KAHABA MLOKOLE
Sehemu ya 1
Siku moja nilikuja kustuka nimeamka na pemben yangu kulikuwa na mwanaume ambae sikuwa namfahamu, mwanaume huyo alikuwa amelala, na nilipo jiangalia nikaja kugundua kuwa alikuwa amelala na mimi, kiukweli haikuwa mara yangu ya kwanza kulala na wanaume ila kikawaida huwa kila mwanaume ambae huwa nalala nae huwa namkumbuka, ila siku hio ilikuwa tofaut kwani hata nilipokuwa navuta kumbukumbu zangu sikuwa nakumbuka kama huyo mwanaume ndio ambae alinichukua pale baa….
Naitwa aneth, ni bint wa miaka 23, ni bint wa kawaida ambae ninaishi maisha ya aina mbili, kwa maana kuna sehemu ukinikuta unaweza ukadhan mm ndio mfano wa kuigwa ila kuna mahala pengine ukinikuta unaweza ukanilaani kwa mavazi ninayo vaa na matendo ninayo yafanya…..
Basi baada ya kuamka na kutaka kuondoka Yule mwanaume akanishika mkono na kusema , ‘ nahisi kama sijaridhika, unaweza kunihudumia zaidi, nilimgeukia na kumuangalia na kukataa, kwa maana kwa muda huo nilikuwa natakiwa kufika nyumban, kwa maana mimi ndio mfanya usafi wa kanisa ambalo lilikuwa pale mtaani kwetu, sasa kama ikitokea sijafika mpaka wakat huo , basi watumishi wengine wakanisa wanaweza wakaanza kunitafuta kwa maana wanaamin huwa nalala kanisani, kumbe huwa napiga kishe zangu na kanisan ni kama kimbilio la mwisho na huwa naenda asubuh, nikitoka kwenye mambo yangu….
“ hapana siwez kulala na wewe tena, naomba niondoke , nikasema
Yule mwanaume akacheka kwa dharau kisha akasema “ tangu lini Malaya akakataa pesa, haya nambie unataka kiasi gani, kwa maana shoo yako nimeielewa, akasema Yule kijana…
Niliangalia saa, ilikuwa tayar saa kumi na mbili na nusu, na saa moja kamili kuna ibada fupi inatakiwa kufanywa kanisani, nikaona niondoke tu…
“ laki mbili, unaonaje nikikulipa laki mbili kwa sababu ya kunihudumia, akasema Yule mwanaume, na kiukweli nilipokuja kusikia hicho kiwangon cha pesa ni kama moyo wangub ulianza kulegea, nikageuka kisha nikasema “ sawa laki mbili kwa dakika kumi…
Yule mwanaume akakubali, na nikampa shoo, ila zile za haraka haraka, baada yab hapo akanilipa pesa yangu, nikaanza kuondoka, nikashangaa ananiita kisha akasema “ unaonaje kama ukiniachia namba zako za simu, kwa siku nyingine ambayo nitakuhitaji…
“ nafanya kazi pale kwenye baa ya golden flower, kama unashida na mimi, unaweza kuja pale na utaniona, nikajibu kisha nikaanza kuwah kanisan, na kumuacha Yule mwanaume akiwa ananiangalia tu…
Najua kuna watu watashangaa, ila siku zote kwenye maisha hakikisha haumhukum wala kumlaumu mtu bila kujua anayoyapitia…
Basi nikaenda kanisan na kweli nilikuwa nimechelewa na nilikuwa nimeshaanza kutafutwa, kwa maana sio kawaida kwangu kwa mtu kuja kanisan na kunikosa…
Kila mtu alieniona alitaka kujua kuwa nilikuwa wapi, haikuwa kazi sana kwangu kuwajibu kwa maana ni mara ya kwanza kukosekana kanisan hivyo ni ngumu sana kwa mtu yoyote Yule kunitilia mashaka….
