Watu wengi wanafikiri kimakosa kuwa kuna lugha moja tu ya mapenzi. Hebu
tuliangalie hili kiundani. Dhana ya Lugha 5 za Upendo ilibuniwa na Dk. Gary
Chapman mnamo 1992. na hizo Lugha tano za mapenzi ni:
1. Maneno ya uuhakika
2. Muda bora
3. Mguso wa kimwili
4. Matendo ya utendaji
5. Kupokea zawadi
Tangu wakati huo, watu wengi wamekuwa wakitaka kujua "Lugha ya mapenzi ni
ipi?" Ukweli ni kwamba, uhusiano/ndoa yako inahitaji Lugha hizi zote za
Upendo kwa kipimo kamili.
Ngoja nikuelezee.
MANENO YA UHAKIKA: Mpenzi wako atakuhitaji umhakikishie. Upendo huwekwa
hai kwa uthibitisho. Ndiyo maana tunasema "nakupenda", kwa nini
tunaitikia vizuri bila kujali sisi ni nani au tuna umri gani. kuna Wakati
kutakuwa na siku ngumu, ambazo zitakuwa nyingi hata kama ni chache, tutahitaji
wenza wanaotukumbusha ili tufanikiwe. Watu wanaosema kauli hii "Sihitaji
kukuhakikishia", kuna uwezekano mkubwa kuwa walikua kwenye mahusiano na
watu wasio wathamini na hivyo wamekuwa sugu ndani ya mioyo yao. Lakini upendo
unahakikishwa. Ndiyo maana wakati wa kifo/msiba, cha kusikitisha huwa tunayatoa
yaliyopo mioyoni mwetu na kuwahakikishia wale tunaowapenda wakiwa wamekufa
tayari lakini tulishindwa kufanya hivyo wakati wakiwa hai.
MUDA BORA: Hakuna uhusiano unaoweza kudumishwa bila muda bora. huwezi
kuingia kwenye mahusiano/ndoa na ukafanya mambo ya kupuuzwa na kuachwa. bila
Upendo. Kuna umuhimu gani wa kuwa na mtu ikiwa wewe sio chaguo lake na wakati
hatakutengea muda bora wa kuwa nae? Watu wanaotoa kauli hii, mimi sina uwezo wa
kutenga wakati bora, kuna uwezekano mkubwa wamezoea kuishi peke yao tokea awali
na nafsi zao zimezoea.
MGUSO WA MWILI: Huwezi kuingia kwenye uhusiano na kuepuka kuguswa na
mwenzi wako. Katika ndoa, mtalala pamoja, mtafanya mapenzi pamoja,
mtakukumbatiana. Hakuna anayetaka kuguswa tu halafu aachwe wakati lengo ni
tendo la ndoa. Mara nyingi watu ambao hawapendi kuguswa katika ndoa zao ni kwa
sababu tu wao ni wagumu kuamsha hisia zao. Au labda kwenye mahusiano yake ya
awali alikua ananyimwa haki yake. Ngozi yako iliumbwa na mungu ili kuguswa.
MATENDO YA UTENDAJI: Huwezi kumpenda mtu na usimfanyie vitendo ili
kurahisisha maisha yake na kumstarehesha. Huwezi kujitoa kikamilifu kwaajili ya
mwenzi wako katika mahusiano na usifurahie wakati mwenzi wako anafikiria na
anaangalia jinsi ya kutimiza mahitaji yako Upendo ni kufanya maisha yenu yawe
ya pamoja, kila mmoja kjituma kwaajili ya mwenzie.
ZAWADI: Kwa bahati mbaya, tunapenda sana kulinganisha binadamu na zawadi
ya mkufu, chupa ya manukato ya gharama kubwa au maua. Zawadi intakiwa kuwa na
thamani zaidi ya hivyo vitu. Zawadi ni kitu chochote cha msaada unachompa
umpendaye. kama anasoma Kumlipia ada ya shule mwenzi wako ni zawadi kubwa,
kumnunulia mwenzako simu ni zawadi kubwa, kama anamiiki gari basi mnunulie
mafuta ya gari ni zawadi kubwa, kumnunulia t-shirt yenye chapa ya Manchester
United kama ni shabiki wa soka kwa mtu wako ni zawadi kubwa, kumnunulia laptop
kwa ajili ya masomo yake ni zawadi kubwa. kumnunulia mwenzi wako kipande cha
ardhi kwaajili ya ujenzi ni zawadi kubwa. Sio kwamba watu wengine hawajali
kutoa zawadi, ni kwamba watu wana mapendekezo tofauti ya zawadi wanazohitaji.
Mpe zawadi mapenzi wako kulingana na yeye anachopendelea
Lugha zote hizi tano za mapenzi zinahitajika katika uhusiano/ndoa yako.