MTOTO WA AJABU
PART: 10
ILIPOISHIA,
Bonge atembelewa na akina mama Vanesa ili kumpa hongera ya kujifungua, huko mtoni Mamba tayari kamrukia mtoto wa ajabu . Nako nyumbani kwa Braison, mazishi yalipangwa kufanyika saa 9 ya alasiri kwa maiti yenye utata….
SONGA NAYO…
Akiwa ameshikilia kikombe cha uji,aliinamisha kichwa chini kisha akajifanya anakohoa ili kupoteza lengo mahususi la mazungumzo.
“Khoh…!..khoh…!’kho..!..ee Yesu na Maria” Bonge alikohoa huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi.
“Pole inakuwaga hivo pindi ukijifungua nami ilinitokea pindi nimemzaa Vanesa..”‘Mama Vannesa aliongea.
“Asante” Bonge alijibu.
“Tunaomba tumuone mtoto maana tunawahi ili kuwaandalia chakula watoto wa shule..” walimwambia huku wakiwa wanaangaza huku na kule.
“Mtoto yupi mnamzungumzia?” Bonge aliwauliza kwa sauti ya juu kidogo.
“‘Jamani kwani si umejifungua au tumeambiwa visivyo?”
“‘Aliyewambia ni nani?, mnajua nilikuwa nawachora tu!”
“Mhh basi samahani “
“‘Mmejaa umbea mchana kutwa badala kufanya kazi mnazurura tu. Mtoto wangu sitaki mumuone. Ondoka kwangu!..ondoka!” Bonge aliwaka kwelikweli na kuwafukuzia mbali akina mama Vannesa na wenzake.
Baada ya kutimuliwa, walibaki na mshangao mkubwa huku wakiwa hawaelewi kwanini imekuwa hivo.
“Ila huyu mwanamke atakuwa amevurugwa sio bure. Sasa kwenda kumuona ndo maneno hayo!. Abaki na mtoto wake nasi haturudi tena” waliongea wanawake hao.
Bonge akiwa amekunja uso wake kama mbuzi, alimuita mlinzi na kumuuliza,
“‘Hawa wanawake wameingia ndani ukiwa wapi?”
“‘Nilikuwepo boss..” alijibu.
“‘Unaruhusu watu usiowajua kuingia ndani!, wakifanya uharifu je?”
“‘Hapana Boss niliwahoji kwanza na ikaonekana ni watu wema..”
“‘Sasa tangia mda huu!, usifungue mlango wa geti na usiruhusu mtu yeyote kuingia. Kama anashida atanipigia na usimpe mtu namba yangu..”
“‘Sawa boss ntafanya hivo…”
“‘Sasa naona watu wameshajua kuwa nimejifungua lakini mtoto hatuna hapa, chakufanya unapaswa uchimbe kaburi na badaye utafuata jeneza pamoja ..”
“Hee!, halafu tunafanyaje!?” Mlinzi aliuliza kwa mshangao
“Tutazika ili wakija kuulizia wambie mtoto alifariki na ameshazikwa..”
Mlinzi aliinamisha kichwa chini bila kuongea chochote ndipo alipoulizwa tena,
“Umenisikia?”
“‘Ndiyo boss..”
“‘Ayaa andaa vifaa uanze kazi sasa hivi..”
Kwa unyonge huku akiwa anatetemeka, mlinzi alichukua vifaa na kuanza kuchimba kaburi.
Alikata jembe la kwanza la pili likaambatana na damu iliyotoka na sauti,
“Usinikate unaniumiza”
“Hee!, ” mlinzi alibaki ameganda.
Alitupa vifaa vyote chini kisha akakimbilia ndani,
“‘Boss…boss..boss” mlinzi aliita.
“‘Nini…?”
“‘Nakuomba samahani…”
Bonge alitoka chumbani na kumuona mlinzi.
“Samahani sana boss, naomba unilipe hata nusu ya mshshara wangu wa mwezi huu niondoke..”
“Uondoke uende wapi?”
“Nikatafute maisha pengine..”
“‘Hee hapa umekosa nini?”
“‘Njoo uone…”
Alimpeleka eneo alilokuwa anachimba kaburi na kumuonesha jembe likiwa limelowana damu.
“‘Hee!, ni nini hiii!?!” Bonge alishangaa.
“Kuna mtu anasema usinikate japo simuoni?” Mlinzi aliongea.
Bonge alipenga kamasi laini kisha akasogea pembeni huku mlinzi akisubiri alipwe chake aondoke.
Huko upande wa Braison, watu wa madhehebu mbalimbali, watoto, vijana, wanaume na wanawake, walikusanyika kwenye nyumba ya milele kwa ajili ya kuulaza mwili wa marehemu.
Katekista aliongoza ibada ya mazishi kabla ya kuulaza mwili wa marehemu huku Braison akishindwa kujizuia na kuangua kilio cha uchungu kama mtoto mdogo..
