
za Mapenzi, Maisha na Uchawi Mautundu Kitandani
CHUMBA CHA MASSAGE
Sehemu ya 25 na 26
Basi nikaanza kufanya kazi pale kama msimamizi mkuu wa ule mgahawa, lakin kitendo cha kuwa simsikii wala simuoni jmo nikajikuta nakosa raha, bila kujua kuwa nakosa raha kwa sababu gani, sikuwa na amani, sikuwa sawa kabisa yaan, kila siku nikawa najikuta kama nammiss sana…
Nilifanya kazi pale kwa karibu miezi mitano, mpaka lile eneo nikawa nimezoeleka sana, kila mtu akawa ananijua, mpaka wakawa wananipa oda za kupika kwenye maharusi yanayotokea pale kijijini, mpaka wakawa wananiita dada mpishi, jina langu likawa maarufu sana pale kijijini, hakuna mtru ambae alikula chakula kwenye ule mgahawa akaacha kutoa sifa, ila nilikuwa najikuta kama sina amani hivi, yaan sikuwa na raha kabisa, kuna kitu nilikuwa kama nakikosa kwenye maisha yangu, sikuwa na aman kabisa, na sikuwa najua hio hali inatokana na kitu gani…
Maisha yakaenda, ila pale kijijin akaja kijana mmoja, alikuwa ni mtoto wa mmoja wa wakulima, alikuwa kama ndio msomi wa kijiji, kwa maana ndio alikuwa kijana pekee ambae alibahatika kufaulu kuendelea na kitato cha tano na ndio kijana pekee ambae alifika chuo kikuu, sasa pale kijijin yeye na familia yake ilikuwa inaheshimika sana, kila mtu alikuwa anawaongelea wao tu,sasa alipofika pale kijijin akaambiwa kuna mgahawa ambao ulikuwa na msichana mrembo, ni kama wazaz wake walitaman kijana wao awe na mm…..
Basi bibi mimi siku hio nimekaa zangu napika, nikashangaa kuna mtu anakuja kunisalimia jikoni, n nilishanaa sana kwa maana hatujawah kuruhusu mtub yoyote Yule aje jikon tofauti na wapishi, nikaitikia salamu yake ila nikawa kama namshangaa hivi, kwa maana kwanza sikuwa namfahamu kabisa yaan….
Naitwa Hassan, yaan unaweza kuniita Hassan, akanambia…
“ nashkuru sana kukufahamu, lakin sidhan kama unastahili kuja huku kama wewe sio mpishi, sasa sijajua lengo lako n inn, nikasema …
“ owww am soo sorry cute, hapa kijijini wananiita enginer, au raisi wa kijiji, siunaniona the way nipo very handsome na nina harufu ya hela, akasema Yule kijana….
Nikaona ananizingua na engilish yake, kwanza hana adabu, anaweza vipi kuingia jikon bila idhini yetu, na kingine, nilikuwa namuona kama mshamba tu, maana mwanaume mzima sifa kibao, si kujidhalilisha huko….
“ why are you loking to me like that cute, nina hela, nambie unachotaka nitakifanya si unajua natakiwa to marry beutifull girl like you, akasema Yule kijana….
Nikaanza kujiuliza, yaan na uzungu na usomi wake wote anaojishauwa nao kumbe amekosa wanawake huko mjini wenye hadhi yake anakuja kutafuta wanawake kijijini, nikaanza kumuona kama zwamwamwa tu, asie na mbele wala nyuma, nikamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha nikassema “ nakuona kibosile, fanya siku basi unitoa out kali mjini, yaan tukale pesa na tutumie pesa ituzoee si unajua…
“ don’t worry beutifull pesa sio kitu, nambie kwanza umenikubali, akasema Yule Hassan …
‘ hakuna mwanamke yoyote hapa kijijin ambae anaubavu wa kukukataa wewe, so nadhan hata mimi ni mwanamke ni ngumu kumkataa mwanaume msomi na mwenye pesa kama wewe, nikasema, nilikuwa najisemea ili aondoke tu kwa maana nilikuwa naona kama ananikera na sifa zake za kipuuzi …
Kumbe alikuwa anapata kichwa na nikawa namshangaa kwamba hajion hata kama amekaa kishamba shamba, au ndio watu wa kijijini wamezidi kumuongopea tu, kwa kuwa amesoma kidogo na amefika mjini….
