Thursday, May 1, 2025

Tabia ya Kutaka KUM-CONTROL Mwenza inavyosababisha Migogoro ya Kimapenzi

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


Tabia Ya Kutaka Kumdhibiti Mwenza Husababisha Migogoro Ya Kimapenzi


Fahamu viashiria vya tabia hiyo,vyanzo vya tabia hiyo na ufumbuzi wake

migogoro ya kimapenzi yenye kujirudia rudia huwa inajitokeza pale ambapo mwanaume au mwanamke anachukua jukumu la mzazi wa mwenza.Kwa maana inaitwa parenting your partner kwa maana ya tabia ya kumchukulia mwenza wako kama vile ni mtoto mdogo hivyo muda wote unakuwa unamrekebisha tabia na kumuelekeza nini cha kufanya.

badala ya mahusiano kuhusisha watu wawili wenye akili timamu inakuwa kinyume chake inakuwa mama-mtoto au baba-mtoto .
Mwanamke anachukua tabia ya mama mzazi au mwanaume anachukua tabia ya baba mzazi mahusiano yanakuwa na taswira ya mzazi-mtoto badala ya mke-mume.

katika mahusiano haya Mwanamke au mwanaume anajiona malaika,anajiona mkamilifu,anajiona mwerevu sana,anajiona hana dosari yoyote kisha mwenza wake anaonekana mjinga, anaonekana mzembe, anaonekana hajielewi saa 24.



VIASHIRIA VYA MWANAUME/MWANAMKE MWENYE TABIA YA KUTAKA KUM-CONTROL MWENZA WAKE KATIKA MAHUSIANO NI:


Viashiria vya mwanaume au mwanamke ambaye anataka KUM-CONTROL mwenza wake ni kama ifuatavyo:


1. KUMKOSOA MARA KWA MARA
Kama utakuwa na tabia ya kutaka KUM-CONTROL mwenza wako au Mwenza wako yupo na tabia ya kutaka kukucontrol ataonyesha tabia zifuatazo.
Ikiwa wewe ndiyo mkosoaji kupitiliza juu ya tabia za mwenza wako utaona viashiria vifuatavyo
-Unamkosoa mwenza wako kwenye kila kitu utakosoa muonekano, lafudhi,harufu ya mwili, matumizi ya fedha, utembeaji wake, uvaaji wake,utakosoa marafiki zake, vipaumbele vyake,tabia zake, elimu yake,utakosoa kazi yake,

-utakuwa unapata hasira kupitiliza mara kwa mara ukimuona mwenza wako kwa sababu utamuona mkosaji saa 24,makosa ya mwenza wako ni kama vile kuchelewa kurudi nyumbani,kutumia simu muda wote,usafi, uvaaji,afya yake na namna anakabiliana na matatizo yake binafsi,

mara kwa mara utamuona mwenza wako hana tabia nzuri inayokufaa ukiwa mbele ya marafiki zako pamoja na ndugu zako,mara kwa mara utamuona mwenza wako anakuaibisha tu,hauwezi kuona jema lolote kwa mwenza wako.

Tabia ya kumkosoa mara kwa mara inaweza kusababisha muanze majibizano, kupeana kashfa na tuhuma za usaliti, kutishiana kuachana, kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kugombana,kuitana majina ya wanyama kama vile "mbwa",kuambiana maneno makali sana kama vile "hauna akili" mara kwa mara.

2. KUBEBA MAJUKUMU YA MWENZA WAKO
Kama utakuwa na tabia ya kutaka KUM-CONTROL mwenza wako au mwenza wako yupo na tabia ya kutaka kukucontrol utaona mambo yafuatayo.

kwa mfano wewe ni Mwanamke unaweza kufanya kazi za usafi nyumbani ,kulea watoto,kupika,kufua, kuuguza wagonjwa nyumbani,kulipa ada za watoto shuleni,kulipa kodi ya nyumba au utajenga nyumba kwa gharama zako tu,utasimamia kazi au biashara wewe pekeako wakati huohuo upo na mwanaume ndani ambaye hana kazi,hana biashara, hajishughulishi kwa chochote,hana MSAADA wowote kwako,hana MSAADA wowote kwa watoto,mwanaume akipewa mtaji anakula, akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuacha kazi,akipata fedha anakwenda kuhonga au kunywa pombe mpaka zinaisha pesa zote anarudi nyumbani kukaa.

mwanaume akija nyumbani kazi yake kuuliza chakula akikuta hakuna chakula anaanza kufoka, kutukana, kutoa vitisho, kuvunjavunja vitu, kukugombeza, kukudhalilisha, kukujibu vibaya, kukushambulia kwa maneno makali sana,kusema "hauna akili" mara kwa mara,kusema unatoa harufu mbaya sehemu za siri mara kwa mara baada ya ugomvi anataka unyumba kwa nguvu.

inapotokea hali kama hiyo na wewe ni Mwanamke ni wazi kwamba mahusiano yenu yamebadilika kutoka mke-mume mpaka yamekuwa mama-mtoto.

kwa maana umekuwa mama mzazi kwa huyo mwenza wako.

