π‘ππππ©π¬π’ππππͺπ π‘π π ππππ ππππ, π ππππ π¬π π π¨π π πͺππ‘ππ¨ π‘π π πͺππ‘ππ‘ππ¨
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 10
β Kwangu? Inamaana ni mimba yangu?β Aliuliza kwa mshangao sana James.
β Ndio jamaa anavyosema..β
Hiii ilinipasua kichwa, nilianza kuhisi maluw luwi. Sikuelewa imekuwaje waje, mtu alale nae siku moja apate mimba.
Pale pale kwa kuvurugwa nilienda chumban na kuwaacha wao barazani.
Dakika kum na tano mbele mume wangu alifika chumbani!
β Kuwa na amani mke wangu! Nina uhaka ile mmba sio yangu.β Aliniambia.
β Iwe ya kwako au isiwe ya kwako! Hili ni tatizo tayari. Tena ni tatizo kubwaaa.β Nilimwambia.
β Nitalishughulikia.β
β Huyo mwanamke yuko wap?β
β Yupo barazani, nimempa shuka! Kwa leo atalala pale , ila kesho asubuhi tutaongea na kujua tunalitatua vip.β Aliniambia.
β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦.
Asubuhi ya siku ya pili, james alimchukua mke wa juma na kumpeleka kwao lilambo, aliwatafuta wazee wawili wakaenda kwa juma.
Juma kuwaona akawatimua kwa panga. Wote wakatawanyika, baadae walikutana na kushauriana.
Wale wazee walishauri mke wa juma aende kwa wazaz wa Juma. Akakae huko mpaka pale atakapojifungua.
β kwa wazazi wa juma ni mbali, na mimi sina nauli! Na huko nitaishije?β Aliulza mke wa juma. James alimtoa wasiwasi. Alimuahid kumpa nauli , pia alisema atampa hela ya matumizi akiwa huko mpaka pale lile swala litakapoisha.
Walikubaliana hivyo.
Siku ya pil yake mke wa juma akaenda kwa wazazi wa juma Mbeya.
β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦.
Baada ya mke wa Juma kuondoka, juma alianza tabia ya kututisha. Mara kadhaa alimtumia ujumbe mume wangu wa kumtishia maisha.
β Hii hali hadi lini/β Aliniuliza james.
β Dawa hapa ni kumshtaki! Kwakuwa njia za kawaida zimeshindkana kilichobak ni mbwai mbwai tu. Huyu mtu tukamfungule kesi polisi.β Nilimshaur mume wangu.
Wazo langu alilichukua. Siku ya pil mapema sana tulienda kituoni na kufungua kesi ya kutishiwa maisha,James alitoa maelezo yake nami nikatoa yangu.
β Tutamkamata huyu mshenzi, kuweni na amani.β Polisi walituambia.
Kes tulikuwa tumefungua kituo kikuu cha polisi kilichokuwa nyuma ya uwanja wa maji maji. Baada ya kutoka pale polisi, james alinishauri tuzunguke zunguke mjini kuondoa stress.
β Sawa.β Nilimjibu.
Sehemu ya kwanza kwenda ilikuwa ni majengo mnadani. Tulizunguka kwenye banda moja hadi lingine kuchagua nguo. Katika kuzurula zurula , nilifika sehemu nikakuta nguo zimemwagwa chini Niliinama kuchambua, lakini nikifanya hivyo, alitokea Juma na kunishika makalio.
Haraka sana James alimuwahi! Alimkaba shingoni na kutaka kumpiga.
β Nimekosaaa..nisameheee nimekosaaaa.β Juma aliigiza kuomba msamaha kisha akacheka.
ile hali niliona kabsa ilikuwa imemkera sana James, niliishuhudia mikono yake ikicheza kwa hasira, Lakini kabla hajafanya lolote nilimuwahi na kumsihi asamehe. Alimwacha juma akaondoka.
Tuliendelea na mambo yetu.
Tukiwa eneo lile tunachagua chagua nguo, mbaba mmoja muuza nguo alituambia jambo lililotushtua sana.
β Kijana shukuru MUNGU hujagombana na yule kijana.. pale alikuwa anatafuta ugomv makusudi ili haharibu maisha yako.β Aliongea yule mbaba.
