamwambie Kwamba
“Mme wake Bandima alipata ajari siku ya jana
“kwa sasa yupo kwenye hosipitali ya mhimbili.
* ok sawa nimwambie nani kaleta taarifa hii.
* Mwambie Dokta benjamen.
baada ya kujitambulisha yule Dokta akaondoka zake.
Dada wa kazi nae alienda akamwambia Mama.
” Mama alipopewa habari hiyo,”kila kitu aliacha alichukua ufungoa wa gari kisha akatoka.
baada ya mda Mama akawasiri mhimbili alipofika akakuta watu wanasubiri kwenye beanch alipoangalia vizuri akaniona nimekaa kichwa chini.
wakati mama anapiga mahesabu yake.
Dokta akatoka chumba alicholazwa Baba,
* Mama tina au Tina kama yupo mmoja wapo aje
Dokta alisema hivo Nikainuka kiuchovu.
* Dokta mimi hapa ndio mama Tina.
Nilimsikia mama anasema hivo.
* basi ingia ndani
Mama alipoambiwa hivyo akapiga hatuo moja tu ili aingie Lakini nilimuwahi nikamvuta akarudi nyuma harafu nikamuuliza,
* Wewe maraya unakwenda wapi
“baada ya kumuuliza hivyo mama alichonijibu……
Sehemu ya 34
Wewe malaya unakwenda wapi Baada ya kumuuliza hivyo mama alichonijibu..SONGA MBELLE…
*kama mimi ni malaya basi hata wewepia ni malaya tu. sababu mtoto wa mbwa ni mbwa.
mama alinijibu hivyo huku ananitazama kwa hasira.
* mh vipi mama kwani huyu ni mwanao.
Doktar akamuuliza mama.
* Ndio ni mwanangu.
* Sasa hapa mbona mnanichanganya nani ameolewa kati yenu.
* Mimi dokta.
nilijiwahi nikajibu hivyo.
* Dokta mimi ndio mke wa halali wa Bandima tulifunga ndoa kabisa lakini huyu shetani alikuja akavunja ndoa yangu.
akanipofua macho.
Mama aliongea huku machozi yanamtoka.
” Wakati mama na doktar wanaongea Mimi nilipata nafasi nikaingia chumba alicholazwa baba.
* Mme wangu unaendeleaje jamani.
* Tina naendelea vizuri kidogo. lakini samahani najua nitakuuzi ila nisamehe nakuomba umuite mama yako aje hapa niongee nae japo maneno wawili tu.
” Baba aliniammbia hivyo.
* unaongea nae kuhusu nini.
* Nataka niongee nae kuhusu nyumba pamoja na magari yangu.
* Unataka kumpatia au unatakaje.
* Nataka akupatie wewe maana wewe ndio chaguo langu. baba aliponiambia hivyo nilifurahi sana nilienda kumuita mama. pale nilipotoka nje nikamkuta bado wanaongea na doktar Sasa nilichokifanya nilimvuta kwa nguvu adi akaingia ndani.
* Tina nakuomba uende nje maana ukikaa hapa tutapoteza kila kitu.
baba akaniambia hivo.
Basi nilitoka nje nikawaacha yeye na Mama.
* Mama Tina hebusogea hapa, Baba alimwambia Mama.
* Nimesogea nambie unasemaje.
* Mama tina nakuomba unisamehe sana najua nimekukosea najua nilikunyanyasa.
najua nimekuzalilisha. Lakini naomba unisamehe maisha yangu yapo mkononi mwako.
* Mme wangu mimi nilishaga kusamehe siku nyingi na nilijua kwamba ipo siku utarudi kwangu.
* Labda nikuambie ukweli mama tina Taalifa zote mlizo sikia kwamba nimevunjika kiuno za uongo. mimi mzima kabisa ila katika ile ajari niliumia kidogo tu.
Mama alipoambiwa ukweli alishangaa akajikuta anafurahia.
* jamani mme wangu unaseme kweli.
* Ndio mke wangu ila nataka unipeleke nyumbani ila Tina asinione
* usijari mme wangu, ngoja nifanye utalatibu , mama alijibu hivyo kisha akatoka nje akaondoka zake kabisa. Nilipomuona mama ametoka na mimi nikataka kuingia Lakini doktar akanizuia akidai kwamba mda wa kuona wagonjwa umeisha, Basi ilibidi niondoke ili nikamtafutie chakula baba Nilikwenda kwenye hotel niliyoweka kambi kwa mda nikaweka oda ya chakula.
kisha nikaenda kutafuta nyumba ya kupanga, mungu alisaidia niliweza kupata.
Sasa ilipofika mchana nikaenda kupeleka chakula hosipitali nilikuwa nampelekea Baba ambae ni mme wangu,
Nilipofika nikakuta habari za kushangaza.
