PENZI LA KILAZA NA MWALIMU WAKE
PART: 09
ILIPOISHIA,
“Liwalo na liwe, kama nitafukuzwa shule nifukuzwe lazima kieleweke kati ofisini humo
Nilimuona kwa macho yangu akiwa na mpenzi wangu bila shaka yoyote, atakuwa anajua alipo. Hata kama hajui, nitamkomesha aache kabisa.” Sofia alitamka huku mwili mzima ukiwa unamuwasha kupigana.
Alichomoka darasani, huku uso ukiwa umejikunja kwa hasira kisha..
SONGA NAYO. ..
Wakati anaendelea kupiga hatua kuelekea ofisini kwa Madamu Eliza, gafla Sofia alimuona mama Kilaza akiwa anaelekea ofisini ndipo alipostuka.
Alisimama na kuganda mithili ya chuma na sumaku huku usoni mwake akijihisi aibu kali sana kama baba aliyekamatwa akiiba kiporo cha mtoto.
Pembeni mwake kulikuwa na kipande cha karatasi ndipo alipokiokota kisha akaelekea shimo la taka.
“Mama mkwe kaja kufanya nini?” Alijiuliza huku akichungulia lakini hakupata jibu.
Baada ya mda kidogo, alirejea darasani huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi mithili ya malaya aliyesubiri majibu ya vipimo vya UKIMWI.
Wakati mambo yakiwa hivyo kwa Sofia, huko ofisini Mama Kilaza alikaribishwa kisha akaelekezwa kwa mwalimu wa zamu ili kutoa shida yake.
“Shikamoo mama:” Mwalimu wa zamu alimsalimu huku.akiwa ameshika kalamu na karatasi.
“Marhaba za kazi…”,alitamka
“Ni nzuri karibu tukusaidie…” alimwambia huku akiwa amekaa mkao wa kusikiliza.
“Asante. Nimekuja kuulizia juu ya kijana wangu Kilaza ambaye aliaga kuwa anaenda kusoma na wenzake sijui TUITION lakini mpaka sas hajarejea nyumbani”
“Hee!, sisi hatuna masomo ya jioni…wala hatuna taarifa yake. Ngoja nikaulizie darasani kwake na kama hatoonekana basi tutalifikisha kwa mkuu wa shule tuone tunafanyaje” Mwalimu wa zamu alitamka.
“,Asante sana…” aliitikia.
Mda huohuo, Mwalimu wa zamu alielekea darasani huku akiwa ameshika fimbo mkononi na kumuulizia Kilaza lakini hakuna aliyetoa taarifa ya wapi alipo Kilaza.
Taarifa hiyo, Mwalimu aliifikisha moja kwa moja mpaka kwa mzazi ambaye alielekezwa kwenda kwa mkuu wa shule ili kupata usaidizi wa ziada.
Akiongozana na Mwalimu wa Zamu, Mama Kilaza alieleza tukio zima ndipo mkuu wa shule alipostuka huku kwa mbali wakihisi kakutwa na baya jambo.
” Nenda kagonge kengere wanafunzi wote waje (,parade)” mkuu wa shule alitamka.
Mda huohuo, kengere ya dharura alilia ndipo wanafunzi wote pemoja na stafu nzima ya walimu walipokusanyika.
Bila kupoteza mda, mkuu wa shule alitangaza kupotea kwa Kilaza katika Mazingira ya kutatanisha na yeyote mwenye taarifa naye ajitokeze ili kujua wapi alipo.
Taarifa hiyo ilimshutua sana Madamu Eliza ambaye alikuwa anajihisi uchovu kwa shughuli nzito aliyoifanya.
“Mama yangu!, nitakuwa wa nani mie!” Alijisemea kimoyomoyo huku akiwa ameshika tama.
Baada ya zoezi la kumpata Kilaza kuonekana gumu, mkuu wa shule alimwambia Mama Kilaza arudi shuleni mara baada ya siku tatu huku zawadi nono ikitangazwa kwa yeyote ataķayemuona Kilaza.