3. UNATAKA KUMBADILISHA TABIA
Kiashiria tosha kwamba mahusiano yenu yamebadilika kutoka mke-mume mpaka yamekuwa mama-mtoto ni kwamba unataka kumbadilisha tabia mwenza wako.

mwanaume anapotaka kumbadilisha tabia mwenza wake huonyesha tabia zifuatazo
badala ya mwanaume kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye hulka ya kike kama huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu,kujitoa ,kukufurahisha,kudeka,inakuwa kinyume chake mwanaume anajikuta anavutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye hulka ya ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na dharau, Mwanamke anakuwa mjuaji sana, anakuwa na misimamo mikali sana,anakuwa haambiliki, hashauriki, anakuwa hataki kuambiwa makosa yake, hataki kukosolewa, hataki kupangiwa cha kufanya,siku zote Mwanamke anajiona mkamilifu, anajiona mwerevu sana, anajiona malaika, anajiona ni mzuri sana.

kisha mwanaume anajichanganya kwa kuamua kuogopa kukwazana naye, kumnyenyekea, kuomba msamaha saa 24,kupiga magoti mara kwa mara, kumbembeleza mara kwa mara,kuruka kupishana naye kauli,kutumia fedha nyingi sana kwa ajili ya kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama kubwa sana,kumchukulia mkopo,kulea watoto ambao Mwanamke huyo anakuwa ametelekezwa nao.

Mwanamke anapotaka kumbadilisha mwanaume tabia atajikuta kwenye hali kama ifuatavyo
mwanamke anajikuta anavutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye hana hisia naye,yaani mwanaume hamtaki Mwanamke lakini Mwanamke anakuwa king'ang'anizi,Mwanamke anapigwa bila kosa lolote lakini anaomba msamaha,mwanaume hana kazi,hana biashara, hajishughulishi kwa chochote, hataki kukosolewa wala hataki kuambiwa mapungufu yake,mwanaume anakuwa na hasira kupitiliza na misimamo mikali sana (rigid),mwanaume anakuwa amezaa watoto wengi kila mtoto na mama yake lakini hahudumii chochote wakati huohuo Mwanamke huyo anakuwa anataka kutegesha ujauzito ili amlazimishe mwanaume huyo amuoe wajenge naye familia lakini mwanaume anakuwa hataki.

Mwanamke anakwenda mbali anamchukulia mkopo,anajenga ,anamfungulia biashara,anamtafutia kazi yote hayo anafanya lakini anashindwa kujizuia.

4. HUZUNI NA UPWEKE KUPITILIZA
kiashiria tosha kwamba mahusiano yenu yamebadilika kutoka mke-mume mpaka yamekuwa mama-mtoto ni kwamba hauna furaha hata kidogo na mara kwa mara unajikuta upo na hasira,moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu,hisia za kisasi, kupoteza hamu ya kula, kupoteza nguvu za kufanya kazi,kutamani kujiua au kumdhuru mwenza wako,tumbo kuvurugika,kuumwa kichwa na mgongo,kujikuta upo na chuki na kinyongo moyoni.

5. MNAGOMBANA MARA KWA MARA
Kiashiria tosha kwamba mahusiano yenu yamebadilika kutoka mke-mume mpaka yamekuwa mama-mtoto ni kwamba ugomvi na mwenza wako ni matukio ya kila siku.
kwa maana hamuwezi kumalizia masaa mawili bila ugomvi ,mara kwa mara mnapishana kauli kwa vitu vidogo vidogo sana mpaka mnaanza majibizano, kupeana kashfa na tuhuma za usaliti, kutishiana kuachana, kutukanana, kudharauliana, kushutumiana,kuitana majina ya wanyama kama mbwa,

