1. Mwite jina lake kimapenzi
2. Mruhusu atumie mamlaka yake akiwa kama kichwa cha familia.
3. Usimuongezee changamoto anapokuwa hayupo sawa.
4. Jaribu kujishusha anapokuwa na hasira. Unaweza kuutumia muda wakati
atakapokuwa katika wakati wa utulivu na atakuomba msamaha na kukuelezea kwa
nini alifanya hivyo ambayo vilikukasirisha.
5. Kuwa mwepesi wa kusema neno"Samahani mpenzi" wakati wowote
unapomkosea, msisitizie msamaha wake, thamini na kumbusu anapokukosea.
6. Mzungumzie vizuri mbele ya Marafiki zake na ndugu zake.
7. Waheshimu wazazi wake
8. Jitahidi kuwanunulia wazazi wake zawadi na hivyo hakikisha kwamba nayeye
anafanya hivyo kwa wazazi wako
9. Mshangaze kwa kutumia sahani au vyombo anayopenda hasa wakati akiwa hana
pesa mkononi na usicheleweshe chakula chake.
10. Usimruhusu kijakazi kumhudumia chakula mmeo unapokuwa nyumbani. Kwa sababu
unaweza kumpoteza mme kwa kijakazi wako.
11. Mpe mapokezi mazuri kwa kumkumbatia anaporudi nyumbani, kwa kumpokea mizigo
yake na kumsaidia kumvua nguo.
12. Tabasamu unapomtazama na kumpa midomo ya hapa na pale mnapokuwa nje ya
jamii.
13. Msifie mbele ya watoto wenu nyakati fulani.
14. muogeshe mgongo wake mkiwa bafuni wakati wa kuoga.
15. kuna wakati uwe unaweka ujumbe wa upendo kwenye meza ya chakula cha mchana au
usiku.
16. Piga simu na mwambie kuwa umemumis.
17. Piga simu yake na ukisikia neno "hello" mwambie tu unampenda.
18. Ikiwa yeye ni mtu wa umma au mwanasiasa, mwamshe kwa upole asubuhi na
mapema na umuandalie vitu kwa kiwango cha mahitaji yake..
19. Mwambie jinsi unavyojisikia kuwa na bahati yeye kuwa mume wako.
20. Mkumbatie bila sababu.
21. Mthamini Mungu kwa ajili ya Adamu wa maisha yako.
22. Kumbuka daima kumwombea dua.
23. Ombeni pamoja na pia salini pamoja kabla ya kwenda kulala usiku