Basi nikafanya majukum yangu na kwenye majira ya kama saa nne nikaenda ninapoishi, nilikuwa naishi na dada yangu yeye ndio aikuwa kahaba anaefahamika na mara kadhaa watu wa nje walikuwa wanasisitiza nimuhusie abadilike, kweli sikupenda tabia yake kwa maana yeye ndio kasababisha mm nikawa najiuza, kwa maana kwanza pesa yake hakuwa ananipa hata mia, na kingine tulikuwa tunahitaji pesa nyingi sana, na tukajiwekea kila siku kila mmoja wetu aweke elfu hamsini, ilikuwa ni ngumu sana kwangu kupata kiasi chote hicho cha pesa, ndipo siku moja dada akanitaka niende nae kwenye mizunguko yake ya ukahaba, nilikataa sana, ila alinilazimisha na kuniambia kuwa kanitafutia kazi ya usiku, ndipo nikakuta nikazi ya baa…
Nilikataa pia kufanya ile kazi, dada akanambia kua nikikataa basi anaomba nikapange mwenye maana hata mimi najua ni kiasi gani tulikuwa tunahitaji pesa, sasa antalau nikaona kama kazi ya baa ina nafuu kuliko kujiuza, na vile nitakuwa nafanya usiku ndio kabisa, kwa maana usiku naenda kazin lakin asubuh naendeLea na utumishi wangu wa mungu…..
Lakin haikuwa rahisi kufanya kazi tu ya baa usiku bila kujiuza, na kwa aina ya baa niliokuwa nafanya kazi, kila muhudumu pale alikuwa ni changudoa, na meneja alikuwa anazingatia sana kumfurahisha mteja, kwa maana mteja akikutaka kimwili ni kosa kumkatalia, kwa maana unamfukuza na baa yake inapoteza mvuto…
Mara ya kwanza ambayo nilitakiwa na mteja, nilikataa, ila sijui hata ilikuwaje maana mara ya mwisho nakumbuka huyu mteja, baada ya mimi kumkataa akataka nimpe kampan, basi nikakaa nae tukawa tunakunywa pale, na mm huwa situmii kabisa kilevi, lakin nilipokuja kuamka asubuh, Yule mwanaume ambae nilikuwa nakunywa nae alikuwa amelala pamben yangu, na mapaja yangu yalikuwa yananiouma sana, kwa maana nilikuwa nimetolewa bikra kipuuzi sana…
Nikaamka na kutaka kuondoka ila sikuwa naweza hata kupiga hatua, Yule mwanaume akaamka na kuanza kucheka kisha akasema ´una shoo mbovu sana, njingejua kama ni bikra wala nisingekugusa, akasema Yule mwanaume…
“ kwann umelala na mimi bila ridhaa yangu? Nikauliza kwa sauti ya ukali kidogo…
Yule mwanaume akacheka kidogo kisha akasema “ bila ridhaa yako ila kwa ridhaa ya meneja wako, pesa zako hizo hapo mezan, akasema Yule mwanaume akiwa anavaa kana kwamba alikuwa anataka kuondoka, nikaenda kumshika na kuanza kulalamika, ila alinisukuma huko kisha akawa ananambia kuwa anajuta sana kuninunua kwa maana hata hajafurahia shoo, kwa kuwa nilikuwa bikra..….
Maneno yake yaliniumiza sana kwa maana kwa fikra zangu niliamin kuwa mwanaume akikukuta bkra basi anakuheshimu sana, ila ilikuwa tofaut sana kwa huyu kijana, basi kwa tabu nikaanza kujiandaa na kurudi nyumban, na siku hio sikuwa naweza kabisa kwenda kanisan, kwa maana nilikuwa najisikia vibaya sana, dada yangu alirudi na kuanza kumlaumu na kumsimulia kilichonikuta, akacheka sana kisha akasema “ hio bikra ulikuwa unataka kuitunza mpaka lini, yaan ni bora ilivyotolewa ili uweze kukifanyia kazi kipochi manyoya chako vzr, akasema dada yangu alikuwa anaitwa wema….
