Thursday, May 1, 2025

Sifa za Mwanaume ambaye Atasumbuliwa na Mwanamke maisha yake yote

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 Sifa Za Mwanaume Ambaye Atasumbuliwa Na Mwanamke Maisha Yake Yote

Na jinsi ya Kuwa Mwanaume Imara


- Anakuwa hajiamini mbele ya Mwanamke,akiona mwanamke mwenye muonekano mzuri tu anapagawa,anatetema sana,anahisi Mwanamke huyo ni malaika na mkamilifu,kisha anajiona yeye yupo na dosari nyingi sana na mapungufu mengi sana ambayo yatamkwaza Mwanamke huyo,hivyo ataanza kuonyesha kumnyenyekea sana, kumbembeleza sana, kujitutumua sana, kujieleza sana, kumuahidi mambo mengi sana,kutumia fedha nyingi sana ili kumfurahisha akiamini atapendwa sana kuliko wanaume wote lakini huambulia kuchunwa fedha zako zote na kuachwa mifuko mitupu,hujibiwa kwa maneno makali sana yenye udhalilishaji,hufokewa,hutukanwahuambiwa wewe sio wa HADHI yangu kisha mwanaume anaanza kulia, kuomba msamaha, kumpa ushauri,n.k

- Hana sauti ya mamlaka,akianza kuongea anatetemeka sana,anarudiarudia maneno,anakosea kosea maneno,anaongea kwa upole sana au anaongea haraka haraka sana,

- Anaogopa ugomvi na migogoro,hivyo mara kwa mara anaomba msamaha hata kama hajafanya makosa

- Hana msimamo, anaweza kumtishia mwanamke kumuacha lakini hana ujasiri huo,muda wote anataka kupendwa sana na kuonewa huruma

- Anaamini kwa sababu yeye ni mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu,anajali sana,ni mstaarabu sana itakuwa sababu ya kupendwa sana na wanawake kuliko wanaume wengine lakini uhalisia ni kwamba Mwanamke anahitaji ULINZI sio tabia za kunyenyekea, kusamehe makosa haraka, uvumilivu uliopitiliza, ustaarabu sana ndiyo maana anaweza kuvumilia kung'ang'ania kwa mwanaume mbabe,jeuri,asiekuwa na huruma wala unyenyekevu kwa sababu anajua huko anaweza kulindwa kwa urahisi.Hauwezi kumlinda mwanamke ambaye unatetemeka ukimuona kwa sababu inaonekana haujazoea kuona wanawake wenye muonekano mzuri.

- Anakuwa anataka kumbadilisha Mwanamke wake tabia.Anaamini akiwa anajali sana,anamsifia sana,anatoa fedha nyingi sana ataweza kumbadilisha Mwanamke wake tabia ukweli ni kwamba Mwanamke akipenda huwa anabadilika tabia yeye mwenyewe bila kuambiwa na mtu yeyote.

- Huwa anaishi kwenye mahusiano yenye kuendeshwa na upande mmoja.Yaani yeye pekee ndiyo anapiga simu,kutuma sms mfululizo,kutuma zawadi za mara kwa mara lakini anajibiwa kwa mkato,anagombezwa,anafokewa,anatolewa dosari za muonekano lakini anakuwa mvumilivu sana.

- Huwa anamfuatilia Mwanamke ambaye amemkataa anamfuata kimyakimya,anapokataliwa hakati tamaa,anakuwa king'ang'anizi,hata akifokewa anajishusha,akijibiwa vibaya analia na kuomba msamaha hata kama hajafanya makosa,huwa anatishia kujiua,huwa hawezi kustahamili kuachana na Mwanamke ,akiachana na Mwanamke anashindwa kumtoa kichwani hivyo anaweza kuangukia kwenye ulevi kupindukia,kuvuta bangi au dawa za kulevya baada ya mahusiano kuvunjika.

- Huwa anatumia fedha nyingi sana kubadilisha maisha ya mwenza wake akiamini itakuwa kinga ya usaliti,kinga ya mahusiano kuvunjika lakini kilekile ambacho alitaka kuzuia huwa chenye kumtokea baada ya kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama,kulea watoto wa mwenza wake.

- Huwa yupo tayari kuongea kitu chochote,au kufanya kitu chochote ilimradi athibitishe kwamba yupo na upendo wa dhati kwa Mwanamke mwenye kauli za mkato, mwenye hasira kupitiliza,mwenye misimamo mikali sana na masharti magumu sana.



ZINGATIA HAYA MAMBO 4 UWE MWANAUME RIJALI


1.UHURU
Mwanaume Rijali anathamini uhuru wake kuliko kitu chochote,mwanaume Rijali hawezi kuishi kwa kumtegemea Mwanamke wake kwenye fedha,salio,kula,kuvaa, nyumba ya kuishi, gharama za matibabu, usafiri,zawadi n.k mwanaume Rijali anajua ni wajibu wake kuhakikisha maisha ya mwenza wake yanakuwa salama.

mwanaume Rijali haishi kwa kutegemea sapoti ya Mwanamke bali Mwanamke akitoa sapoti inakuwa bonus ili kuepuka kumlaumu Mwanamke pale ambapo haonyeshi ushirikiano.