* Dokta Nimemleta chakula cha mme wangu,
* Dada mme wako amechukuliwa na ndugu zake wamesema wanampeleka akatibiwe Sehemu nyingine hapa tumeshindwa,
* unasemaje Dokta mme wangu amechukuliwa.
* Ndio dada.
* Dokta aliponijibu hivyo hakika nilichoka mno. nikakaa chini kwanza nikafikiria Badae nikaondoka zangu nikarudi kwenye makazi yangu.
nilipofika tu.
* Dada tunakuomba uchukue kila kilicho chako uondoke maana tumepata wazungu wanataka kupanga mwezi mzima. Mfanya kazi wa hiyo hotel akaniambia hivo Sikuona tatizo sababu nilikuwa nimepata sehemu ya kuishi. nilichukua begi langu nikaondoka. mawazo yalikuwa yametawala kichwa changu Mara Ghafla nikajikuta nimepita njia ya wahuni. wakanipola begi langu ambalo lilikuwa na vitambulisho vyangu kadi ya bank pamoja na pesa.
kisha wakakimbia Nilipiga kelele za kusema mwizi watu wakaja wachache lakini hawakunisaida chochote zaidi ya kuniambia.
* kuwa makini dada hii ndio bongo. Basi nilienda hadi nilipo panga chumba kwa bahati nzuri nilikuwa nimelipa kodi ya mwezi mzima. nilifika nikaingia ndani nikaanza kulia kwa uchungu maana ile kadi ya bank ndio ilikuwa ni tegemeo langu. kibaya zaidi kadi hiyo nilipewa na baba tu nikaanza kutumia hata sijui alitumia mbinu gani kuipata, Tangu siku hiyo maisha yangu mapya maisha mabaya ya kaanza, Baada ya siku tatu Nikaanza kulala njaa maana nilikuwa sina kazi yoyote wakati mwingine Mama mwenye nyumba alinisaidia chakula.
Nilikuwa sina wazo la kutafuta kazi. mda wote nilikuwa namfikiria baba tu. Nilikonda kwa mawazo.
” Sikumoja nikaamua kwenda nyumbani kwa wazazi wa baba. Nilipofika nikagonga kengele getini Punde akafungua linzi.
* vipi dada nikusaidie nini,
* kaka mimi nimekuja kufuta mme wangu anaitwa, Bandima.
* Ooh bandima mtoto wa humu ndani
* Ndio.
* Alikuja hapa mida ya saa nne lakini amesha ondoka ameenda kwake.
* Kwake ni wapi.
” Yule mlizi akanielekeza nikagundua ni kulekule tulipokuwa tunaishi mwanzo.
Basi nikaondoka nikaenda mpaka nyumbani.
Nilipofika tu getini nikakuta gari nzuri ya kisasa imepaki pale nje mara Ghafla Nikamuona mama anatoka alikuwa amependeza mno wakati nashangaa nikakuona baba nae anatoka.
* Wewe kinyago umefata nini hapa.
Baba akaniuliza hivo. aki sikuamini kama baba anaweza kuniita mimi kinyago.
* Nimekufata wewe mme wangu.
* Nani mme wako hapa ety mke wangu huyu nae anamme.
* Namshangaa Mama akajibu hivyo harafu sasa akamkumbatia Wakaanza kunyonyana mate Live hakika niliumia sana nikatamani kuanzisha ugomvi lakini ngumu nikakosa. walipo maliza kungonyana sasa wakanifukuza nani avae koti la maumivu yangu nilitamani hata kujiua lakini moyo ulikataa.
Niliporudi kule nilipokuwa nimepanga chumba mwenye nyumba nae akanifukuza sababu kodi yangu imekwesha. Ukisikia mtu kaibeba dunia ndio mimi Sasa nikawa sijui pa kwenda. Niliteseka mno usiku ule nikalala kwenye mtalo kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani Wakati nimelala wakaja watu wakanichoma sundano ya ganzi harafu wakachomoa munguu wangu wa bandia.
asubuhi ilipofika nikaamka ile kujiangalia ule mguu wangu wa bandia ulikuwa haupo Hapo nililia kama mtoto mdogo watu walikuja wakanitoa mle mtaloni kwa bahati nzuri wengine walikuwa wananijua. ikabidi wanipeleke nyumbani kwa mama walipo nifikisha wakaelezea walipo nitoa.
Mama alikuwa hajui kama mimi nilishaga kuwa kilema alinionea huruma Mkali Sana Hakika damu nzito kuliko maji Mama akanipokea na kunisamehe makosa yangu. Hata baba nae pia aliporudi kutoka kazini nae alikuja akanisamehe.
Siku hiyo hiyo Mama akaninunula kigali cha walemavu wasio weza kutembea nikaanza kukitumikia.
Siku iliyofata baba na mama wakanipeleka kanisani nikatubu zambi zangu na kuokoka nikaanza kumtumika mungu,
MWISHOOO……..