KATOTO KA MADRASA
EPISODE 1 – 4
Ilikua majira ya saa saba mchana Husna alikua akirudi kutoka msikitini. Kwa sheria za nyumbani kwao kina husna ni lazima watu waswali tena swala zote kwani baba yake ni Amiri mkuu wa msikiti kwaiyo familia yake ameiwekea katika misingi ya kidini.
Husna aliporudi tu aliingia chumbani kwake moja kwa moja na kuvua baibui alilokua amevaa huku akijisemea ” hili
linguo linanikera yani navaa kwa kumwogopa baba tu” Akiwa chumbani alihakikisha kama mlango wake kafunga kisha akaelekea kabatini na kuingiza mkono chinj ya uvungu wa kabati na kutoa simu. Duuuuh alijisemea haya maisha ya humu ndani siyawezi yani hadi kutumia simu pia haturuhusiwi eti mtoto wa kike asiwe na simu mpaka amalize kusoma.
Akaiwasha simu yake ilivyowaka akatafuta namba iliyoandikwa baby. Alipoipata akaanza kuchat nae huku akiwa na furaha sana ila ghafla mlango wachumbani kwake ukagongwa