Thursday, May 1, 2025

Siri Tisa Kubwa katika NDOA ambazo Unapaswa Kuzifahamu

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 SIRI 9 KUBWA KATIKA NDOA!


Siri ya 1:
Kila unayemuoa ana udhaifu. Hakuna mtu aliye mkamilifu, anayekuja katika vivuli vyote vya ukamilifu ndiye aliye hai ndani ya mwenzi wako, na huyo ni Mungu tu. Kwa hiyo ukizingatia udhaifu wa mwenzi wako huwezi kupata kilicho bora kutokana na nguvu zake. Tazama, wanandoa wanaodumu ni wale wanaokuza nguvu za kila mmoja, badala ya udhaifu wao.

Siri ya 2:
Kila mtu ana historia mbaya kwenye mzunguko wa maisha yake. Hakuna mwenye umalaika. Unapooa au kuolewa acha kuchumbia zama za mtu. Cha muhimu kwenye maisha ya ndoa ni kujari maisha ya sasa ya mpenzi wako. Mambo ya zamani yameshapita. kama kakukosea Samehe na sahau yaliyopita. Zingatia ya sasa na yajayo mnayojenga pamoja.

Siri ya 3:
Kila ndoa ina changamoto zake. Ndoa sio kitanda cha waridi. Kila ndoa unayoiona nzuri imepitia tambua kuwa imepitia mtihani mgumu. Upendo wa kweli huthibitishwa wakati wa changamoto za kimaisha. Pigania ndoa yako. Pambana, Pambana hadi adui atoke nje ya ndoa yaki. Fanya maamuzi ya kubaki na mwenzi wako kwenye heka heka zenu.

Siri ya 4:
Kila ndoa ina viwango tofauti vya mafanikio. Usilinganishe ndoa yako na ya mtu mwingine yeyote. Ndoa mbili zinaweza kuonekana kuwa Kithibitisho, lakini kamwe haziwezi kufanana. Natumai unanisikia nachokwambia Kamwe usilinganishe kiwango cha upendo kutoka kwenye ndoa nyingine na yako. Jifunze kuwa na subira,

Siri ya 5:
Kuoa ni kutangaza vita. Unapooa lazima utangaze vita dhidi ya maadui wa ndoa yako. Baadhi ya maadui wa ndoa yako ni:
Ujinga
Kumsahau mungu
Kutosamehe
Kuomba ushauri mtu wa tatu
Ubahili
Ukaidi
Kutokuwa na upendo
ufedhuli
Uvivu
usaliti
.

Ili kuweka ndoa yako kuwa sawa inabidi uwe tayari kupigana na chochote kwa maombi na bidii. Ndoa yenye furaha si ya wanandoa wanaotaka kuwa wasafi.

Siri ya 6:
Hakuna ndoa iliyokamilika. Hakuna ndoa utakayoikuta ipo sawa. Ndoa ina kazi ngumu. Jitolee kufanya kazi kila siku juu ya ndoa yako. Ndoa ni kama gari linalohitaji matengenezo na huduma inayofaa. Hili lisipofanyika itavunjika mahali fulani na kumuweka mmiliki kwenye hatari au hali fulani zisizofaa. Tusiwe wazembe kuhusu ndoa zetu.

Siri ya 7:
Mungu hawezi kukupa mtu aliyekamilika. Anakupa mtu katika mfumo wa malighafi ili umtengeneze wewe mtu hasa mtu unayetamani. Je, unakumbuka kwamba Mungu ni Muumbaji? Hii ina maana kwamba wewe pia ni uliumbw kama Yeye, na Mungu amekuumbia uwezo wako wa kuyashinda baadhi ya mambo. Jitahidini kila mmoja wenu kwa sala, upendo na Subira.

Siri ya 8:
Ndoa haina mkataba. Ni jambo la kudumu. linanahitaji kujitolea. Upendo ni kama gundi inayowaunganisha wanandoa. Talaka huanzia kwenye akili na kumchanganya shetani kucheza na akili yako. Kamwe usije kutoa taraka mapema kwenye maisha yako. Usijaribu kumtishia mkeo kwa neno talaka. Kadiri unavyohangaika basi, chagua msaada wa Mungu ili kubaki katika ndoa.

Siri ya 9:
Kila ndoa ina gharama ya kulipa. Ndoa ni kama akaunti ya benki. Ni pesa unazoweka ambazo unazitoa. Usipoweka upendo, amani na matunzo katika ndoa yako,

Add Comments


EmoticonEmoticon