Mama alirejea nyumbani, huku Sofia akijikuta analia peke yake mara baada ya taarifa ya kupotea kwa Kilaza.
Mda huohuo, akiwa kama mbongo aliyejeruhiwa kwa mshale, aliondoka darasani huku wanafunzi wenzake wakiwa hawaelewi nini kimemsibu.
Moja kwe moja huku mkononi akiwa ameshikilia kipini kilichokuwa na ncha kali, alifika ofisini kwa Madamu Eliza ambaye alikuwa anajiandaa kuomba ruhusa kuondoka kisha akagungua mlango uliokuwa umeegeshwa.
Aliingia ndani kwa haraka kisha akamvamia Madamu na kuanza kumdunda ngumi,
“Uache tabia ya kutembea na mpenzi wangu!, unikome kuanzia leo…, jitu zima huna adamu…uache! ..uache!” Sofia alitamka huku akimdunda ngumi.
Madamu Eliza alitafuta upenyo lakini Mlango tayari Sofia alikuwa ameshaufunga ndipo alipoamua kujibu mashambulizi….😂😂…
JE ILIKUWAJE?
PART: 10
ILIPOISHIA,
“Uache tabia ya kutembea na mpenzi wangu!, unikome kuanzia leo…, jitu zima huna adamu…uache! ..uache!” Sofia alitamka huku akimdunda ngumi.
Madamu Eliza alitafuta upenyo lakini Mlango tayari Sofia alikuwa ameshaufunga ndipo alipoamua kujibu mashambulizi….😂😂…
SONGA NAYO…
Madamu Eliza akiwa ameshapokea ngumi moja ya usoni iliyomfanya ajisikie kizunguzungu, alijitutumua kwelikweli kwa kutanga kumn’gata Sofia kwenye ziwa lake la kushoto lakini aliambilia ngumi ya usoni iliyomuangusha chini mithili ya vipigo anavyopokea Mandonga.
Wakati anadondoka, aligonga kichwa chake juu ya meza na kubinuka nayo hali iliyomuogopesha Sofia aliyekuwa amechachamaa kama kiboko kwenye hasira.
“Ole wako nije nikusikie umetoa taarifa yoyote ile!, tutafukuzaa wote..” Sofia alimtahadharisha.
Taratibu huku kwa mbali hasira zikiwa zimepungua, alifungua mlango kisha akachomoka ofisini haraka na moja kwa moja akaelekea maliwatoni ili kujisafisha.
“Nimempatia dozi yenyewe!, ..” alijisemea mwenyewe huku akiendelea kujisafisha.
Baada ya mda kama dakika 5 hivi, Madamu Eliza akiwa amechafuka kwelikweli, alinyanyuka huku akiwa amejawa na hofu kubwa kisha akajifutafuta.
Aliwaza kutoa taarifa kwa mkuu wa shule lakini aliogopa Sofia asije toa siri juu ya Kilaza.
Alitikisa kichwa chake kisha akaamua kwenda kwa mkuu wa shule huku akiwa amevimba uso.
Baada ya kumuona, mkuu wa shule alishangaa na kushtuka kisha akamuuliza,
“Hee!, Madamu umekuwaje?” Aliuliza kwa mshangao huku akiwa ametoa macho.
“Nimeteleza na kudondoka ofisini…::,Madamu alijibu kwa sura ya wasiwasi.
“Hee!, pole sana….umeumia kweli..” mkuu alitamka.
“Sasa nilikuwa naomba ruhusa nikapumzike nyumbani maana najisikia kizunguzungu..: Madamu alitamka.
“Haina shida kama kesho hutopata nafuu basi utarejea kesho kutwa…”
“Asante. ..”,Madamu aliishukuru kisha akaelekea ofisini mwake ili kubeba mkoba wake na kuondoka.
Baada ya dakika kama 5, alianza safari ya kuelekea nyumbani kwake huku akiwa ana hasira juu ya binti Sofia.
