
za Mapenzi, Maisha na Uchawi Mautundu Kitandani
PISI YA KIJIJI
EPISODE 1
Hadithi inaanza katika nyumba moja hivi ambako ndiko anakoishi kijana aliyejulikana kama kelvin . Alikuwa akitengeneza baiskeli tayali kwenda kuchukua mzigo aliotumwa na baba yake ..
Alikuwa akiimba nyimbo ambazo mimi sikuelewa zilikuwa ni nyimbo maana kingereza kwenye hizo nyimbo zilikuwa zakuunga unga sana yaani kiasi kwamba mpaka unajiuliza hiyo ni nyimbo ya kweli ama ni
remix.Haukupita muda mrefu sana
alikuja rafiki yake kipenzi aliyejulikama kama Gabriel.
walikubaliana kuwa wangeenda kufuata mzigo pamoja mara ghafla mama kelvin alimuita “weee kelviiiiiiiiiiii”. Kelvin alimwambia rafiki yake ama kweli sasa kumekucha na makucha yake . kisha akaitika
“namuuuuu mama nakuja ” basi aliondoka na kumuacha rafiki yake akitengeza ile baiskeli
“mama niko hapa ze gen dabo six “
mama alicheka na kuniambia “acha masihara yako”
kisha akasema “Haya nenda kanunue chapati mnywe chai kabla
ya kwenda alikilokutuma baba yako”. Basi kelvin alitoka spidi ya boxer mpyaaaaaaaaaaaa!!!! haikuwa mbali sana na nyumbani . lakini alipofika mbele kidogo alikuta watu wamekusanyika . Kama kawaida kwenye watu kuna mengi haya sasa kelvin ikabidi asogee aone pana nini pale.
Alibaki anacheka baada ya kugundua
kuwa ilikuwa ni vijana viwili waliokuwa wanapimana nguvu na kisa ilikuwa ni binti mmoja ambaye mtaa mzima hakuna asiyemjua ..
Aliitwa ” Lucy” tena usimuite lucy tu muite lucy “cha wote” yeye ni kusambaza upendo kwa wote uwe fom 1 twende uwe babu twende …..gusa achia twende kwao.
Mwenyewe huwa anasema anacheza namba zote Rafiki yake Gabriel aliwahi kumwambia
“lucy ni mtamu sana ,anajua kila stairi ya mapenzi. kama nikijaribu kwenda mimi na uoga wangu huuu kimoja chaliiiiiiii. Anakuwekea bango stand …. na waume za watu walikuwa wakimpenda sana . kutokana na
ufundi wake katika uwanja wa benjamini mkapa (,kitandani)
Sasa hawa jamaa sijuwi kwanini wamepigana nilomfuata jamaa mmoja na kumuuliza
“hawa kwanini wamepigana ??? .
jamaa alikuwa anaitwa cholo au ukipenda muite ,(MMBEYA WA MTAA, kipara wana man ) Alikenua meno yake na ilionyesha anafuraha maana domo limejaa umbeya kwa kumwagia ndo shida kelvin kayakanyaga maana aliwaza ule umbeya angemwambia nani ,?? na kwa kuwa nimejileta wacha nipewe material makali ….
” huyu jamaa mwenye ngeu usoni alipewa utamu na lucy jana saa mbili usiku , kelvin alimwambia
enhe !!!!(,ikimaanisha anataka udaku zaidi a.ka.a umbeya )
Cholo aliendelea huku akinyoosha kidole kwa mwingine baada ya kumulezea mmoja akasema
” huyu mwingine aliyevimba shavu huyu alipewa utamu na lucy saa nane usiku wote walikuwa hawajuani sasa leo asubuhi wapo kijiweni wanasimuliana kila mtu akimsifia mwanamke aliyelala naye wasijuwe mwanamke wanayemzungumzia ni lucy cha wotena unachokiona ndo kilichotokea” alimaliza huku akitabasamu sana. sio siri moyo wake
ulisuzika sana yaani ulikuwa ni
mwepesi sana baada ya kupata sehemu ya kutua umbeya wake …..
