Saturday, May 3, 2025

Mke wako Atakupenda sana iwapo Utakuwa na hizi Sifa

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 MKE WAKO ATAKUPENDA SANAAAA IWAPO TU!


1. Unaleta pesa ya matumizi nyumbani.
Moyo wa mwanamke utachoka kukupenda iwapo utaacha kuleta hela ya matumizi kwa ajili yake na watoto nyumbani.(Women are materialist in nature!), wao ni watu wa kupenda vitu sanaa kutoka kwa mwanaume na ndiyo upendo wao na heshima kwa mwanaume wanavyoutafsiri. Usipompatia pesa kwa ajili ya matumizi yake na watoto, ndivyo atakavyozidi kukudharau siku hadi siku atafika hatua atakukinai vibaya sana, kiasi kwamba anaweza kutamani kukupa nguo zake za ndani umfulie.KWANINI? ATAKUSHUSHA HADHI YA UANAUME, MWANAUME LAZIMA AKUBALI KUBEBA MAJUKUMU YA KUHUDUMIA FAMILIA. Upate, ukose wao hawajui! Wanachotaka wewe uhudumie na kutunza familia tu!. UTAPATAJE PESA, hiyo inabaki juu yako! Kama mwanaume unalelewa na mwanamke, tambua kwamba heshima yako haipo, kuna siku atakuchukulia wewe kama mfanyakazi wake wa ndani na sio MUME WAKE, SIKU ZOTE MAPENZI YA KULELEWA NA MWANAMKE HAYADUMU. Anza sasa kujenga heshima yako kwa kuacha CHOCHOTE MEZANI.

2. Ni mtu wa ibada na kusali sanaaa.
Aisee, church boys( wanaume wanaopenda kusali) wanapendwa sana na wake zao. Why? Kwasababu wanaamini sio watu wa mambo mengi hasa ya kupenda wanawake, ulevi na starehe nyingine ambazo zinaweza kusababisha ndoa ikavunjika. Kiufupi watu wanaosali sana wanaaminika sana ndani ya ndoa ndiyo maana hata wakati wa kuoa watu wanapenda sana kuchagua mke au mume kutoka kwenye nyumba za ibada.M

WANAUME ILI UANZE KUPENDWA NA MKE WAKO, KAMA AMEPOTEZA IMANI NA WEWE, ACHA MAKANDO KANDO YAKO NA ANZA KUSALI KWA SANAA! HAKIKISHA HAUKOSI IBADANI, LAZIMA ATARUDISHA IMANI NA MAPENZI KWAKO.

3. Una nguvu za kiume(WEWE NI MWANAUME KAMILI)
Aisee, iwapo jogoo wako hawiki, iwapo huwezi kushiriki tendo la ndoa,mke wako atakushusha thamani na anaweza kukuacha kabisaa. Kwanini? Kwasababu kuwa mwili mmoja kuna kamilishwa na tendo la ndoa, kama hamshiriki tendo la ndoa, maana ya mwili mmoja INAPOTEA na kubakia kwenye makaratasi ya vyeti vyenu vya ndoa pekee. Wapo wanaume walipata ajali wakapoteza uanaume wao, wapo ambao wameugua wakapoteza uanaume wao lakini hawajaachwa na wake zao, nawapongeza sana wanawake wa aina hiyo maana wana imani kubwa. INAHITAJI UPENDO, IMANI KWA MUNGU NA KUMTEGEMEA SANA MUNGU ILI AKUPE UJASIRI WEWE MWANAMKE WA KUMLINDIA MUME WAKO HESHIMA YAKE MPAKA HATUA YA MWISHO YA MAISHA YENU. Sio rahisi kwasababu sote ni binadamu tumeivaa miili yenye tamaa za kimwili kibaiolojia lakini peke yako hauwezi isipokuwa kwa msaada wa Mungu. WANAUME TUNAPASWA KULINDA UANAUME WETU KWA NGUVU ZOTE ILI HESHIMA YA NDOA ZETU IWEPO TUSIDHARIRIKE. TUTALINDAJE UANAUME WETU? KWA KUACHA KUJICHUA, KUACHA KUTAZAMA PICHA ZA NGONO,KWA KUACHA VINYWAJI VIKALI, SIGARA, VYAKULA VYA MAFUTA, KWA KUFANYA MAZOEZI LAKINI PIA KWA KUMTEGEMEA MUNGU MAANA KUACHA KUJICHUA, POMBE NA SIGARA SIO RAHISI PASIPO MUNGU.

4. Unamshirikisha kwenye maamuzi yako.
Aisee, kama unamshirikisha mke wako wakati wa kufanya jambo lolote basi wewe unaijua maana ya ndoa. Hupaswi kuamua mambo yote mwenyewe kwasababu wewe ni mwanaume, hapana! KWANINI? KWASABABU KUNA LEO NA KESHO. Ukiamua mwenyewe tena kwa siri pasipo mke kufahamu, utaondoka na kuacha mali zingine hazifahamiki, watoto wako wataishi maisha ya kimasikini huku wanafaidi jasho lako watu wengine kabisaa. NDIYO MAANA WANAWAKE WANAWAAMINI NA KUWAPENDA SANA WAUME ZAO WANAOWASHIRIKISHA KWENYE MAAMUZI HASA YA UCHUMI WA FAMILIA

Add Comments


EmoticonEmoticon