Nilianza kukemea kimoyo moyo na kumuona kama anataka kunipeleka kwenye njia ya kuzimu, sikutaka kuendelea kumsikiliza, nikala zangu kisha nikalala…
Nimekuja kuamka da wema huyu hapa, alikuwa na juice na chips akanipa nile, ila hata sijui ilikuwaje, kwa maana mara baada ya kula kile chakula nikawa kama mwenda wazimu, nikaanza kumuomba dada wema anifundishe style mbali mbali za kukatika, akaanza kunifundisha pale, nikawa najifunza kwa juhudi, kana kwamba nikishamaliza kujifunza naenda kufanya mtihani, baada ya kunifundisha kwa masaa kadhaa, akaondoka zake kwenda kwenye kazi zake, na kuniambia kuwa leo nisitoke kwa maana afya yangu haikuwa sawa…
Basi siku hio ikapita na majogoo ya siku mpya yakapambazuka, na kama kawaida yangu misa ya asubuh haikunipita, na dada yangu alirudi, maana anakawaida ya kurudi kwenye saa nne hivi, alikuwa kachoka sana, na aliporudi alipitiliza moja kwa moja mpaka kitandani, alilala, na baada ya kulala aliamka kwenye majira ya kama saa moja kasoro usiku ambapo alienda kuleta chakula, ila safar hii nilipokula kile chakula nilikuwa na hamu sana ya mwanaume, na nikama kuna kitu alikuwa ameniwekea…
Basi nikaondoka nae mpaka kule baa, na siku hio mwanaume ambae alikuwa ananihitaji alikuwa ni baba mtu mzima, nikaenda kulala nae na ndio ikawa ni kawaida yangu sasa kulala na wanaume, na asubuh na mapema nawah kanisan, kushiriki kwenye misa ya kwanza na kufanya usafi kanisan, mpaka ilipofika ile siku ambapo niliamka pemben ya mwanaume ambae sikuwa namjua, na nilishangaa kwnn sikuwa namkumbuka Yule kaka, kwa maana sio kawaida kabisa, nilale na mwanaume ambae simjui hata mara moja….
Na ndio akaniomba shoo nyingine akanilipa laki mbili….
Kumbe Yule mwanaume alielewa shoo yangu bana, kwa maana siku inayofuata alikuja mpaka pale baa ambapo nilikuwa nafanya kazi, akataka siku hio ahudumiwe na mimi tu, nikakubali, kwa maana kwenye ile baa niliokuwa nafanya kazi , moja ya kosa kubwa sana ambalo linaweza kukufukuzisha kazi ni kukataa anachokitaka mteja kutoka kwako, ila nikawa namshangaa ananiangalia sana, yaan alikuwa ananiangalia mpaka nikawa naona aibu…
“ unajua wewe ni mzuri sana, nambie kwanini umechagua kuwa kahaba? Akaniuliza…
“ haikuhusu, wewe kama unataka huduma sema nikuhudumie na sio unakuja kuniuliza maswali ambayo sijaelewi kabisa, nikajibu…
“naona kama nimeshatosheka na unywaji, unaonaje kama ukienda kunipa ile huduma nyingine, akasema Yule mwanaume…
“sikukataa, kwa maana kwanza analipa pesa nyingi kulko mteja mwingine yoyote, kwa maana siku hio nayo aliniwekea laki mbili, nikasema sasa huyu ndio mteja bora, yaan leo naenda kumpa vyote alivyonipa mama…
Basi tumefika kwenye mtu kati nikaanza kazi, kidume kikaanza kutoa miguno polepole, mara ghafla akaanza kupiga kelele za utamu, ndio akawa kama ananizidisha munkari wa kujituma, nikajituma mpaka akawa hoi, kisha nikataka kuondoka pale chumban, nikashangaa ananivuta kisha akasema “ unaenda wapi?…
“ naenda kutafuta mteja mwingine , nkajibu…
Akashusha pumzi kisha akasema “ vipi kulala na mimi mpaka asubuh ni bei gani, kwa maana nilishawah kukuambia kuwa wewe ni fundi na kweli wewe ni fundi, na nakuhitaji mpaka asubuh, akasema Yule mwanaume, na wakat huo sikuwa hata namjua jina….
“ ongeza laki moja, akatoa wallet yake kisha akanipa laki na nusu, ikabidi nikubali, nikakaa nae mpaka saa kumi na moja na nusu, kisha nikamtoroka kwa maana nilikuwa natakiwa kwenda kuudhuria ibada ya asubuh kanisan na kufanya usafi, na mara baada ya kutoka kanisan, si nikashangaa namuona mtu kapaki gari kwenye ule mtaa wetu, nilipomuangalia vzr nikamuona ni Yule kijana, nilishtuka sana, kwa maana nilihisi atakuja kuivunja na kuiharibu taswira yangu pale mtaani, kwa maana ni yeye pekee ndio anajua kuwa najiuza, ila kila mtu anajua kuwa mimi ni bint mstaarabu na mwenye hofu ya mungu tena ni mfano wa kuigwa …..
