KIJANA ALIYECHUKIA UMASIKINI NA KUSAKA UTAJIRI
Ni stori ya kweli ya kimaisha ya namna nilivyopata utajiri wangu.. Nimezaliwa kwenye familia masikini sana,na nauchukia umasikini, home tulikua tunaweza kupitisha siku nzima bila kula,au tunapiga pasi ndefu tunakula usiku tu.
Nilipomaliza la saba kwa shida sana,ikabidi nianze heka heka kutafuta maisha.Piga sana spana gereji,piga sana saidia fundi,nimehangaika sana.Nikakimbilia Dar kwa kuunga unga hivyi hivyo.
Kufika Dar life lilikua gumu sana,ikawa nalala tu mitaani yaani nilikua chokoraa proper.Katika gang niliyokwepo ikatokea jamaa akasema kuna mchongo Mererani huko machimboni, tukaenda.
Kufika Mererani life lilikua gumu zaidi, ni hatari kule nikawa ‘nyoka’, ni kazi ya hatari sana ile kufa nje nje, mnafanya kazi masaa 24 na kula mara moja tu. Nikaona nitafia huku. Baada ya miaka 2, jamaa mwingine nilietengeneza nae urafiki kule akaniambia kuhusu utajiri wa FUNZA.
Jamaa aliniambia unapatikana Tunduma huko,na kuna jamaa zake wamenufaika na hiyo. Sikuwaza sana,tukakusanya nauli baaada ya miezi 2-3 tukaingia Tunduma.
Kufika kule,tukaenda kwa mganga,tukapewa masharti.Kubwa ni kufuata masharti, inatakiwa kila mwisho wa mwezi unatoa sadaka unachinja mbuzi/ng’ombe na msosi kama mchele unapeleka kwa watoto yatima na wenye shida.Pia,marufuku kuzini.
Funza wanavyotoka wengi na kuwekwa kwenye viroba hizo ndo hela sasa. Kwa hiyo kiufupi, tulikaa pale mwezi na mwenzangu (nilianza mimi,yeye akiwa msaidizi,kisha akafuata yeye mimi nikiwa msaidizi wake). Tuliondoka kwa mganga na maburungutu ya fedha tumeyajaza kwenye masanduku.
Maana ilibidi tukanunue masanduku.Sharti lingine nilisahau ni kwamba haturuhusiwi kwa namna yoyote ile kuweka pesa bank,so sisi ni cash kwa cash tu.Sometimes challenge kwenye business mtu anataka kulipa kwa bank, but siwezi accept.Now nina investiments nyingi sana, na pesa mingi sana, niliwekeza kujenga nyumba.
Ila nimechoka utumwa wa huu utajiri,nina mtoto mmoja tu,maana ndie nilieruhusiwa kuzaa. Siwezi fanya starehe nyingi japo nina pesa. Sometimes najuta sana. Vijana msitamani sana utajiri wa
haraka,una vifungo vingi na mateso! Lakini pia umaskini ni mbaya. Dunia Haina huruma.