β Unamaana gani?β Nilmuuliza.
β Yule jamaa aliyemshika makalio mkeo ni jambazi sugu sana, hapa mnadani pote watu wanajua na wanamuogopa.. Anatisha sana. Ukigombana nae ni vyema tu ukamuomba msamaha yaisheee. Pale alipo kaua watu weng sana.β Aliongea yule mbaba.
Aliendelea.
β Nakupongeza sana haukuanzisha ugomv pale alipomshka mkeo makalio, lasivyo mngepata tabu sanaβ¦ yule kijana sio mzuri kabisaa.β Aliongea yule mzeee.
EP 11
Maneno haya ya yule mzee yalituvuruga.
Nilishuhudia sura ya james ikibadilika.
β Tuondoke.β Aliniambia.
Alinishika mkono tukatoka eneo lile na kurudi nyumbani! Kufika nyumban hakukaa sana. Aliniacha peke yangu na kuondoka.
Sikujua anaenda wapi na anaenda kufanya nini.
Dakika zilikatika, muda uliyoyoma pasipo james kurudi nyumbani! Hadi giza linaingia james halikuwa hajarud nyumbani. Hiii ilikuwa mpya kwangu. Ilikuwa ni tofauti kabisa na mazoea yake.
Na ile siku alikuwa zamu, hivyo ilibidi awahi kurudi ili ajiandae kwenda kazini. Nilijaribu kumpigia simu, lakini bahati mbaya simu yake haikupokelewa.
Iliita na kukatika pasipo James kupokea.
β Kaenda wapi huyu?β Nilijiulza. Nilitazama saa ilikuwa saa moja usiku.
Nilihis kuchanganyikwa, nilimpigia simu baba na kumuomba kama anaaskar anawajua wapo kikosi cha chandamali basi awapigie simu na kumuulizia james.
Baba alinitoa waswasi.
β¦β¦β¦β¦β¦β¦β¦..
Nusu saa mbele baba alinipigi na kusema kazini kwake hajaenda, na wale aliowapiga hawajui wapi alipo.
Tiiii. Taaa nyekundu iliwaka kichwani. Nilianza kuhisi uenda juma kamfanya kitu mume wangu. Haraka nilimpigia tena simu baba. Nimueleza kuhusu wasiwasi wangu na yote yaliyotokea.
β Ndio mana sikutaka uolewe na mwanajeshi..ona sasa unavyoteseka.β Alibwata baba. Wakati akiongea hayo, mama alikuwa pembeni. Nilimsikia akimfokea baba na kumtaka anisaidie baada ya kunilaumu.
Baba aliniambia nisifanye lolote lile anakuja.
Wakati namsubri baba aje, nilipata wazo lingine. Haraka nilijianda na kutoka. Moja kwa moja niliekea kanisani.
β Upo sawa?β Mchungaji aliniuliza.
β sipo sawa mchungaji.β
β Shida nini?β
β James hayupo nyumbani! Kaondoka katika mazingira ya ajabu sana. Na kwasasa ilbid awe kazini, lakin hadi muda huu kazini hajaenda na hapatikani.β
β Simu umempigia?β
β Ndio! Nimempigia sana lakini hapokei. Nimepiga mpaka nimechokaβ
β Simu inaita?
β Ndio inaita.β Nilimjibu.
β Kama inaita basi hili ni swala dogo! Tutalitatua sasa hiv, hiyo simu tutaipata na tutajua yeye yuko wapi.β Aliniambia mchungaj. Alichukua simu yake na kumpigia kijana wake.
β Kuna simu nataka uifatilie ipo wapi.β Aliongea mchungaj kisha kakata simu.
Alinitaka nimpe taarifa fulani kuhusu simu ya james, nilienda nyumban nikachukua taarifa alizohitaji na kumpa. Alimtumia kijana wake na ndani ya nusu saa alisema kaiona kwenye mtandano simu ilipo. Anatutumia location il tuweze kwenda.
β Ahsante sana.β Aliongea mchungaji.
Muda ule ule tuliingia kwenye gari la mchungaji ili tuweze kwenda sehemu ambayo simu ilikuwa ipo. Lakini kabla hatujatoka, baba na mama walikuwa wamefika.
