KAHABA MLOKOLE
SEASON TWO
Sehemu ya 31 na 32
“ sasa ni bora huyu ambae anajiuza ila hapendi kujiuza, ila anajiuza kwa sababu ya shida, na mwanao alikuwa anapata kila kitu nab ado alikuwa anajiuza, sasa naomba nisisikie tena mtu anamuongelea vibaya mwanamke wangu, kama ni kumuongelea vibaya mama, muongelea bint yako, ambae ametimuliwa kwenye ndoa yake na mumewe kwa sababu ya kuendelea kukitembeza, au ujui kama mwanao amefumaniwa ndio maana tupo nae leo hapa, akasema Julius …
“ kumbe umefumaniwa tena wewe mjinga, akasema mama yake Julius kwa sauti ya jazba kdg..
“ ilikuwa bahat mbaya mama , akajibu veronica kwa sauti ya uoga, ila sisi hatukutaka kuendelea kubishana nao, nikaingia zangu chumban, Julius akaja kunipoza kisha akanambia kuwa, haweza kuvumilia kumuona mtu yoyote Yule ananikoseha imani, na atahakikisha kama ni kuondoka basi wataondoka wao kwa maana ya veronica na mama yake na sio kmimi, kwa maana ni kama mimi ndio nimeshikilia funguo ya maisha yake, na nuru ya moyo wake……..
Basi kesho yake asubuh, nikaamka kwenye morning prayer, nilimka na Julius, na mama yake hata hakushiriki kabisa, pamoja na mwanae, tumemaliza ni mwendo wa vikumbo, ila hata sikutaka kusema nao, kwa maana mimi naolewa na Julius na sio na mimi…..
Basi nikafanya usafi na mara baada ya kumaliza kufanya usafi nikaandaa chai, wao hapo wamelala kana kwamb kwenye ile nyumba mimi ndio nilikuwa mwanamke pekee yangu, kwa maana hakuna aliejisumbua kuja kunisaidia wala kujigusa, sikuwajali hata kidgo, nikamuangaa Julius wangu kwaajili ya kazi, basi akaondoka zake, na kitendo cha Julius kuondoka ndio kero halisi zikaanza…
Picha linaanza, nilienda zangu kulala mara baada ya kumaliza majukum tyangu, sasa nimelala weee, nikaanza kusikia njaa, kwa maana huwa silag cha maana wakat namtengenezea Julius chai, natoka ukumbin nakutana na mifupa ya kuku nyumba nzima, na jikon kulikuwa hakufai, kwa maana kulikuwa kumemwagwa mwaga vitu, nilijisikia vibaya ila hata sikutaka kubishana na mtu, nikaanza kufanya usafi, nimemaliza usafi, nikamsikia dada yake Julius , bibie vero akisema, nitahakikisha nakuondoa kwenye nyumba ya kaka yangu, maana hii nyumba haitakiwi kuwa na mwanamke kahaba, akaendelea kusema veronica, hata sikutaka kubishana nao, nikaenda zangu chumban na kuanza kupaki kila kilichochangu, kwa maana niliona kuendelea kukaa nyumba moja na hawa wapuuzi ni kujisababishia maumivu mara dufu ya moyo kwa maana siwez kuendeleas kuvumilia kukaa na watu wanaonichukia sana…
Nikampigia simu Julius kuwa nimeshindwa kukaa nan dg zake kwa maana ni kero tu, Julius akanambia nichukue usafiri mpka kazin kwake, nay eye ndio ataamua niishi wapi na niishib vipi, nimefika nikamkuta Julius kwenye mkutano, na baada ya kama nusu saa akatoka kisha akanambia kuwa, “ ni bora uondokane na wale wajinga, usije ukakonda bure my wangu, kwa maana nataman watu wakikuona wakuambie ‘ mume wako anakutunza sana sio kwa nuru na mashavu hayo uliokuwa nayo, akasema Julius nikajikuta naanza kucheka…
Basi akatoka pale kazn na kwenda kunitafutia apartment, kisha akaweka kila kitu cha msingi na kusema ‘ mke wangu hautakiwi kuteseka tena kwa maana siku zote nitakuwa kwaajili yako…
Basi siku hio mara baada ya Julius kutoka kazin , alikuja pale kwangu, tukapika tukala, akapasha na mwili kwa burudani zetu zile, kisha akaondoka zake, amefika nyumban, tukawa tunaongea na simu tu muda mwingi, kesho yake asubuh nashangaa anakuja kwangu na mabegi yake, nikamuuliza kulikoni…
“ siwez kukaa mbali na wewe, nimewaachia nyumba waifanye wanachotaka, ila mimi natulizwa moyo huku na aneth wangu, akasema Julius nikajikuta nacheka, akanikiss pale kisha akaenda zake kazin…….