Mwanamke yeyote akiona unamhitaji sana ili mambo yako yaende huanza kuonyesha dharau waziwazi,atakuwa na kiburi, majivuno,ataanza kuonyesha jeuri kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.Lakini kama unaishi bila kumtegemea kwa chochote hauwezi kumlaumu kwa jambo lolote.

mwanaume Rijali anabeba majukumu yake yote kisha majukumu ya watu wengine anawaachia wahusika.

Ukibeba majukumu yako ipasavyo hauwezi kumlaumu mtu yeyote.

2.KUJIHESHIMU
Mwanaume Rijali anajiheshimu sana kuliko anavyoweza kumheshimu mtu yeyote.Binadamu yeyote ukionyesha kumheshimu kupitiliza anakupanda kichwani.

mwanaume Rijali hana muda wa kutaka kumbadilisha tabia mwenza wake isipokuwa anaweka sheria na taratibu za kuongoza mahusiano kisha anatimiza wajibu wake na kumuacha mwenza wake atimize majukumu yake.

mwanaume Rijali hawezi kushobokea muonekano wa Mwanamke bali anaona ni kitu cha kawaida hivyo hawezi kubabaika kwa uzuri wa Mwanamke,Bali anathamini sana heshima ambayo anapewa na Mwanamke .

mwanaume ambaye anashobokea muonekano wa Mwanamke huwa ja wakati mgumu sana kuachana na Mwanamke pale ambapo Mwanamke anapofanya usaliti, kumdhalilisha mwanaume, kumnyima unyumba kwa muda mrefu.

Mwanamke akijua hauna ujanja juu ya muonekano wake anakuwa hana muda wa kujali tabia zake kwa sababu anajua unasamehe makosa yote na utakuwa mvumilivu miaka yote kwa sababu yeye ni mzuri sana.

3.KUSTAHIMILI HISIA
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujitegemea yeye,akiwa mpweke haitaji simu,faraja,sms ,zawadi kutoka kwa Mwanamke ili apate kujisikia vizuri.
mwanaume Rijali anakuwa kama komandoo kwenye uwanja wa vita kwa maana anabeba furaha yake yeye mwenyewe vilevile anabeba maumivu yake yeye mwenyewe.
Mwanaume Rijali akiwa na huzuni,upweke, majonzi anajua ni wajibu wake kubeba maumivu hayo siyo jukumu la Mwanamke .

Kama hauna furaha kwa sababu Mwanamke hajapiga simu,hajatuma sms,hajakufariji,hajakupa pole kwa kazi utakuwa na malalamiko, manung'uniko,utanuna, kususa,kuishi ukiwa na chuki, kinyongo moyoni kwa sababu unampa Mwanamke wako jukumu la kukufurahisha jambo ambalo husababisha migogoro ya kimapenzi mara kwa mara.

Mwanamke yeyote akiona haulalamiki juu ya ukimya wake,au tabia zake ataanza kutilia shaka kama ûnampenda.Kwa sababu Mwanamke anaweza kukupuuza kwa makusudi lengo aone kama utaanza kulalamika ili ajue kama ûnampenda sana,akijua anapendwa sana huanza kuonyesha dharau waziwazi kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.

Lakini kama upo na furaha yako wewe mwenyewe akiwepo au akiondoka haiwezi kukusumbua wala kwake hauwezi kuonekana msumbufu.

4.KUJIWEKEA MIPAKA
Mwanaume Rijali anajua tabia gani za kuvumilia na tabia gani siyo za kuvumilia.
mwanaume Rijali anajua makosa ya kusamehe na makosa ambayo siyo ya kusamehe.

mwanaume Rijali anamuongoza Mwanamke , mwanaume Rijali hampigi,hamdhalilishi,hamtukani Mwanamke bali anaishi naye kwa misingi ya kuheshimiana na uadilifu.

mwanaume Rijali anajua Mwanamke akiwa mgonjwa anahitaji faraja,anajua Mwanamke akiwa na huzuni anahitaji faraja, anajua Mwanamke akiwa amefanya kazi nyingi anahitaji kupewa pongezi, vilevile mwanaume Rijali anajua hawezi kumnyenyekea Mwanamke kama njia ya kuzuia mahusiano kuvunjika.

mwanaume Rijali anampa onyo Mwanamke pale ambapo anaonyesha utovu wa nidhamu,anampa onyo siyo kwa kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya n.k bali anamweleza wapi amefanya makosa na vilevile anamuonyesha wapi pa kujirekebisha.

Mwanaume Rijali hana gubu, kisirani,chuki, kinyongo,wivu wa mapenzi uliopindukia.
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujiongoza.

mwanaume Rijali anajua kumlinda na kumtetea mwenza wake dhidi ya kukosolewa, kusemwa vibaya, kutukanwa, kujibiwa vibaya kutoka kwa mama yake mzazi pamoja na dada zake.

mwanaume Rijali anasimama katikati hayupo upande wa mama yake mzazi,au dada zake vilevile hayupo upande wa mwenza wake.

mwanaume Rijali anafanya uadilifu,mwanaume Rijali anakuwa mtenda haki,mwanaume Rijali hafanyi upendeleo,mwanaume Rijali anaongozwa na akili siyo hisia za mapenzi.

mwanaume Rijali hana uwezo wa kumpenda Mwanamke kwa hisia kali bali anampenda Mwanamke kwa kuongozwa na akili sio hisia.

Add Comments


EmoticonEmoticon