MLENDA WA PORINI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 41
ILIPOISHIA..
“mke wangu, kwanini umetumia fedha kupika chakura icho, na huku unajuwa kuwa, hatuna fedha humu ndani?” aliuliza Abdulazizi, ambae alizuwia hasira kwa mke wake, ni kawaida yake kuongea kwa busara.
Endelea…
Huku akiwa mwenye furaha, na kujiamini yakuwa, ile fedha amepata kwa Shadya, kutokana na urafiki wao, akaachia tabasamu, “baba Ratiff, nimetumia elfu nne tu, kati ya elfu hamsini, nilizo zipata leo” alijibu Zuleiya.
Na hapo akazidi kumchanganya mume wake, yani Abdulazizi, ambae alimtazama mke wake, kama ndio anamwona leo, kwa mara ya kwanza, kitu ambacho kilizidi kumfanya Zuu, atabasamu.
“amenipa mama mwenye mwenyenyumba, alikuja leo, hivi unajuwa ni nani?” aliuliza Zuleiya, ambae furaha yake aikukoma usoni mwake, “mh!, nitamjuwaje, wakati sijawai kumwona” alijibu Abdulazizi.
“tena anamfahamu mama yako, kama uliwai kwenda kwao, na wewe utakuwa unamjuwa” alisema Zuleiya, na hapo Abdulazizi, akahisi sauti kama ya mvumo wa nyuki, kichwani mwake.
“ninani huyo, mbona uniambii?” aliuliza Abdulazizi, kwa sauti yenye shahuku, “ni yule mschana mwarabu, mtoto wa mzee mwarabu, wa kule mashambani Songea” alisema Zuleiya, kwasauti changamfu.
Hakika hii, ilimfanya Abdulazizi, atulie kwa sekunde kadhaa, akijaribu kutafakari, na kuvuta kumbu kumbu kichwani mwake, alijiuliza kama alisha wai kumsimulia Zuleiya kuhusu Shadya, kama alimsimulia basi ata kuwa anamtania,
Lakini katika kumbu kumbu zake, akuwai kumsimulia habari zake na mschana huyu, ambae ni kama tayari alikuwa na familia, na wamesha pata mtoto, kwanini ampatie fedha hiyo, ili hali, anawadai fedha nyingi sana.
“wewe umefahamiana vipi na Shadya, na imekuwaje mpaka akupe ela yote hiyo” aliuliza Abdulazizi, kwa sauti yenye mshangao na mashaka, “siyo ela tu, ametusamehe kodi, amesema tuishi mpaka tutapopata fedha” alijibu Zuleiya.
Zuleiya akuishia hapo, akaendelea kusimulia, jinsi alivyo fahamiana Shadya, mkasa ambao tunaufahamu vyema, “alikuja na mume wake?” aliuliza Abdulazizi, huku anabadiri nguo, usingejuwa kuwa, alikua anasubiri jibu, kwa hamu kubwa.
“mh!, sizani kama ameolewa, ila alikuja peke yake” alisema Zuleiya, na kikapita kimya kigupi, kabla Abdulazizi ajauliza swali jingine, “ajaniulizia?” aliuliza Abdulazizi.
“aliuliza kuhusu mume wangu, nilipomweleza akasema, anamfahamu mama yako” alisema Zuleiya, ambae sasa alikuwa anaandaa chakura, kwaajili ya wote, huku uso wake ukiwa wenye furaha tele.
Hakika habari hii, ni kama ilitonesha kidonda, alicho umia siku nyingi zilizopita, na sasa kilishaanza kupona, Abdulazizi alijikuta anaanza tena, kumfikilia Shadya, japo upendi kwa mke wake Zuleiya.*********
Kwaupande wa Shadya, ilikuwa tofauti kidogo na Abdulazizi, yeye ali Shadya alijikuta akiwa mwenye furaha kubwa sana, “nimemwona mdogo wako Shafii” alisema Shadya, akimwambia Shafii mtoto wake, ambae alikuwa likizo.
“utanipeleka lini nikamwone, vipi baba yangu, nae umwona?” aliuliza Shafii, ambae, alishauliza sana kuhusu baba yake, “tutaenda, siku moja, nitakuambia” alisema Shadya, ambae pia alipiga simu kwa wazazi wake.
Wakati huo tayari simu za mikononi, zilikuwa zimesha anza kutumika nchi nzima, japo mtandao ulikuwa unakamatama baadhi ya maeneo, Shadya alipo waeleza wazazi wake, kuhusu Abdulazizi, na kuwa ameoa tayari.
Bwana Radhaq alikili yakuwa, lilikuwa kosa lake, “lakini akijaaribika kitu, kama unampenda sikufundishi cha kufanya, kutana ongea nae, kama anaweza kusimama kama baba na mume wa wake wawili, basi mkubaliane” alisema mzee mwarabu.
Ilo pia lilikuwa ni hapizo la Shadya, kabla ata ajaambiwa na baba yake, hivyo akakubaliana na wazo lile, japo ilimuwia vingumu, kumkabiri Zuleiya, kutokana na urafiki wao.
Na aliona itakuwa mbaya zaidi, endapo Zuleiya, atakapo ambiwa kuwa mume wake anaowa mke wapili, na mke mwenyewe ni yeye, japo ata kama angemkasirikia, isinge muathiri chochote, lakini aliona ingekuwa vibaya sana, kutokana na kufahamiana kwao.