Sehemu ya 33 na 34
Basi nikawa naishi na Julius, na akakata kabisa mguu nyumban kwao, akamuachia nyumba mama yake pamoja na dada yake, kwa maana hakuwa anapenda kukaa mbali na mimi, na kingine walikuwa wananiongelea vibaya kana kwamba wao wamekamilika, na wakat huyo veronica mwenyewe alikuwa anajiuza na mama yake anajua…
Basi maisha yetu yalikuwa mazuri sana, kwa maana Julius alikuwa ananipenda sana, akaanza kufatilia utaratibu wa mama yangu kurudi nchini, na kweli mama yangu alirudishwa, skutegemea kama Julius angeweza kuingia gharama kiasi kile kwaajili yangu, na hapo ndio nikaamin kuwa hakuna mwanaume bahili kwa mwanamke anaempenda…
Hakuwa na pesa za kutosha kwa maana aliushatumia pesa nyingi kwa sababu ya matibabu ya mama yangu, hivyo mama akaenda kukaa na dada yangu, na maisha yetu yakawa yanaendelea, na akawa anataka dada akae nyumban kwa maana yale mahitaji ya nyumban Julius alikuwa anapambana sana kuyatimiza, sasa hakukuwa na sababu ya dada kujiuza tena, kwa maana kama ataamua kwenda kujiuza basi aende kujiuza kwa sababu anapenda na sio kwa sababu hana pesa……
Maihs yakaendelea, siku moja mama yangu akanipigia simu, akanambia kuwa anajisikia vibaya sana, anataka kuniona, nikampigia Julius, kwa maana sikuwa naweza kutoka bila kuomba ruhusa ila hakuwa hata anapatika, hivyo nikaenda zangu nyumban, ila nimefika nikakutana na giza, sasa akili zangu zikawa zinanituma kuwa dada kaenda kujiuza na amemuacha mama pakee yake nyumban…
Nikaanza kupiga simu ya dada yangu ila ilikuwa inata tu bila kupokelewa, “yaan huyu dada yangu ni mshenzi sana, yaan anamuacha mama pekee yake nyumban na anaamua kwenda kwenye mambo yake, nikawa nasema huku nikielekea kwenye mlango ambao ndo alikuwa anaishi mama na dada yangu kwa kwa wakat ule…
Ila wakat nafungua mlango, nikashangaa taa inawashwa na Julius alikuwa amepiga goti kisha akasema “ will you marry me…
Yaan sikutegemea, nikajikuta chozi la furaha linanitoka, na pemben nikamuona mama yangu, dada yangu, japhet pamoja na mchumba wake, na yule rafiki yao Emmanuel pamoja na mke wake, kwa maana yeye ndio alikuwa ameoa…
Sikuwa na ubavu wa kukataa proposal ya Julius kwa maana nilikuwa nampenda mpaka nataman kuzimia, nikasema “ yes..
Julius alitabasamu kisha akanivisha pete na baada ya hapo akasimama na kunikumbatia kisha akasema ‘ nakupenda sana posh baby wangu, nikajikuta nacheka……
Basi kulikuwa na kaparty uchwara, na wakaita na majirani , maana Julius na wenzake walikuja na chakula so watu ilikuwa ni kula tu, na kingine Julius wangu hakutaka kufanya hii shughuli mbali kutokana na hali ya mama yangu…
Basi kapary kakaisha kisha wale wapishi waliokuja na chakula,wakaondoka na vyombo vyao na wakasagfisha pale, kisha kila mmoja akatawanyika…
Sikuamin kama Julius angenifanyia hio surprise, ila nikashangaa kwanini
Mwandishi bahari ya simulizi) hajamualika mama pamoja na dada yake, akanijibu kuwa “ hawez kuwa karibu na watu ambao wanapambana kututenganisha, nikajisemea ehee mwisho nionekane kama nimempa kijana wa watu libwata…..
Basi tukaerudi nyumban, na tukaanza mafundisho ya ndoa kanisani, kwa maana ndoa ilikuwa ni miezi miwili mbele, kwa maana tuliona tusiendelee kumkosea mungu…
Sasa siku moja niko zangu ndani naangalia zangu tv, nikasikia mlango unagongwa, nilihisi ni Julius anarudi kwa maana anakawaida ya kuondoka baada ya dakika chache alaf anarudi ananiambia amenimiss, anakuja ananikiss kisha anaondoka zake, nikaenda kufungua kwa shauku, kwa maana nilikuwa nimeshazoea tabia ya mume wangu mtarajiwa…
Sehemu ya 35 na 36
Ila siku hio ilikuwa ni siku hiyo, hakuwa ni Julius, kwa maana nilipoenda kufungua mlango nikakutana uso kwa uso na mama yake Julius …
“ mwanangu unaendelea je? Akasema mama yake Julius huku akiwa anaingia ndani…
‘ salama mama shkamoo, nikajibu…
“ karibu sana mama, nikaendelea kusema, kweli akaingia ndani na nikaenda kumletea kinywaji….