kelvin alijisemea “katika maisha yangu siwezi nikapigana sababu
ya pisi kali. Mademu wote hawa nigombane yanini nivimbe suramaisha yenyewe ndo haya haya’ akapiga mikono kisha akaondoka
Basi kelvin aliondoka na kwenda kwa mama olesta kununua chapati alifika
pale na hakukuwa na
mtu akajisemea hawa asubuhi wako wapi ………kisha akaita
.” mama olestaaaaaaaaaa! “
Sauti ilisikika kutoka ndani “nakuja ” lakini kelvin aligundua aliyeitika ni Olesta na sio mama yake
alOlesta ni binti ambaye
hawakupishana umri sana na kelvin na ni watu ambao hawana ushikaji. sio kwamba wamegombana ni basi tu. ni maisha kuna watu tunakua nao pamoja lakini hatuna mazoea nao kutokana na maisha yanavotaka tuishi hususana zikiwa ni jinsia mbili me na ke ….. twendeleee
“eeeeeeehe olesta mambo” “powa umeamkaje kelvin” “niko powa kabisa “
“umerudi lini toka chuo” “juzi tu jamani “
“kwa hiyo unajifungia tu ndani maana huonekani”
“hapana si unajua wazazi ” “oooh basi apo nimrkupata” “karibu sana kelvin “
” Asante naomba chapati olesta” “nikufungie ngapi kelvin”
“weka sita apo chapu”
” zote izo unakula wewe ” alikuwa
akimtania tu huku akiliachia tabasamu
……
“hapana ni za familia bhana “
“mmmmmmh acha uongo kelvin ” huku olesta akitabasamu …..
“nakuapia bhana namalizaje zote sita na zilivyo kubwa hivi”.
Olesta alimfungia chapati. kelvin alimshukuru na kuamua kuondoka
Alirudi nyumbani na wakanywa chai
chapu chapu i , na safari iliwadia walichukua baiskeli . na safari ilianza .
Na walitumia kama saa zima hivi, mwisho walifika walipokuwa wamekwenda.Basi walifanya walichotumwa na ikikuwa ni kwenda kukata ndizi katika shamba lao …
Lakini baada ya kukata na kufunga kwenye baiskeli walisikia kelele kutoka kwa mtu aliyekuwa karibu na shamba hilo ….
Alisema ” jamni msaada nmen’gatwa
na nyoka”
Basi waliacha ndizi kwenye baiskeli na kwenda kumkimbilia kujua nini kimetokea kumbe alikuwa ni baba yake Olesta ….
“baba pole sana ngoja
nikusaidie kelvin alichana shati lake na kumfunga sehemu ya juu aliyon’gatwa kama huduma ya kwanza
…..
Na kelvin alijaribu kufyonza sumu kidogo ili kumpunguzia mzee makali ya
sumu mwilimi mwake kisha baba
olesta alimwambia kelvin
“toa kwenye mfuko wangu wa nyuma
,nipe “kelvinalitoa simu na kumpa yule mzee..
mzee alipiga simu na ilikuja bodaboda baada ya muda mfupi na kumpakia .
kelvin alipanda naye akimtaka gabriel yeye arudi na ndizi mpaka nyumbani yeye ampeleke hospitali yule mzee
.Basi walifika hospitali na mzee
aliingizwa kwenye chumba cha matibabu.
lakini kelvin akiwa ametulia tulia kama maji mtunguni kwenye benchi moja karibu na chumba ambacho mzee yule alifanyiwa matibabu . Ghafla kwa
mbali alitokea binti mmoja mrembo sana na huyu ni nesi mpya katika hiyo hospitali.maana sura yake ni ngeni hapa jijini sio kwa wenyeji wa jiji hata kwa wageni pia ..
Ni binti mrembo sana ngozi
ukimtazama miguu yake aliyevaa raba nyeupe hakika mtoto mguu mdogo
hafu mweupe sio hivo tu .
Ukimtazama lipsi mtoto lipsi denda yaaan kwenye macho ndo
shida yalikuwa meupe hafu mazuri sana akikukonyeza unaweza kuuza shamba la urithi…
muda huo kelvin alikuwa hata hajagundua maana mawazo yake yalikuwa mbali sana.
Binti yule alipofika karibu na kelvin kumbe kulikuwa kuna maji
yalimwagwa hivyo kwa bahati mbaya aliteleza
“mamaaaaaaaaaaaaaaaa”. alipiga kelele kwa sauti
kelvin ile anashtuka binti anataka kuanguka
huwezi amini alimdaka kwa kumshika kiuno macho yao yakawa yakitazamana binti akiwa katika hali ya woga akawa kafumba macho lakini baada ya kushikwa kiuno alianza kuyafumbua taratibu na mbele yake alimuona kelvin. walibaki
wanatazamna katika pozi la mahaba
…..
PISI YA KIJIJI
EPISODE 2
basi tunaendelea pale tuliopoishia
srhemu ya kwanza baada ya kelvin kumpeleka baba Olesta hospitali na lile tukio la kelvin kumdaka yule nesi
…..