Lakini siku ya alkhamis, iliyo fuata, baada ya kujadiri kwa muda mrefu moyoni mwake, Shadya akaaona iswe tabu, akapiga simu kwa mama Tony, na kumtaka amtume mtoto, apelike simu kwa mama Ratiff.
Mama Tony, akamtuma Tony, apeleke simu kwa mama Ratiff, na alipoifikisha ndipo maongezi yakaanza, “Asalam Aleykum dada” alisalimia Shadya upande wa pili wa simu, kwa sauti yenye upole, na nyenyekevu.
Upole na nyenyekevu wa Shadya ulimshtua Zuleiya, “Waleykum Salam, dada Shadya, za huko” alisema Zuleiya, kwa sauti ile ile changamfu, akijaribu kumchangamsha Shadya.
“huku salama tu, sijuwi wewe mtoto na shemeji” alisema Shadya, kwa sauti ile ile tulivu, yenye unyenyekevu, ungesema mschana huyu, anamaisha ya chini, na anaitaji kuomba msaada flani.
Ilimshtua na kumshangaza Zuleiya, “wao wapo salama kabisa, sijuwi shemeji na watoto” alisema Zuleiya kwa sauti changamfu, yenye furaha, Shadya akaachia kicheko laini.
“mwanao ajambo, lakini bado sijabahatika kuolewa” alisema Shadya kwa sauti yenye kupoa, huku kichwani mwake, akijiliza itakuwaje, kama akijuwa mume anaemtarajia ni mumewake Abdulazizi.
SEHEMU YA 42
“inshallah, mwenyezi mungu akufanyie wepesi, upate anae kufaa” alisema mama Ratiff, kabla ajatulia na kusikiliza nia na dhumuni ya simu ile, “dada mimi nina shida, naombe nije kesho tuongee” alisema Shadya, kwa sauti yenye upole.
Hapo kidogo, Zuleiya alishtuka, maana akujuwa ni maongezi ya aina gani, ambayo mwanamke huyu, anataka kuongea na yeye, “uwezi ukaniambia haraka dada, kabla ujasumbuka kuja huku?” aliuliza Zuleiya, kwa sauti yenye tahadhari.
“ni muhimu tunikija tukaongea, maana nijambo lenye kuitaji utulivu” alisema Shadya, kwa sauti ile ile ya upole, “unanitisha dada, uwezi ukanidokeza kidogo” alisema Zuleiya, ambae alikuwa na shahuku kubwa, ya kusikia jambo ilo.
“usijari dada, ni ombi tu, wala usiwe na wasi wasi” alisema Shadya, kabla awajaagana na kukata simu, na simu ika rudishwa kwa mama Tony, ambae akujuwa, kulikuwa na maongezi gani.*********
Jioni ya siku ile, Abdulazizi alirudi mida ya saa mbili za usiku, akiwa amechoka kweli kweli, na bahati mbaya zaidi ni kwamba, siku ile ilipita bila yeye kupata fedha yoyote, kama zilivyo siku nyingine zilizo pita.
“mke wangu, kama hali itaendelea kuwa hivi, nazani tunaitaji kurudi Songea, ambako tunaweza kuishi maisha mazuri, kuliko huku” alisema Abdulazizi, ambae onekana kukata tamaa ya maisha.
Kiukweli mwonekano wa Abdulazizi, ulimshanganya ata Zuleiya, ambae alisahau, kabisa kama alipigiwa simu na Shadya, akimtaka kesho waongee jambo flani.
“wazo zuri baba Ratiff, yani huku naona kama maisha magumu sana, tena Songea, tunaweza ata kujenga nyumba yetu” alisema Zuleiya akiunga mkono, wazo la mume wake Abdulazizi.*******
Naaaaam!, Zuleiya nikama akuamini alicho sikia, toka kwa mwanamke mwenzie, na siyo tu mwanamke, ila ni mwanamke, mwenye sifa ambazo, kila mwanamke anatamani kuwa nazo.
Yani uzuri wa sura na umbo, uwezo wa kifedha na maisha mazuri, elimu na kila kitu alicho jaliwa kuwa nacho Shadya, sasa amekosa nini mpaka anataka kuwa na Abdulazizi, mwanaume wake yeye, ambae maisha yake ya kuunga unga.
“samahani dada Shadya, naomba nikuulize swali la mwisho” alisema Zuleiya, ambae ni kama bado alihisiku kuwa, ombi la Shadya likuwa utani, au kumpima imani.
“niulize tu dada yangu, ila naomba ulielewe jibu nitakalokupa” alijibu Shadya kwa sauti ya unyenyekevu, “unaweza ukanieleza, ni kitu gani, ambacho kimekufanya uone kuwa, Abdulazizi ndie pekee anaekufaa” alisema Zuleiya, huku anamtazama Shadya kwa umakini.
“kweli Abdulazizi namfahamu toka utoto, na yeye ndie mwanaume pekee nilie wai kuwa nae, sijawai kuwa na mwanaume mwingine, isitoshe ndie baba wa mtoto wangu Shafii” alisema Shadya, ambae nikama alikuwa ajamiliza.