Kwa kuwa mtoto alikuwa mchanga sana, walitoa nafasi kwa watu wa ndani kuaga mwili huo kisha wakamuita fundi kupigilia misumari ya mwisho.
Akiwa ameshika nyundo yake, aligonga misumari lakini cha maajabu ilivunjika yote.
Kuona hivo, wazee walileta kamba kisha wakalifunga jeneza hilo.
Baada ya kulifunga, sasa nilipelekwa moja kwa moja mpaka kweye kaburi.
Katekista aliomba tena kisha akawambia waingize mwili wa marehemu kwenye nyumba yake ya milele.
Walipitisha kamba mbili kisha wakazishika vijana wanne na kuanza kutaka kuhifadhi mwili huo.
Wakati wananyanyuua, jeneza liliwashinda kulitoa hapo lilipokuwa na kuwaacha midomo wazi.
Watu waliongezeka na kufika nane lakini hata halikuweza kusogea.
Watu waliokuwa maeneo hayo, walianza kuunguruma huku wengine wakidai kuwa Braison amemtoa mtoto wake kafara kwa Freemason.
Baada ya kizungumkuti hicho, katekista alianzisha maombi mafupi kisha akawambiwa waingize mwili huo tena.
Walifanya kunyanyua tena wakiwa 10 lakini jeneza halikunyanyuka ndipo walipobaki na sintofahamu.
Wakiwa wanashangaa, jeneza lilifunguka na mwili wa maiti ukawa juu kisha ukaanza kuongea,
” Nipeleke nikazikwe nyumbani”
Watu wote walikimbia hata katekista, na viongozi wote walikimbia na kusogea mbali sana…huku wenye roho nyepesi wakizimia na kuzirai.
Na huko mtoni, mamba baada ya kumrukia mtoto huyo wa ajabu, alimuweka kwenye himaya yake huku akiwa na tabasamu .
Alimuweka mgongoni mwake na kusafiri naye ili akapate kitoweo sehemu salama.
Mtoto alizidi kupiga kelele lakini mamba hakuwa wala na wasiwasi naye….
💥💥Huko kwa bonge mambo mazito. Kwa Braison maiti kagoma kuzikwa, na huko mtoni mamba ndo tayari anatokomea na mtoto….
JE NINI KILIFUATA?
PART: 11
ILIPOISHIA,
Huko kwa bonge mambo mazito. Kwa Braison maiti kagoma kuzikwa, na huko mtoni mamba ndo tayari anatokomea na mtoto…
SONGA NAYO…
Hali ya sintofahamu ilizidi kutada nyumbani kwa Braison mara baada ya maiti kushindwa kuzikwa huku kwa mara ya kwanza wakishuhudia maiti inaongea.
Kelele za hapa na pale zilizidi kuongezeka huku habari zikizidi kusambaa kila sehemu kwa kasi ya ajabu.
Vikao vya hapa na pale viliendelea vikiongozwa na Mzee Kipara huku wakijiuliza wapi wamekosea lakini hawakupata jibu.
Ilipofika saa 12 za jioni, waliungana watu wote kisha wakaanza maombi yaliyoongozwa na baba Paroko ambaye alikuja kwa dharura.
Baada ya maombi hayo, aliwambia wakaupumzishe mwili lakini kabla hawajagusa mwili huo, maiti iliongea ,
“‘Naomba mnizike nyumbani”
Watu walikimbia kwa mara nyingine akiwemo na Paroko.
Akiwa hospitali anaendelea kuuguza kidonda, Sarah alipata taarifa za kushindwa kuzikwa kwa mwili wa marehemu mtoto wake.
Alilia sana peke yake huku akiongea,
“‘Kwanini mimi lakini?” Alitikisa kichwa huku akitamani kujionea lakini ilishindikana .
Wakati anaendelea na maumivu hayo, wazee waliwaza na kuja na wazo hili,
“‘Hii mimba iliyozaa mtoto huyu itakuwa siyo ya Braison hivo mke wake anajua vizuri nani alimpa mimba. Chakufanya twende tumuulize atwambie ukweli laa sivyo hatutoboi..”Kipara aliongea.
“‘Ni kweli maana Braison amekaa naye bila kupata mtoto hivo tunaunga mkono ” wajumbe walisema.
Wazo lilipita na wakaandaliwa wazee watatu wakiongozana na Mzee kipara kwenda kumuhoji Sarah awambie nani alimpa mimba.
Walifanikiwa kupata usafiri . Ndani ya saa 12 na nusu za jioni walifika hospitalini hapo na kuomba kuonana na Sarah .
Bahati nzuri walikubaliwa kisha wakangia mpaka chumba alichokuwemo.
Sarah alikuwa amesinzia ndipo walipomuamsha polepole.
Ile anazinduka, alishangaa kuwaona wazee hao wakiwa na sura ya tabasamu.
“‘Pole sana” walimwambia.