Basi hali ilikuwa vilevile kama tulivyoona ni baada tu ya kelvin kumshika kiuno yule binti kumbuka pale hawachezi dance bali alimsaidia tu asianguke.Macho yao yalizidi kutazamana na macho yanaongea zaidk kuliko mdomo . Kelvin alikuwa akijisemea toka “your beautfully kill all woman in this world for me(uzuri wako unawaua wanawake wote kwa ajili
yangu),hakika huyu binti ni mrembo
sana” huku akimtazama kwa tabasamu muda huo binti kauweka mkono wake mabegani mwa kelvin .
Lakini sio nafasi ya kelvin ndio ilizungumza tu pia hata nafsi ya binti nayo” jamaani ngeakua asingekuwa huyu handsome boy, mmmmh mkaka huyu leo amekuwa kama malikia mlinzi kwangu” huku naye akamtazama .Mara ghafla alishtuka baada ya kusikia watu wakiita ” kelvin!
,kelvin! ,kelvin! “.Hapo
ndipo wakaachana maana mawazo yaliwapeleka dunia nyingine ,dunia tamu yenye kumfanya kila mtu ahisi furaha na amani.
Olesta naye alifika lakini alionyesha kutopendezwa na kelvin kumshuka kiuno yule binti alikasirika sana maana yeye tukio aliliona toka mwanzo
,alivomdaka alivomshika kiuno na walipotzamana. yeye muda wote huo alikuwa amesimama mlangoni…
“mwanangu kelvin ” alisema mama olesta
“namu mama yangu” “baba olesta yuko wapi”
“anafanyiwa matibabu ya haraka ndani”
“mi huwa na mwambia shambani vaa buti ,ila ubishi ndo umemponza”
“pole sana mama “
“Asante sana kwa msaada mwanangu”
Basi yule nesi alimsogelea kelvin na kumwambia
“Asante kelvin nahisi bila wewe ningeumia vibaya”
“usijali tupo pamoja “
binti akamka kelvin mkono kelvin
aliupokea na wakashikana kila mmoja akiwa anatabsamu akimtazama mwenzako.
Hali hiyo ilizidi
kumkasirisha Olesta na aliukunja uso kama ngumi ya mtoto … ..
Yule nesi baada ya yale mazungumzo akawa anaondoka zake . lakini kelvin alikumbuka hakumuuliza jina yule binti alisema kwa sauti kubwa
iliyofanya watu waliokuwa eneo la
karibu washtuke “dada samahani “
Binti aligeuka kwa mapozi na kuachia tabasamu “bila samahani kelvin “
kelvin alimtazama na kukuta nywele za binti zinataka kumfunika uso alizishika na kuzipanga vizuri…
Muda huo binti anajisemea ” huyu kaka ujue smuelewi hafu haoni watu
hapa kweli ana nini lakini”. kelvin
alimsogelea zaidi mapigo ya moyo yanadunda “puuuuuuuuh puuuuh” kijasho chembamba kikimshuka
.Huwezi amini kelvin alimsogelea kama anataka kumpiga kiss mpaka binti akafunga macho na kujiziba sehemu ya mdomo ili asije akapigwa busu bila sababu yoyote ile …..
Lakini cha ajabu kelvin alimfuta vumbi nyuma ya shati lake na kusema
“ujuwe kwa uzuri ulionao inatakiwa
ujiangalie kwenye kioo mara tano kabla ya kuja kazini ,unatazamwa na wengi” Binti alitabasamu na kusema
“kweli eeeh”
kelvin alimjibu “ndiyo lakini hata hilo tabasamu lako jaribu kulificha ,maana wakiliona wengine watapagawa zaidi yangu”
olesta hakusikia kilichozungumzwa lakini alikuwa kanuna muda huo mama yake kaenda kumtazama
mumewe baada ya huduma ya kwanza
…
Kelvin kabla hajaongea kitu kwa yule nesi lilisikika jina likiitwa “mariamu
” yule binti alisema “nakuja” ndipo kelvin akagundua kuwa yule binti anaitwa mariamu. Mariamu aliondoka mbio mbio lakini kila mara aligeuka kumtazama kelvin hali hiyo ilizidi kumkasirisha Olesta ……. kelvin alirudi alipokaa olesta na kumuuliza ” mbina unaonekana na wasiwasi??
“hapana niko sawa chapati sita”
“mmmmh nilikwambia za familia “
“sawa chapati sita ” Olesta alikuwa akimtania kelvin . ilibidi kelvina aanze kucheka then akaachia smile moja ambalo lilimfanya Olesta mawazo yaende mbali sana.