“pia Abdulazizi ni mwanaume wakipekee sana, alisababisha nijiapize kuwa mke wake, ikibidi kuwa mke wapili kama hivi” alisema Shadya, akisimulia kifupoi historia yao, kuanzia kuanza kwao, mapaka kilicho watenganisha.
Pia alimsimulia jinsi alivyo msaidia baba yake, asipoteze maisha yake, kwakifupi historia ya Shadya na Abdulazizi ilimsisimua Shadya, ambae alimini, kuwa pengine dua zake na kutaka kuishi na Abdulazizi, ndizo zilizo wachelewesha wawili awa.
Kwamaana ata kama yeye alipangiwa kuwa mke wa Abdulazizi, hakika isingewezekana kuwa hivyo, endapo Abdulazizi angekuwa bado yupo na Shadya, kwahiyo kutengana kwao, ilikuwa ni lazima itokee, ili na yeye aanze kupata nafasi.
“hakika kila kitu utokea kwa sababu” alisema Zuleiya, kwa sauti tulivu, kama ya mtu alie fikia tamani ya kufikili, “kwanini unasema hivyo dada” aliuliza Shadya huku anamtazama Zuleiya.
“ilipangwa utengane na Abdulazizi, angalau na mimi nipate nafasi, kwamaana hiyo, siwezi kukuzuwia kurudi kwenye maisha yako, na mwanaume unae mpenda” alisema Zuleiya, ambae sasa alijuwa ni kwanini Shadya anamwita dada.
Naaaaam!, Zuleiya anatafakari kile alicho ambiwa, na kuona ya kuwa hakuna na namna ya kukubaliana na Shadya, kwamba awe mke mwenzie, kutokana na mabo kadhaa.
Kwanza kabisa, achana na swala dini, ambalo lina luhusu mke zaidi ya mmoja, ila sasa tuangalie upendo waliokuwa nao wawili awa, kiasi cha mwanamke kuamua kumsubiri mwanaume, mpaka katika umri huu.
SEHEMU YA 43
Zuleiya alikumbuka siku ambayo, alikuwa anaonge ana Abdulazizi, na kumwuliza kuhusu zinaa, nae alimwambia amezini utotoni, na mwanamke, mmoja tu, inamaanisha kabla ya kukutana kwao, Abdulazizi alikuwa ametembea na mwanamke mmoja tu, ni vigumu kwa wanaume wa umri wao.
Achana na kupendana kwao, pia wawili awa tayari walikuwa na mtoto, swala ambalo bado Abdulazizi alikuwa ajalifahamiu, na mbaya zaidi yeye ndie alikuwa anajukumu la kumuomba mume wake, amuoe Shadya rafiki yake.
Mpaka hapo Zuleiya akaona busara ni kumluhusu mume wake, aoe mwanamke wapili, maana hakika ni kazi ngumu kuacha mwanamke kama Shadya, vinginevyo angesababisha uthariti katika ndoa yao.
“sawa nimekuelewa dada, ndoa ni jambo la kheri, kuliko zinaa, mpaka umeamua kuniambia, naamini ya kuwa, unampenda sana Abdulazizi, na uwezi kujizuwia” alisema Shadya, kwa sauti tulivu, huku anaachia tabasamu.
Hapo Shadya akaachia tabasamu la furaha, na kabla Shadya ajasema kitu, Zuleiya aka ongea, “lakini ninaombi moja dada Shadya” alisema Zuleiya, ambae aliongea huku akionyesha hali ya uchangamfu.
“niambie dada, nitatekeleza kwa moja mmoja” alisema Shadya, ambae nikama vile alishaanza kupata matumaini, ya furaha, kwa kuona dalili ya kuopata faraja ya moyo wake.
“nakuomba dada yangu, vyovyote itakavyo kuwa, usiluhusu Abdulazizi aniache kwaajili yako” alisema Zuleiya, kwa sauti ya kuombeleza, kiasi cha kutia huruma.
“usiseme hivyo dada Zuu, na kuhakikishia, nje ya kosa la uaminifu, nguzo kuu ya ndoa yetu, ni Abdulazizi kuto kumwacha mmoja wetu, atatakiwa kutupenda wote bila upendeleo” alisema Shadya, na wote wakatabasamu.
Hapo yakaanza maongezi ya hapa na pale, na kupanga namna ya kuongea na Abdulazizi, wakakubariana kuwa, licha ya kuwa atakae mwambia ni Zuleiya, lakini Shadya ataandaa siku ya kuongea, na walipanga iwe siku inayofuata, yani jumamosi.*********
Naaaaam!, saa tisa jioni, Shadya aliwaaga wakina mama Tony, na wapangaji wengine, kisha wakaondoka kwa pamoja, na mama Abdullratiff, kuelekea upande wa barabarani.
Njiani, Shafii alikuwa anamwita Abdullratiff mdogo wake, na huku Zuleiya akimwita mama mkubwa, ni wazi alishaelekezwa kabla ya kufika hapa, na ndivyo Ratiff nae alivyo fanya, kumwaita Shafii kaka, huku akimwita Shadya mama mkubwa.
Safari yao ilienda mpaka mbezi, ambako walizunguka madukani, wakanunua nguo nzuri, na viatu, kwaajili ya Abdulazizi mke wake, yani mama Ratiff, na Abdullratiff mwenyewe, pia walinunua vitu viwili vitatu.