Sehemu ya 2
Kuna watu wanauliza hizi hisia za kila siku tunazitoa wapi, labda niwajibu kabla sijaendelea na kisa change kuwa, tafuta kungu manga, saga kisha pika uji wako changanya na kungu manga, ina harufu mbaya ila kunywa, alafu jipe masaa, kuna ambao hisia zinapanda chap, kuna ambao mpaka muda flani upite, haya sasa tuendelee
Nilishtuka sana nikataka kumkwepa ila ni kama aliniona, akaja mpaka nilipo kisha akasema “ posh baby, nikajifanya sijasikia kwa maana jina langu la kwenye udanguro ndio hilo, nikawa naendelea kutembea, kuna mmama akapita akamuuliza “ samahn mama huyu bint anaitwa nani?
“ vipi kijana wangu na wewe unataka kumuona kwa maana kila familia inataman kijana wake aoe mwanamke kama huyu, kwa maana kwanza anaadabu sana na anahofu ya mungu mno, kila mtu hapa mtaan anampenda aneth wetu, akasema Yule mama, na mimi wakat huo nilikuwa naendelea kutembea…
baada ya kusikia jina langu nikamsikia Yule kijana anasema “ asante sana mama, kisha akaanza kunikimbilia na kuita aneth ..
sasa safar hii nikageuka na aliponifikia nikaanza kumuambia “ bwana yese asifiwe huku naangalia chini, Yule kijana akashangaa sana kisha akajibu milele amina, na kuanza kusema “ samahan, sijui kama ni nimekufananisha au kama ni wewe, kwan unalo jina lingine ambalo unaitwa posh baby? Akaniuliza ….
“ hapana sina jina kama hilo, mimi naitwa aneth Julius, hio posh baby ndio nini? Nikauliza, nikawa najifanya kama sijamuelewa vile, kwa maana niliogopa sana asije kuniharibia cv yangu pale mtaani….
“ owww sorry nitakuwa nimekufananisha nadhani, kama hutojal naomba tukae sehemu tuzungumze,akasema Yule kijana …
“ naogopa sana kuongea na wanaume maana naogopa sifa mbaya zisije kwenda kanisan kwetu, nakuomba kama unataka kunambia jambo lolote lile niambie mapema niondoke zangu, nikaanza kuongea kwa sauti flan ya aibu sana, kana kwamba ni bint flani nisie na hatia kabisa….
“ naitwa Julius , ni enginer, yaan nimesomea civil engeniering, na hapa nilikuwa namtafuta mtu ambad umefanana nae sana, kwani mpo mapacha? Akaniuliza….
“ hapana mimi naishi na dada yangu na dada yangu hata hatujafanana, yeye amefanana na baba na mimi nimefanana na mama, ila kuna mtu anasema pia kuna sehemu alishawah kuniona, nikamshangaa sana, kwa maana mimi mchana nashinda nyumban ila usiku huwa nalala kanisan kwa sababu mimi ndio huwan nafanya usafi asubuh kanisan na naandaa mazingira ya morning prayer kanisan kila siku, so huenda umenifananisha au kuna mtu kafanana na mimi kama unavyosema, nikajibu….
Yule kaka akahemA Kidogo kisha akasema “ sawa nimekuelewa mamaa, kwani unamahusiano….
“ shindwa kwa jina la yesu, shindwa pepo mchafu, unataka niwe na mwanaume ili nivunje amri ya sita ya mungu bwana wangu, mimi siwez kuwa na mahusiano halleluya, labda niwe na mume ila bado sijaqpata mume, nikasema na wakat nimeshanyanduliwa mpaka hata sijui idadi ya wanaume ambao nimeshawah kutembea nao….
“ samahan sana dada yangu, nahisi nitakuwa nimekosea sana, naomba unisamehe kama nitakuwa nimesema jambo ambalo halijakupendeza, akasema Julius na mimi nikasema “ hakika mwanaadamu yoyote anaemsamehe mwanadamu mwenzie basi mungu bwana wake atamsamehe na yeye siku ya mwisho, nikajibu, sasa Julius akahisi amekutana na mlokole mmoja kumbe ni bonge la danga, ila akawa kama anataman kuongea na mimi zaidi, ila sikuwa nataka, kwa maana mpaka wakat ule sikuwah kuonekana nimesimama au hata naongea na mwanaume hovyo barabaran so nilikuwa naogopa sana kuharibiwa taswira yangu….