Sara alishindwa kuitikia na badala yake aliishia kumwaga machozi tu.
“Nyamaza ni mpango wa Mungu…” walimwambia.
“‘Ninau..u..u.umia sana..”Sarah aliongea kwa mkato..
“‘Pole nasi tunaumia sasa bila kupoteza mda tunaomba utusaidie wala usione aibu yoyote ili tuweze kumaliza balaa lililoko nyumbani” wazee waliongea.
“Niwasaidie nini mimi niliyelala hapa?!”
“Sio nguvu bali maneno tu…”
“‘Ok…”” alitikia kwa hofu kidogo
“‘Sasa tunaomba utwabie baba wa mtoto aliyefariki ni nani?”
“Hee!, kwanini mnauliza hivi?, kwani hamumjui mme wangu?!” Sarah aliongea kwa ukali kidogo.
“‘Come down, come down…hatuna nia mbaya ndo maana tumekuomba na tutatunza siri…”
“‘Niacheni …!niacheni nipumzike…” Saral aliongea kwa uchungu.
“‘Sio utani hali ni tete na tayari kuna ushahidi wote kuwa mimba uliipata kwa mme mwingine. Kushindwa kutwambia unafanya maiti ya mwanao ishindwe kuzikwa na unatengeneza picha mbaya ya uzinzi kwenye ukoo..” walimwambia.
“‘Sina cha kuwambia Mungu pekee ndo anajua ukweli wote. Sijawahi kulala na mwanaume yeyote tangu nimeolewa nje ya ndoa. Kama kweli mmenichoka nipo tayari kwa uamuzi wenu..” Sarah aliongea.
“‘Tulia usipanic mpaka mda huu wanasubiri majibu kutoka kwako na kama umeshindwa kuongea, chochote kitakachokupata usitulaumu maana tumekwambia..”
“‘Nipo tayari kwa lolote ila mtetezi wangu ni Mola ambaye anajua ukweli wa mambo yote…” Sarah aliongea kwa uchungu.
“‘Haya sisi tunaondoka ila kuanzia sasa usitulaumu. Kwanini mnashindwa kukaa kwenye ndoa zenu na kutulia?, ona sasa!, ulikuwa unaheshima kumbe ..”
Wazee walifoka na kuondoka. Sarah alibaki ameshika tama huku akijuta kwanini amezaliwa katika dunia hii yenye mateso.
Wakati wamesubiria majibu, wazee walifika nyumbani kwa Braison huku moto mkali ukiwa unawaka kwa nje.
Wazee walitoa mrejesho kuwa,
“Mwanamke amekataa kabisa !, Braison unatakiwa kumfukuza mke huyu kuanzia mda huu afu asiende mtu yeyote kumuangalia hospitali. Ametuaibisha sana tutamfanyia kitu kibaya usiku wa leo” Kipara aliongea kwa hisia kali.
“Lakini kiukweli mke wangu sikuwahi kusikia hata fununu yoyote juu ya kutoka nje ya ndoa…labda nisimtetee sana..” Braison aliongea.
“‘Hee!, unamtetea mwanamke kwani ndugu yako, mama mzazi ndo mtu anakupenda wewe hivo achana na viumbe hivi mpaka kwenye vitabu vitakatifu tumeambiwa tuishi navyo kwa akili…. kama hutaki kutusikiliza, tutaondoka..”
“Samahani kama nimeteleza maana ulimi hauna mfupa. Nipo tayari kwa uamuzi wowote..” Braison aliongea kwa hofu kubwa.
Saa tatu za usiku, walijaribisha kuzika mwili huo lakini wapi haikuwezekana ndipo kwa hasira walipoenda kwenye mti mkubwa walipokuwa wanafanyia matambiko wakiwa na kondoo na kuku mweupe kisha wakachinja na kukinga damu kwa kitenge cha Sarah kama ishara ya kuuawa kwa Sarah.
“Tunakuomba kwa huruma yako uweze kumuondoa mwanamke huyu mzinzi aliyeleta balaa . Tunakuomba pia baada ya kumaliza tukio hili, utusaidie tumpumzishe kwa amani mtoto wetu maana hakuwa na hatia yoyote..”
Baada ya kumaliza, walirudi nyumbani kwa siri huku wakisikilizia nini kitatokea baada ya mda mfupi kwani mti huo ulikuwa unajibu maombi yao mara nyingi na kwa uharaka zaidi.
Wakati wanazidi kusubiria, huko mtoni mwanga mkali ambao ulikuwa na rangi kama upinde wa mvua, uliangaza kwa gafla ndipo mamba aliyekuwa amembeba mtoto wa ajabu kwa ajili ya kitoweo alipojikuta amebeba gogo la mti tu.
Alijiviringisha na kujinyoosha huku akiwa na njaa kwelikweli lakini hakuona hicho kitoweo.