Mwisho wakaagana, huku wakipeana maelekezo muhimu, kuhusu kesho, siku ambayo walipanga wamweleze Abdulazizi, kuhusu ombi la Shadya la kumowa,.
Baada ya hapo, Zuleiya na mtoto wake, akakodiwa taxi, na kurudi malambamawili, huku Shadya akielekea mjini, nyumbani kwake, akiwa na mtoto wake na dada wakazi.
Ukweli ni kuwa, Zuleiya au mama Abdullratiff, licha ya kukubari ombi la Shadya, kiukweli alilazimika kufanya hivyo, maana moyo wake, ulijawa na hofu kubwa sana, ya kumpoteza mume wake.
Lakini Zuleiya akajipa moyo wakuwa, mueme wake alikuwa anmpenda, na pia alipata moyo, kwa kile ambacho Shadya alikiahidi kwake, kwamba, shariti la ndoa hii ya pili, ni Abdulazizi kuto mwacha mmoja wao.*******
Njiani Shadya alikuwa na furaha kubwa sana, ambayo kiukweli aliwaambukiza mpaka wenzake, nao wakajikuta wanafurahi, huku safari yao inaendelea.
Lakini moyoni mwake, alikuwa na mashaka kadhaa, na yte ni kuhusu Abdulazizi mwenyewe, je bado anampenda, itakuwaje kama ampendi tena, na upendo wote amewekeza kwa mke wake.
Je, Abdulazizi atakubari kumuoa, tena akiwa tayari anamke wake, itakuwaje akimkataa, kiukweli swali ilo, lilimfanya Shadya, awe katikatikaati, yani hamsini kwa hamsini.********
Naaaaaam!, wakati hayo yanaendelea, huko kibamba, gereji kwakina Abdulazizi, anaonekana bwana Abdulazizi, akiwa amekaa, katika mikao mbali mbali.
Njaa zimewashika, huku kazi moja waliyo ipata, ilikuwa ndogo sana, kiasi cha kushindwa, ata kununua chakura cha kuwatosha wote, hivyo walinunua juice na kugawana wote wanne.
SEHEMU YA 44
Lakini bwana Abdulazizi, licha ya yote aliyokuwa anayapitia, leo alikuwa katika mawazo mazito sana, akimfikilia Shadya, kuna wakati alitaka kukubari kuwa, penzi lao lilikuwa ni utoto.
Lakini alipokumbuka, mara ya mwisho kuonana kwao, mambo waliyo ya fanya, na ahadi walizopeana, siku zile walizokaa pamoja pale nyumbani kwa mwarabu.
Abdulazizi alikuta anajifanya, kuwa yeye ni mtambuzi, wa maswala ya mapenzi, yakuwa, usimwamini mwanamke, ata akisema anakupenda kiasi gani, licha kuwa utafiti wake huo unakataa na ukweli harisi.
Maana anapo fikilia kuhusu Zuleiya, mschana ambae mpaka anatimiza miaka ishirini, alikuwa ajaijuwa dudu ya mwanaume, alie amua kusafiri na baskeri toka jijini, mpaka mjini, akiwa na mafurushi ya zawadi, kuja kumletea kitumbua.
Hapo Abdulazizi, anaona kuwa, mapenzi yakweli bado yapo, anapo fikilia ilo, anawaza kutena kuhusu Shadya, anakumbuka kuwa, Shadya akumwacha kwa kupenda kwake, ilikuwa ni baada ya baba yeke Shadya kufahamu swala ili.
Lakini mpaka hapo, Abdulazizi anajuwa kuwa, amesha poteza, penzi la mwanamke huyo wa totoni, ambae sasa atakuwa na mwanaume mwingine, tena mwenye fedha nyingi, na wanapendana.
Kwakifupi kuna wakati alijilalamikia, na kuna wakati alishukuru na kukubari matokeo, japo mawazo ayakumtokea kichwani mwake, mpaka alipofika nyumbani, ambako alimkuta mke wake, ametulia waza jambo flani.
“Asalam Aleykum mke wangu” alisalimia Abdulazizi, huku anakaa kwenye mkeka, “Waleykum Salam mume wangu, pole na kazi” aliitikia Zuleiya, kwa sauti flani, aliyo jitaidi kuichangamsha.
“asante sana, vipo lakini, mbona umepooza mke wangu…..” kabla bwana Abdulazizi ajamaliza swali lake, mtoto Abdullratiff akaja mbio mbio sebuleni, akitokea chumbani.
“Asalam Aleykum baba” alisalimia Ratiff, kwa sauti yenye uchangamfu na furaha, “Waleykum Asalam Aleykum, umeshindaje Ratiff” aliitikia Abdulazizi, huku anamshika mtoto wake na kumsogeza kwake, akikaa nae karibu.
“alikuja mama mkubwa mzungu, na kaka Shafii” alisema Ratiff kwa sauti yenye ushangamfu, na kumfanya Abdulazizi amtazame mke wake, kwa macho ya kuuliza, mama mkubwa mzungu yupi.
Kabla Zuleiya ajajibu, Abdullratiff akajibu swala ilo, “we umjuwi mama mkubwa mzungu, mwenye gari lake, tukapanda gari mpaka hukoooo” alisema Shafii, kwa sauti changamfu.
