HIZI NDIYO ALAMA KUU ZA UAMINIFU NA MAANA
ZAKE...
1. Kulala karibu na mwenzi wako bila uoga, na kuwa na uhakika kwamba
hatokudhuru.
2. Kuzaa watoto mkiwa pamoja nyakati zote za malezi pasipo kumtelekezea mmoja
majukumu ya ulezi
3. Kutambulishana kwa wazazi na familia zenu, ikiwa unauhakika kwamba
utawaheshimu na kuwapenda wazazi wake kama wako.
4. Kula chakula ambacho amepika mwenzi wako bila uoga, ukijiamini kuwa hakiwezi
kuwa na sumu.
5. Kukutazamana hasa mmoja wenu akipita mlango wa nyumba, ili kuhakikishiana
kuwa hatafanya chochote cha kuhatarisha familia yenu isije kuingia kwenye
maisha hatarishi.
6. Kuwekeza mapenzi thabiti pasipo kuingiza uwezo wa kipesa ni kufanya juhudi
kwa hisia zenu wenyewe, huku mkijua kuwa kuna msingi thabiti unaofanya penzi
lenu liende
7. Kukabidhiana miili yenu kitandani bila hofu ya kuwa mwenzio sio mwaminifu
kuwa anakuchezea tu au kuhisi kuletewa magonjwa ya zinaa .
8. kuishi na mwenzio pasipo na haja ya kukagua simu ya mwenzio kila mara simu
na meseji zinavyoingia, kwa sababu huenda akawa hafanyi chochote cha aibu huko
nje.
9. kutokujali kiburi cha mwenzio hasa akiwa na ww
10. Kuwa na amani unapokuwa mbali na na mwenzio kimwili na kiakili, na kuondoa
mawazo ukijua utafanya ujinga
11. kuhifaddhi maneno mnayozungumza mkiwa wote maana kesho mengine hujirudia
12. kujipa ujasiri wa Kufumba macho yako kwa kujiamini, ukijua upo salama
mikononi mwake.
13. Kukuteteana pale wengine wanapowashambulia bila sababu za msingi, hasa
mkijua kwamba mnafaa kupiganiana.
14. Kupeana maisha na kuishi pamoja, huku mkijua hamtajuta kwa maisha
mliyoyachagua.