6. UMEANZA KUJITENGA NAYE
Kiashiria tosha kwamba mahusiano yenu yamebadilika kutoka mke-mume mpaka yamekuwa mama-mtoto ni kwamba unajisikia upweke kupitiliza ukiwa na mwenza wako.
Kila unapotaka kujenga ukaribu na mwenza wako unaibuka ugomvi mkubwa sana kisha kila mtu anaondoka akiwa na hasira kupitiliza juu ya mwenza wake



VYANZO VYA KUTAKA KUM-CONTROL MWENZA WAKO NI:


Sababu za kutaka kumbadilisha tabia mwenza wako ni kama vile:


1. KULELEWA BILA BABA NDANI YA FAMILIA.

Sababu za kumkosa baba ndani ya familia ni kifo, talaka, kutengana kwa wazazi kutekelezwa,baba kukataa ujauzito,baba kufungwa gerezani,baba kusafiri safiri hivyo unakuwa haujui majukumu ya baba na haujui majukumu ya mama.

Ukiwa mwanaume unakuwa haujui majukumu yako ni yapi kama mwanaume vilevile unakuwa haujui majukumu ya mwenza wako ni yapi..

vilevile kwa Mwanamke ambaye amekuwa bila baba anakuwa hajui sifa nzuri za baba wa kujenga naye familia,hivyo kila mwanaume ilimradi anapumua anamkubali.
Madhara yake mwanaume anakuwa hataki kulea watoto,hataki kujenga familia hapo Mwanamke anatumia nguvu nyingi sana kumshawishi mwanaume ampende.

wakati huohuo Mwanamke anakuwa hana hisia zozote kwa mwanaume mpambanaji,muwajibikaji kwa sababu Mwanamke anakuwa hajiamini wala hana imani kama anaweza kustahili kupata mwanaume ambaye anajielewa.

2. KULELEWA NA BABA DIKTETA
Mwanamke ambaye amekulia familia yenye baba dikteta wapo huanza tabia ya ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali sana na hasira kupitiliza kama njia ya kujilinda dhidi ya vipigo vya baba.
Hivyo Mwanamke huyu akiwa mkubwa hawezi kukubali kuongozwa na mwanaume wala kupangiwa cha kufanya badala yake atakuwa tayari kuzaa na waume za watu au wale wanaume player boys ambao wanampa mimba na kumtelekeza bila huduma zozote kwa sababu hapo atakuwa na uhuru wa kuishi anavyotaka.

mwanaume ambaye baba alikuwa dikteta huamua kuwa jeuri, kuonyesha dharau, kiburi,ubabe na misimamo mikali sana hivyo anakuwa hana huruma kwa Mwanamke ,japokuwa wapo wanaume huamua kuwa kinyume chake ambapo wanakuwa na tabia ya upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu, kujitoa mhanga kuwafurahisha wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na dharau.

Hivyo mwanaume mpole kupitiliza huwa anachanganyikiwa wapi anakosea lakini hapati jibu.

3. KULELEWA NA BABA LEGELEGE
Wapo wanaume ambao tangu utotoni hawana ujasiri wa kufanya kazi yoyote,wanakuwa marioo,wanakuwa vibenteni kwa sababu tangu utotoni wamezoea kula bure,kuvaa bure,kila kitu wanapewa bure hivyo hawajui majukumu yao mpaka uzeeni kwa mwanaume wa aina hii anaweza kuzaa watoto wengi lakini hatoi huduma zozote,hata akiwa na fedha hatoi huduma zozote kwa sababu amezoea kufanyiwa kila kitu.

wanawake ambao wamekuwa na baba legelege huzoea kuishi maisha ya uhuru uliopitiliza hivyo hawawezi kukubali kuongozwa na mwanaume ambaye anajielewa badala yake wao wanavutiwa kimapenzi na wanaume wapenda starehe , lakini wakipewa ujauzito na kutekelezwa huanza kutafuta mwanaume mpole kupitiliza alee watoto wasiokuwa wa kwake.

4. KUPUUZWA NA KUPITIA MANYANYASO
Baadhi ya watu huwa na huruma kupitiliza kwa sababu wamepitia vipigo, matusi, unyanyasaji, udhalilishaji,kwa miaka mingi sana hivyo mpaka ukubwani hawana uwezo wa kutofautisha mwanaume mzuri yupo na mbaya yupo au Mwanamke mzuri yupoje na mbaya yupoje hivyo wao kuvumilia wanaona ni njia ya kudumisha mahusiano.
 

Add Comments


EmoticonEmoticon