Safari mama Ratiff akusubiri mume wake ajibu, “alikuja Shadya na mtoto wake, ndio anasema mama mzungu” alisema Zuleiya, “hooo!, kumbe alikuja, sasa aliwapeleka wapi?” aliuliza Abdulazizi kwa sauti yenye mashaka.
“tutaongea baada ya insha mume wangu” alisema Zuleiya, na hapo Abdulazizi akatulia kidogo, kisha akaenda kuoga kabisa, na baada ya hapo wakaswali insha, na mwisho wakala chakura cha jioni, na kutulia wakianza maongezi.
“mume wangu, kwanza samahani nimekubari mwaliko wa Shadya, bila kukusubiri, maana nisingekuwa na njia ya kumjulisha kama tumekubari au la” alisema Zuleiya, akifwata mpango wao na Shadya mwarabu.
“wapi, mwaliko wa nini?” aliuliza Abdulazizi, kwa sauti ya mshtuko, na yenye usikivu wa ukali kidogo, inamwogopesha kidogo Zuleiya, ambae anainamisha kichwa chini.
“nyumbani kwake upanga, ila ameomba twende wote” alisema Zuleiya, kwa sauti ya upole, inamshtua Abdulazizi, ambae sasa anaona wazi, kidonda chake cha miaka saba, iliyopita, kinaenda kutufuliwa upya.
Maana hiyo lazima akamwone mwanaume ambae, sasa anatafuna kitumbua cha mwanamke ambae, siyo tu kujifunzia mahaba, ila pia na yeye amefundisha baadhi ya mikao, ambayo sasa wanatamba nayo.
SEHEMU YA 45
“jamani mama Ratiff, unawezaje kukubari mwaliko, kama huo, na hali yenyewe hii tuliyo nayo” aliuliza Abdulazizi, kwa sauti ya kulahumu, huku anawaza sababu ambayo itamfanya akatae mwaliko huo, wa mwanamke alie waonyesha upendo kwa kuwafutia kodi ya miezi sita.
Wakati huo Zuleiya nae, akaona dalili za Abdulazizi kukataa safari, na endapo atakataa, itaonekana yeye, ndie alie shawishi kukataa huko, lakini wakati anawaza neno la ushawishi, Abdulazizi akaongea tena.
“kwakweli atuwezi kwenda, hatuna nguo za kuvaa, tutakutana na watu wengi matajiri, na mimi nasikia huko upanga kuna matajiri tu” alisema Abdulazizi, na hapo Zuleiya akatabasamia chini, kwa kuona hofu ya mume wake.
“hapana mume wangu, ni mwaliko wa familia tu, isitoshe tumenunua mavazi kwaajili ya kesho” alisema Zuleiya, na kumshangaza tena mume wake, “mavazi, kwafedha gani mama Ratiff?” aliuliza Abdulazizi, kwa sauti ya chini, huku anamkazia macho makali Zuleiya.
Japo awakuwai kugombana wawili awa, lakini Zuleiya aliona wazi anaenda kugombana na mumewe, kwasababu ya Shadya, alitamani maongezi yaishie hapa, lakini aliona kuna umuhimu wa mume wake kumwoa Shadya, maana zaidi yahapo ingefwata uthariti, na, mwisho yeye kuachika.
“samahani mume wangu, nimepokea nguo alizo nunua yeye kwaajili ya kesho, lakini aliniambia kuwa, nyie ni marafiki wa utotoni, tena ata wazazi wake, wanakuchukulia kama mtoto wao” alisema Zuleiya, kwa sauti ya upole.
Hapo Abdulazizi anatulia kwa sekunde kadhaa, huku mke wake alie inamisha kichwa chini, anamtazama kwa jicho la wizi, “sawa tutaenda, lakini sijuwi tutapajuwaje hapo kwake” alisema Abdulazizi, kwa sauti kama ya kishingo upande.
Ukweli baada ya jibu ilo, Zuleiya aliachia tabasamu pana la furaha, ata kabla awajalala, Zuleiya alitafuta nafasi ya siri, na kwenda kupiga simu kwa mama Tony, maana Abdulazizi mwenywe, bado alikuwa ajaanza kumiliki simu.******
Siku ya pili ambayo ilikuwa jumamosi, mida ya saa tano za asubuhi, tayari Abdulazizi na familia yake, walikuwa wamesha jiandaa, gari likaja na kuwa chukuwa, lilikuwa ni gari aina ya Nissan patrol.
Njiani, wakiwa wanaelekea upanga, Abdulazizi alionekana mtulivu sana, akiwaza jinsi atakavyoweza kukabiriana, na kitendo cha kumwona Shadya akiwa na mume wake.
Hakika alihisi wivu mkali unamuumiza moyo, “lakini tukai sana” alisema Abdulazizi, na hapo mke wake akatania, “nitakusikiliza wewe, pangine unaweza kubadiri mawazo na ukata tulake huko huko” alisema Zuleiya, na wote wawili wakacheka, wakisaidiwa na dereva.******
Saa sita na robo, walikuwa wanashuka toka kwenye gari, mbele ya jumba moja kubwa, lenye uzio mkubwa, huku bustani ya maua, ikizunguka jumba lile na vile viunga vya mbele, vyenye magari kadhaa ya kifahari.