Baada ya Julius kuona kama inashindikana mimi kukaa nae akakubaliana na mimi, ila akasema kuwa “ naomba kama hautojal unipe namba zako za simu…
“ sina simu mtumishi wa bwana, na kama ni namba za simu labda nikupe za dada yangu yeye ndio huwa anasimu, ila naogopa kwa maana sijui nitamuambia ww ni nani, nikasema na wakat huo nilikuwa naonge sauti flani ya unyenyekevu sana, yaan kama mtu angeniona angejua kuwa huyu dada ameiva kwenye mafundisho ya dini…….
Basi Julius aliongea ongea mwish akaondoka zake, ila akanambia atakuwa anakuja kunitembelea, nikakubali, na alipoondoka nikaanza kuhema kwa wasiwasi, kwa maana nilishangaa kwanini aje mtaan kwetu, na kingine nani amemuelekeza, na namna ambavyo nimeigiza ni kweli hajanishtukia au labdaq ameshtuka ila kaamua kuvunga tu, au ni kweli kwamba hajajua mimi ndio huyo posh baby baamed na mdangaji, nilikuwa na maswali mengi sana, ila hakuna swali hata moja ambalo nilikuwa na jibu nalo, nikaona nipuuzie na kuamin kuwa hajanigundua ……
Basi mida ilienda na kama kawaida nikawa najiandaa kwenda kazin, na kikawaida huwa natoka na nguo za heshima sana naenda kuzibadilishia mbele ya safar , na kama kawaida nikafika pale night club and bar nikaanza kazi yangu, nikiwa nahudumia wateja nikahisi nimeshikwa bega….
Kugeuka ni Julius, nikamuangalia nikashangaa anaanza kucheka kwa dharau kisha akasema “ unadhan mzuri ni wewe pekee yako, kuna watu ni wazuri bana na wanahofu ya mungu na sio kma wewe mdangaji , unaelalwa na kila mwanaume…
“ ndio umekuja kuniambia hicho tu au kun jambo lingine , nikauliza …
Akacheka kwa dharau kisha akasema “ lingine lipi na wakat wewe mwenyewe unajua kuwa wewe ni kahaba a.k.a mdangaji, mungu ananipenda sana, kwa maana nilikuwa nataka kuangukia kwenye mikono ya kahaba, la mungu akaona sio sawa, kijana wake kama mimi nianze kumpenda kahaba na kuna mabint wanahofu ya mungu na wameokoka na kumpenda bwana huko mitaani, ambao wapo kama wewe tu. So mungu kaamua kuniuonesha hawa wangu, na kwa taarifa yako kuna mtu amefanana na wewe kila kitu ila hana tabia kama zako, sasa nakupa tu taarifa Yule nitahakikisha namuona na wewe nakutumia tu, akasema Julius na hapo ndiopo nilipojiaminisha kuwa hajagundua kuwa mimi ndio alikuwa na mimi mchana na usiku yuko na mimi huyo huyo kwenye muonekano mwingine, sasa nikawaza huyu ni lazima nimchezee movie nan asije akajua kuwa anakuwaga na mtu mmoja huyo huyo kwenye maeneo tofaut……
“ unataka huduma au, maana sijui ni kwanini mpaka muda huu unaongea sana, nikasema …
“ nina laki moja, njoo unipe raha na ujue kuwa sitakaa nikuoe nitaoa mwanamke ambae ametulia, akasema Julius, nikawa namshangaa na kuna muda nikawa nahisi kama kalewa vile ila sikujal, nikaenda nae chocho nikaanza kumpa mauno, yaan alikuwa analia tu kuwa sitakuoa wewe, hata kama ukinichanganya siwez kuoa kahaba mimi, badala apige kelele za utamu anakaa kusema hatonioa, kwani alisikia mimi nikisema kuwa nataka kuolewa nae, nikawa najisemea…..
Basi tumemaliza, akawa kama kawaida yake hataki niende kutafuta wateja wengine, yaan kila akija pale anataka kulala na mimi mpaka asubuh, nilikuwa namshangaa sana kwa maana alikuwa anaonekana kama anapesa sana yaan kutoa laki mbili kila siku kwaajili ya kulala na mwanamke haikuwa shida kwake, niliona kama ananipa pesa nyingi sana na niliamin kuwa anauwezo mkubwa sana….