Huko kwa bonge nako, mipango mizito iliendelea kupangwa mnamo mida ya saa 4 za usiku ikiwemo kumuongezea mshahara mlinzi ili asiondoke.
Wakati wanaendelea na Mazungumzo, gafla walishangaa kwa pembeni akiwa amekaa mtoto huyo wa ajabu akiwa amefungwa Nepi .
“Mmemaliza kupanga?, kama mmemaliza naombeni chakula..” mtoto aliongea.
“Hee! Mama yangu huyu ni mtoto au jini! Si nilikwambia umtupe mtoni!”
“Ndiyo nilimtupa…”mlinzi alijibu
“‘Twafaaa. .” Bonge akiwa amejifunga kanga, ali…
PART: 12
Bonge akiwa amejifunga kanga pekee, alitimuka ndani ya nyumba huku akiwa anahema mpaka nje.
Alihema huku mapigo ya moyo yakiongezeka kwa kasi mithili ya mwanafunzi aliyecheza kamali ada ya shule .
Akiwa kwa nje, mlinzi alibaki ndani pamoja na mtoto wa ajabu kisha akampatia chakula.
Baada ya kupewa chakula, alifurahi sana na kuanza kula ndipo mlinzi alipotoka na kumfuata bonge kwa nje.
Bonge alishika simu yake na kumpigia Mariatabu ambaye mda huo alikuwa nyumbani kwake pamoja na Asia.
(Duuh!..duhhh!..duuh!) Simu ya Maritabu iliisha kisha akapokea.
“‘Helloo..”
“Heloo umenikumbuka?” Bonge alisema.
“‘Ndiyo wewe si Bonge?”
“Ndiyo ndo mimi…”
“‘Niambie…”
“‘Sina usemi ila nakuomba wewe na Dokta Asia mrudishe pesa yangu haraka iwezekanavyo kabla sijawafanyia kitu kibaya..”
“‘Hee! Kwanini?, si tulikubaliana? “
“‘Yaani mmeniuzia jini mpaka mda huu nimeshindwa kuingia ndani. Mtoto anaongea na kufanya mambo ya ajebu!, naomba tuheshimiane laa sivyo …”
“Sasa kwanini unatulaumu?. Ulikuja mwenyewe na hela ukatoa mwenyewe. Usitutishe bwana..”‘Asia aliongea kupitia simu ya Mariatabu.
“‘Ayaa mtanitambua mimi ni nani!. Siwezi kutafuta hela kwa tabu hivi afu nyie muitumie kizembe hivi!, tutaelewana tu… “
Baada ya kuwatishia, Mariatabu alikata simu kisha akaanza kuongea na Asia,
“‘Shoga angu hii imekaaje?, maana anaweza kutuletea shida kwa kuvujisha siri…”
“‘Anatutisha tu wala hana cha kutufanya…kesho asubuhi twende kupokea magari yetu na uzuri wote tuna leseni..”
“Mhh..mwenzio ujue naogopa sana maana hata haya magari inawezekana tusiyaendeshe kama siri ikifichuka..”
“Kwa hilo kuwa na amani kabisa. Hawezi kutoa siri kwani na yeye ataingia mtegoni na watamuweka ndani..”
“Mhhh..ngoja tuone…”
“Usiogope nimeshakwambia…”
“Ayaa shoga angu….”
Huko upande wa Bonge mara baada ya kukatiwa simu, alichukia sana na kuvimba mashavu kama chura anayetaka kutema mate.
Alimuita mlinzi kisha akamwambia,
“‘Kuna kazi nataka uifanye hakika nitakupa hela nyingi zaidi ya milioni 20”
“Kazi gani hiyo?”
“‘Kuna hawa wanawake wamekula hela yangu na wananijibu majibu ya ovyo…”
“‘Kwo unataka nifanyeje?”
“Nitakupa ramani nzima wanapokaa na namba zao . Ninachotaka watoweke kwenye ulimwengu huu maana ndio wanaofanya majanga kwa mtoto huyu “
“‘Ni ngumu sana kufanya hivo maana damu ya mtu ni nzito sana..”
“Hao hawana ugumu wowote. Bila kufanya hivo maisha yangu yatakuwa magumu sana kwa balaa hili.”
”Ongeza pesa zifike hata milioni 30 ili nimpange mwenzangu tumalize kazi…”
“‘Haina shida hata ikiwa milioni 40 ntawapa tu wala hakuna shida …”
“Sawa…”
Bonge hapohapo alimpatia mlinzi namba ya Mariatabu pamoja na Dokta Asia.
“‘Lakini pia huyu mtoto kwa kuwa naona humuogopi sana, naomba nikupatie bastola ummalizie kabisa ili tupoteze ushahidi wote ..”
“‘Asee kwa hilo naogopa sana labda nikusaidie kumfunga lakini unipe milioni 3”
“‘Swala la hela usijali nitakupa. Mmalizie afu tutamtupa mtoni..”