Walipokelewa ile wanashuka tu toka kwenye gari, mara mlango wa nyumba kubwa unafunguliwa, na hapo akatokea Shadya mwenyewe, ambae ukimwona unaweza kusema ni mwarabu, na siyo chotara.
Shadya ambae uso wake ulijawa tabasamu, lenye uzani wa aibu, muda mwingi akiinamisha uso wake chini, aliongozana na waschana wawili weusi, pamoja na mtoto wake Shafii.
Zuleiya anamtazama mume wake kwa macho ya wizi, anamwona akiwa anamtazama Shadya kwa macho yenye mshangao na ubwataha, “Asalam Aleykum” alisalimia Shadya alipowafikia.
“Waleykum Asalam Aleykum” aliitikia Zuleiya kwa ushangamfu, huku mtoto Shafii nae, akisamfwata Abdulazizi na kumsalimia, “Asalam Aleykum aleykum baba” ndivyo alivyosalimia Shafii.
SEHEMU YA 46
“Waleykum Salam, ujambo” aliitikia Abdulazizi, kabla Shafii, ajamsogelea mdogo wake, Abdullratiff, na kumshika mkono, kisha kumwongoza ndani, wakionekana kufurahiana.
“karibuni ndani jamani” alisema Shadya, huku anawaongoza wageni hawa, kuingia ndani, Abdulazizi licha ya kuduwazwa na uzuri wa Shadya ulio zidi mara dufu, kiasi cha kumwongezea wivu, lakini akuacha kuduwazwa na uzuri wake.
Naaaam!, wawili awa wanaingia ndani na kuibukia sebuleni, ambapo pame pambwa na zuria la manyonya ya njano na nyupeee, huku meza kubwa ndogo ya kioo, ikiwa kati kati, ya sebule, imezungikwa na makochi ya sofa, zagarama kubwa.
“karibu jamani mjisikie mpo nyumbani” alisema Shadya, na hapo wafanyakazi wakaanza kuwa hudumia vinywani, huku Shadya ambae siku ile alivaa gauni refu kama kawaida, akifunika nywele, ka ijab, akipendeza kama vile na yeye ni mgeni.
Kiwa na wageni wake sebuleni, muda mwingi akishindwa kumtazama Abdulazizi usoni, alie kuwa anamtazama kwa macho ya wizi, japo mara kadhaa, walikutanisha nyuso zao, na Shadya aliishia kutabasamu, kwa aibu.
Matukio hayo Zuleiya aliyaona, lakini akuwa na la kufanya, zaidi ya kutabasamu, na kuendelea kuwaangalia, watoto wote wawili, walikuwa wanacheza kwenye magari ya watoto, ambayo Shadya aliyanunua kwaajili ya Shafii.
“habari za siku nyingi Abdulazizi” alisalimia Shadya, kwasauti yenye utulivu na unyenyekevu, tofauti na ile ambayo, Abdulazizi aliizowea siku zote, sauti yenye ucheshi na uchangamfu.
“salama kabisa, sijuwi wewe” huku anatazama chini, hii ni baada ya kuona mgeni huyu, akuwa na mpango wa kuanzisha maongezi, alijibu Abdulazizi, ambae pia alijifanya kuto kumtazama Shadya.
“mimi nipo salama, karibu sana, hapa ndio nyumbani” alisema Shadya, kwa sauti ile ile ya upole na aibu, akiwa amekaa karibu kabisa na Zuleiya, kwenye kochi, lililokuwa linatazama na lile alilokaa Abdulazizi.
“asante sana” alisema Abdulazizi, baada ya hapo Zuleiya akaingilia na kuanzisha maongezi mengine, ambayo yalidumu mpaka muda wakula, wakati huo Abdulazizi alikuwa anashahuku ya kuuliza kuhusu mume wa Shadya.
Saa saba, walichukuwa udhu, na kwenda kuswali hadhuhuri, walipomaliza wakenda kwenye ukumbi wa chakura, na ukaaji wao sasa, Zuleiya alikaa kulia kwa Abdulazizi, na Shadya akakaa kushoto kwa Abdulazizi.
Hapo yakaanza matendo flani ambayo, matendo ambayo, yalimshangaza ata Abdulazizi mwenyewe, nakujikuta anaanza kusahamu hukusu mume wa Shadya.
Maana wakiwa mezani, wawili awa, kila mmoja alimhudumia Abdulazizi, kama Zuleiya angemsongezea maji, ya kunawa, basi Shadya angemsogezea maji yakunywa.
Kama Shadya angemsaidia Abdulazizi, kuweka chakura kwenye sahani yake, basi Zuleiya angemwekea mboga, wakati huo wote wawili wakipeana maelekezo, “msogezee kile, mpe iki” kwasauti zenye utulivu, wa kimahaba, na nyuso za furaha.
Mwisho walipomaliza kula, chakura hiki kitamu kizuri kama cha sikukuu, walikaa tena sebuleni, na watoto wakatoka nje kucheza, na kuwaacha wapendanao awa, wakiwa wamebadiri mkao, safari hii, Zuleiya, alikuwa amekaa na Abdulazizi, kwenye kochi moja.
Huku Shadya, akiwa amekaa kochi la mbele yao, yani wakiwa wanatazamana na wakina Zuleiya, kimya kilikuwa kimetawara, ndani ya sebule hii kubwa, yenye vitu vya thamani, huku nyimbo za kaswida zikiwatumbuiza.