Sehemu ya 27 na 28
Kwanamna alivyo namasifa akaingiza mkono mfukoni kisha Akatoa elfu kumi kisha akanipa na kusema “ ukiendelea kunifurahisha nitakupa zaidi, niliona kama ni pesa ndogo sana, kwa maana jmo anaweza kukumwagia hata laki mbili alafu hata haring, ila huyu nyang’au anakuja na elfu kumi anajiona fogo kumbe hamna kitu, ila sikutaka kumvunja moyo nikapokea …
Nikajichekesha chekesha pale kama nimeona bia vile lengo aondoke tu, basi akaniaa akanambia kuwa jumapili ya wiki hio atakuja anichukue anipeleke mjini, na ataniletea na nguo, nikamshukuru pale kisha akaondoka zake…
Basi siku zikaenda na ile jumapili ikafikia, akaniletea lisket la marinda, aiseee nikawa najiuliza huku vijijini ndio nguo za maana nn, kwa maana mm kweli nikae navaa nguo za marinda kweli, labda kama sio mimi, basi nikaenda kutupia mitupio yangu, yaan nilivyotoka hata hakuamini, akanishika mkono hao mpaka kwenye pikipiki ya kijiji, hapo tukapanda mshikaki mpaka sehemu ambapo ndio kuna magari ya pale kijijini, tukapanda gari na kwenda mpaka mjini…
Tulifika sehemu sikuwa najua hata inaitwa je, kulikuwa kuna mgahawa mkubwa na kakibanda cha chipsi pemben, sasa kwa mawazo yangu nikajua kuwa Yule kijana anataka kunipeleka kwenye ule mgahawa, kumbe hana ushuzi, hata mm naweza kumtoa out na nisitangaze…
Akanambia kuwa anaenda kutoa hela nimsubiri hapo, nikaona nisijicheleweshe nikaingia kwenye ule mgahawa nikatafuta sehemu nikakaa, nilivyokaa nikamuona kwa nje,
yuko kama ananiangalia kama haamin vile, akaja mpaka nilipo kisha akaninong’oneza na kusema “ nilikuambia unisubiri pale nje lakin mbona umeingia hapa…
“ hata kama ningekusubiri si tungekuja tu hapa si ndio, nikasema …
“ wewe mimi sina hela za kununua chakula hapa, hapa sahani ya chakula ni elfu arobaini na tano, sina hio hela mimi, akaanza kulalamika…
Nikaanza kumshangaa, kwa maana kwa namna ambavyo alikuwa na masifa nilijua ni lazima atanipeleka pale, la hata hakuwa anajisumbua kabisa, kwa maana pemben ya lile eneo kulikuwa na kakibanda cha chips nikahisi ndio alitaka kunipeleka pale naanze uongo uono wake nimuamin, na hajui kuwa nimeshawah kufika town, sina ushamba kiasi hicho……
Basi bana nikamuona kakosa raha, nikaagiza chakula nikamuona kama anataka kulia vile, yaan aliona kuwa ile
siku ya kuosheshwa vyombo imeshafika, na nikaagiza sahani mbili za chipsi kuku, yaan yangu na yake, na juice kubwa zile za azamu, yaan jumla ya bili ilikuwa ni elfu themanini na kitu,
alikosa raha hata kula hakuwa anaweza kabisa, nilijua, na nilitaka kumfundisha adabu kuwa sio kila mwanamke ni mshamba kama anavyofikiria, sasa tukiwa pale nikamuona jmo anaingia eneo lile na mwanamke pisi huyo, alafu amevaa hovyo, yaan kitendo cha yeye kuingia pale macho yetu yakagongana, nikaanza kusikia wivu wa ajabu, roho ilikuwa inaniuma kinyama, nikampa Yule mwanaume laki ambae nilikuwa nae, nikamuambia akalipi, hakutegemea, lakin kitendo cha Yule Hassan kunyanyuka, nilijikuta nashindwa kujizuia kumtazama jmo, na alivyokuwa anamakusudi akanikonyeza mpaka nikajikuta napaliwa na kuanza kukohoa….
Yule kijana alipo rudi nikaanza kumnyishwa juice kwa mapozi, hapo kijana wa watu haelewi kama nafanya vile kwa sababu gani, akajua ndio mapenzi hayo, kwanza nimemlipia pesa ya chakula, pili nimenanza kumnywisha juice, akaona kama nimekolea kwenye penzi lake kumbe kuna mtu namkomoa, yeye anacheka cheka tu kama kapewa bia ya offer vile…
Jmo akanikata jicho, yaan nilipomuona anaumia ndio nikaanza kujisikia vizuri sasa, nikaona kama dawa inaanza kumuingia sasa , nikazidisha mbwembwe, yaan mara
nimbus mara nimsike kidevu basi tafrah tu ilimradi nimuone anahangaika ……………
Basi bana kuna muda Hassan akaamka akawa anataka kwenda uani, nikabaki mwenyewe, nikamuona na jmo nae anaamka pale alipokaa lakin muda wote macho yake yako kwangu, yaan alikuwa ananiangalia kama ananidai vile………….
Sikumjali kabisa nikawa naendea zangu kunywa juice kwa maana nilikuwa nimeshamaliza kula chakula, nikashangaa anakuja kwenye meza ambayo nilikuwa na kaa akanipamia, aliponipamia nikamuuliza vipi, aiseee alinigeukia akanikata jicho kisha akaondoka zake…..