“‘Lakini huyu mtoto sio wa kawaida hata kidogo ..”
“Kwenye risasi hakuna mjanja hata mmoja..”
“‘Haya andaa hiyo hela .”
Bonge akiwa anatetemeka, aliingia chumbani akiwa na mlinzi ili ampatie bastola.
Baada ya kumpatia bastola, mlinzi aliiweka kwenye mfuko wa pembeni kisha akamfuata mtoto huyo aliyekuwa anakula.
“‘Umeniletea zawadi?” Mtoto alimuuliza mlinzi.
“‘Ndiyo nimekuletea “
“‘Naomba basi..”
‘Mlinzi alichomoa bastola na kumuwekea kwenye koromeo.
“‘Nawewe kumbe unataka uniue?, nimekukosea nini lakini?, kama wewe utaishi milele basi niuwe” mtoto aliongea.
Mlinzi alibaki amestaajabu lakini alijitahidi akafyatua risasi ambazo zote ziligonga ukutani.
“‘Hee!..” mlinzi alikimbia na bastola nje .
“‘Vipi umemaliza kazi?” Bonge alimuuliza.
“‘Kwakweli hili ni balaa jingine!, yaari risasi zinakwepa na kugonga ukuta mpaka moja kidogo inipasue uso.
“Huuuuh…!”‘bonge alishusha pumzi huku kijasho chembamba kikimtoka.
Wakati kijasho chembamba kinamtoka Bonge, huko kwa Braison hali iliendelea kuwa tete kwelikweli mara baada ya jitihada zote za kuzika mwili wa mtoto kushindikana.
Wazee wakiongozwa na Kipara mara baada ya kufanya tambiko la kumtoa kafara Sarah , waliendelea kusubiri taarifa kutoka hospitali maana mti huo mara nyingi ulikuwa unajibu sana maombi yao..
Kama miujiza hivi, hali ya Sarah ilibadilika gafla akiwa kitandani amelazwa bila msaada wowote wa kiuangalizi.
Nesi aliyekuwa zamu usiku huo, aliingia na kumkuta Sarah anatapika damu huku akiwa amelegea sana.
” kichomi..kichomi…hooo! Mkuki unanichoma tumboni…! Nakufa mimi” Sarah aligalala kwa kurusha miguu ndipo Nesi alipokimbia kumuita mhudumu mwenzie ili amsaidie.
Wakati wanaingia, walishangaa kuona Sarah akiwa amelala kwa kunyoosha miguu huku akiwa hajitingishi..
” Hee! Jamani mbona alikuwa anaendelea vizuri huyu dada?” Nesi aliongea kwa huruma kisha akamsogelea kwa karibu kuona kama amashafariki….
PART: 13
ILIPOISHIA,
” Hee!, jamani mbona alikuwa anaendelea vizuri huyu dada?” Nesi aliongea kwa masikitiko makubwa…
SONGA NAYO..
Wakiwa hawamini mabadiliko ya gafla yalitotokea kwa Sarah, Manesi walimsogelea kisha wakamgusa miguuni ndipo walipohisi miguu kuwa ya baridi sana kama ishara ya kuonesha tayari ameshatangulia mbele ya haki.
Iliwauma sana kwani hawakutegemea kuwa hivo kulingana na hali aliyokuwa nayo Sarah.
Walichukua shuka jeupe kisha wakamfunika ili taratibu za kuzafisha mwili wake zifuatwe kabla ya kumpeleka kwenye chumba cha maiti.
Wakati hayo yote yanaendelea, Wazee wakiongozwa na Kipara walikaa wametega masikio yao kuona kama Saraha kashafariki ili wajaribu kuzika maiti iliyowagomea kuzikwa.
Walisubiria mpaka wakafikia hatua ya kupiga simu kwa mlinzi ambaye aliulizia japo na kwa siri na kuambiwa hali yake ni mbaya na mda wowote linaweza tokea jambo.
Aliwapa taarifa hiyo ndipo walipofurahi huku Braison kwa mbali akianza kuhisi uchungu na kumkumbuka mke wake kwani walitoka mbali sana.
Katika hali ya kushangaza huku wakiwa wanaanza kumfunga kitambaa cheupe, Manesi waliona Sarah kwa mbali akiwa anapumua , walishutuka kisha wakamshika masikio ndipo walipoona hajafa bado.
” Duuh hiki kituko..!”waliongea kisha wakamtoa shuka hilo.
Wakiwa wamesimama, gafla mwanga mkali uliangaza chumbani humo kisha ukatoweka gafla ndipo Sarah alipozinduka na kuwa kwenye hali yake ya kawaida.
Nesi walikimbia kwa woga mkubwa kisha wakatoa taarifa lakini walipokuja tena hawakuona chochote.
Mambo yalionekana kwenda ndivyo sivyo kwa wazee mara baada ya kusubiria mpaka usiku wa manane bila kupata taarifa yoyote juu ya kifo cha Sarah.