Ukweli Abdulazizi, mpaka hapo, alikuwa ajaelewa chochote ambacho, kimepelekea mwaliko huu, japo alifurahi kwa chakura kitambu, na vinywaji vitamu, kama juice ya matunda waliyokuwa wanainywa sasa hivi.
Wakati Abdulazizi anawaza hayo, kwa bahati mbaya akamwona Shadya anamkonyeza Zuleiya, na kabla ajamwuliza chochote Zuleiya, Zuleiya mwenyewe akaanza kuongea.
“samahani mume wangu, kunajambo nitaka kuombe” alisema Zuleiya kwa sauti tulivu, yenye unyenyekevu, huku uso wake ameuinamisha chini, “mama Ratiff, ilo jambo aliwezi kusubiri nyumbani” aliuliza Abdulazizi, ambae alionyesha kuto kupenda jambo lile.
“lina tuhusu sisi watatu, ni vyema dada Shadya akiwepo kati yetu” alisema Zuleiya, kwa sauti ile ile, “ombi gani, ilo, bila shaka nitakuwa na uwezo nalo” alisema Abdulazizi, huku anajiweka sawa.
“mume wangu, sijawai kukuomba jambo kubwa, kama wanawake wengine wanavyo fanya, sijawai kuomba ununue gari, au uninunulie vitu vya gharama, ila ninaombi langu moja tu” alisema Zuleiya kwa sauti ile ile tulivu.
SEHEMU YA 47
“mama Ratiff unazunguka sana, au nikitu ambacho unajuwa sina uwezo nacho?” aliuliza Abdulazizi, huku anawatazama wawili awa kwa zamu, wote walikuwa wameinamisha vichwa chini.
“naomba unikubalie, dada Shadya awe mke mwenzangu” alisema Zuleiya, kwa sauti yenye unyenyekevu wa hali ya juu, huku ameinamisha uso wake chini, nakumfanya Abdulazizi, ashikwe na mshtuko na mshangao wa hali ya juu.
Abdulazizi, ambae anamtazama Zuleiya kwa macho yenye kuhakiki, kama anacho kisema ni kweli au wanatania, lakini anakosa jibu, maana Zuleiya, ameinamisha uso chini, anamtazama Shadya, Shadya nae alikuwa ameinamisha uso chini.
Abdulazizi anaangua kicheko kikubwa, kama vile wapo kwenye utani, “kiasi cha kuwafanya zuleya na Shadya watazamane, kwa macho yenye viulizo, wakizania kuwa Abdulazizi anakataa mpango wao.
“mama Ratiff ujawai kunifanyia utani kama huo, umefikilia nini mpaja unitanie hivyo” aliuliza Abdulazizi, huku anamtazama Zuleiya, “siyo utani mume wangu” alisema Zuleiya kwa sauti ya upole, na kuendelea.
“najuwa kuwa, ndoto yenu ilikuwa ni kuishi pamoja, mimi ndie nilieingia kwenye ndoto yenu, nitaurahi kama utatimiza ndoto yako na ndoto ya dada Shadya, kwa kumuoa pia, ata dini inaluhusu” alisema Zuleiya.
Hapo kiukweli, ilimshangaza sana Abdulazizi, ambae anajiuliza je ni kweli anaombwa kumwoa Shadya, vipi kuhusu mume wake, na kwanini Shadya aongei chochote.
“lakini mama Ratiff, Shadya anafamilia yake, uliwai kuona wapi jambo ilo linatendeka ikiwa mwanamke anamum…..” aliuliza Abdulazizi, lakini swali ili, alie jibu alikuwa ni Shadya mwenyewe.
“hapana Abdulazizi, bado sijaolewa, na sijawai kuwa na mwanaume yoyote zaidi yako” alisema Shadya kwa sauti ya unyenyekevu, huku ameinamisha kichwa chini.
Inamshangaza kidogo Abdulazizi, ambae anamtazama Shadya, alie kuwa ameinamisha kichwa chake, “inawezekana vipi, wakati umepata mtoto?” aliuliza Abdulazizi kwa sauti ya chini, iliyo jawa na mashaka.
“huyu mtoto unaemwona ni wa kwako, na ndio chanzo cha baba, kutaka kumshambulia mama yako, na pia alinizuwia nisije Songea, mpaka baada ya kujifungua” alisema Shadya, kwa sauti ya chini, uso ameinamisha chini.
Inamshtua sana Abdulazizi, ambae sasa, anamtazama Shadya kwa macho ya mshangao, kabla aja mtazama Zuleiya, alikuwa anamtazama, huku anatabasamu, “inawezekana vipi, na wewe ulikuwa unajuwa?” aliuliza Abdulazizi, huku anamtazama mke wake.
Zuleiya ainaitikia kwa kichwa, kukubalikuwa alikuwa anajuwa, “mbona ukunimbia, nilikuwa najuwa umesha olewa, nilikuona mara mbili, ukiwa na mtoto, nikashindwa kukusogelea” alisema Abdulazizi, kwa sauti yenye lawama nyepesi.
“nilikutafuta sana, sikujuwa unapatikana wapi, nilifika kwenye gereji uliyokuwa unafanyia kazi, nikaambiwa umeamia Dar_es_salaam” alisema Shadya, akiwa ameinamisha usoni chini.
