1. Ukiolewa utawavutia sana wanaume wengine. Jifunze kuweka mipaka
2. Kila ndoa ina changamoto zake, zitambue njia za kuzitumia changamoto hizo
kutunza ndoa yako
3. Unaweza kuwa tayari kuwa kwenye ndoa lakini ukiolewa na mtu ambaye hayuko
tayari kuwa chaguo lako utachanganyikiwa sana. Usiwe unampenda mtu asiye sahihi
kwako kwa njia sahihi
4. Tambua Kuna maisha ukiwa kwenye ndoa, Jaribu kufuata lengo lako binafsi
lakini timiza kwa pamoja na mumeo
5. Mkioana lakini mkawa mnapenda ushindani tambua kuwa ndoa hiyo haitakufaa
6. Tafuteni shughuli za kufanya nyinyi nyote kwa pamoja kama wanandoa. Upendo
hujengwa na shughuli mbalimbali
7. Kuwa mwangalifu unayependa kumsikiliza mmeo/mkeo. Baadhi ya watu hawafurahii
kuwa katika ndoa zao au katika uchumba wao na huwafanya wenza wao kukosa furaha
katika ndoa zako
8. Ndoa ina vipindi mbalimbali tofauti. Msimu wa pamoja, msimu wa migogoro
ambapo nyote wawili mtastahili kutafuta suruhisho zenu ndani ya ndoa yenu
kupitia mizozo mnayokutana nayo mara nyingi, kuna msimu wa majaribu ambpo nyinyi
wawili mtakabiliana na sababu za kuachana na msimu huo wenye nguvu kwa pamoja
na hapo mtapata ushindi wa pamoja.
9. Usipojitayarisha kwaajili ya watoto wako, watoto watakuwa na sababu ya
kupunguza upendo na umakini mliokuwa nao kwa kila mmojawenu. Ndoa nyingi
huingia kwenye mateso pale uzazi unapoanza tu
10. Kuna mtu anaangalia ndoa yako na anajifunza kutoka kwako. sasa jiulize
anajifunza nini?
11. Masuala yote katika maisha yako ambayo hukuyamaliza ukiwa single,
yatakuletea shida kipindi umeoa katika ndoa yako.
12. Kwa sababu ndoa ya baba yako ilifeli, haimaanishi kuwa na ndoa yako
itafeli. na haimaanishi kuwa ndoa ya baba yako ilisitawi na kuwa njema basi na
yako itakuwa hivyo. jifunze kupigania majukumu yako kibinafsi
13. Usimpe mke wako madaraka makubwa kiasi cha kukufanya upoteze maadili ndani
ya ndoa yako, utaakakosa usingizi, utaishi maisha duni ya kimaskini na kuua
ndoto zako.
14. Ndoa yoyote inaweza kustahimili anguko lolote ili mradi tu wawili hao
wakiwa tayari kusameheana, kubadilika, kujitahidi kuhakikisha kwamba upendo
unadumishwa, kuinuka na kuyashinda mapito.
15. Unapoanza kuzingatia sana na kuyaweka akilini madhaifu na mapungufu ya
mwenzi wako, utayumbishwa na vituko vya muda mfupi.
16. Pesa inaweza kuwa sababu ya nyinyi kutoelewana chukua maamuzi ya
kushughulikia hilo swala mnapokuwa wekeni urafiki ndani ya ndoa yenu na
kuchukulia kuwa ndiyo msingi wa ndoa yenu.
17. Ukaribu ni zaidi ya kufanya mapenzi. Unganishaneni ndani zaidi ya kufika
kileleni hasa miguso, kukumbatiana, kubembelezana, busu na mazungumzo mazuri
18. Wazazi wako wanaweza kuwa na nia njema lakini wanaweza kuharibu ndoa yako
wanapofanya au kusema kwa kuzingatia mapendekezo yao, chuki, upendeleo,
ukabila, kurudi nyuma, uchungu, ubinafsi, maumivu ya zamani au habari potofu.
kumbuka wao Walikuwa na maisha yao, sasa na wewe ni wakati wa kujenga maisha
yako.