Walijaribu kupiga simu tena kwa Mlinzi wa hospitali lakini hakuwapa mrejesho wowote ndipo walipojawa na taharuki.
Asubuhi yake kulikucha ndipo walipotaarifiwa kuwa Sarah yu mzima kabisa na anaendelea vizuri.
Walishika vichwa kama watu waliochanganyikiwa huku maombi ya hapa na pale yaÄ·iendelea lakini maiti ilikataa kuzikwa.
Mbinu ya kumuua Sarah kwa kupitia matambiko ilionekana kwenda mlama ndipo walipoanza kuwaza njia nyingine .
Huko kwa upande wa Asi na Mariatabu, walikwenda kupokea magari yao ambayo waliagiza lakini cha kushangaza hawakukuta gari lolote sehemu waliyokuwa wameelekezwa.
Walimuuliza kijana aliyekuwa anafanya kazi sehemu hiyo ndipo alipowajibu kuwa wao hawahusiki na magari wala mtu huyo yaani Mkali hawamjui.
Kijasho chembamba kiliwatoka wawili hao ndipo Mariatabu alipompandia hewani Mkali.
Alijaribu kupiga simu lakini haikupatikana. Alipiga tena simu haikupatikana.
” Duuh !” Mariatabu aliishiwa Pozi
” Naomba unirudishie hela yangu maana wewe ndo uliniambia huyo ni ndugu yako…” Asia alimshika Mariatabu
” Hee! Kwanini unanishika?, subiri kwanza huenda simu yake haina chaji afu swala la hela hata mimi sijachukua hata shilingj mia..” Mariatabu alijitetea.
” Kwanini adanganye?, mmepanga wote ili mchukue hela yangu!, . Walahi leo kitaeleweka..” Asia alizidi kumbana Mariatabu.
” Sasa mimi nina makosa gani?”
” Tusiongee mengi, naomba hela yangu. Milioni kumi ni hela nyingi sana. Si bora ningejenga nyumba…!, tuheshimiane tafadhari..”
“Niache kwanza nimpigie tena..” alipiga tena lakini simu haikupatikana
Wakati anajaribu kumpigia simu Mkali, kumbe yeye alishatupa laini hizo na kusajili mpya huku hela yote akiwa ameenda kuifungulia Duka Sinza.
Ama kweli laitia angejua basi asingefanya hivo.
Baada ya muafaka kukosekana, Asia alianza kuzichapa na Mariatabu .
” Nipe hela yangu..nipe hela yangu…” Asia alimtwanga ngumi moja ambayo ilikwenda moja kwa moja kutua kwenye jicho la kushoto ndipo Mariatabu alipodondoka chini kisha akapiga kelele.
Asia alimrukia na kumziba mdomo kisha akamwambia ,
” Fumba mdomo wako huo!!, leo utaniambia wapi umeweka hela yangu!” Aliendelea kumtwanga ngumi mpaka akampasua midomo iliyoanza kumwaga damu.
Wapita njia wawali waliwaona ndipo walipokimbia na kumtoa Asia aliyekuwa amekasirika kweli kama mbogo aliyechomwa mkuki.
” Lione na sura mbaya kama popo… unanipiga unanitunza wewe…” Mariatabu akiwa anachuruzikwa na damu aliongea.
“Bado unaendelea!,, ngoja nikuoneashe sasa”
“Hapana …hapana…” wapita njia walimshika Asia
” Muache anipige aone..muache..” Mariatabu aliongea
” Ohh nitakuzibua!!..”
” Kwani nini shida watu wazima kugombana na kuumizana namna hii?” Waliwauliza.
” Huyu mpuuzi kanitapeli hela yangu kiasi cha shilingi milioni 10 akishirikiana na ndugu yake ambaye anadai yupo Dar..” Asia alieleza.
” Hela yako ipo mjinga wewe. Uliifanyia nini kama sio kuuza watoto wa watu hospitali..” Maritabu aliongea kwa hasira.
” Hee! kuuza watoto tena!, kivipi..” walishangaa.
” Yaani huyu ana roho mbaya sana kiasi cha kumuuza mtoto wa mwanamke mwenzie na kisha akamdadilisha na maiti ya mke mwingine”
” Msimsikilize huyu ni kichaa anawapotezea mda wenu tu..” Asia alijibu kwa hofu kubwa huku mapigo ya moyo yakiwa yanamgonga kwa kasi.
” Sio uongo ni ukweli na ninaongea haya nikiwa na akili timamu..” Mariatabu akiwa anaugulia maumivu aliongea.
” Huyo mtoto alimuuzia nani?” Walimuuliza
” Kuna mama fulani anaitwa Bonge afu ndo alimuuzia afu mama wa mtoto anaitwa Sarah..” Mariatabu alizidi kumwaga mboga.
” Mnapoteza mda kumsikiliza huyu kichaa, ebu niache kwanza nimnyooshe ile aseme vizuri upuuzi wake huu..” Asia aliongea..