Akiwa sebuleni anaangalia movie, gafla alisikia mtu anagonga mlango ndipo Kilaza alipostuka na kubaki ameganda kama maji ya mtungi huku akisikilizia.
“Nifungulie…” Madamu Eliza alitamka.
Moja kwa moja Kilaza aliipata sauti ya Madamu ndipo alipofungua mlango.
Alimtizama na kubaki na mshangao mkubwa huku Madamu Eliza akitaka kumwaga chozi.
“Hee!, mpenzi wangu umepatwa nini?” Alimuuliza kwa mshangao.
“Niache kwwnza nipumzike maana nina hasira…: “,alitamka
“Hee!, kulikoni!, niambie basi…”,Kilaza alitamka huku akiwa na hamu ya kujua nini kimemsibu.
Madamu Eliza hakujibu wala kuongea chochote kile kisha akaelekea bafuni kuoga.
Baada ya kumaliza kuoga, alikwenda kitandani kisha akajipumzisha ndipo Kilaza alipomfats hukohuko.
“Baby…nyongo mkalia ini langu niambie basi…”
“Nilikuuliza unamahusiano gani na Sofia?, alimuuliza.
“Sina mahusiano yoyote!, kwani kumetokea nini?”
“Naomba uwe mkweli, …”
“Yaani Sofia wala sina uhusiano naye. Mimi nakupenda wewe kwa moyo wangu wote…” alimwambia.
“Sasa kanivamia ofisini mwangu na kunipiga na kitu kizito usoni…”
“Hee!, amepata wapi ujasiri wa kumpiga mwalimu?, kwahiyo wamemfukuza shule?”
“,Sijatoa taarifa yoyote kwa lengo la usalama wako na wangu…”
“Usalama upi wakati amekuumiza hivi?”
“Leo mama yako kaja kutoa taarifa juu ya kupotea kwako na mkuu wa shule ametangaza donge nono kwa yeyote atakayetoa taarifa juu yako”
“Hee!, imekuwa hivyo tena!” Kilaza alitamka kwa mshangao
“Mpaka najihisi kuchanganyikiwa maana sijui nifanye nini..”
“Usiogope lazizi wangu, nitayamaliza na wala hakuna kitakachotokea…”
“Utayamalizaje …?” Alimuuliza huku akiwa ameshika tama.
“Hii ni suala dogo wala lisikuumize kichwa…ila nimesikitika kwa kitendo ulichofanyiwa na Sofia. Nitamfanyia kitu kibaya sana” Kilaza alitamka huku akiwa anampapasa Madamu kwenye mapaja yake.
“Sorry nakupenda sana lakini naomba uende nyumbani…ili nipumue kidogo maana naogopa sana ikija kugunudulika’
” Kwahiyo mpenzi wangu unanifukuza?” Alimuuliza huku akiwa amemuangalia kwenye mboni ya jicho lake
” Sikufukuzi lakini…” alitamka kwa kukatisha maneno.
” kwakweli niwe mkweli, siwezi kuishi hata dakika 5 bila kuwa na wewe, nipo tayari kuacha shule au kufukuzwa lakini siwezi kukupoteza…” Kilaza alitamka kisha akataka kumpiga busu la kifuani Madamu Eliza
” Hee!, unasema…!” alitamka kwa mshangao mkubwa kisha….
PART: 11
ILIPOISHIA
” kwakweli niwe mkweli, siwezi kuishi hata dakika 5 bila kuwa na wewe, nipo tayari kuacha shule au kufukuzwa lakini siwezi kukupoteza…” Kilaza alitamka kisha akataka kumpiga busu la kifuani Madamu Eliza
” Hee!, unasema…!” alitamka kwa mshangao mkubwa kisha….
SONGA NAYO….