Basi kama kawaida asubuh nikamtoroka, ila ile nafika tu mtaani naona gari lake, sikutaka hata kupita maeneo lilipo, nikapita vichochoron nikaingia zangu kanisani, sasa ile morning prayers ilipoisha huwa tunaomba kabla ya kuondoka, sasa nikiwa nimefunga macho naomba zangu nikashangaa nashikwa mikono kana kwamba kuna mtu anatakan kuomba na mimi kisha akasema “ namuomba mungu dua zako zipokelewe mrembo, kufungua macho Ni julius…
Sehemu ya 3 na 4
Alikuwa ananukia pafyumu yangu, ila wakat huo nilikuwa nimeshabadilisha nguo na nikiwa kwenyeb upande wangu wa uchamungu hata manukato sipakagi….
Nikashangaa Julius amenikumbatia kisha akasema “ naomba nisamehe sana mamaa, naomba nisamehe mno, ni tamaa tu zinaniponza ila wewe ndio mke, wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, nakupenda aneth…
“ samahan kaka Julius kwanini unaomba msamaha na wakat mimi sio mke wako wala sio mpenzi wako? Nikajifanya nauliza…
akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ nataman sana kukuoa , sijui kama utakubali kuwa na mimi, na kingine nataman leo kutoka kidogo na wewe, ikiwezekana unipelek unaposihi na nikununulie baadhi ya vitu..
“ nakuomba kaka yangu, mimi nawajua wanaume, sitaki kuanzab kufanya mambo ya kumuudhi na kumkera bwana mungu wangu, huwa naogopaga sana kutoka na mwanaume, kwa maana sijawah kuwaamin hawa viumbe na ikibidi kutoka na mwanaume kwenda nae sehemu ypoyote ile, basi niwe natoka na mume wangu na sio wanaume wa mtaani tu, nikaanza kujielezea hapo, mpaka Julius akaanza kutabasamu na kusema “ hakika wewe ni zaidi ya mke mwema ….
Basi akawa anataka kushinda na mimi mchana kutwa, nilikuwa nachukia mno, kwa maana mchana ndio muda wangu wa kupumzika, sasa mtu anakuja na kutaka niwe napiga nae story tu, mpaka nikawa namshangaa huwa anaenda kazin saa ngapi, kwa maana namuona kama muda mwingi anahangaika na mimi, yaan mchana anahangaika na mimi aneth mlokole na jion anahangaika na mimi posh baby mdangaji……
Basi siku zikaenda, sasa siku moja Julius akaniuliza, na hapo sijamuona club kwa karibu mwezi mzima, akawa anakuja kukaa na mimi mchana tu, akiniambia kuwa hataki tena kuvunja amri ya mungu na wakat mimi nipo, na hapo sikuwa direct kama nimemkubali au laa, japo vihela hela vyake nilikuwa nakula, na alikuwa anaonekana kama anania thabit kabisa ya kunioa, ila nilikuwa naoopa hatab kukubali, kwa maana niliogopa sana siku ambayo akija kujua kuwa Yule anaemkatikiaga mauno ndio huyu huyu ambae anataka kutangaza nia nae….
Julius akabadilisha hadi kanisa la kufanyia ibada, kwa maana mimi nilikuwa mlokole nay eye alikuwa ni mkatoliki, ila akawa kila jumapili anakuja kusali kwenyen kanisa ambalo nilikuwa nasali, na alikuwa ni miongoni mwa watu ambao wanatoa sadaka sana kanisani….
