UNAPOBAHATIKA KUPATA MWANAMKE MWENYE
MAPENZI YA KWELI NA ANAYEKUTHAMINI KILA SIKU UTAKUWA UNAAMBIWA MANENO HAYA
1. Habari ya Asubuhi mpenzi, natumai ulipata usingizi mzuri sana. Habari za
leo? Amka ujiandae kuelekea kazini. Usisahau kuomba dua na maombi kwaajili ya
kazi.
2. Ndiyo kipenzi, nimekukumbuka sana, natumaini unafurahia siku yako, naelekea
jikoni kuandaa chakula cha mchana. tutazungumza baadaye.
3. Usiwe na presha mpenzi wangu, najua utafikia malengo yako ya maisha. Mimi
nasimama kama msaada kamili kwako.
4. Usisahau kusali kila ifikapo saa ya kufanya ibada kuanzia asubuhi, ,mchana
jioni na usiku. Kumbuka nguvu zetu ziko kwa Mungu. Nipigie ukiwa tayari kwa
maombi ili tuombe pamoja mtandaoni.