Thursday, May 1, 2025

Kuwa na Busara - Epuka Kumuuliza Mtu haya Maswali

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 Kuwa Na Busara Epuka Kumuuliza Mtu Maswali Haya


1. Hujaolewa tu?

2. Kwanini Huna Watoto?

3. Utazaa lini, umri unaenda!

4. Unafanya kazi wapi?

5. Kwanini Umenenepa/Umekonda?

Watu wanapitia mambo mengi magumu ambayo huna taarifa nayo wala hujawahi kuyasikia, jitahidi kuwa mwenye ufikirio unapozungumza na wengine.

Ikiwa wewe umefanikiwa kupata vyote jitahidi kutoropoka maneno unayodhani yako sawa kwa upande wako.

Kuna watu wanapitia changamoto za mahusiano, uzazi, uchumi na mambo mengine ya kifamilia, try to be kind!

Nakumbuka kuna siku sikuwa najua lolote lile nikapata mawasiliano kwenye group na school mate mmoja hivi, maana miaka mingi ilipita bila mawasiliano, mule kwenye group wakasema kaolewa. Mimi bila kujali na usingo wangu nikauliza ana watoto wangapi?

Sikuwa na nia mbaya nilitaka tu kujua kwa wema tu ili nimpongeze. Yule dada alileft group, ndio nikapata maelezo ya changamoto nyingi anazopitia, kusema ule ukweli nilijilaumu sana.

Nilijifunza wapo watu wanajitenga na jamii sio kwa sababu hawapendi watu, hapana! Ni kwa sababu wanepuka kero na mazingira ya kuongezewa stress kwenye maisha yao ambayo tayari yanawahangaisha, wapo watu hata sherehe na mikusanyiko mingi hawashiriki sababu ya maswali kama hayo hapo juu.

Tunakosa ushirikiano wa watu wengi sababu ya midomo yetu. Kuna mtu haji kwako kukusalimia sio sababu hakupendi, ni huo mdomo wako huchelewi kuanza kutoa ushauri au masimango kibao, mtu anakuja kukusalimia we unaanza kumfanyia interview .

Maisha sio mashindano! Kila mtu ana mzigo wake anahangaika nao kimya kimya tusiwaongezee uzito.

Unaweza kumuona mtu yuko vizuri kiuchumi lakini kuna mwiba wake anahangaika nao, na kadhalika yule unayemuona ana mahusiano yenye furaha naye ana mwiba wake

Add Comments


EmoticonEmoticon