“Kama ulivyosikia, siwezi kuishi bila wewe nipo tayari kuacha hata shule lakini siyo kukupoteza wewe kipenzi cha moyo wangu, Nyongo mkalia ini langu…. Nakupenda.”Kilaza alitamka kwa sauti ya mkwaruzo mithili ya redio iliyotafuna kanda.
“Utaniletea matatizo makubwa sana. Please and please!, nakupenda sana kuliko unavyodhani na nipo tayari kuwa mke wako maana umri ni namba tu kama ilivyo kwa Harmo na Kajala lakini kwanza hili liishe tena kwa mda huu..” Madamu Eliz alitamka huku akiwa amekunja uso kwa mbali.
“Basi sawa kama hunipendi mimi naenda kujinyoga nikutakie kila la kheri maishani mwako..” Kilaza alitamka huku akitaka kuamka kitandani hapo.
“Baby…Baby!, usifanye hivyo..nakupenda sana. Nakuomba tu….: ” Madamu alitamka huku akiwa ametoa macho.
“Sasa kwanini unanifukuza kama wananipenda?” Alimuuliza
“Hapana sijakufukuza lakinj msako unaoendelea kukutafuta ni mkubwa sana . Kibaya zaidi Sofia ni kama anajua wapi ulipo ndo kinanigopesha…”
“Sasa sikia nikwambie na nikutoe hofu, kesho ukienda kazini, tutaongozana huku ukidai umenikuta mtaani nazurura…”
“Halafu,…!” Alitamka kwa mshangao.
“Hapo najua mkuu wa shule atataka kunipa adhabu nami nitakataa na nikishakataa atanifukuza …” Kilaza alitamka
“Mhh..kwahiyo hutaki kuendelea na shule tena”? Alimuuliza
“Sitako kabisa!, inanipotezea mda maana sielewi chochote..”
“Mhh haya lakini….” Madamu aliguna.
Kesho yake mnamo mida ya saa 3 ya asubuhi, Kilaza aliongozan na Kipenzi chake kuelekea shule huku akiwa amemfunga kamba mkono mmoja mithili kuku mgeni kutoka shamba.
Baada ya kukaribia shule, Madamu Eliza alianza kuwa na uso wa hasira ili kumuaminisha mkuu wa shule
Hatimaye Kilaza alifikishwa ofisini kwa mkuu wa shule ndipo mkuu alipobaki na mshangao huku akiwa haamini.
“Hee! Madamu umemtoa wapi huyu mtoto jeuri..!”
“Nilipata taarifa kuwa yu mtaani anazurula ndipo nilipowaandaa vijana na hatimaye wamemkamta..” alitamka
“Wewe!, piga magoti…piga magoti…”,Mkuu wa shule alimuamuru
“Nipige magoti kwa kosa lipi?” Kilaza alitamka
“Nitakuumiza wewe dogo!, hivi unanifahamu vizuri!, ngoja kwanza nieapigie wazazi wako ” Kwa hasira mkuu wa shule alitamka kisha akampigia simu mamaye juu ya kuonekana kwake.
Mda huohuo Mama Kilaza ambaye alikuwa anajiandaa kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa , aliwasili shuleni hapo huku hasira zikiwa zimempanda.
Baada ya kuona mama mkwe wake, Madamu Eliza alijihisi aibu kwa mbaaali..lakini alijikaza kisabuni ili kutunza siri.
“Mama tumekuita hapa, mwanao huyu hapa kaletwa na mwalimu ambaye amemkuta anazurula mtaani. Sasa tunaenda kutoa adhabu mbele yako na mbele ya wanafunzi wenzake!,viboko 6 vya nguvu ili iwe fundisho kwake na wengine…” alitamka
“Nami nitamuongezea adhabu yangu!, sijalala siku ya pili hii…:” Mama Kilaza alitamka.
Baada ya mda mfupi, mkuu aliagiza kengere kungongwa ili kutoa adhabu kwa Kilaza,
Mlio ulisikika kila kona kisha kisha wanafunzi wote wakakusanyika.
Akiwa amesimama ( parade) Sofia alimuona Kilaza akiwa mbele huku mkuu wa shule akiwa ameshikilia bakora.