β Mmefikia wapi?β Aliuliza mama.
β Tumepata location ya simu, hivyo tunaenda huko.β Aliongea mchungaji.
β Sio vzuri kwenda wenyewe tu! Ni vyema tukawaataarifu polisi.β Aliongea baba.
β Polis wanafaida na hasara yake, nazani kwasasa ni vyema tukaenda sisi. Kama kuna lolote tutatoa taarifa polisi.β ALiongea mchungaji.
Wote tuliingia kwenye gari la mchungaji na safari ya kuanza kwenda sehemu ilipo simu ilianza.
EP 12
Saa moja mbele tulifika, ilikuwa ni maeneo ya msamala makinginda karibu na msitu wa chandambali.
β Location inaonesha simu ipo humu ndani.β ALiongea mchungaj. Wote tulishuka kwenye gari na kuifata ile nyumba.
β Wenyeweee..β tuliita.
β Karibu..β ilisikika sauti ya mtu ndani.
Muda ule ule alikuja kufungua mlango.
Niliduwaa yule mtu alikuwa kashika simu ya mume wangu james mkononi.
Pale pale nilimrukia na kumtaka aniambie alipo mume wangu. Baba haraka sana alinishika na kunitaka nitulie.
β Mume wangu yuko wapi?β Nilmuulza yule jamaa kwa sauti ya ukali sana.
β jamani kuna nn? Mbona siwaelewi nyie watu.β Aliongea yule mtu.
β Tunamtaka mwenye hii simu .β Mchungaj alimwambia.
β Sjui aliko.β ALijbu.
β Hujui vipi na simu yake unayo wewe?β Baba alimuuliza kwa ukali. Jamaaa alipotuona tupo serious sana alikuwa mpole. Alitutaka tutulie na kutuahidi kutupeleka kwa mwenye simu. Alituambia hayupo mbali, yupo nyuma ya ile nyumba.
Muda ule ule tuliongozana kuzunguka ile nyumba. Tulipita uchochoro wa kwanza, tukatokea tena uchochoro wa pili. Tulitokea karibu na secondary ya msamala day, Pale tulishuka chini hadi kwenye uwanja wa mpira wa msamala day.
β Aliyenipa simu yupo pale..β Alituonesha kwa kidole nyumba iliyokuwa upande wa chini wa kile kiwanja.
βtwende..β
βAaah mimi kule siendi! Nyie nendeni mtamkuta pale.β Alituambia.
β Hapana, ni lazma twende na wewe.β Aliongea baba kwa ukal sana. Yule jamaa alikuwa mpole. Kinyonge alikubal kwenda na sisi. Tuliongozana mpaka kwenye ile nyumba.
Alibisha hodi dada mwenye kanga moja kifuani akaja kutufungulia.
Kitendo ch kumuona dada anakanga moja kifuani kilinishtua sana. Akili yangu iliniambia kuna jambo lisilo la kawaida lazima linaendelea. Wivu wa mapenzi ulinishika . Pale pale nilimvaa yule dada na kumakaba shingoni.
β Mume wangu yuko wap?β Nilimuulza kwa ukali sana.
β We dada hebu jiheshimu..unanijua mimi nani?β Aliniuliza yule dada kwa nyodo.
β Namtaka james wangu.β Nilibwata .
β Mwanangu hebu tulia kidogo!β Mchungaji aliniambia. Alimgeukia yule dada na kumtaka atuambia mwenye ile simu yuko wapi.
β Aaaah! we mudy kumbe ndio umeiba simu hapa?β Yule dada alimuuliza kwa mshango yule kijana tuliyeenda nae pale.
β Hapana! Nilichukua tu mara moja, sikuiba mimi.β Alijtetea Mudy.
β Ngoja jamaa apate taarifa! Utajuta kuzaliwa.β ALiongea yule dada. Maelezo yake yalitupa matumaini kuwa james yupo mle ndani, ubaya yule dada hakutaka tuinge ndani. Kwa hasira na kwakutumia nguvu tulimtoa pale mlangoni na kuingia ndani.
Loooh! Huwezi amini.
INAENDELEA