” Sahamani sisi hapa ni jeshi la polisi, mnaweza kutusaidia kutoa taarifa kituoni” Wapita njia hao waliongea kisha wakachomoa vitambulisho na kuwaonesha.
Ndani ya sekunde 5, haja ndogo ilikuwa imemtoka Asia huku akiwa anatetemeka.
Askari walimtia pingu Asia kisha wakaambatana na Mariatabu kuelekea kituoni.
Walipokaribia kituoni, Mariatabu alihisi kama kesi inaenda kuwa ngumu hata kwake ndipo alipoanza kujutia kwanini alisema hivo.
Aliangaza huku na kule kisha akasema,
“Samahani taarifa hii nimewapa sio ya kweli labda mshike kwa kesi ya kunipiga” alitamka kwa wasiwasi.
” Hee! hivi sisi unatuoana wajinga eeh. Wewe ni kichaa..!?”
” Hapana”
” Una upungufu wa akili!”
” Hapana…”
” Twende ukweli utajulikana kituoni” Mariatabu naye walimtia pingu huku akiwa anaendelea kutokwa damu kwenye midomo yake iliyopasuliwa na Asia….
JE ILIKUWAJE???
PART: 14
ILIPOISHIA,
” Twende …ukweli utajulikana kituoni” Mariatabu naye walimtia pingu huku akiwa anaendelea kutokwa damu kwenye midomo yake iliyopasuliwa na Asia
SONGA NAYO…
Waliongozana nao kwa mwendo haraka mithiri ya mgambo wanofanyishwa mazoezi mpaka kituo cha polisi.
Baada ya kuwafikishisha waliwatia ndani kisha wakawafungi kwa mda kama nusu saa hivi.
Wakiwa ndani, Asia alimgeukia Mariatabu kisha akamwambia kwa sauti ya chini,
” Usiseme chochote kile !, ugomvi wetu nitakulipa gharama za matibabu lakini kesi yetu ni ngumu sana”
” Chanzo ni wewe, unafikia hatua ya kunifanya hivi na kunituhumu kula hela zako!, i..” Mariatabu alimjibu.
” Sasa kwanini umefikia hatua ya kunitaja kuwa niliuza mtoto ili hali wewe ndo ulimuuza?”
” Hee ! Naomba unikome !.. sihusiki na chochote” Mariatabu alimkana Asia.
” Thubutu!, yaani ukinitaja nami nakutaja kama ni mbaya na iwe mbaya..” Asia aliongea.
Wakati wanzodoana huko Cello, askari walikuwa wanapitia simu zao kwa uhakiki wa kina kabisa hasa kwa kusoma meseji.
Baada ya kujiridhisha waliandaa utaratibu wa kiuchunguzi kwa kuwaita wote kwa pamoja.
Waliwafungulia huku wakiwa ndani ya pingu kisha wakaanza kuhojiwa.
” Asia, ebu twambie ilikuwaje mpaka ukamuuza mtoto wa Sarah na Braison na huyo mtoto yuko wapi!? ” Askari alimuuliza kwa sauti ya ukali .
” Mi sijui chochote . Aliongea hivo ili kunichongea kwa hasira zake”
” Una uhakika na unachokiongea?” Walimuuliza.
” Nina uhakika kwa asilimia 100 na wala sijawahi kusikia kitendo hiki cha kinyama”
.
” Sogea pembeni hapo kwanza” Walimsogeza pembeni kidogo kisha wakaanza kumuhoji Mariatabu,
” Wewe kama mtu ulitetupa taarifa , tunaomba maelezo mazima ya tukio zima..” walimwambia.
” Nilikuwa nadanganya wala hakuna tukio kama hilo..”
” Kwahiyo unatunaribu akili sio!”
” Hapana ndio ukweli huo..”
“Sawa nawe sogea pembeni hapo..”
Mariatabu akiwa anatetemeka, alisogea kidogo.
Askari wa kike aliitwa kisha akawambie waingie chumba cha giza.
Waliingia chumba ambacho kilikuwa kinanuna mikojo huku nzi wakirukaruka.
” Lalaleni kifudifudi…” Askari wa kike aliwambia.
Wawili hao walihisi utani kwani kwa hali ya kawaida mtu asingekubali kulala katika maji hayo machafu.
Wakiwa wanazidi kushangaa, walilambwa mitama na kushuka mpaka chini ya maji machafu yaliyokuwa na harufu kali sana.
Walianza kumwagiwa maji kisha wakaambiwa wajiviringishe kushoto kulia, kulia kushoto.
” Nisamehe ngoja niwambie ukweli…nisamehe..” Mariatabu
” Nyanyuka ukaoge ndani na uje utoe maelezo ya kutosha. Wewe endelea kujiviringisha mpaka utakapokubali kuongea ukweli” waliwambia.
