Thursday, May 1, 2025

Ukimheshimu Mke wako na Watu watakuheshimu pia - Fahamu haya

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 UKIMHESHIMU MKE WAKO NA WATU WATAKUHESHIMU PIA

 

Kanuni ya kwanza ya maisha: Ili kuheshimiwa kama mwanaume, ni lazima watu wamheshimu mwanamke wako! Najua inaweza kuonekana kama jambo dogo, lakini ndiyo ukweli. Kama watu hawamheshimu mwanamke wako, basi jua hata wewe wanakudharau. Iwe ni mama yako mzazi, dada yako, au marafiki zako, ni lazima wamheshimu mwanamke wako. Hapo ndipo utajua kwamba wanakuheshimu wewe.

Labda nikupatie mfano: Umeoa, kama mama yako anamtukana mke wako, kama dada yako anamtukana mke wako, au kama jirani au rafiki wanamzungumzia vibaya mke wako mbele yako, si kwamba hawamheshimu mke wako tu, bali wanakudharau wewe. Wanakuona kama mwanaume ambaye huna uwezo wa kuwa na mke anayestahili.

Mfano: Wanasema, "Mke wako hana akili," usichekelee, kwani ni kama wanakuambia, "Huna akili ya kuoa mwanamke mwenye akili!" Mfano mwingine, mama yako anamtukana mke wako na kusema, "Mjinga umekuja kula tu hapa, unajaza tu choo na kutumia pesa za mwanangu!" Hapo hawamtukani mke wako tu, bali ni kama mama yako anakuambia wewe ni fala huna uwezo wa kumchagua mwanamke mwenye akili.

Ndiyo maana mimi, hata kama mke wangu amekosea, hata kama mke wangu humpendi, nilazima ujue kwamba unapaswa kuongea na mimi kwanza! Huwezi kumtukana mke wangu na mimi nikacheka. Hata kama ni mama yangu mzazi au ndugu, ukianza kumtukana mke wangu na kisha unakuja kwangu kunichekea, nitakuona kama mnafiki.

Kama kuna kitu, njoo uniambie! Shida inakuja pale ambapo wewe mwanaume unamtukana mke wako mbele za watu, unamdhalilisha na kusema hana akili. Hapo, wale watu wanakudharau kwa kuona huna akili ya kuchagua na kumiliki mke mwenye akili. Kwa hiyo, mheshimu mke wako na watu watakuheshimu pia!

Add Comments


EmoticonEmoticon