Aliwatangazia na kuwaonya wote wenye tabia ya kutoroka shule kama Kilaza, watapata adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.
Baada ya kauli hiyo, alimuita Kilaza asogee mbele ili apokee bakora.
Kilaza akiwa ameweka mikono mfukoni huku akiwa kama anatafuna (bigijii), alisogea ndipo wanafunzi wenzake walipokaa kwa kutoa macho kuona nini kitatokea kwa Kishoka huyo.
“Inama shika viatu..nasema shika viatu!, ” mkuu wa shule alitamka.
Kilaza alugeuza shingo lake kisha akamtizama mkuu wa shule kisha akaweka mikono mfukoni na kuanza kuondoka kwa madaha mithili ya kinyonga atembevyo hata akiwa hatarini.
“Woyo…woyoo..!, Kilaza. ..Kilaza” Wanafunzi walishangilia shule nzima huku mkuu wa shule asijue cha kufanya mda huo….
PART: 12
ILIPOISHIA,
“Inama shika viatu..nasema shika viatu!, ” mkuu wa shule alitamka.
Kilaza alugeuza shingo lake kisha akamtizama mkuu wa shule kisha akaweka mikono mfukoni na kuanza kuondoka kwa madaha mithili ya kinyonga atembevyo hata akiwa hatarini.
“Woyo…woyoo..!, Kilaza. ..Kilaza” Wanafunzi walishangilia shule nzima huku mkuu wa shule asijue cha kufanya mda huo….
SONGA NAYO….
Mkuu wa shule hakuamini kile anachokiona ndipo alipowaamuru wanafunzi kurejea darasani huku akiwa amejawa na hasira kali sana mithili ya mtu aliyemeza nyuki.
“Mama..nadhani umejionea mwenyewe! Mtoto ni mtovu wa nidhamu kiasi cha kupitiliza. Kama shule na kwa mamlaka niliyonayo, basi ninamfukuza shule mpaka hapo bodi itakapokaa” alitamka huku akiwa anaandaa barua.
“Msamehe maana watoto hawa wana mengi..” Mama Kilaza alitamka huku akiwa anataka kumwaga chozi.
“Kwa kitendo alichokionesha, hakuna msamaha wowote. Hii ni taasisi inayoongozwa kwa kanuni na taratibu” alitamka kisha akampatia barua.
Mama Kilaza aliondoka huku moyo wake ukiwa umejaa makunyanzi.
Baada ya kufika nyumbani, huku akiwa amejawa na hasira, moja kwa moja alikwenda mpaka chumba cha Kilaza lakini hakufanikiwa kumkuta.
“Huyu mtoto..huyu mtoto labda kama sikumzaa mimj” alitamka.
Mnamo mida ya jioni, Madamu Eliza alirejea nyumbani kisha akamkuta Kilaza anaangalia Tv ndipo walipokumbatiana,
“Sikuwahi kuamini kama una ujasiri wa namna hii” Madamu alimwambia.
“Yaani na hapo nilimuheshimu mama tu ila…” Kilaza alitamka huku akitabasamu.
“Nasikia mkuu wa shule amekufukuza shule mpaka bodi itakapokaa na haijulikanj itakaa lini..”
“Hilo halina shida kikubwa kipenzi changu upo…” Alitamka.
“Sasa unatakiwa kukaa ndani humu hasa chumbani ili usionekane maana itakuwa balaa”
“Si nimeshafukuzwa,.. hata nikionekana haina shida japo nitajitahidi sana..” alitamka.
Mnamo mida ya usiku , wawili hao walikwenda kulala ndipo kama kawaida yake Kilaza alipoanza kumuimbia nyimbo laini huku akimtomasa mithili ya mnunuzi wa parachichi.
“Baby unajisikiaje?” Kilaza alitamka huku akiwa anabinya ziwa la Madamu taratibu
“Mhh…niache kwanza maana nipo siku za hatari baby…” Madam alitamka huku akiwa anahema kwelikweli.