Alikuwa ni mtu mwenye kitu kizito alichokibeba moyoni mwake alizidi kumtazama kelvin alnavyocheka …..
Mara ghafla akaja mama yake na kusema “wee Olesta hutaki hata kumuona baba yako.? haya twende nyumbani na kelvin mkokote mzee hadi kwenye pilipiki apande mpaka nyumbani “. Basi kelvin alifanya hivyo…..
kama alivyoeleza lakini kipindi anamkokota yule mzee ghafla alikutana macho tena na mariamu aliyekuwa kaenda katika dirisha la
mapokezi kuchukua chaja ya simu
yake ….
kelvin alimwangalia sana yule binti huku akimkokota mzee ghafla alipamia na daktari mmoja maaarufu ambaye hakuna mtu asiyemjua daktari huyo kutokana na umaarufu wake wa kazi yaani ilikuwa mgonjwa hata aje na ugonjwa upi lazima atafute namna mpka amsaidie hivo alikuwa ni
kipenzi cha kijiji ….
Alikuwa ni daktari mstaarabu sana
,anayejali wagonjwa mpole na mnyenyekevu sio hivyo tu ni mchapakazi na mpambanaji hivyo anastahilo maua yake kabisa
Basi kelvin alisema “samahani daktari kwa usumbufu wangu ” kwa sauti ya unyenyekevu lakini daktari alimjibu “usijali kuwa na amani mzee afike salama basi nilimpakia kwenye pikipiki na kumpeleka mpaka kwake
Basi kelvin alirudi na kumsimulia rafiki
yake Gabriel ishu ilivokuwa
“yaani Gabriel yule mtoto nahisi akijamba ,ambulance ipo mlangoni kumpeleka hospitali ni karembo kanavitua tumacho twa kusinzia hiki ni zaidi ya chombo “
” mmmmmmh kaka unamsifia sana huyulo demu usikute wa kawaida tu ” alisema Gabriel
“Gabriel tema mate chini , tema mate chini ile pisi sio mchezo mchezo wewe
. unadhani mtaani hapa kuna
anayemgusa …sijaona broooh”
Basi walipomaliza maongezi kila mtu alirejea kwake basi majira ya jioni mida ya saa kumi na moja na nusu . Gabriel alielekea sokoni kuchukua chochote kitu . Alifika kwa mangi na
kuchukua nyanya kabla hajaondoka alisikia sauti nzuri nyuma yake ikisema
“mangi naomba nyanya …….” sauti
ilikuwa nzuri ilimfanya Gabtriel ageuke na alipigwa na butwaa baada
ya kumuona yule mwanamke alisema “she is so beautfully” (ni mzuri jamani )
ALliendelea
“toka nimefika matema, nimekutana napisi kali nyingi ila hii ni moto
yaani maana halisi ya pisi kali ni hii macho ya Gabriel yalitazama miguu ya yule binti aliyevaa raba nyeupe hakika miguu ilikuwa ni mizuri halafu myeupe sio hivo tu akatazama lipsi mtoto lipsi
denda yaaan kwenye macho ilikuwa ni
shida yalikuwa meupe hafu mazuri sana akikukonyeza unaweza kuuza shamba la urithi….LAKINI
kumbe mwanamke aliyemuona ni mariamu nesi aliyekutana na kelvin asubuhi
PISI YA KIJIJI
EPISODE 3
Tunaendelea palepale tulipo ishia ambapo Gabriel baada ya
kukutana na mariam na kuonyesha dalili zote za kumtamani na kuvutiwa naye bila kujua ni mwanamke ambaye kelvin kila mara anamuimba kama wimbo wa taifa. Basi
alimsogelea kama ilivyokwa wanaume wengi na waliweza kuzungumza kidogo
“mama mrembo”
“poa habari yako” alimjibu kawaida tu
“ooooh nakuona jioni unafanya
manunuzi”
“yaaah si unajua muda wa mapishi”
“oooh jamani nahisi chakula chako kitamu kama ulivyo uzuri wako”
mariamu alicheka kwa aibu na kusema “mmmmmh ata mi sijuwi kupika “
“acha kunitania kwanini usijuwe ” “kweli kaka l sijuwi nakula ili niishi”
“okay sawa unaishi wapi”
“mmmmh Gab una maswali mengi mengine nitakujibu tukionana”
“so naweza nikapata namba yako” “noooooop huwezi “
“kwanini jamani sistahili au”
“hapana unastahili lakini sio haraka ivo”
“ujuwe naogopa mwenzako”
“unaogopa nini tena “aliuliza mariam kwa mshangao
“ukisubiri embe liive wenzako wanakula na chumvi”
mariam alicheka na kusema “sio kila embe litachumwa kaka mengine subiri yakomae kwa heri” kisha akaondoka zake
Gabriel hakusita kuendelea kumtazama yule mrembo yaani hatua aliyopiga kwa kelvin ilikuwa ikimtanya asichoke kumtazama na alijisemea “nitampata tu huyu binti nachojikubali muda ni shahidi wa kweli”
Baada ya binti kuondoka naye aliamua kuondoka lakini kipindi anaondoka alikuwa kadata kwanza kasahau nyanya gengeni …
Pili,alikuwa kama kadata basi muda huo na olesta alifika na alipoona Gabriel kasahau vitu alimuita sababu anamfahau kwa muda mrefu sana ” Gabriel, Gabriel,Gabriel”.Gabriel aligeuka akakumbula kumbe alisahau vitu pale alirudi na kubeba vitu
“Gabriel umeanza lini kusahau vitu???”