Akawa anakunywa huku akiwa ananiangalia , akaniangalia kwa dakika kadhaa na mimi nilikuwa kimya, kwa maana sikuwa najua amekuja pale kwa lengo gani…
“ aneth mwanangu, akasema mama yake Julius …
‘ abee mama, nikaitikia…
“ naomba unisamehe sana bint yangu, kwa maana niliamua kufunga macho na wakat nilikuwa najua kuwa wewe ndio mwanamke sahihi kwaajili ya mwanangu, licha ya mapito uliopitia, naomba unisamehe sana , na uniombee msamaha kwa kijana wangu, kwa maana mimi ni mama, na sitaman kumuona mwanangu ananichukia kwa sababu ya mambo ya ajabu, akaendelea kusema mama yake Julius …
‘ huna haja ya kuomba msamaha mama, kwa maana hata kama ni mimi ningekuwa kwenye nafasi yako, huenda ningefanya ulichokifanya, so nisamehe na mimi kwa kukuibia mwanao, nikasema na mama yake Julius akatabasamu kisha akasema “ nimekuachia unitunzie, na mimi nikacheka…
Basi nikampigia simu Julius na kumuomba akipata nafasi aje nyumban mara moja…
“ unataka nije kufanya nini, au ndio umekiosha unataka nije kukiona, akasema Julius ..
“ wewe usiongee hivyo unajua, kwa maana hapoa nipo na mgeni so wewe ukipata nafasi nakukma urudi nyumban mara moja mume wangu…
‘ kwani huyo mgeni ni mama yangu, kwamba akinisikia kijana wake akisema kuwa napenda mapenzi, tena mapenzi yenyewe napenda kufanya na kamodo change, posh baby wangu yaan nimkunje mpaka achanganyikiwe, akasema Julius, nikaona nikate simu kwa maana namjua Julius huwa anapenda kuongea ujinga sana….
Sasa kumbe Julius alipoona nimekata simu akaanza kuogiopa akahisi kuna jambo baya huenda limenikuta, akaacha kila alichokuwa anakifanya na kurudi nyumban, alipofika si ndio akakumkuta mama, yake, akamsalimia pale kisha akanifata na kuninong’oneza kuwa “ kwa hio nilipokuwa naongea pale mama yangu alikuwa ananisikia, nikaitikia kwa kichwa, kwa ishara ya kukubali, aisee aliona aibu, ila mama yake hakutaka kuzunguka, akaomba msamaha pale,kisha akasema kuwa anaomba tusimsahau kwenye ndoa yetu, na tukakubali pale, kisha akaondoka zake…
Sehemu ya 37 na 38
‘ sasa kwanini hukuniambia kuwa kupo na mama yangu na wewe, akasema Julius ..
“ sasa ulikuwa unataka nikuambie vipi, na mama yako alikuwepo, nikasema ..
“ aaa umeshaniondolea mood ya kufanya kazi, siende tena kazin, akasema Julius kisha akanambia kuwa anataka tucheze mchezo..
“ mchezo gani? Nikamuuliza…
‘ yaan kila nitakachokiomba unatakiwa kusema amen, kwa maana nataka kukuapiza kisha nikisha kuapiza na wewe unaniapiza, na yoyote Yule ambae atakeuka kiapo lolote limkute, akasema Julius na nikakubali…
‘ haya sasa, upofuke ukinisaliti, sema amen, akasema Julius..
“ amen , nikajibu…
“ uingie period kila ukiwaza kunicheat sema amen..
“ amen, nikajibu…
“ ujikwae ukitoka nyumban bila kuniaga, sema amen ..
“ amen nikajibu…
‘ haya sasa na wewe niapize kabla hatujafunga ndoa, akasema Julius …
“ haya sasa, ukatike korodani kila ukiwaza kunicheat sema amen, nikasema nikashangaa Julius katoa macho kisha akasema amen ila ni kama hakuwa anataka vile…
“ uwawe ukikata kunitoa out sema amen, nikasema na Julius akajibu amen …
“ ufe ukitazama nyash sema amen , nikasema …
“ aweee mbona una viapo vigumu hivyo, aaa sitaki bwana, kwanza wewe hujui kucheza hata huu mchezo,yaan nife kwa vitu vya kijinga, sitaki bana, akaanza kulalamika Julius ..
‘ lakin si wewe mwenyewe ambae ulikuwa unataka maswala ya viapo, nikasema…
‘ basi yaishe na tunatakiwa kuwaza mambo mazuri kwa maana tunatakiwa kufunga ndoa soon, akasema Julius nikaanza kucheka na kumuambia , “ safari hii nimekukamata…
Basi mambo yakaendelea, na siku yetu ya ndoa ikafika, tukafunga ndoa, na Julius akaatatua tofaut zake na ndugu zake, na dada yangu nae ameacha kidanga, na amepata mwanaume na ameshamvisha pete, na japhet na mke wake, wameshafunga ndoa siku chache kabla ya ndoa yetu, na mama yake Julius ameenda kumuombea msamaha mwanae kwa mwanaume wake, na mumewe alikuwa hataki ila mwisho akamsamehe, na mama yangu anaendelea vizur sana….
MWISHO