“Kwani unaogopa nini?” Alimuuliza
“Sitaki kupata mimba kwa wakati huu..”
“Usijali hutopata…” Kilaza alitamka.
“Basi siku nyingine maana naogopa kweli..”
“Mbolea nitaimwagilizia kwa nje hivo haina shida…” Kilaza alitamka
:Mhh..kweli…!”
“Ndiyo baby usijali…”
“Haya ila ufanye hivyo…”
Baada ya kauli hiyo, ukimya ulitawala huku Madamu Eliza akijihisi msisimko mkali sana kiasi cha kumkumbatia Kilaza huku akiwa kama anataka kumn’gata hivi.
Kumbatio hilo lililoambatana na miguno laini la kimahaba, lilimfanya Kilaza kujikuta anamwagilia mbolea ndani bila kujua na aliposhtuka tayari alikuwa amechelewa.
Madamu Eliza alikosa uvumilivu kisha akajikuta anatamka,
“Baby…taamu”
Kauli hiyo ilizidi kumchanganya Kilaza.
Wakati mambo yakiwa hivyo, huko shuleni Sofia aliendelea kumpiga tarehe mkuu wa shule huku bifu kali likiendelea kati yake na Madamu Eliza hali iliyopelekea waimu wakawa wanamuadhibu sana Sofia hata kwa kosa dogo.
Ama kweli ukishindana na mkubwa utaumia mwenyewe. Siku moja mida ya saa 10 za jioni mara baada ya wanafunzi kutawanyika, Sofia alikwenda moja kwa moja mpaka ofisini kwa mkuu wa shule kisha akamwambia,
“Samahani nimeshindwa kuvumilia lakini leo ngoja niseme ya moyoni. Kiukweli sipo tayari kuwa na mahusiano na mwalimu yeyote hivyo nakuomba unisamehe..!” Alitamka akiwa ameinamisha kichwa chini.
“,Hee ndo kimekuleta hapa! kama hutokubali, shule utaiona chungu sana” alimwambia kwa sauti ya juu.
“Sawa kesho nakuja na mzazi wangu ili uongee naye..”
Baada ya kutamka hivyo, mkuu wa shule alibaki mdomo wazi huku kwa mbali akijihisi kiubaridi kwa mbali.
“Nilikuwa nakutania wala sina mda huo..” alitamka.
“Asante…”,Sofia alishukuru kisha akaondoka huku moyo wake wote ukihamia kujua wapi alipo kipenzi chake Kilaza.
Baada ya mwezi mmoja, Madamu Eliza alianza kujihisi kichefuchefu kilichoambatana na homa kwa mbali.
Aliamua kwenda hospitali ndipo alipokutwa na ujauzito kisha akaambiwa aje na mwenza wake.
Madamu alijihisi kuchanganyikiwa huku akiwa haelewi.
Alirejea nyumbani kwa kushutukiza ndipo alipomfumania Kilaza akiwa amelala na mrembo aliyekuwa anauza baa maeneo ya karibu na nyumba yake.
“Hee!, ..”,Madamu alipiga kelele iliyoambatana na mshangao mkubwa
Mrembo aliyekuwamo ndani.humo!, alitimua mbio huku akiwa amejifunga kanga tu.
“Toka nyumbani kwangu..nasema toka ..” Madamu Eliza alimfokea Kilaza huku akiwa anamsukuma.
“Nisamehe mpenzi wangu. Ni shetani alinipitia tu…” alitamka.
“Nasema ondoka malaya mkubwa wewe…” alitamka
Kilaza akiwa hajui kipi akifanye, alitoka nje kisha Madamu Eliza akafunga mlango na kuanza kulia peke yake.
Baada ya kuona mambo yamekuwa magumu, Kilaza aliamua kurejea nyumbani huku akiwa anatetemeka sana.