Baada ya Julius kuzoeleka pale kanisan, alienda kumueleza baba mchungaji jia yake kuhusu mimi, mchungaji akawa ananimwagia sifa na kusema , kila kijana ambae anakuja kwenye hili kanisa huwa anataman sana kumuoa huyu bint kwa maana anaadabu na maadili mazuri sana, kuliko mabint wengi wa huu mtaa, akawa anasema mchungaji na kumtaka Julius awe anaenda na mimi kila siku jion kuhudhuria ibada ya ndoa, kwa maana Julius alikuwa serious sana na kunioa, na hapo amepunguza sana kuja club akihisi kama mimi nampeleka kwenye njia mbovu…
Siku ya kwanza ambayo alikuja kanisan kwaajili ya elimu ya mahusiano, sasa wakat ambao tunatoka, nikashangaa ananikumbatia, hapo mimi najifanya naangaliua chini tu, kana kwamba naonewa, kisha akasema “ sitaman nivunje usichana wako kabla ya ndoa, ila naomba walau tukiss tu, kwa maana mimi ni mwanaume na nakupenda sana aneth, nashindwa kukaa mudea mrefu na mwanaume ninae mpenda na nisifanye nae chochote, nashindwa mamaa, akawa anasema Julius ……
“ hakika Yule anaeitaman dhambi nay eye ni mtenda dhambi, kwanza tunaambiwa, muovu atamuoa muovu mwenzake, nadhan unatakiwa ukatafute muovu mwenzio ili akupe unachokitaka kwa maana najua nikikubali leo utataka tuvunje na amri ya sita, kwa maana wanaume mimi nawajua, nikaanza kujitetea hapo…
“ no mamaa just a kiss, yaan bus utu kwa maana am soo high, akasema julisu, nikajifanya najinunisha na kumuambia kuwa sitakaa niwe karibu nae tena, kwa maana anataka kunipeleka dhambini…….\
“ sijamaanisha hivyo naomba usiende mbali na mimi, akawa analalamika Julius ila mimi nimejinunisha na nikawa nataka kuitumia hio kama ticket ya kuachana nae, kwa maana niliona kama siku akija kujua ukweli atanilaumu sana….
Akawa ananiita ila sikuwa hata naitika nikawa anendelea zangu na safar zangu nay eye anakazana kuniita tu…
Nimefika nyumban nikamkuta dada yangu ndio anajiandaa ili aende kwenye shughuli zake, akaniona kama siko sawa ikabidi aniulize nina shida gani…
“ una kumbuka nilishawah kukuambia kwua kuna mwanaume ambae nikiendaga kwenye zile kazi zetu yeye ndio huwa ananinunua kila siku, nikasema …
“ ndion nakumbuka, akajibu dada yangu..
“ sasa Yule mwanaume amekuja mtaan na anataka kunioa mimi, nikawa sijamkubali wala sijamkataa, kwa maana anajua kuhonga , sasa leo akawa anataka kunibusu, nikakataa kwa maana naogoa tusije kufika mbali na aje kugindua kuwa mimi ndio Yule wa club na ndio huyu mlokole, kwa maana anaonekana kuamin kama wa club ni mwingine na huyu anaeshinda kwenye nyumba za aibada ni mwingine, nikasema….
Dada yangu akaanza kucheka kisha akasema “ safar hii umepatikana …….
Basi muda ulienda na huwa dada yangu anaondoka mapema kabla yangu, kwa maana kwanza kila mtu mtaan anajua kuwa anajiuza, ila mimi hakuna anaejua na mara nyingi huwa wananiambia kuwa niongee na dada yangu aache hizo kazi, bila kujua hata mimi nazifanya sana….
Basi mida yangu ikafika, na kama kawaida yangu nikatoka mtaan na mavazi yangu ya heshima, nikaita boda hadi kazin, nimefka kazin nikaambiwa kuna wageni wangu….
Nimefika, nikamkuta Julius, na watu wengine wawili, ila mmoja aliponiona alisimama na kusema “ wewe unafata nn huku, alikuwa ni kijana mmoja ambae nilisoma nae chuo, na alikuwa ni rafiki yangu sana, kiasi kwamba tulikuwa tunaweza kusoma wote mpaka asubuh na tukalala sehemu moja bila hata kutamaniana, aliposimama nikamkumbatia kisha nikamuambia kuwa , naitwa posh baby7, plz naomba usiniite jina langu hapa, na usimuambie mtu yoyote Yule jina langu halis, akakubali ila wakat wote Julius ananikata jicho mimi pamoja na huyo kaka alikuwa anaitwa japhet, kisha akasema “ huyo sasa hivi ni chagudoa, kwa hio usifikiri yuko kama rafiki yako wa zaman, sasa hivi ni kahaba, akawa anasema Julius mpaka japhet akawa anahsngaa kwann mwenzake ananiongelea vibaya hivyo….
Sehemu ya 5
Julius kuwa na adabu, kwann unamuongelea kama mtu unaemchukia sana, embu nambie amekukosea nini? Akauliza japhet ..