“mmmmh bahati mbaya olesta ” “ooooh uwe makini basi “
“okay asante nashukuru Gabriel” Kisha Gabriel akaondoka zake…….
UPANDE WA KELVIN
Majira ya usiku kabisa kelvin katulia zake hana hili wala lile kivlchwani mwake inamjia taswira ya mariamu tu . toka walipokutana walipozungumza moment zote tamu za mapenzi..
Alicheka sana na kusema kesho
nitakuja tena ……Hajakaa sawa akakumbuka alivomdaka na walivotazamana yaani sio kadata. kelvin kawasha data ya mapenzi hajuwi nini Afanye …..
UPANDE WA MARIAMU
naye anakumbuka tukio hilo hilo la kudakwa na kelvin na jinsi kelvin alivyomsogelea zaidi alijisemea “aisee kuna wanaume jasiri sana, yaani haoni
hata aibu mbele za watu ananishika
kiuno mmmmmh au yule kaka ni playboy akapiga makofi ya
kusikitika kisha akaweka mikono shavuni . Akakumbuka tena kipindi kelvin anaondoka na baba olesta alivyokuwa akimtazama kwa macho fulani hivi alijikuta olesta anajiziba na mto kisha anacheka pekeee yake …..
UPANDE WA GABRIEL yeye alikuwa bize anaosha vyombo na alipoanza kukata nyanya tu .Nyanya moja iliweza
kuanguka alipoiokota akili ilimpeleka
palepale kwa mangi alipokutana
na mariam ambaye hajajua mpaka leo kuwa rafiki yake kelvin huyu binti ndio amuimbaye kila siku kakosa beat tu … alijisemea “ikiwa bado tunaishi nitakutafuta mariamu wewe umenikaa hapa ningekuwa msanii ningekuimbia kila wimbo ujue umenibamba kinoma. aliendelea na kazi zake
UPANDE WA OLESTA
Olesta yeye hakuwa na mawazo sana
zaidi zaidi alikasirika lile tukio la kelvin kumshika kiuno mariamu. “yaani kelvin mbona huniheshimu mimi wala hisia zangu najuwa sijawah kukwambiya nakupenda lakini sometimes jiheshimu unapomshika kiuno mwanamke mwengine mi naumia sana huwezi amini alikuwa mpaka anatoa machozi. duuuh hali hii inatisha sana kwa huu mlolongo wa
mapenzi inaonyesha huko mbele kuna vita ya tatu ya dunia ya mapenzi kati ya kelvin na Gabriel , Olesta na Matiamu
SIKU ILIYOFUTA
Majira ya asubuhi na mapema kelvin aliamka na kwenda kuchota maji kwenye bomba iliyokaribu sana na kina Olesta . Olesta kumuona kelvin
kabeba ndo akajifanya naye kuchukua ndoo na kwenda kuchota maji ilimradi amuone kelvin na hata ajaribu kuzungumza naye .nyie nyie mapenzi….
Basi alipofika pale bombani hakuweza kumuona mtu yoyote yule alijiuliza “
kaenda wapi tena huyu kaka” . Si sasa
hivi alikuwa hapa jamani daaah” alikuwa akitazama pande zote lakini hakuweza kumuona mtu zaidi zaidi ni wapita njia ….
Ghafla sauti ilisikika nyuma yake ilikuwa ni nzito kidogo lakini Olesta alitambua ni ya nani “unanitafuta mimo au ???” olesta alishtuka na kugeuka taratibu huku kashila kifuani karibu na moyo wake maana sauti ilikuwa kama imemshtua ……..