Sehemu ya 29 na 30
Nilishangaa kwann alikuwa ananifanyia vile ila sikumjali, baada ya dakika chache alirudi, na aliporudi akaenda mpaka alipo mwanamke wake kisha akamshika mkono kana kwamba anataka wanyanyuke ili waondoke, na mimi sijui
hata kichwa change kilikuwa kinawaza nn, nikamuomba Yule mwanaume anyanyuke na aniinue kisha anikiss, sasa
lilivyoboya likafanyab hivyo kweli, akaamka kisha akanipa mkono na mara baada ya kunipa mkono akaninyanyua , wakat huo jmo na mwanamke wake wanakuja tulipo kwa maana walikuwa nyuma yetu na sisi tulikuwa mbele, so nilazima watupite ili waweze kutoka nje, basi bana Yule hassan akawa anataka kunikiss, nikashangaa mkono umewekwa kwenye mdomo wake kisha nikashikwa mkono jmo akawa anataka kuondoka na mimi….
“wewe vipi mbona anaondoka na mwanamke wangu, akaanza kulalamika Hassan….
Jmo hata hakumjibu, akamgeukia Yule mwanamke aliekuwa nae kisha akasema “ naamin nimeshakulipa, hizo raha ambazo ulikuwa unataka kunipa mimi mpr huyo kijana na utanipigia nikuongezee malipo, akasema jmo akiwa anaondoka na mimi…
“ wewe vipi unanipeleka wapi?, mbona unanikokota nikaanza kulalamika, ila hata jmo hakunijibu kitu akawa kimya tu akanipandika kwenye gari kisha nikashangaa tunaenda kwenye nyumba moja kubwa kumbe kulikuwa ni kwa wazaz wake, kisha akanishusha na kusema “ naamin mtaweza kumchunga vyema maana kuna muda kichwa chake hakifanyi kazi vzr, naomben msimruhusu alisogelee
geti au mlango kwa namna yoyote ile, akasema jmo kisha akaondoka zake…
Sikujua kwann alisema vile, na baada ya yeye kuondoka akaja mfanya kazi akanipeleka chumban kisha akanambia nikitaka chochote nitampigia, kwa maana kuna simu ya mezan hapo, nikakubali nikaanza kushangaa nyuma yaan, na ushamba wanu nikaona kama nipo ikulu vile………
Basi nilikaa pale ndani mpaka jioni hivi, nikawa nasikia nje vigelegele, hata sokuwa naelewa kuna nn, ikabidi nitoke nje nichungulie kuna nn…
Nikashangaa namuona mama yangu na Yule mdogo wangu wa kiume, pamoja na sikujua na sikuzani na Yule shoga yangu neema na mama bonge, yaan walikuwa wamevaa kama wanaenda harusini vile….
Mara mlango ukafunguliwa akaingia bint hata sikuwa namjua, alikuja na gauni akanambia kuwa kuna mwanafamilia pale alikuwa anafanyiwa birthday hivyo natakiwa na mm nijiandae, nikakubali hapo bila kujua kama ni kweli au laa, basi akaanza kunipaka na makeup pale kisha
akasema nakuja, akaondoka zake, akaniomba nisitoke mpaka nitakapo kujab kuitwa, baada ya kama nusu saa hivi, akaja jmo akiwa amevaa kanzu kaangalia chini, hapo sikuwa naelewa kumbe ndio nimeshaolewa hivyo, akaambiwa muombee dua mkeo kisha umpe glass ya maziwa na mswali rakaa mbili, jmo ni kama alikuwa na wasiwasi kwa maana hakujua lile jambo nimelichukulia vipi, akawa ananisogelea akiwa ananiangalia kwa makin, kana kwamba anajiadhari kama kuna jambo lolote lile nitataka kumfanyia, n nikapewa karatasi nikaambiwa nisigni nikasign pale na hapo ndipo jmo kidogo akapata nguvu ya kunisogelea….
‘ bwana juma umeshamuoa bibie nachien na mwenyezi mungu awasimamie kwenye ndoa yenu, akasema shehe kisha akatoka zake nje, na alipotoka mama yangu akaja akaanza kunipa usia pale, wakat wote juma aka jmo anaangalia chini tu, kana kwamba hayupo vile, na baada ya mama kutoa usia akatoka zake nje tukabakishwa sisi wawili, jmo ni kama alikuwa na wasiwasi kunisogelea……
“ mama samahan sana, najua nimechukua maamuzi bila kukushirikisha na tumepiga ndoa ya mkeka tu, ila sikuwa na namna, nilitaman siku ambayo nikioa nifunge ndoa kubwa
ya kifahari ila huenda mungu ndio alipanga ndoa yetu iwe hivi, sina uhakika kama unanipenda au laa, ila nina uhakika kuwa mimi nakupenda sana na hicho ndio cha msingi, kwa maana Mwenyeb zi mungu mwenyewe anasema wanaume wawapende wake zao na wanawake wawaheshimu waume zao, so jitahidi uniheshimu hata kama hunipendi, akasema juma…