Julius alicheka kwa dharau kisha akasema “ tangu lini mimi nikawa na muda wa kuchukiana au kugombana na Malaya, naomba uniheshimu, nilikuwa nakupa tahadhar tu kuwa huyo mwanamke ambae unamuona kama rafiki ni changudoa, tena wale machangudoa waliobobea kabisa, yaan hachagui umri 3wala rika, hawaangalii sura wala tabia, wao ni pesa tu, yaan pesa ndio kipaumbele chao, so nikama nilikuwa nakupa tahadhar tu, kwa maana nakuona kama umeshachanganyikiwa sana, akawa anasema Julius ..
Nina uhakika haumjui huyu mwanamke so naomba usimuongelee kama unamjua sana, akasema japhet kisha akanishika mkono na kutoka na mimi pemben…
“ embu nambie aneth unashida gani mamaa, kwa maana naona kama maisha yako hayapo sawa, na kwanamna ambavyo nilikuwa nakujua ulikuwa ni bint wa kanisa, bint ambae ulikuwa na maadili sana, ila sasa sijui hapa katikat ukakutwa na kitu gani mpaka umekuwa hivi, akasema japhet …
Maisha ndo yamenifanya nikawa baamed, maisha ndio yamenifanya nikawa kahaba, maisha ndio yamenifanya niwe nilivyokuwa leo, ila hata mimi sipendi kuwa hivi, kwa maana naumia sana, kuona kuwa nautumia mwili wangu kama chanzo cha kipato, nikawa nasema kwa sauti ya majonzi…
“ lakin una cheti kizuri sana na wewe ni miongoni mwa wanafunzi bora sana pale chuon na najua pia ulipata GPA nzuri sana, lakin bado sielewi kabisa kwanini umekuwa hivi, akawa anaendelea kuuliza japhet..
ila wakat wote Julius hakuwa na aman, alikuwa anajipitisha pitisha tu kana kwamba kuna kitu anatafuta kumbe roho inamuuma kama nini, alitaka kujua naongea nini na japhet, ila ndio ujasiri wa kuja na kutuuliza kuwa tunaongea nini ndio hakuwa nao kabisa…
Alijipitisha pitisha mpaka ikawa kero sasa, kwa maana alikuwa kama hataki kuniona naongea na japhet, basi muda ulienda na Julius ni kama uzalendo ukawa umemshinda, ikabidi atufate kisha akasema “ unajua leo sirudi kabisa nyumban, so kama hautajal naomba tukawah vyumba kwa maana hii sehemu naijua vizuri, ukichelewa kidogo unaweza ukakosa chumba, ukajikuta unalala kwenye kordo, akasema Julius kumuambia japhet na mimi alikuwa ananiangalia kwa jicho la chuki, kana kwamba nimemuibia kitu….
“ na siunajua nilivyokuwa nimechoka, akawa analalamika Julius na japhet akakubaliana nae, kwa maana hakuwa anaujua utaratibu mzuri wa ile sehemu,…..
Na kweli vyumba viliisha vikawa vimebaki viwili, na wao walikuwa wapo watatu, kwa maana ya Julius , japhet na mwenzao mwingine ambae alikuwa anaitwa Emmanuel, huyu emanuele muda wote alikuwa kimya, na ni kama wenzake hawakuwa wanamfanyia vzr, kwa maana japhet alikuwa amekuja kukaa na mimi, na Julius akawa anazunguka zunguka kana kwamba amepotea au amekanyaga mdudu …
Ikabidi japhet na Julius walale chumba kimoja na ima ndio akaenda kulala kwenye chumba kingine…
Wamefika chumban akili ya Julius haikuwa sawa kabisa, kwa maana aliamin kuwa, kwa kuniacha pale reception basi ni lazima nitanunuliwa na mwanaume mwingine, akawa anajishangaa ni kwanini ana wivu sana na mimi, na wakat anampenda mwanamke mlokole huko na mimi alipanga kunitumia tu, yaan malengo apange na aneth ila hamu zake mimi ndio nimtoe, akiamin kwa kufanya hivyo, atakuwa anahisi yuko na aneth kitandani, kwa maana kwa namna aneth alivyo , aliamin asingekubalia kulala nae mpaka ndoa, na wanaume ni ngumu sana kuvumilia hilo, ila ndio akawa anajipa moyo kuwa Yule ambae amekutana nae ambae ana taswra ya kilokole, na anakutana nae kila wakat ndio mwanamke wake sahihi bila kujua ni mwanamke mmoja….