Alimkuta mamaye ambaye aliishia kuli tu na mda si mrefu, mzee wake alirejea kisha akataka kumfukuza lakini mke wake akamtetea.
Kilaza alitulia nyumbani ndipo Sofia aliposikia fununu za Kilaza kuwapo nyumbani.
Bila uoga wowote, Sofia alikwenda mpaka nyumbani kwa akina Kilaza na bahati nzuri alimkuta peke yake.
Kilaza hakuamini macho yake na wawili hao wakakumbatiana.
” Baby ulikuwa wapi” alimuuliza
“Nitakwambia ila unaweza kunisaidia ili nirejee shule ? “
“Mhh sasa nifanyeje maana mkuu wa shule alikuwa ananitaka nikamkataa..”
“Kumbe alikuwa anakutaka!”
“Ndiyo..”
“Sasa hapo ndo pazuri, mpange umlete guest afu mimi nitawafumania na tutampa masharti ya kurudi shule”
“Mhh ni ngumu!, lakini unanipenda kweli na hutonisaliti?” alimuuliza.
“Nakupenda sana..”
“,Vipi kuhusu Madamu…!”
“Madamu alikuwa anajipendekeza ila simpendi”
“Mhh..” aliguna
“Ndo hivyo basi fanya hivyo..”
” Sawa ntajaribu siku ya jumamosi”
( waliagana).
Sofia alijihisi mwenye furaha sana huku akiwaza ni njia ipi ataweza kumnasa mkuu wa shule.
Wahenga wasema ” hakuna mkate mgumu mbele ya chai”
.
Sofia alimuandaa mkuu wa shule naye akajaa kwenye mfumo huku akiwa haamini kama kigori huyo kakubali kutembea naye.
Mbamo mida ya saa11 za jioni siku ya jumamosi, Sofia alitangulia kwenye Guest kisha akajiandaa vizuri na chini yake alilala Kilaza yaani uvunguni.
Mda si mrefu mkuu wa shule iliingia chumbani humo, kisha akamkuta Sofia akiwa amevaa nguo za ndani tu.
Udelele ulimtoka kisha akamkumbatia kisha Sofia akaanza kumchezea mkuu wa shule.
Ambaye taatibu alijikuta anameshavua nguo zote.
Wawili hao walila ndipo Kilaza alipoinuka kutoka uvunguni kisha akawapiga picha wawili hao wakiwa watupu kisha akajitokeza.
“Hii ndo michezo yako!, leo umekamatika!, unatembea na mwanafunzi!” Kilaza alitamka huku akiwa ameshika simu na kisu.
Mkuu wa shule alijikuta haja ndogo ikimtoka huku akiwa anatetemeka.
“Chagua adhabu gani nikupatie”
“Nisamehe kijana wangu ni mara yangu ya kwanza!” alitamka huku akiwa ametoa macho.
“Kwanini mimi hukunisamehe?”
“,Jumatatu njoo shuleni bila pingamizi lolote..” alitamka huku kijasho kikimtoka
“Ole wako sasa maana picha zako ninazo. Ondoka hapa!”
Mkuu wa shule alikimbia huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi
Jumatatu Kilaza alirejea shule huku wazazi wake wakiwa hawaamini.
Baada ya kufika shule mkuu wa shule alimpokea Kilaza kwa furaha huku penzi zito likitaradadi kati ya Kilaza na Sofia huku Madamu Eliza akiwa hatamani hata kumuona Kilaza.
Baada ya miezi 9, Madamu Eliza alijifungua mtoto wa kiume aliyekuwa anamfanana Kilaza moja kwa moja hali iliyowashtua wengi lakini kitanda hakizai haramu.
Maisha yaliendelea ndipo mwisho wa siku mara baada ya matokeo kutoka na Kilaza kuja amefeli, alijikuta anampigia magoti Madamu Eliza kisha wakarudiana na kufunga ndoa kati yake na Madamu Eliza huku Sofia akiapa kutokupenda tena katika maisha yake.
………………….MWISHO. ……………