Baada ya dakika chache, Asia naye alizidiwa uvumilivu huku akiwa anatematema mate kwa harufu kali sana kisha akakubali kuongea ukweli.
Baada ya kuogeshwa kwa kumwagiwa maji, walirejeshwa tena kisha wakaanza na Mariatabu.
” Ehee ebu twambie ilikuwaje!..”
” Aliyemuuza mtoto ni huyu hapa wala sio mimi. Alimuuzia mama mmoja anaitwa bonge…” aliongea.
” Ni muongo yeye ndo alimuuza…” Nyamaza wewe! Zamu yako bado !, kimya ..! Mpuuziwewe!” Askari walimtisha Asia kisha akakaa kimya.
” Ehee alimpa kiasi gani?”
” Alimpa milioni 20″
” Na wewe ulijuaje na ulichukua hatua zipi?”
” Aliniambia nikimtaja ataniua..”
” Kuna hela yoyote umetumiwa na wewe au?”
Mariatabua alikaa kimya kwa mda kisha akajibu,
” Hapana hata mia siijui..”
” Dada unatutakia ubaya eeh!, ongea ukweli “
” Asia alinipa milioni 5 tu”
” Na huyo bonge yuko wapi?”
” Nyumbani kwake japo sipajui..”
” Sawa, Asia ebu twambie ilikuwaje?”
” Mheshimiwa Raisi..”… alikatishwa..
” Hakuna Rais hapa..”
” Sorry mheshimiwa afande mimi sikuhusika na chochote bali ni Mariatabu aliyemuuza mtoto kwa Bonge..”
” Wewe ulikuwa wapi mpaka ukajua hivo?”
” Nilikuwa namhudumia mgonjwa..”
” Wewe ni daktari!!”
” Ndiyo na mwenzangu ni Nesi hivo mtoto alimuuza mda mfupi baada ya kuzaliwa”
Polisi walibaki wameduwaa kwa taarifa hiyo.
” Tunaweza kumpata bonge?” Walimuuliza Asia.
” Sina namba yake labda rafiki yangu..”
” Sasa mda huu unatakiwa umpigie Bonge kisha mwambie mkutane kwenye Mnara wa simu afu umwambie aje achukue hela yake kama mlivyokuwa mnachati”
” Sawa” Mariatabu akiwa anatetemeka, alipewa simu kisha akampigia Bonge.
Bonge akiwa nyumbani anawaza mpango upi autumie ili kuwamaliza Asia na Mariatabu, alishangaa kuona Anapigiwa simu kutoka kwa Mariatabu,
” Heloo..” Bonge alipokea..
” Habari ya kwako unaendeleaje?”
” Sitaki hata kusikia chochote isipokuwa pesa yangu tu!, naomba tuheshimiane..”
” Hata mimi nilijua tu ndo maana nimeamua kukupigia simu. Mda huu njoo hapa kwenye kwenye mnara wa mtandao wa Hallotel . Ukichelewa usinisumbue ila hela yako nimeshatumia laki 5″
“Hapo unayo shilingi ngapi?”
” Nipo na Asia tuna milioni 19 na laki 5″
” Hela yangu naitaka yote!, mda huu nakuja na ndani ya dakika 10 ntakuwa hapo”
” Sasa hiyo niitoe wapi?, nisubirie mwisho wa mwezi..”
Bonga alikata simu kwa haraka kisha akamwambia mlinzi wake awashe gari na kuongozana naye.
Wakati wanafanya hivo, huko msibani hali ikiwa imeendelea kuwa tata mara baada ya maiti kugoma kuzikwa, askari walilazimika kufika katika tukio hilo ili wasaidie lakini nao walichemka kabisa huku ikidai kuzikwa kwenye udongo wa nyumbani kwao.
Mshangao mkubwa na taharuki vilizidi kutanda huku hatima yake ikiwa haijulikani.
Mnamo mida ya saa 5 za asubuhi, Bonge alifika katika maeneo aliyoambiwa na Mariatabu kisha akashuka kwenye gari.
Aliangaza lakini hakumuona Mariatabu isipokuwa vijana wawili waliokuwa wanapita kama wapita njia.
” Samahani kaka umemuona mwanamke mmoja ni mwembamba vile afu mrefu..”
” Kuna aliyekuwa hapa alikuwa anazungumzia rafiki yake anaitwa Bonge sijui ndo nani?”
” Ohh Bonge ndo mimi…”
Hapohapo Vijana hao walichomoa bastola na kumwambia Bonge,
” Uko chini ya ulinzi! Nyoosha mikono!..” walimuamrisha.
” Hee! Nyie kina nani na mnataka nini?” Bonge aliwauliza.
” Sisi ni askari polisi tunakuhitaj kituoni kwa mahojiano..” walichomoa vitambulisho na kumuonesha Bonge ndipo alipobaki kinywa wazi.. huku akiwa anatetemeka mwili mzima….
INAENDELEA…..