“kwanini nilifumbwa kiasi hiki, sikuweza kufikili kama mtoto anaweza kuwa wangu” alisema Abdulazizi kwa sauti ya kujilahumu, “ilipangwa usijuwe mapema, ili utuowe sote wawili, naomba nikubalie, Shadya awe mke wenzangu” alisema Zuleiya.
SEHEMU YA 48
Hapo Abdulazizi akatulia kwa sekunde kadhaa, akiwatazama wote wawili kwa awamu, na kabla ajasema lolote, Zuleiya akamwonyesha ishala Shadya, kwamba aje kwenye kochi walilokaa wao.
Akiwa na wasi wasi mwingi, Shadya akamtazama Abdulazizi, ambae aliachia tabasamu jepesi, huku ananyoosha mkono wa kuume, nae akainuka na kuushika mkono wa Abdulazizi, kisha akaja kukaa kwenye kochi lile, upande wa kushoto.
“asante mume wangu, kwa kukubari ombi langu” alisema Zuleiya, huku anaegemea kwebega la kulia la mume wake, na Shadya akafanya hivyo kwenye bega la kushoto la Abdulazizi.
“lakini mume wangu ninaombi moja” alisema Shadya, inamshtua kidogo Abdulazizi, ambae alijuwa fika ya kuwa, kinacho takiwa ni taratibu za kufunga ndoa, “ombi gani tena?” aliuliza Abdulazizi, huku anageukia upande wa Shadya.
“naomba mmoja wetu asiwe chanzo cha mwingine, kukosa upendo, au kuachika” alisema Shadya kwa sauti yachini yenye furaha, akiwa bado ameegemea bega la mwanaume alie mtamani, toka siku nyingi.
“nawapenda sana wake zangu, pia asanteni sana kwa kuuangalia moyo wangu, maana ni vigumu sana kwa mwanamke kukubari mke mwenzake, nawaahidi, sito thubutu, kuandika taraka kwa mkono wangu, kwaajili ya mmoja wenu” alisema Abdulazizi, ambae mpaka hapo nika alihisi yupo ndotoni.
Furaha iliyokuwepo pale ilikuwa ni kubwa sana, wote watatu walifurahi, na kupanga namna ya kufanya taratibu za kisheria, ili Shadya na Abdulazizi wafunge ndoa.
Ata baadae wakina Shafii na Abdullratiff, walipomaliza kucheza, waliingia ndani, huku Shafii akionekana alisha juwa kuwa, Abdulazizi ndie baba yake, maana muda wote aliamwita baba, nikama alivyofanya kwa mdogo wake Ratiff.******
Naaaaaam!, wiki moja baadae, siku ya jumamosi, Abdulazizi na Shadya walifunga ndoa, kwenye msikiti wa upanga, karibu na muhimbili, wazazi wa pande zote mbili walikuwepo, ongeza wazazi wa Zuleiya.
Wote walikuja Dar_es_salaam kwa gari la binafsi, yani gari la mzee Radhaq, au mwarabu, ambao tayari walisha mwomba msamaha, mama Abdulazizi, yani bi Khadija, ambae aliwasamehe.
Lakini licha ya hayo, pia bi Khadija, alikili yakuwa, lilikuwa tukio baya kwa watoto, kufanya michezo kama ile, hivyo kama mzazi, mzee Radhaq alikuwa na haki ya kukasirika, na kutaka kuchukuwa hatua mbaya kama ile.
Harusi ilikuwa nzuri, japo waliita ni ndogo, lakini walikuja watu wachache wenye fedha nyingi, wakiwemo wanaume matajiri, ambao walisha wai kumtongoza Shadya, ambae aliwakatalia.
Naaaaaam!, Zuleiya na Abdulazizi waliama, kwenye ile nyumba ya kupanga, mara baada ya kununuliwa nyumba kubwa huko kibaha mkoani, huku wakipewa gari aina ya Nissan patrol kwaajili ya kutembelea.
Abdulazizi alifungua gereji kubwa sana, ambayo mpaka naandika hadithi yao, ilikuwa inaumiwa na shirika la bima, na pia ilikuwa ina nunua magari mabovu, na kuyakarabati, kisha kuyauza tena, biashara ambayo ilikuwa yake mwenyewe.
Ama hakika Abdulazizi abawapenda wake zake, ambao kwa sasa, kila mmoja anawatoto wa nne, huku Zuleiya akiwa anamiliki duka la vifaa vya watoto, lililopo karibu na hospital ya mloganzira.
Zuleiya na Shadya, wanapendana sana, wanaishi kwa kushirikiana, ungesema wameolewa na ndugu wawili tofauti, na siyo mtu mke mwenzie, kitu kizuri kwao, wanapata haki yao kwa ufasaha toka kwa mume wao, ambae anazingatia zamu ya kulala kwa wake zake.
Wakati namaliza kuandika hadithi hii, Shafii ambae sasa anaishi USA ana karibia kuja kumtambulisha mke wake, na mtoto wao mmoja, wakati huo mdogo wake Abdullratiff akiwa ndio anaanza maisha huko huko USA.
NAAAAAM!, huo ndio mwisho wa hadithi hii ya #MLENDA_WA_PORINI, kaa tayari kwa hadithi nyingine nyingi zitakazo kujia hapa hapa.


